Michael B Jordan na Taraj P Henson wanauhusiano gani na kiswahili?

Michael B Jordan na Taraj P Henson wanauhusiano gani na kiswahili?

Kuna watu wanaitwa malaika hawana uhusiano wowote na Tanzania ni majina tu wanayapenda. Wengine hupenda kutumia majina ya nchi au miji. Kuna Paris. Na wengine wanaitwa Kenya.kama Maria Carey mtoto wake mmoja anaitwa Moroccan na Alicia keys mtoto wake mmoja anaitwa Egypt.
 
Umeona eee,kuna taraji na kuna yule sijui nani nimemsahau jina kwenye how did i get married yupo ana mdomo sana hata kwenye empire yupo ndo dadake taraj,kwenye desperate house wives yupo yaani ni kivuruge jamani,hawa mentor na don c wasitutoea kwenye mstari wale ni ndugu zetu kabisa
Bila shaka unamaanisha WHY Did I Get Married... na kama usingeitaja Desparate Housewives, ningesema huyo kivuruge chamdomo bila shaka atakuwa Tasha Smith!
Tasha.png

 
Majina ya nyota hawa wawili wa hollywood yananifanya niwaze kwa sauti kutokana na kuwa na uhusiano na lugha ya kiswahili

Michael B Jordan ambae jina lake limekuwa likifananishwa na mcheza basketball maarufu Michael Jordan, amefunguka akisema kuwa jina lake yeye ni Michael B Jordan, herufi B ikiwa inasimama badala ya jina la kiswahili Bakari likiwa na maana ya 'noble promise'

Anasema " B stands for Bakari, it's Swahili and it means noble promise"

Tuje kwa Taraj P Henson ambae jina lake kamili ni Taraj Penda Henson.

wikipedia inaandika kuwa "Her First and middle names are of swahili origin, Taraj means 'hope' and Penda means 'love' "
'_
Nawazaje kwa sauti?
Ni kuwa huenda watu hawa wazazi wao au bibi zao walihamia America kutokea East Africa(hasa Tanzania) na wakabadilisha identity zao na kuwa za huko maana majina yao ya kiswahili yananikanganya, tena Michael B Jordan ana Dada aitwae Jamila ( jina limekaa kiswahili kabisa), dictionary.com inafafanua jina Jamila kuwa " a female given name from a Swahili word meaning 'beautiful'

Kiukweli hawa Waamerika wenye majina ya kiswahili wamenikanganya kunifanya Niquestion originality identity zao.
Waamerika weusi wanapenda sana kujiita majina ya kiswahili. Kule California kunafanyika sherehe za kwanzaa festival kila December. Na hayo majina yao ya kiswahili huyapata kwa kutumia Google search, mfano unakwenda Google halafu unaandika swahili names boom walaa.
Kuna siku nilipokuwa kule USA nilikutana na mdada mmoja yupo light skin(mix) jina lake anaitwa Malay...a. na kweli ameemdana na jina lake wala halikumtupa😀😀
 
Back
Top Bottom