Michael B Jordan na Taraj P Henson wanauhusiano gani na kiswahili?

Michael B Jordan na Taraj P Henson wanauhusiano gani na kiswahili?

Umeona eee,kuna taraji na kuna yule sijui nani nimemsahau jina kwenye how did i get married yupo ana mdomo sana hata kwenye empire yupo ndo dadake taraj,kwenye desperate house wives yupo yaani ni kivuruge jamani,hawa mentor na don c wasitutoea kwenye mstari wale ni ndugu zetu kabisa
Gabrielle union
 
Ni muda mrefu hawa wenzetu wanahusisha kiswahili na uafrica.

Na kuna ile sikukuu yao wanaiita "Kwanzaa"....wakimaanisha ni sikukuu ya asili ya ki africa ndio maana wameipa jina la kiswahili....na ina nguzo zake saba na zote zipo kwa kiswahili, Umoja, Kujichagulia,Ujima, Ujamaa, Nia, Kuumba na Imani.


Yeah Kiswahili ni lugha kubwa tofauti na lugha za nchi nyingine, nchi nyingi wanatumia lugha za wakoloni wao au lugha za kikabila na lugha ndogo ndogo zisizojulikana na watu wengi, lakini sisi- tujivunie kiswahili chetu jamani
 
Joseph Zitto
Ni director wa movies Hollywood,
Aliwahi kudirect movies za Chuck Norris iitwayo "missing in action"

Ni mzungu huyo jamaa
 
Taraj wakati mama yake ana mimba yake alikuja Zanzibar kiutalii na akampata rafiki Mzanzibari..Akamwambia kwa upendo ulionionesha,natarajia kupata upendo mkubwa kutoka kwa mwanangu nitakayemzaa..ndo Chanzo cha jina la Taraj..na kiufupi Taraji anaitwa Tarajia Pendo/a Henson
 
Ila Taraj atakuwa mswahili tu tena mswahili pasee si kwa mdomo ule
kuna siku nilimsikia alisema jina la Penda yes ni swahil origin ila uzao wao umetokea Mauritious,
 
Taraj wakati mama yake ana mimba yake alikuja Zanzibar kiutalii na akampata rafiki Mzanzibari..Akamwambia kwa upendo ulionionesha,natarajia kupata upendo mkubwa kutoka kwa mwanangu nitakayemzaa..ndo Chanzo cha jina la Taraj..na kiufupi Taraji anaitwa Tarajia Pendo/a Henson
.
Screenshot_2018-06-03-01-02-55.jpg
 
Wa marekani weusi kama inavyojulikana wana historia ndefu sana ya sintofahamu ya asili yao kwa hapa Africa hivyo kufikia miaka ya 50 wakaanza kutafuta asili zao

Vipindi kama FINDING MY ROOTS vilianza kutengenezwa baada ya kugundulika vipimo vya vinasaba DNA na kupata umaarufu sana

Prof. Maulana Ndabezitha Karenga (born Ron Karenga) alikuwa ni mweusi msomi aliyesomea lugha na utamaduni wa africa katika kiswahili na kiarab, yeye aliamua kuchagua kiswahili kama identity na signature ya watu weusi ndani ya marekani

Wazo lake hili lilipelekea kuanzisha sikukuu aliyoipa jina KWANZAA kutoka katika kiswahili na yeye mwenyewe kujibadilisha jina lake kuja katika kiswahili na jambo hili lilifanikiwa sana miaka ya 60 mpaka kufikia 80

Hivyo wamerekani weusi wakawa tayari wamepata identity na hii ikapelekea kuanza kukiona kiswahili na utamaduni wake kama ndio asili yao na kuanza kutumia majina yake kama mnavyoona hao waigizaji mbalimbali

Ndio matumizi ya kiswahili kwa kipindi hicho yalikuwa makubwa sana hata Michael Jackson katika nyimbo yake ya Liberian Girl anataja maneno ya kiswahili "Nakupenda pia nakutaka pia" akiamini Africa yote kwa ujumla identity yetu ni kiswahili

Ingawa kwa miaka ya hivi karibuni harakati za kutaka utambulisho zimepotea na zinapuuzwa na zinaonekana zimepitwa na wakati

Lakini Kiswahili bado kitabaki kuwa kama ndio utambulisho wa wamerekani weusi kuonyesha asili yao ndio maana hata katika Comic books za Black Panther WAKANDA TERRITORY katika ramani inaonyesha ipo East Africa maeneo ya Tz na Kenya ambapo kiswahili ndio lugha yake
 
Kuna Msanii mwingine wa Kimarekani origin yake ni Kenya Anaitwa Fundisha mcheck kwenye video hizo chini huyo mwanadada kwenye chorus na jina lake ni la Kiswahili kabisa Fundisha Johnson.

 
Back
Top Bottom