Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
-
- #2,501
Rukwa United yakaa kileleni
Imeandikwa na Peti Siyame, Sumbawanga; Tarehe: 4th January 2011 @ 23:45
TIMU ya soka ya Rukwa United imefanikiwa kukaa kileleni mwa ligi ya taifa ngazi ya wilaya ya Sumbawanga mjini kwa kufikisha pointi sita baada ya kuwaangusha maafande wa Polisi Rukwa kwa bao 1-0.
Katika mchezo huo uliochezwa juzi kwenye uwanja wa Nelson Mandela mjini hapa, bao pekee la Rukwa United lilifungwa katika dakika ya 80 na mshambuliaji wake Raymound Chambi baada ya kuunganisha krosi toka wingi ya kulia iliyomshinda golikipa wa timu ya Polisi Rukwa.
Katika mchezo huo uliokuwa mkali na kusisimua timu zote zilishambuliana kwa zamu lakini walikuwa Rukwa United walioibuka kidedea kwa kupata pointi tatu na kufikisha jumla ya pointi sita ikimzidi mpinzani wake wa karibu timu ya Kantalamba FC iliyojikusanyia jumla ya pointi nne ikifuatiwa na Magereza Rukwa yenye pointi tatu.
Katika ligi hiyo ya timu sita bora, Poilisi Rukwa inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi tatu huku CHAKI FC ikiwa katika nafasi ya tano baada ya kucheza michezo miwili na kujipatia pointi moja, wakati timu ya Kingston Fc ikiburuza mkia ikiwa imecheza mechi mbili kama timu zingine lakini ikiwa imepoteza michezo yote.
Ligi hiyo imeingia katika hatua ya sita bora baada ya kukamilika kwa mzunguko wa kwanza ambapo jumla ya timu 18 zilishiriki ligi hiyo kwa kugawanywa kwenye makundi mawili tofauti ya timu tisa kila kundi.
Timu tatu zinatarajiwa kushiriki katika ligi ya mkoa wa Rukwa baada ya kukamilika kwa ligi hiyo.