Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #2,481
Watanzania waaswa kununua filamu halisi
na Andrew Chale, Zanzibar
MKURUGENZI wa Zanzibar International Film Festival (ZIFF), Prof. Martin Mhando, amewataka Watanzania kujitokeza na kununua kazi halisi ili kukuza soko na uchumi wa nchi. Prof. Mhando alitoa wito huo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ndani ya ukumbi wa Ngome Kongwe mjini Zanzibar.
Alisema kuwa tayari wasanii wa Tanzania wamewewza kupiga hatua katika kutoa filamu mbalimbali, ambazo nyingi kati ya hizo zina mafundisho.
"Tumetoka mbali katika tasnia hii ya filamu kwa nchi yetu, hivyo kwa kuwa hii ni ajira rasmi, Watanzania tujitokeze kununua nakala halisi ili kukuza soko letu na filamu ziendelezee kukuza uchumi wa nchi yetu" alisema Prof. Mhando.
Mbali na hilo, pia alishahuri Tanzania kuundwe Kamisheni ya Filamu, ambayo itasaidia kuiletea nchi matunda mazuri, huku bodi ya filamu iliyoundwa ikiendelea kusimamia ushauri na kamati mbalimbali za maadili.
Pia alisema, kwa mwaka huu ZIFF imejipanga katika kuzipeleka filamu za Watanzania nje ya nchi ili kushiriki katika matamasha makubwa, ikiwemo tamasha la Afrika litakalofanyika nchini Bukinafaso Februari mwaka huu.
"Jumla ya filamu mbili zitakazoshinda leo (jana) kwenye tamasha hili dogo la ZIFF (Mini-Festival), zitaiwakilisha nchi kwenye tamasha la filam Afrika nchini Bukinafaso na bado tunaendelea na taratibu nyingine ili kuona filam zetu zinaonekana sehemu nyingi Duniani" alisema Prof. Mhando.
Aidha, kwa upande wake, Meneja Masoko wa Steps Entertainment, Ignatus Kambarage, aliwataka wananchi kujitokeza kununua nakala za filamu halisi ili kuweza kukuza vipato vya wasanii.
Alisema, ukinunua nakala halisi unaongeza kipato cha serikali na hata kwa wasanii na wananchi kwa ujumla.

PRINT