Miaka ya 90 pale uwanja wa ndege mzee Mwinyi aliwahi kunipa hela, fulana kwa mkono wake mwenyewe kisha akanambia maneno haya...

Miaka ya 90 pale uwanja wa ndege mzee Mwinyi aliwahi kunipa hela, fulana kwa mkono wake mwenyewe kisha akanambia maneno haya...

1992 alinibeba na kunipa dhawadi alipokuja kufungua Kijitonyama nursery school baada ya kusoma shairi kwa weredi na udogo ule niliokuwa nao. Alinitabiria mazuri nitakapokuwa mkubwa na 90% yametimia.
Huyu mzee hakuwa mpenda makuu, hakuwa mpenda sifa na majigambo, hakupenda au kulazimisha media ziandike mazuri yake kama wenzake. Aliishi katika wema wake, na sisi tunaomfahamu vizuri aliishi katika mioyo yetu. Ndio maana wale ambao hawakufanikiwa kuwepo katika enzi zake wengi hawayafahamu mazuri yake aliofanya kwa taifa lake, na wananchi wake.
Roho yake ipumzike mahali pema
Amiin 🤲
 
Back
Top Bottom