Michele Obama vs Donald Trump Uchaguzi Mkuu wa Marekani

Michele Obama vs Donald Trump Uchaguzi Mkuu wa Marekani

Hicho kionyesha mapaja mnataka ndio kiwe Rais wa America 😄

Yeye na Trump na hicho kyehu Biden wote hawafai kuwa ma Raisi.


Kwa ujumal America wana vote nini ni ujinga tu, kuwasimamisha watu masaa kupiga kura.

Rais anakuwa kisha pangwa na AIPAC, sijui kelele za media sijui Electoral votes au Electoral College hizo ni mchanga kwenye macho tu.


Ukitaka kuwa Rais wa America lazima ukagonoke kule AIPAC 😄
Wachambuzi wa siasa za Marekani wakitokea Tanzania, kazi kweli kweli.
 
Swali.
Ya Rula Da Silva wa Brazil na Mkewe yanaweza tokea Marekani this time?
---

MAREKANI - Michelle Obama, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama, ndiye mgombea pekee kwa tiketi ya demokrati ambaye anaweza kumshinda mgombea wa Republican Donald Trump katika uchaguzi wa Novemba, Reuters imetangaza ikinukuu kurampya za maoni za Ipsos.

Wasiwasi unaoongezeka miongoni mwa wapiga kura wa Kidemokrasia juu ya uwezo wa Rais Joe Biden kupata muhula wa pili madarakani mwaka huu, haswa baada ya mjadala wake na Trump, ambapo kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 81 alionekana kuelemewa hata wakati wa mazungumzo yake.

Mnamo Julai 1 na Julai 2, kampuni ya utafiti wa soko ya Ipsos ilichunguza sampuli wakilishi ya watu wazima 1,070 wa Marekani kwa niaba ya Reuters, wakiwemo wapigakura 892 waliojiandikisha, 348 Democrats, 322 Republicans na 303 wa kujitegemea.

Kulingana na kura za maoni, ikiwa kura ingefanyika sasa, Biden na Trump wote wangeshinda wastani wa asilimia 40 ya kura.

Hata hivyo wapiga kura watatu kati ya watano, ikiwa ni pamoja na karibu theluthi moja ya Wanademokrasia, wanaamini Biden anapaswa kujiondoa kwenye kinyang'anyiro kabisa na kwamba chama chake kinapaswa kuweka mgombea mpya, hata katika hatua hii ya mwisho.

Wengi wa wanaoweza kuchukua nafasi za Biden hawaonekani kuwa na idhini ya umma unaohitajika kumshinda Trump siku ya Novemba 5, kulingana na kura ya maoni.

Katika ulinganisho wa kidhahania dhidi ya Trump, Makamu wa Rais Kamala Harris alikuwa na pointi moja nyuma ya mgombea wa Republican, wakati wengine, kama Gavana wa California Gavin Newsom na Gavana wa Michigan Gretchen Whitmer, walifanya vibaya zaidi.

Mtu pekee ambaye angeweza kumshinda Trump ni Michelle Obama, aliyepata takriban asilimia 50 ya kura za maoni ya wapiga kura, ikilinganishwa na asilimia 39 ambao walisema watampigia kura Trump.

Je haitakuwa njia nyepesi zaidi Kwa Trump?
Wengine wanasema Kamala Harris ndio 👇👇

View: https://twitter.com/TheCitizenTz/status/1808544068659785779?t=wj9tGJX32DQ_i41hH4fo5w&s=19
 
Sasa itakuwaje kwa Bi Kamala Harris, wakati alikuwa akiingojea nafasi hiyo kwa hamu na ghamu?
Na ni bora mtu mweusi asipitishwe kugombea, hawana utu wala huruma kwa nchi za kiafrika/kiarabu, refer Simba wa Afrika marehem gadafi kilichomkuta kwenye utawala wa obama
 
Na ni bora mtu mweusi asipitishwe kugombea, hawana utu wala huruma kwa nchi za kiafrika/kiarabu, refer Simba wa Afrika marehem gadafi kilichomkuta kwenye utawala wa obama
Trump yule ni kenge kabisa, aliichukia sana Afrika akasema ni shithole countries! Kkmk! Mbaguzi sana yule!
 
Huo ni ujamuishaji wa mambo. Utu hauna uhusiano na rangi ya ngozi ya mtu wala mahali atokapo.

Marais wa marekani wanajulikana hawana utu kwa ukatili wao, but mtu mweusi mf obama tulijua Afrika imepata mtu wa kuwatetea na haitakuja kufanyiwa ushenzi+dhulma na mauwaji chini ya obama, na haikua hivyo ndio yale yale ya George W. Bush

Saddam chini ya utawala wa G. Bush
Gaddafi chini ya utawala wa Obama
 
Huo uchaguzi unaovutia hisia zako, then unafaidika na nini?
Mimi siwezi kufanana na wewe hata kama tungekuwa ndugu tusingeweza kufanana kihivyo. Watu hawawezi kufanana bwana kama karatasi za A-4.
 
Na ni bora mtu mweusi asipitishwe kugombea, hawana utu wala huruma kwa nchi za kiafrika/kiarabu, refer Simba wa Afrika marehem gadafi kilichomkuta kwenye utawala wa obama
Gadaffi aliuwawa na Walibya wenzake waliokuwa wamechoka na utawala wake wa kiimla wa zaidi ya miaka 40 na hakuwa simba wa Afrika bali alikuwa ni gaidi tu kama magaidi wengine.
 
Gadaffi aliuwawa na Walibya wenzake waliokuwa wamechoka na utawala wake wa kiimla wa zaidi ya miaka 40 na hakuwa simba wa Afrika bali alikuwa ni gaidi tu kama magaidi wengine.
Watu wengi wanadanganywa na wanasiasa wa Afrika kwamba alikuwa mtu mwema, aliyeeijenga na kuiheshimisha Libya. Ila ukweli Gaddafi alikuwa Gaidi na mhalifu kama wahalifu wengine.
 
Back
Top Bottom