Michango ya harusi ni mzigo kuliko Ada ya shule

Michango ya harusi ni mzigo kuliko Ada ya shule

Nikuulize mkuu

Hizo kadi kumi hao wote walikuchangia na wewe ktk harusi yako?au jambo lolote ktk circle ya maisha yako lenye thamani ya kuwapa kila mmoja 100K even nusu ya hiyo pesa?kama hapana then achana nao.

Mimi mapema kabisa mtu akija na haya mambo ya kuchangiana harusi simung'unyi maneno namwambia kama hujawahi kutia hata cent tano ktk mzunguko wa maisha yangu then tuendelee kusalimiana kwa mbali kwanini mtu akutie hasara zisizokuhusu?
 
Nina kama 4 years hivi sijawahi guswa na hii michango sababu nilitimuliwaga kazi na kila mtu akala kona na hadi leo wanajua nimefulia kumbe nilishainuliwa tena kitaaambo na siwahitaji tena. Wakati kipindi nipo job michango ilikua bandika bandua hadi wanaku-group kama ndugu ili wakukamue vizuri
 
Changamoto kweli,mimi nilioa miaka kumi na sita iliyopita tena ndoa ya bomani tulikuwa mimi,mke wangu,rafiki wa mke wangu,rafiki yangu (mashahidi) na mpiga picha Jumla tulikuwa 5 baada ya hapo tutafuta sehemu tukala bia zetu na nyama jioni rafiki akatupa lift katupitisha kwangu,maisha yakaendelea hadi wa leo tunaishi kwa furaha with five kids.Tulitumia pesa chini ya laki 5,make hata pete hatukununua.Simple like that.

Ila nashangaa michango michango inakaribia kutumaliza.Mimi siku hizi ukiniletea kadi ya mchango nakuahidi mpk unaoa mchango sikupi.
Vijana mnatuuua jamani
No mkuu unakosea,usichukue kadi ya mtu kama unajua hutompa hela mara mia ukamwambia ukweli utamsaidia sana kujua afanyenye.
 
Nikiangalia kadi nilizonazo zinazodai michango Ni Kama kumi. Kiwango Cha chini Ni laki mojà. Hivyo nahitaji milioni Moja mpàka end of May kukidhi michango hiyo.

Sawa ni hitaji la kijamii, lakini ni changamoto! Lazima michango iwepo ila, Swali langu kuu Ni Hili:

Je tunawezaje kufanya harusi zetu bila michango mikubwa au harusi bila michango?
Dini ya haki haina harusi za michango kma ivo
 
Nikiangalia kadi nilizonazo zinazodai michango Ni Kama kumi. Kiwango Cha chini Ni laki mojà. Hivyo nahitaji milioni Moja mpàka end of May kukidhi michango hiyo.

Sawa ni hitaji la kijamii, lakini ni changamoto! Lazima michango iwepo ila, Swali langu kuu Ni Hili:

Je tunawezaje kufanya harusi zetu bila michango mikubwa au harusi bila michango?
Yani hii imekuwa kero sana mtu akuganda sana utafikiri kuoa ni suala la emergency [emoji22]
 
Michango ya harusi sio mzigo umaskini wako ndio mzigo wewe mleta mada

Pambana na umaskini wako utoke mleta mada .Umaskini ukikutoka hutaona michango ya harusi mzigo lofa mkubwa wewe pamoja na malofa wenzie walio like mada yako na kukuunga mkono

Mo Dewjiau Bakheresa hata apeleke kasi za michango laki moja haimpi shida kuchangia

Ulofa unakusumbua
 
Nikiangalia kadi nilizonazo zinazodai michango Ni Kama kumi. Kiwango Cha chini Ni laki mojà. Hivyo nahitaji milioni Moja mpàka end of May kukidhi michango hiyo.

Sawa ni hitaji la kijamii, lakini ni changamoto! Lazima michango iwepo ila, Swali langu kuu Ni Hili:

Je tunawezaje kufanya harusi zetu bila michango mikubwa au harusi bila michango?
Mwombe Mungu akuondolee umaskini
Kifupi Tatizo sio michango una umaskini wa kufa mtu
 
Nikiangalia kadi nilizonazo zinazodai michango Ni Kama kumi. Kiwango Cha chini Ni laki mojà. Hivyo nahitaji milioni Moja mpàka end of May kukidhi michango hiyo.

Sawa ni hitaji la kijamii, lakini ni changamoto! Lazima michango iwepo ila, Swali langu kuu Ni Hili:

Je tunawezaje kufanya harusi zetu bila michango mikubwa au harusi bila michango?
Nani kakupangia hicho “kiwango cha chini”?

Sio lazima uchangie kila kadi. Wengine unaweza kuwapa twenty tu ukawaambia itawasaidia kuchangia hela ya zawadi then ukaendelea na maisha yako

Hizi stress nyingine tunajipa wenyewe bila shuruti
 
Nikiangalia kadi nilizonazo zinazodai michango Ni Kama kumi. Kiwango Cha chini Ni laki mojà. Hivyo nahitaji milioni Moja mpàka end of May kukidhi michango hiyo.

Sawa ni hitaji la kijamii, lakini ni changamoto! Lazima michango iwepo ila, Swali langu kuu Ni Hili:

Je tunawezaje kufanya harusi zetu bila michango mikubwa au harusi bila michango?
Pole, Ada ni lazima, michango ni jambo la uhiari. Hata hivyo, fanya kwa kadiri ya uwezo na si vinginevyo! Jitahidi kupangilia mambo tu na vyote vitaenda vema.
 
Mo Dewjiau Bakheresa hata apeleke kasi za michango laki moja haimpi shida kuchangia

Don't be fooled... Michango ni mtazamo tu wa mtu,, kuna watu sio masikini na bado hawatoi michango...
 
Hakuna kitu kibaya kama umaskini uogope kama ukoma vikao vya harusi vya matajiri wala hata hawapangiani viwango

Wanauliza bajeti shilingi ngapi ? anaibuka mmoja tu anaandika cheque ya bajeti yote anasema pelekeni kadi bure kwa ndugu na marafiki waje hakuna mchango ila zawadi kuja nazo ruksa ruksa

Umaskini ndio Tatizo usipochangia kiharusi cha mtu anaapa kutokuchangia chochote cha shida au kufika hata msiba wa familia yenu kisa wewe lofa hukumchangia kaharusi kake au nduguye kanakomhusu!!!

Umaskini mbaya sana
 
Gharama za maisha zimepanda si busara tena kufanya harusi za gharama kubwa kwa kutegemea michango ya watu. Bajeti za harusi zipunguzwe kutosha kula na kunywa kwa wanafamilia tu ya wanandoa
 
Back
Top Bottom