Michano/Hiphop/Freestyle

Michano/Hiphop/Freestyle

👉Lisemwalo lipo Kama halipo laja/
👉Ukitaka mwenda ng'ambo Kwanza Jenga dalaja;/
👉Maranyingi maiti haiamki
kwafaraja/
👉Nakira baada chozi Basi kifwatacho faraja/


👉Polisi na raia skuizi ukatili
👉Sosiri kila sehemu ukatili
👉Uongozi ulo ukataa madarakani umesha jiri
👉Madaraka yanatumika kujiongezea utari

👉Skuizi binti ZAKO Wana vaa vimini
👉Ndoa Zina vunjika waumezao Hawa waamini
👉Baba anavaa kibode mama Ana vaa kimini
👉Tanzania ya Skuizi haki ya mungu huwezi amini

👉Skuizi bungeni zinapigwa
👉Pesa ikohuru haki imefungwa
👉Inchi IPO huru raia wafungwa
👉Wanaya wapo huru raia wafungwa

👉See the life through my eyes
👉Polisi lao moja na jambaazi
👉Wasomi wapowengi Ila hawanakazi
👉Na ukosefu wa ajira ndo chanzo Cha uja mbaazi👊👊👊😂😂
 
Niite Mzee Mpili, maana Jamii Forums nina watu/

Ukinikosa jukwaa hili, nipo uzi wa warembo wanaoshika safu/

Chit chat kwangu sio dili, maana wana mambo machafu/

Habari mchanganyiko siwezi subiri, japo kila muda habari za wafu/

Mauaji yamekithiri, mara moto mara risasi za mapafu/

Kule MAHUSIANO sio shwari, kutwa kuwaponda madem halafu/

Ndio hao hao wanaanzisha habari, Pm kwa watoto wa watu/

Kule SIASA ni mabishano makali, usiwaamini hata washike Msahafu/

Na nimeshaizoea hii hali, JF kila mtu ana Sarafu/
Siku hizi ukiona bila woga, demu kapost eti aolewe/

Ujue kuna Member kayakoroga, ni kitengo na mtego wa mwewe/

Jukwaani imekuwa ni soga, na matusi hayana mwenyewe/

Muda wowote unayaoga, hata kama ulihoji uelewe/

Dini zinafanywa mboga, na hawamuogopi Mungu mwenyewe/

Lete mada za kuroga, na mapenzi Like upewe/

Ukileta Elimu haiwezi noga, lazima ipotezewe /

Rabda ihusu kula boga, na mti wake wenyewe/

Humu kila mtu hajui zongo, hilo halina utata/

Na kila mtu anajua kimombo, na hakuna wa shule ya kata/
 
Leo nawapa kisa cha demu wa Charambe/
Nilikutana nae nikatamani nimrambe/
Mtoto ana shape mweupe yange yange/
Kumtongoza haikuwa tabu ikawa pambe/
After 2 weeks ishu guest Magwepande/
Mtoto line zote Buza na kwa Mpalange/
Baada ya viwili fresh ikabidi nimpange/
Tuagane aende nyumbani asitange tange/
Kutoka akarudi mbio huku akitaja Chande/
Ndio nani? Akasema ni mumewe Afande/
Hivyo tujifungie kisha tusali ama tuwange/
Maana anakuja halafu ni kichwa bange/
Kumbe umeolewa kwa nini usinipange/
Akasema imeisha hiyo yajayo tugange/
Nimeyakanyaga dah! ikabidi tu nisande/
Ghafla nje nikasikia mikwara kabambe/
Funguaaaaaaa' ikasika sauti ya gambe/
Na zikapandikiza chuki sauti za wapambe/
Hii sio saa ya kumuacha bwege atambe/
Kushtuka dah! njozi tu za kula makande/
Ikabidi nilale maana bado kuna umande/
 
Rhymes zangu Al Shababi, napiga kwenye shingo/
Watoto beki hazikabi, wamekimbia ulingo/
Manyota 'inchaji', mi' suka mi' utingo/
Wako wapi wafa maji, niwamalizie na tindo/
Hawataweza kupima, mi nacheza na vina/
Natembeza mboko/
Nawapoteza mazima, wanageza kama China/
Na wanatoa boko/
Mvumbo ni zawadi, kwenye hiki kizazi/
Cha watoto wenye midadi, halafu wali nazi/
Wanakuja wanajinadi, tena shazi/
Ila ninapotema radi, wananiita mkuu wa kazi/
Game dakika tisini, ila life jihadi uelewe/
Maana hata mke wa masikini, kuwadi mumewe/
View attachment 1619670
Mistari bampa to bampa, niliishia kwenye ngumu nyeusi/
Tayari Mvumbo nipo hapa, nachana zaidi ya Msusi/
Hii ni bahari ya mapapa, dagaa hakikisha haugusi/
Na ukileta shanapa, usije ukatuona ni nuksi/
Hatufanyii hii kwa kutumwa/ kusukumwa/
Wala utumwa/ ila tusipo Rap tunaumwa/
Hivyo vina siyo vya kuchanga, ni kisanga ni faya/
Mistari naipanga, zaidi ya shanga kwa Malaya/
 
Mistari bampa to bampa, niliishia kwenye ngumu nyeusi/
Tayari Mvumbo nipo hapa, nachana zaidi ya Msusi/
Hii ni bahari ya mapapa, dagaa hakikisha haugusi/
Na ukileta shanapa, usije ukatuona ni nuksi/
Hatufanyii hii kwa kutumwa/ kusukumwa/
Wala utumwa/ ila tusipo Rap tunaumwa/
Hivyo vina siyo vya kuchanga, ni kisanga ni faya/
Mistari naipanga, zaidi ya shanga kwa Malaya/
Asante mvumbo we Ni mkali wa hizi kazi/
Kitambo tu nakusoma we Ni noma iko wazi/
Leo nakupa tano ile ki nunda Kama Daz/
Oi oi ka saigoni sema hawakusomi vichwa panzi/
Naandika nasikitika jinsi zilla alivoacha pengo/
La freestyle Ila sikuhizi naona yupo kado kitengo/
Acha niishie hapa nimeshea tu mapendo/
Tukutane tena mwakani kwa Leo nimemaliza mwendo....
 
Asante mvumbo we Ni mkali wa hizi kazi/
Kitambo tu nakusoma we Ni noma iko wazi/
Leo nakupa tano ile ki nunda Kama Daz/
Oi oi ka saigoni sema hawakusomi vichwa panzi/
Naandika nasikitika jinsi zilla alivoacha pengo/
La freestyle Ila sikuhizi naona yupo kado kitengo/
Acha niishie hapa nimeshea tu mapendo/
Tukutane tena mwakani kwa Leo nimemaliza mwendo....
RIP Zilla na Albert Mangwea/
Na masela wote mnaaozea Segerea/
Pengo mliloacha kuliziba Kazi/
Leo Tuko na Unju anaongoza Kikosi Kazi/
 
Wanasema Mvumbo chonde/ acha Hip hop ili usonge/ hiyo ni kinyonge/
Madee ilibidi aiponde/ vipi unaendeleza mistari konde?/
Timba kwa vibonde/ imba kama Konde/
Watakuwinda watoto shombe/ kama Simba upate ubalozi wa Pombe/
Muziki unaofanya hauna hata kumi/ unapendwa na jicho nyanya wahuni wahuni/
Mnachofanya ni maneno kubuni buni/
Kisha mnachanganya inakuwa Rap katuni/
Wenzenu wanapanga sauti/ Melody stress hazitupi/
Ukimsikilizisha aliyekupiga kibuti, hakika anakuvulia chupi/
Sio nyinyi kutwa harakati/ mnafoka na burudani hatupati/
Beat zinachapa kama vita/ rabda muwaimbie akina Mwita/
Huku pwani tunataka za Senyorita/ teamo teamo huku mtoto umemshika/
Mnatugombanisha na Mama/ kila kitu nyinyi mnakosoa/
Mistari imejaa malawama/ kizuri mtakitia doa/
Mnajisifu mna mashairi/ Shaaban Robert nae aseme vipi/
Bora fani ughairi/ maana Hip Hop hailipi/
Rabda ulegeze kidogo/ uweke vionjo/ vya Twanga au Msondo/ au sebene za Kongo/
Fuata mkondo/ ukiona uongo/ jiulize yuko wapi Msafiri Kondo/
 
Ona usiku silali mara naona simba/
Akinionyesha majabali na miamba/
Akisema kwa ukali na kujigamba/
Niende kupewa kibali niwe mwanga/
Nisiwe mzembe niende chini ya Mkuyu/
Nikachukue Pembe pamoja na vibuyu/
Baada ya hapo nitakuwa na uwezo/
Babaako angani nasafiri dezo dezo/
Na ambae hatupatani namtupia chezo/
Analala kitandani inabaki maombolezo/
Ukinizidi maendeleo kujifanya una 'vieite'/
Naipiga inakuwa kimeo gereji muda wote/
Eti mnapendana hamsikii ya watu/
Nitakachowafanya punde mbwa na chatu/
Vyote hivi ni visa vya bibi, anataka anikabidhi ndumba/
Vipi nirithi tunguri, wenzangu warithi nyumba/
Eti nile maiti bila kujali, hata kama ana sanda/
Na hilo nisipo kubali, hakika nitavuta kamba/
 
RIP Zilla na Albert Mangwea/
Na masela wote mnaaozea Segerea/
Pengo mliloacha kuliziba Kazi/
Leo Tuko na Unju anaongoza Kikosi Kazi/
[emoji110]
 
Mvumbo nika Comment wapi, ili wasinivunjie heshima/

Maana ukikosea hawakuachi, wanakushukia mazima/

Jf ina wajuzi safi, na wanaojua ya Dunia nzima/

Majukwaa kama samaki, ni tofauti yanakonga mtima/

Kuna ubishi, wa gari za Japan na za Ulaya/

Kuna ubishi, wa kuoa au kufanya umalaya/

Kuna ubishi, anaongoza mama au Jakaya/

Kuna ubishi, Dini ya Maulid na ya Kwaya/

Kuna ubishi, kwenye mpira ile mbaya/

Kuna ubishi, kwenye Siasa usiguse waya/

Kuna ukweli mchungu, na zingine ni nongwa/

Wengine hakuna Mungu, ila wakikwama wanamuomba/

Humu usiwe mbumbumbu, maana poo utaomba/

Haswa ukiandika mizungu, kwa kutumia akili za mjomba/

Mjuaji anapigwa za utosi, kwa fact sio kienyeji/

Anaachwa mweupe kama Nyoshi, na kupotea bila meseji/

Humu maneno hayakosi, na matusi kama Gereji/

Unaweza ukawa Boss, na bado ukaambiwa unaishi kwa shemeji/
 
Naandika freestyle nikiwa nawaza jinsi ntakavyo toboa/ mafanikio siyo zali hustler lazima jasho utatoa

Ukiishi kizembe kutegemea cha wazazi/ Dunia itakupa jembe ulime uchoke pumzi ikutoke mpaka uache mdomo wazi.
 
Niko bar nakata pombe
Niko hoi Kama Masai aliyepoteza ng'ombe
Wana nipeni mic mi na mzuka wa kufoka
Hali mbaya mtaaani hakuna hata duka la kukopa
Serikali ya wanyonge msitaafu alituita sisi malofa
Leo kalala kaburini huku katinga suti na moka
Kweli maisha Ni safari tangu enzi za mwanamoka
 
  • Thanks
Reactions: y-n
wanangu tuikatae gongo,
inazinguwaga ubongo,
sometimes inaleta kibiongo,
wahuni kupigana magongo,
tusikae kama maninja ya congo,
kuoneshana tu migongo
 
Mvumbo nazama booth mkushi moshi napuliza juu/

Naskia madogo ni Bluetooth kwa wasusi wanasukwa vitunguu/

Tukisema wanatuona wazushi kama Luth wanabinua midomo juu/

Ukiwaasa ni matusi na vifurushi hawakosi vya Badoo/
 
Heshima yangu naikamata, maana kelele nyingi/

Wanam diss Dizasta, kisha wanajiita King/

Madogo ni wa kuchapa, hawastahili hii ring/

Tayari Mvumbo nipo hapa, mimi ndiyo mtunza misingi/

Ya huu utamaduni/ dhidi ya Crew za kihuni/

Wanaowekwa juu na Mawinguni/ nikisema suu waje miguuni/

Wanaharibu Culture/ anajaribu Rapcha/ ila hayupo karibu na Dizasta/ hivyo taratibu anapaswa kufyata/

Kusifiwa kuchana, leo madogo wana pretend/

Mkubwa unamtukana, na bado anakuita Best Friend/
 
Weita leta vikali, nitulie niache nishai/
Maana ndonga imejaa mistari, zaidi ya shuka ya Kimasai/
Ndio maana sina habari, watoto wanapojidai/
Wananipandisha morali, nipo ni vipi wanajimwambafai!?/
Hii ndonga/ ninapobonga/ kwao ni skonga/ acha wasome/
Game kwangu kitonga/ nasonga/ wanachonga/ na washafika ngome/
Ona macho pima, nilipo hawawezi timba/
Nacheza na vina, ka' Masai na Simba/
Enzi za michano/ tenzi volcano/ sipotezi mapambano/

M'bobezi kwenye chano/ hawawezi natimiza agano/

Daima cha mtu siyo chako, usidharau hata kama ni buku/

Na nikichanga kwenye harusi yako, punguza maua ongeza kuku/
 
Heshima yangu naikamata, maana kelele nyingi/

Wanam diss Dizasta, kisha wanajiita King/

Madogo ni wa kuchapa, hawastahili hii ring/

Tayari Mvumbo nipo hapa, mimi ndiyo mtunza misingi/

Ya huu utamaduni/ dhidi ya Crew za kihuni/

Wanaowekwa juu na Mawinguni/ nikisema suu waje miguuni/

Wanaharibu Culture/ anajaribu Rapcha/ ila hayupo karibu na Dizasta/ hivyo taratibu anapaswa kufyata/

Kusifiwa kuchana, leo madogo wana pretend/

Mkubwa unamtukana, na bado anakuita Best Friend/
Dogo kaja juzi tu leo analeta dharau/

Analeta utata atazikwa tutamsahau/

Dizasta ana Vina vya kuuwa career ya Cosmas/

Tribulation alimcha kuwa hajui hata BODMAS/

Kuijua Bange et leo anainyea kambi/

Bora afanye udaku aungane na Mange Kimambi/

Nna mengi ya kusema subir nikijipanga/

Kwa sasa niko kweny basi naelekea Shinyanga/
 
Dogo kaja juzi tu leo analeta dharau/

Analeta utata atazikwa tutamsahau/

Dizasta ana Vina vya kuuwa career ya Cosmas/

Tribulation alimcha kuwa hajui hata BODMAS/

Kuijua Bange et leo anainyea kambi/

Bora afanye udaku aungane na Mange Kimambi/

Nna mengi ya kusema subir nikijipanga/

Kwa sasa niko kweny basi naelekea Shinyanga/
Dogo gani unayemsema yule anayependa visa/
Juzikati nilimcheki masaki anagongea pizza/
Facebook anadorola wanamsorora huko Twita/
Hana Tena manzi tangu nilipompora Lisa!
Sahivi anafuga rasta kweli amedata na shisha/
Ana mistari ya kuunga unga halafu anajiona ticha/
Yaan anasikitisha kabla hajatoka ameshakwisha/
Analeta diss za kitoto yaan Bora angetupisha/
Bora afanye mapiano za lojay na monalisa/
Maana kwenye michano siioni yake picha/
Hata arapu kiarabu kilingeni atafichwa/
Ki ukweli anaua vibe na bado anavimba kichwa/
 
Mama kawafungua kamba, Siasa imeshika namba, mikutano kama awali/

Wangapi hawatampamba, ilihali wameramba, buyu la asali/

Yaani mtu akupe pamba, uvae na kuuramba, ni vipi utamnyali/

Ndugu yangu ni kwamba, Wananchi ndio tunaisoma namba, bei ya sukari/

Usiamini mtu kabisa, iamini nafsi yako/

Gizani unaweza tishwa, hata na kivuli chako/

Achana na umama/ kupigana kisa vyama/ haupo wakipanga njama/

Wanatoa malawama/ kuonyesha tumekwama/ baadae wananyonya kwa mama/


Tunapaswa kudai haki, mimi na wewe/
Bila mtu wa kati, lazima unielewe/

Sisi ndio kapu la samaki, na wale wote ni mwewe/

Hakuna anaetaka kubaki, uongozi asipewe/

Na hata wakikosa, ruzuku zao sio zako/

Hivyo unajikosha, kukausha roho yako.
 
Back
Top Bottom