Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #2,561
Miaka mitano THT Januari 11
na Khadija Kalili
MAANDALIZI ya kusherehekea miaka mitano ya Nyumba ya Kuvumbua Vipaji Tanzania ‘Tanzania House Of Talent' (THT), yamekamilika hivyo wadau wanatakiwa kukaa mkao wa kupata onyesho la aina yake ifikapo Januari 11 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Msemaji wa THT, Kemmy Mutahaba, kiingilio siku hiyo kitakuwa sh 30,000 huku wakipanga kuwa na watu 400 tu katika ukumbi, hivyo mashabiki wametakiwa kuchangamkia kununua tiketi ili waweze kupata fursa ya kushuhudia tamasha hilo.
Mutahaba alisema mbali na maadhimisho ya miaka mitano, pia watazindua albamu sita kwa mpigo za wasanii wanaotamba hivi sasa, ambao ni Mwasiti, Amini, Dito, Barnaba, Lina na Mataluma.
Alisema licha ya kuzindua albamu zao wasanii hao, pia wataudhihirishia umma kwamba wao ni wakali kwa kuonyesha shoo ya aina yake siku hiyo.
Aliongeza kuwa mambo mengi mapya kuhusu THT yataanikwa siku hiyo.