Miaka yangu 6 Jf

Miaka yangu 6 Jf

Hahahaha safi Sana ,uko vzr bibie
Bruno kims nadhani aliwahi kukamatwa kwa kosa la kukashifu polisi

Niliacha FB Ccm walivyotoka Dodoma kuchaguana
Hahaa mimi 2014 ndio nimeacha, nawakumbuka baadhi ya memba akina Kimeta wa Mpui, Bruno Kims, mheshimiwa Bananga, akina Ben daah magroup yalikuwa hot yale
 
Hahahaha, nilichanga km Rafiki tu ,sikua na chama na sikua mchangia Mada za siasa zaidi ya kuzisoma tu

Ingawa washikaji wengi walikua watu wa siasa
Haha mlichangia wote au CCM tu? Mimi nnapojoin alikuwa ndio katoka kuoa
 
Habari zenu wakuu,
Leo nimetimiza miaka sita tangu nimejiunga na huu mtandao wetu pendwa (yaani nilijiunga nikiwa kijana mpaka nimekuwa mzee hahaa). Nampongeza sana mwanzilishi wa JamiiForums kwa kuanzisha hii platform maana ni ya kipekee na ina ladha ya peke yake.
Kusema kweli nimejifunza mengi sana kupitia mada za hapa na zimenisaidia sana katika kubadili mtazamo kuhusu maisha achilia burudani zisizokwisha aisee kweli hii ni stress free zone.
Hum ndani kuna kila kitu, kuna wakati utafurahi, utajifunza,utapenda, utapendwa, utahuzunika, utaumia, yote tumeumbiwa wanadamu cha muhimu ni kusonga mbele huku ukimtegemea Mungu na kuzichukua changamoto kama sehemu ya maisha.
Cha mwisho ninashukuru miaka yangu yote hii sijawahi kula ban [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Hili nalo la kujivunia eti, si kwamba mimi ni mwema sana kuzidi akina fulani wanaokula ban kila baada ya siku mbili ( siwataji [emoji87]), ni neema tu.
Nawapenda nyoote hata msionipenda naomba niwatakie heri ya Christmas na mwaka mpya.

NB
Kwa mtu yeyote niliyewahi kumkwaza katika kipindi nilichokuwepo Jf naomba anisamehe hata akinifungukia hapa sehemu niliyomkwaza au ambayo huwa namkera. Mimi wengi nimewasamehe bado wachache tu [emoji87][emoji87][emoji87]
Mhenga
 
Back
Top Bottom