MUIGIZAJI aliyejipatia umaarufu
katika tamthilia ya 'Prison Break'
Wentworth Miller maarufu kwa jina
la 'Michael Scolfield' ameamua
kujitangaza rasmi kuwa yeye ni
shoga.
Muigizaji huyo ameamua kuweka
wazi kitendo hicho baada ya
kupokea barua ya mwaliko wa
kuhudhuria tamasha la filamu la
kimataifa lililotarajiwa kufanyika St.
Petersburg nchini Urusi
Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa
kupitia mtandao wa 'People.com'
imeweka wazi kuwa Scolfield
amekataa mwaliko huyo wa
kuitembelea nchi hiyo kutokana na
sheria zao zinazowabana wanaume
wanaojihusisha na ushoga.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa baada ya
muigizaji huyo kuipokea barua hiyo
ya mwaliko ndipo alipoamua
kuijibu kwa kuweka wazi kuwa
kitendo cha nchi hiyo kuweka
sheria ya kuwabana mashoga ndio
sababu kubwa inayompelekea
kushindwa kuhudhuria tamasha
hilo.
"Nashukuru kwa mwaliko wenu,
mimi nina asili kiasi ya Urusi
ingenipa faraja sana kuitembelea
nchi hiyo, lakini kutokana na sheria
zenu mimi nikiwa kama shoga
lazima niukatae mualiko huo"
aliandika Scolfield na kuongezea
kuwa."Ninaumiwa kwa kiasi kikubwa
na jinsi mashoga wanavyotendewa
na serikali hiyo".
Scolfield alieleza kuwa kutokana na
sheria hiyo na jinsi serikali ya nchi
hiyo inavyowachukulia mashoga
hao hawezi kushiriki kwa amani
kwenye tukio hilo lililoandaliwa na
nchi inayowanyanyasa watu kama
wao ikiwa pamoja na kuwanyima
haki yao ya msingi ya kusihi.
Mwezi June nchi hiyo ilianzisha
sheria dhidi ya ushoga iliyosainiwa
na rais wa nchi hiyo Vladimir Putin
ambayo imezua mijadala ya wazi
jinsi sheria hiyo inavyokataza
wapenzi wa jinsia moja.
Wentworth ni muigizaji aliyejipatia
umaarufu kwenye tamthilia ya
Prison Break mnamo mwaka 2005
hadi 2009, ingawa ameweza
kushiriki pamoja na kuandaa filamu
nyingine tofauti tofauti ikiwemo
'Stoker'.
Source. Bongoclants.