Leo jukwaani natinga, kuwaeleza habari/
Za Jf kabla ya kina Mobimba, Enzi za Cuf ngangari/
Wajuzi mada walichimba, sio story za Diamond na Zari/
Siku hizi mtu anaandika ujinga, anamalizia na UZI TAYARI/
Mshana Jr alifafanua ulozi, mpaka wafia dini wakapiga kelele/
Pia lilikuwepo jukwaa la mamboz, mapicha live tele/
Kiranga hakuamini uokozi, wala hadithi za Mfalme Sele/
Na ukipambana unaambulia nakoz, na kumfuata ka' mfuasi wa Kibwetere/
Wengi mliishia kuwa wasomaji, kwa kuogopa kuchangia/
Siku hizi ndio wajuaji, na story za vibamia/
@maxmelo alipata kesi nyingi, maana serikali ilipigwa za kidevu/
Kuna muda ilibidi yeye aingie kingi, ili sisi tusifanyiwe uonevu/
Hii ni kabla ya magenge, yanayo andika kusifia wapewe mamlaka/
Viongozi Jf iliwakata wenge, mpaka nao wakajiunga kujibu mashtaka/
Wenzetu wengine walipotea, R.I.P Ben Saanane/
Mods siku hizi wamenywea, zamani Ban mpaka utukane/
Wakulungwa wengi wamenyuti, maana watoto wamekamata usukani/
Dakika mbili matusi, na shari kama tuko Talebani/
Sasa ni makundi, Ccm na Chadema soo/
Diamond, na Kiba mtoto wa Kariakoo/
Simba na Yanga wanatoana roho/
Mabitozi na mademu wanapigana K.O/
Wote wamejipanga, hakuna kusanda kwenye hii shughuli/
Demu unaedhani mtoto utabwaga manyanga, utapoona kiuno kina shanga kama tunguri/