Jackwillpower
JF-Expert Member
- Oct 4, 2017
- 2,467
- 3,687
UNALETA POROJO TU ,UNAWEZA KUIPINGA BIBLIA WEWE?hivi Wewe jamaa utawatenganisha vipi wayahudi na Mila za kale za waashuru?
Tatizo lako wewe umekomaa na historia nusu ya Wayahudi bila kuona chanzo Cha mwanzilishi wa Imani hiyo Yaani Mzee abrahamu na Jamii alizotokea Mimi nimeanza kuchimbua historia ya Abraham kabla hajahama na baba yake Mzee Terra kutoka uru ya wakaldayo mpaka kwenye marago ya kaanani na kuweka makazi pale,
Sasa utamtenganishaje babu ya Wayahudi na Mila za Mesopotamian?
Kwanza huyo Mzee mwenyewe alikua anaabudu miungu ya waashuru mpaka pale Merchizedec mtawala wa Salem alipompa ujuzi wa Mungu El Murduc hapo ndipo jamaa akachange akaanza Jenga madhabahu za Mungu El na kumwabudu
Sasa turudi kwenye source ya huyo mungu wa Merchizedec alikua Mungu Gani katika Aina ya Ile miungu ya ANNUNAKI?
Utapiga chenga weeeeee ila utarudi pale pale kwenye kwenye chanzo Cha miungu napokazia Mimi!
Biblia iliandikwa katika kipindi cha miaka 1,600 hivi. Historia na unabii unaopatikana ndani yake unahusiana na serikali saba kuu za ulimwengu: Misri, Ashuru, Babiloni, Umedi na Uajemi, Ugiriki, Roma, na Muungano wa Uingereza na Marekani. Serikali hizo saba zitazungumziwa katika mfululizo wa makala saba. Kusudi la makala hizo ni nini? Kuonyesha kwamba Biblia inategemeka na imeongozwa na roho ya Mungu na kwamba ujumbe wake unatoa tumaini—tumaini la kwamba matatizo yanayosababishwa na utawala mbaya wa wanadamu yatakwisha.
Yeremia na Ezra wanataja pia kuhusu Farao Shishaki aliyeivamia Yuda, wakitaja kihususa kwamba uvamizi huo ulitukia “katika mwaka wa tano wa Mfalme Rehoboamu [wa Yuda],” au 993 K.W.K. (1 Wafalme 14:25-28; 2 Mambo ya Nyakati 12:1-12) Kwa muda mrefu sana, habari pekee iliyopatikana kuhusu uvamizi huo ilikuwa ile ya Biblia. Kisha mchoro ukapatikana katika ukuta wa hekalu la Karnak (Thebesi ya kale) huko Misri.
Mchoro huo unamwonyesha Shishaki akiwa amesimama mbele ya mungu Amoni, mkono wa Shishaki ukiwa umeinuliwa akiwachinja mateka. Pia majina ya miji ya Israeli iliyoshindwa imeandikwa katika mchoro huo, na mengi ya miji hiyo inahusianishwa na maeneo yanayotajwa katika Biblia. Zaidi ya hilo, maandishi hayo yanataja “Shamba la Abramu”—na hayo ndiyo maandishi ya kale zaidi ya Misri kumtaja mzee wa ukoo Abrahamu anayetajwa katika Biblia.—Mwanzo 25:7-10.
MELKIZEDEKI alikuwa mfalme wa Salemu ya kale na “kuhani wa Mungu Aliye juu sana,” Yehova. (Mwanzo 14:18, 22) Yeye ndiye kuhani wa kwanza anayetajwa katika Maandiko; Akiwa mfalme wa Salemu, jina limaanishalo “Amani,” Melkizedeki atambulishwa na mtume Paulo kuwa “Mfalme wa Amani” na, kwa msingi wa jina lake, anatajwa kuwa “Mfalme wa Uadilifu.” (Waebrania 7:1, 2) Salemu ya kale yaonwa kuwa ndiyo chanzo cha jiji lililotokea baadaye la Yerusalemu, na jina lake likaja kuwa sehemu ya jina la jiji hilo la Yerusalemu, ambalo mara nyingine huitwa “Salemu.Zaburi 76:2.