Michango ya harusi ni mzigo kuliko Ada ya shule

Michango ya harusi ni mzigo kuliko Ada ya shule

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
44,629
Reaction score
83,056
Nikiangalia kadi nilizonazo zinazodai michango Ni Kama kumi. Kiwango Cha chini Ni laki mojà. Hivyo nahitaji milioni Moja mpàka end of May kukidhi michango hiyo.

Sawa ni hitaji la kijamii, lakini ni changamoto! Lazima michango iwepo ila, Swali langu kuu Ni Hili:

Je tunawezaje kufanya harusi zetu bila michango mikubwa au harusi bila michango?
 
Nikiangalia kadi nilizonazo zinazodai michango Ni Kama kumi. Kiwango Cha chini Ni laki mojà. Hivyo nahitaji milioni Moja mpàka end of May kukidhi michango hiyo.
Sawa ni hitaji la kijamii, lakini ni changamoto! Lazima michango iwepo ila
Swali langu kuu Ni Hili: Je tunawezaje kufanya harusi zetu bila michango mikubwa..... Au harusi bila michango

Kiwango cha chini laki 1? Huku kwetu single 50, double 70…. Mkichanga zenu wawili maisha yanaenda kama kuna ulazima lakini
 
Mwanakamati mchango ni kuanzia laki 1 na kuendelea, hiyo 50 kwa 70 ni kadi za ufadhili

We sherehe zote 10 unakuwa mwanakamati? Inamaana ni watu wa karibu sana so jitahidi tu [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Nikiangalia kadi nilizonazo zinazodai michango Ni Kama kumi. Kiwango Cha chini Ni laki mojà. Hivyo nahitaji milioni Moja mpàka end of May kukidhi michango hiyo.

Sawa ni hitaji la kijamii, lakini ni changamoto! Lazima michango iwepo ila
Swali langu kuu Ni Hili: Je tunawezaje kufanya harusi zetu bila michango mikubwa au harusi bila michango
Changamoto kweli,mimi nilioa miaka kumi na sita iliyopita tena ndoa ya bomani tulikuwa mimi,mke wangu,rafiki wa mke wangu,rafiki yangu (mashahidi) na mpiga picha Jumla tulikuwa 5 baada ya hapo tutafuta sehemu tukala bia zetu na nyama jioni rafiki akatupa lift katupitisha kwangu,maisha yakaendelea hadi wa leo tunaishi kwa furaha with five kids.Tulitumia pesa chini ya laki 5,make hata pete hatukununua.Simple like that.

Ila nashangaa michango michango inakaribia kutumaliza.Mimi siku hizi ukiniletea kadi ya mchango nakuahidi mpk unaoa mchango sikupi.
Vijana mnatuuua jamani
 
Back
Top Bottom