Michango kuwanusuru viongozi: CHADEMA imekubali hatia?

Michango kuwanusuru viongozi: CHADEMA imekubali hatia?

Hili jambo linafikirisha.

Nimefuatilia mwenendo wa kesi ya mauaji ya Akwilina tangu mwanzo mpaka hukumu yake iliyotolewa leo katika Mahakama ya Kisutu, Dar.

Kukubali kulipa faini bila kukata rufaa, ni kwamba viongozi na wafuasi wa CHADEMA wamekubaliana na hukumu kwamba wanayo hatia ya kusababisha kifo cha Akwilina?

Je, ingeamuliwa wafungwe jela wasingekata rufaa? Au pesa imeonekana ni rahisi kupatikana kuliko jaribio la kutokukubaliana na hatia? Hawajali rekodi itakuwaje?

Ni jambo jema kuchangisha umma na kuomba wanachama na wananchi wenye huruma kuwanusuru, lakini inafikirisha sana.

Kwa mwenendo huu, mahakama si inaweza kuanza kutumika kama chanzo kipya cha mapato?

Kwangu hili suala limekaa kibinafsi sana!
Nafikiri kesi hukuielewa mauaji halikua shm ya mashitaka wamehukumiwa kwa uchochez na sio mauaji
 
Toeni tena a/c ya michango tuwachangie majeruhi waliopo hospital wapate nguvu haraka kama kuwatoka kwa pesa mingi iliwezakana hatuwezi shindwa za hospital karibuni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzi wa kikuda kwenye afya ya binadamu tena kinamama waliodhumiwa, kwa kufanyiwa ukatili wa ajabu na wanaume makamanda wa Jeshi!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom