Michezo inaendeleza biashara ya watu na utumwa mambo leo

Joined
Jul 22, 2019
Posts
10
Reaction score
27
Michezo inaendeleza Biashara ya watu
Kwenye michezo sahivi ni pesa kwanza, maana yake biashara, watu wanauzwa na kununuliwa kama bidhaa mithili ya ilivyokuwa kwenye zama za utumwa miaka ile. Timu zinakaa mezani kupitia viongozi wao na kujadili bei ya wachezaji kisha kulipana pesa. Hii ni biashara ya watu.

Mfano: Haaland analipwa dola 900,000 kwa wiki, alinunuliwa kwa zaidi ya pound milioni 60 kutoka Borrussia Dortmud. Maana yake alinunuliwa na kununua ni biashara.

Ni Utumwa Mamboleo
Wachezaji wakisajiliwa wanakaa kambini kwa mujibu wa mipango ya timu, wananyimwa kuonana na familia zao kwa wakati, wanapangiwa chakula, ratiba ya kulala na mazoezi. Ukitoroka kambini ni utovu wa nidhamu.

Mfano: Saido Ntibazonkiza alivyotoroka kambini Shinyanga kuelekea mechi ya nusu fainali ya FA dhidi ya Simba kule Mwanza kilichomkuta mnakumbuka - Alifukuzwa.


Tofauti
na utumwa wa zamani ni watumwa kulipwa vinono.

Ninathubutu kutamka kuwa, michezo sahivi inaendeleza biashara ya watu na utumwa mambo leo.
 
Mzee hata wewe unapotoka ofisi moja kwenda ofisi nyingine ni utumwa pia, unakuwwa umenunuliwa, wewe umeenda kwa FREE TRANSFER 😂🤣
 
Unajua hata ofisinii unapofanya kazi (ulipoajiriwa) ni utumwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…