Poleni, siku mkipata hamu ya kula kitimoto safi mnitaarifu mapemaa niwapikie ndani ya dakika 45 unakula msosi wako ukiwa wa motooo.
1. Nyama ya kitimoto uje nayo mbichi, viungo nnavyo ntaipika mwenyewe vile unataka ipikwe.
2. Uje na vinywaji vyako na utajihudumia mwenyewe maana mie ntakiwa busy jikoni napika.
3. Kwa wakati mmoja msizidi watu 4 maana sehemu za kukaa na meza ya chakula ni ya watu 5 tuu.
4. Huduma ya mziki au kuangalia mpira au kusoma vitabu itapatikana
5. Location, mbagala maji matitu.
6. Nyama isiwe chini ya kg 3, hata kama mtu atakuja pekeyake. Dhambi sana kuwasha kuni kwa ajili ya nusu kilo au kilo 2
7. Huduma haina malipo yeyote zaidi ya ustaarabu wa kutokuvunja glasi zangu, kutokuvunja sahani zangu, kutojikojolea na kutokumwagamwaga vinywaji sakafuni.