Nakumbuka hata neno ukimwi likitajwa ,moyo wako unaenda mbio sana maana ilionekana ni mtoa roho. Hata kuna jamaa walikuwa wakikonda ghafla kidogo walikuwa wakihusishwa kuwa na ngoma.
Yani ilikuwa ukipata hili dude haukai sana, hata familia yako inakataa kukuhudumia wakidhani hata kukugusa tu na wao wanaupata.
Watu wengi walikuwa wanasema ukimwi umeletwa na Mungu kwa sababu ya hasira yake juu yetu ndio maana hauna tiba.
Ulifyeka watu kwa kasi sana kupelekea karibia kila nyumba kuwa na mwanajamii, jirani, ndugu, etc anaeumwa ukimwi. Duh ilikuwa tishio, watoto waliachwa yatima wengi sana kupelekea ongezeko kubwa la watoto wa mtaani in early 2010s.
View attachment 3219864
View attachment 3219865