Unaingia unyonge, Jf mambo yanayojiri/
Peke yako msaka tonge, wote matajiri/
Hakuna kibonge, wote body zimeshamiri/
Madem ni shombe, na hawawezi kiswahili/
Wenzako wana Diploma, wewe ndio haujasoma/
Wana mijengo Dar Dodoma, wewe huna hata boma/
Ukichangia maada, utaambiwa bange unachoma/
Na ukihitaji msaada, utaitwa Popoma/
Kuna thread za mandinga, hakuna za mtembea kwa miguu/
So hutaonekana mjinga, ukinyanyua mikono juu/
Na kubaki msomaji, uwaachie wenye majina/
Maana nyuzi zako hazina wachangiaji, wanapita kimya kimya/
Andika ya maana, bado utatoka kapa/
Wenzako wamejazana, thread ya waonyesha papa/
Pm ukizama unakutana, na viingereza vya uwongo/
Wakati wenzako wanaelewana, na kupeana nyama ya udongo/
Wenzako wanatesa, ukimgusa Mama watasema bangi/
Utaambiwa tafuta pesa, au Sukuma Gang/
Ila usiache mbachao, wala kuwa mbogo/
Maana humu hata mwanao, atakuita bwana mdogo/
Sent from my SM-G532F using
JamiiForums mobile app