Michango ya harusi ni mzigo kuliko Ada ya shule

Michango ya harusi ni mzigo kuliko Ada ya shule

Nikiangalia kadi nilizonazo zinazodai michango Ni Kama kumi. Kiwango Cha chini Ni laki mojà. Hivyo nahitaji milioni Moja mpàka end of May kukidhi michango hiyo.

Sawa ni hitaji la kijamii, lakini ni changamoto! Lazima michango iwepo ila, Swali langu kuu Ni Hili:

Je tunawezaje kufanya harusi zetu bila michango mikubwa au harusi bila michango?

Kimsingi kiwango elekezi kinawahusu wale wanaohusika moja kwa moja kwenye Harusi na wanaonekana kuwa na uwezo. Sina hakika kwa harusi zote hizo wewe unahusika moja kwa moja?
Lakini pia watu hutoa udhuru kuwa tayari wana harusi nyingine ili wasiwekwe kwenye kundi lenye kiwango elekezi....
 
Kama uliwang'ang'ania kipindi umeoa (kama tayari umeoa), basi huna jinsi. La! Vunga. Na wewe kama hujaoa siku ukioa hakuna kuchangisha watu unapiga kimya. Waweke wazi huna kawaida ya kuchanga
Mimi washkaji zangu wananijua sichangii mtu. Sherehe ya mdogo wangu mwenyewe nilichanga elfu 50. We umeona wapi sherehe 3, zote za nini? Tena kila sherehe laki 1. Pumbafu!
 
Nikiangalia kadi nilizonazo zinazodai michango Ni Kama kumi. Kiwango Cha chini Ni laki mojà. Hivyo nahitaji milioni Moja mpàka end of May kukidhi michango hiyo.

Sawa ni hitaji la kijamii, lakini ni changamoto! Lazima michango iwepo ila, Swali langu kuu Ni Hili:

Je tunawezaje kufanya harusi zetu bila michango mikubwa au harusi bila michango?
Mkuu kama ulifanya shughuli yako ukachangiwa yakupa nawe kuchangia tu
 
Nikuulize mkuu

Hizo kadi kumi hao wote walikuchangia na wewe ktk harusi yako?au jambo lolote ktk circle ya maisha yako lenye thamani ya kuwapa kila mmoja 100K even nusu ya hiyo pesa?kama hapana then achana nao.

Mimi mapema kabisa mtu akija na haya mambo ya kuchangiana harusi simung'unyi maneno namwambia kama hujawahi kutia hata cent tano ktk mzunguko wa maisha yangu then tuendelee kusalimiana kwa mbali kwanini mtu akutie hasara zisizokuhusu?
Kuna jamaa nilimchangia laki na ni kama alichangiwa km 21milioni make tulikuwa tunaona kwa group tena ndoa yenyewe ilikuwa ya kupasha kiporo kwani walikuwa na watoto 4.Sasa sisi wala pombe ambao tunaendaga harusini tumeishakula makwetu tukajua pombe zitatuua,pyuuuu!!!Tulikuta meza zimejaa nyuki na maji,Ile ndoa sitaisahau bahati nzuri pale ukumbini kulikuwa na bar kwa nje ikabidi tujiongeze kupiga gambe kwa pesa zetu hata muda wa zawadi unafika hakuna aliekuwa na habari
Nyingine nilimchangia 50000 akafanya harusi ila kadi hakunipa,baada ya mambo kuisha nikamwaacha km miezi kwani roho ilikuwa inaumaa jinsi alivokuwa anadai michango;Nikampa hongera,halafu nikamuuliza wangu kulikoni hata kadi hukunitumia akasema samahani mambo yalikuwa mengi mpk wengine tulisahau kuwapa kadi, nilihuzunika sana.Na hawa jamaa ndo wamechangia niwe na roho mbaya.Sitegemei tena kuchangia Kwan ht kipindi naoa hawakuwepo au hata kuzaliwa na sikuombaga mchango wa mtu
 
No mkuu unakosea,usichukue kadi ya mtu kama unajua hutompa hela mara mia ukamwambia ukweli utamsaidia sana kujua afanyenye.
Ndugu kadi unalazimishwa na husipochukua ndo mambo yanaanza kuwa magumu anakukasilikia,majungu nk. Ni heri umpe moyo chukua kadi kadri siku zivosogea unakuwa unampoza kwa maneno matupu upo unapambana mwisho wa siku unamwambia hali imekuwa tete au ikishindikana nawe unampelekea kashida kako humo katkat aidha akukope hela kidogo ulipe karo ya mtoto,akikupa unaitunza harusi ikikaribia unamrudishia na kumshukuru na kumwambia bado unapambana.,akikunyima ndo vile tena ngoja droo hatorudi kwako tena.
Hamna namna,mimi nawependa wale wanaokuuliza;naomba nikuadd kwa group la harusi yangu,unamwambia usini-add ngoja napambania mwenyewe nje ya box,ndo imetoka vile
Hutakataaje kadi wakati anaileta tayari imeandikwa jina lako
 
Unapangaje harusi huna pesa? Harusi za matajiri pia hakuna michango n kadi za bure tu. Hakuna kitu kibaya kama umaskini wa Bwana harusi
Hakuna kitu kibaya kama umaskini uogope kama ukoma vikao vya harusi vya matajiri wala hata hawapangiani viwango

Wanauliza bajeti shilingi ngapi ? anaibuka mmoja tu anaandika cheque ya bajeti yote anasema pelekeni kadi bure kwa ndugu na marafiki waje hakuna mchango ila zawadi kuja nazo ruksa ruksa

Umaskini ndio Tatizo usipochangia kiharusi cha mtu anaapa kutokuchangia chochote cha shida au kufika hata msiba wa familia yenu kisa wewe lofa hukumchangia kaharusi kake au nduguye kanakomhusu!!!

Umaskini mbaya sana
 
Kimsingi kiwango elekezi kinawahusu wale wanaohusika moja kwa moja kwenye Harusi na wanaonekana kuwa na uwezo. Sina hakika kwa harusi zote hizo wewe unahusika moja kwa moja?
Lakini pia watu hutoa udhuru kuwa tayari wana harusi nyingine ili wasiwekwe kwenye kundi lenye kiwango elekezi....
All are close friends. Si unajua kuna "significant others"..... Lakini tunawezaje kuacha kchanga hizi hela bila kuua mahusiano? Mtihani huu umekuwa mgumu kwangu!
 
Daaah! Dada kauzu sana wewe
Harusi ninazochanga ni za ndugu zangu wa karibu sana ambao wapo wachache.

Wengine am sorry..macho makavu kabisa sichangi.

Ndio sina hela!
 
Michango ya harusi sio mzigo umaskini wako ndio mzigo wewe mleta mada

Pambana na umaskini wako utoke mleta mada .Umaskini ukikutoka hutaona michango ya harusi mzigo lofa mkubwa wewe pamoja na malofa wenzie walio like mada yako na kukuunga mkono

Mo Dewjiau Bakheresa hata apeleke kasi za michango laki moja haimpi shida kuchangia

Ulofa unakusumbua
sikutegemea matusi kutoka thread hii. It is a pity umeamua kutukana. Let me think my response to you!
 
Kifupi ukiona mtu analalamikia michango ya harusi kuwa ohhh imezidii ujue huyo lofa sana. Full stop
Aende kwa Mwamposya akaombewe apate Pesa
Muulize mama yako atakwambia kama mimi lofa.
 
.
20220317_112359.jpg
 
Nikiangalia kadi nilizonazo zinazodai michango Ni Kama kumi. Kiwango Cha chini Ni laki mojà. Hivyo nahitaji milioni Moja mpàka end of May kukidhi michango hiyo.

Sawa ni hitaji la kijamii, lakini ni changamoto! Lazima michango iwepo ila, Swali langu kuu Ni Hili:

Je tunawezaje kufanya harusi zetu bila michango mikubwa au harusi bila michango?
Huu ujinga upo tz only.
 
Harusi ninazochanga ni za ndugu zangu wa karibu sana ambao wapo wachache.

Wengine am sorry..macho makavu kabisa sichangi.

Ndio sina hela!
Hahhaha mwenza natamani ningekuwa na hii roho yako
 
Back
Top Bottom