Miaka ya zamani kumiliki T.V ilikuwa ni ufahari

Miaka ya zamani kumiliki T.V ilikuwa ni ufahari

Moto wa volcano

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2018
Posts
1,148
Reaction score
2,815
Hii Dunia imetoka mbali miaka ya nyuma ilikuwa mtu ukimiliki Television mtaa mzima unaheshimika kuna watu hadi walioa kwa sababu ya kumiliki TV na wengine walikuwa wanapata shikamoo kila kona mtaani sababu ya kumiliki TV , ikitokea nyumba inawaka moto mtu alikuwa yupo tayari kumbukumbu zake za picha na nyaraka zake muhimu ziteketee lakini aanze kuikoa TV sasahivi hadi teja anamiliki runinga yake
 
mambo yamebadilika sana.
ila kwa sasa tupo speed kweli kuna wenye pesa hapa bongo wanaweka oda bidhaa ya itakayo achiwa miezi sita ijayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu TV zenyewe zilikuwa inchi 14 sijui macho yalikuwa hayaumii..!!
 
Daah! Sitasahau nilivyopigwa konzi la kichwa na mmja wawatoto wa mmiliki Tv
Siyo siri sikua na hela na ukiangalia picha lilikua kali sana, basi generater lao lilikua linakawaida ya kuzima
Basi lilipozima nikatumia fulsa ile kuingia
Ebhana lilipowaka jamaa akapitisha msako akaniona alinifuata na kunishushia bonge la konzi, nashukuru watu walikua buzy wanaangalia Video hivyo hawakucheka.Daah narudia tena shambo popote ulipo Mungu anakulaani
Ona sasa matv yenyewe yamezagaa kila kona yamekua kama uchafu na hata lile tv lenu lishapitwa na wakati na chogo lake lile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza kabisa ilikuwa kumiliki watoto wengi ndio ufahari ikaja wake wengi ikaja kumiliki baiskeli ikaja Tv ikaja simu ikaja computer desk top ikaja laptop mpk sasa imefikia kumiliki demu mkali,kila zama na nyakati zake
 
Kwanza kabisa ilikuwa kumiliki watoto wengi ndio ufahari ikaja wake wengi ikaja kumiliki baiskeli ikaja Tv ikaja simu ikaja computer desk top ikaja laptop mpk sasa imefikia kumiliki demu mkali,kila zama na nyakati zake
haha mkuu hiyo yakumiliki demu mkali ipo na ilikuepo tangu enzi za samson akamili demu mkali delila
 
Back
Top Bottom