Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Dakika 20 zilitosha kuimaliza Stars- Poulsen Thursday, 06 January 2011 20:12

kocha%20poulsen2.jpg
Mwandishi Wetu, Cairo
KUTOELEWANA kwa wachezaji wa Taifa Stars katika dakika 20 za mwanzo juzi ndiko kulikoiponza timu hiyo na kuisababishia kipigo kikali cha mabao 5-1 kutoka kwa Misri.

Hata hivyo, kocha wa Stars Jan Poulsen ambaye aliungana kikosi hicho mjini Cairo akitokea kwao Denmark alisema kipigo hicho kimewapa funzo, lakini watasahihisha makosa yao.

Akizungumza mjini hapa baada ya mchezo baina ya timu hizo kwenye Uwanja wa Arab Contractors, Poulsen alisema timu yake ilifungwa na timu bora Afrika.

"Tumecheza na timu bora, huwezi ukalinganisha nafasi yetu ya 116 tuliyopo sisi (Tanzania) na wao wakiwa katika 20 bora za dunia, pia ndiyo namba moja Afrika.

"Misri ni timu nzuri, imecheza vizuri, ni mabingwa mara tatu mfululizo Afrika, vijana wangu walipambana vilivyo, lakini walikutana na timu bora, naamini michezo ijayo tutaimarika," alisema Poulsen.

Kocha huyo alieleza kuwa makosa machache waliyoyafanya wachezaji wake yalitumiwa vizuri na wapinzani wao kufunga na hiyo ilitokana na kucheza bila kuelewana dakika 20 za mwanzo.

"Naamini hata Watanzania wamejifunza mengi kwa mechi ya leo (juzi), faida yake itaonekana mechi zijazo," alisema Poulsen.

Kocha wa Misri, Hassan Shehata aliisifu Stars na kusema inahitaji marekebisho madogo, lakini itakuwa nzuri.

Alisema mchezo ambao Stars ilicheza kipindi cha pili, kama ingefanya hivyo kipindi cha kwanza, hana shaka kwamba mchezo ungekuwa mgumu kwao na kusisitiza kuwa timu yake licha ya kupata ushindi mnono, lakini ilikabiliana na upinzani mkali .

Kwa upande wake, nahodha wa Stars, Shadrack Nsajigwa alisema hali ya hewa ya baridi kali nayo iliwaathiri kwa kiasi fulani wachezaji wenzake hasa kipindi cha kwanza,lakini baadaye walichangamka wakati tayari mambo yameharibika.

Aliwaomba Watanzania wasikatishwe tamaa na matokeo hayo na kukumbusha kuwa hata kwenye michuano ya Chalenji iliyomalizika mwezi uliopita jijini Dar es Salaam, timu ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars' ilianza kwa kufungwa bao 1-0 na Zambia lakini ikaibuka bingwa.

Nahodha wa Misri, Wael Gomaa alisema michuano hiyo ya soka kwa nchi za Bonde la Mto Nile ni migumu na kwamba Tanzania si timu ya kubezwa, kwani ina wachezaji wenye miili midogo, lakini wana vipaji.

Juzi, Stars juzi ilikubali kipigo ambacho bao la kwanza lilifungwa na Said Khamdi dakika ya nne, kisha dakika kumi baadaye Mohammed Aboutrika alifunga la pili na dakika tisa baadaye beki Nadir Haroub kujifunga.

Bao la nne lilifungwa na Said Khamdi tena dakika ya 57, wakati lile la mwisho lilifungwa na Ahmed Ally, dakika ya 74 na la kufuatia machozi la Stars likifungwa na mchezaji aliyetokea benchi, Rashid Gumbo, dakika ya 77.

Kesho Stars itacheza na Burundi ambayo nayo juzi ilifungwa mabao 3-1 na Uganda, hivyo ili Stars iweke hai matumaini ya kufuzu nusu fainali italazimika kushinda na kusubiri mchezo wa mwisho dhidi ya Uganda.

Michuano hiyo inashirikisha timu saba zilizogawanywa katika makundi mawili, ambapo timu mbili za juu kila kundi zitacheza nusu fainali, wakati timu zitakazoshika nafasi ya tatu kila kundi zitacheza kuwania mshindi wa tano.

Bingwa wa michuano hiyo atazawadiwa zaidi ya Shilingi 200 milioni za Tanzania.
 
Dakika 20 zilitosha kuimaliza Stars- Poulsen Thursday, 06 January 2011 20:12

kocha%20poulsen2.jpg
Mwandishi Wetu, Cairo
KUTOELEWANA kwa wachezaji wa Taifa Stars katika dakika 20 za mwanzo juzi ndiko kulikoiponza timu hiyo na kuisababishia kipigo kikali cha mabao 5-1 kutoka kwa Misri.

Hata hivyo, kocha wa Stars Jan Poulsen ambaye aliungana kikosi hicho mjini Cairo akitokea kwao Denmark alisema kipigo hicho kimewapa funzo, lakini watasahihisha makosa yao.

Akizungumza mjini hapa baada ya mchezo baina ya timu hizo kwenye Uwanja wa Arab Contractors, Poulsen alisema timu yake ilifungwa na timu bora Afrika.

“Tumecheza na timu bora, huwezi ukalinganisha nafasi yetu ya 116 tuliyopo sisi (Tanzania) na wao wakiwa katika 20 bora za dunia, pia ndiyo namba moja Afrika.

"Misri ni timu nzuri, imecheza vizuri, ni mabingwa mara tatu mfululizo Afrika, vijana wangu walipambana vilivyo, lakini walikutana na timu bora, naamini michezo ijayo tutaimarika,” alisema Poulsen.

Kocha huyo alieleza kuwa makosa machache waliyoyafanya wachezaji wake yalitumiwa vizuri na wapinzani wao kufunga na hiyo ilitokana na kucheza bila kuelewana dakika 20 za mwanzo.

“Naamini hata Watanzania wamejifunza mengi kwa mechi ya leo (juzi), faida yake itaonekana mechi zijazo,” alisema Poulsen.

Kocha wa Misri, Hassan Shehata aliisifu Stars na kusema inahitaji marekebisho madogo, lakini itakuwa nzuri.

Alisema mchezo ambao Stars ilicheza kipindi cha pili, kama ingefanya hivyo kipindi cha kwanza, hana shaka kwamba mchezo ungekuwa mgumu kwao na kusisitiza kuwa timu yake licha ya kupata ushindi mnono, lakini ilikabiliana na upinzani mkali .

Kwa upande wake, nahodha wa Stars, Shadrack Nsajigwa alisema hali ya hewa ya baridi kali nayo iliwaathiri kwa kiasi fulani wachezaji wenzake hasa kipindi cha kwanza,lakini baadaye walichangamka wakati tayari mambo yameharibika.

Aliwaomba Watanzania wasikatishwe tamaa na matokeo hayo na kukumbusha kuwa hata kwenye michuano ya Chalenji iliyomalizika mwezi uliopita jijini Dar es Salaam, timu ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ ilianza kwa kufungwa bao 1-0 na Zambia lakini ikaibuka bingwa.

Nahodha wa Misri, Wael Gomaa alisema michuano hiyo ya soka kwa nchi za Bonde la Mto Nile ni migumu na kwamba Tanzania si timu ya kubezwa, kwani ina wachezaji wenye miili midogo, lakini wana vipaji.

Juzi, Stars juzi ilikubali kipigo ambacho bao la kwanza lilifungwa na Said Khamdi dakika ya nne, kisha dakika kumi baadaye Mohammed Aboutrika alifunga la pili na dakika tisa baadaye beki Nadir Haroub kujifunga.

Bao la nne lilifungwa na Said Khamdi tena dakika ya 57, wakati lile la mwisho lilifungwa na Ahmed Ally, dakika ya 74 na la kufuatia machozi la Stars likifungwa na mchezaji aliyetokea benchi, Rashid Gumbo, dakika ya 77.

Kesho Stars itacheza na Burundi ambayo nayo juzi ilifungwa mabao 3-1 na Uganda, hivyo ili Stars iweke hai matumaini ya kufuzu nusu fainali italazimika kushinda na kusubiri mchezo wa mwisho dhidi ya Uganda.

Michuano hiyo inashirikisha timu saba zilizogawanywa katika makundi mawili, ambapo timu mbili za juu kila kundi zitacheza nusu fainali, wakati timu zitakazoshika nafasi ya tatu kila kundi zitacheza kuwania mshindi wa tano.

Bingwa wa michuano hiyo atazawadiwa zaidi ya Shilingi 200 milioni za Tanzania.
 
Simba kama Yanga Uhai Cup


Na Addolph Bruno

TIMU ya soka ya vijana wenye miaka chini ya 20, ya JKT Ruvu, imetinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Uhai, baada ya kuichapa Simba bao 1-0, katika mchezo wa robo fainali uliochezwa Uwanja wa
Karume Dar es Salaam, jana.JKT Ruvu imekuwa timu ya tatu kuingia hatua hiyo, ikitanguliwa na AFC Arusha iliyowatoa African Lyon kwa mabao 2-1 na Ruvu Shooting iliyowaondosha Yanga kwa mabao 2-1. Yanga iliaga michuano hiyo juzi, baada ya kuchapwa na Ruvu Shooting.

Mchezo huo ulianza kwa timu zote kushambuliana kwa, dakika ya tano Kelvin Chale wa Simba, alikosa bao la wazi baada ya shuti lake kudakwa na kipa Phelemon Ramadhani wa JKT.

Hata hivyo, mchezo huo uliingiwa na dosari dakika ya 20, baada ya mwamuzi Isihaka Mwalile, kumtoa katika eneo la uwanja kocha wa Simba, Seleman Matola, kwa kutoa lugha chafu.

Kitendo hicho kilionekana kuwachanganya wachezaji wa Simba, lakini waliendelea kulishambulia lango la wapinzani wao.
JKT ilikianza kipindi cha pili kwa kulisakama lango la wapinzani wao, na kufanikiwa kupata bao pekee katika mchezo huo, dakika ya 51, lililofungwa na Frank Domayo.

Bao hilo liliwazindua Simba na kujibu mashambulizi, lakini mabeki wa JKT walikuwa imara kuondosha hatari langoni mwao.Simba nusura ijipatie bao dakika ya 75, baada ya Chale kupiga mpira juu na kutoka nje ya uwanja.

Mashindano hayo yataendelea kesho hatua ya nusu fainali, kwa mchezo kati ya AFC dhidi ya Ruvu Shooting na JKT itacheza na mshindi wa kati ya Mtibwa na Polisi Tanzania.

 
Mourinho, Preciado wanusurika kufungiwa


MADRID, Hispania
KOCHA wa timu ya Real Madrid, Jose Mourinho na kocha mwenzake wa timu ya Sporting Gijon, Manuel Preciado, wamenusurika adhabu ya kufungiwa kutokana na jazba waliyoionesha Novemba mwaka jana, baada ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Hispania (RFEF), kuona hakuna sababu ya kuwaadhibu.

Awali, shirikisho hilo lilikuwa limeagizwa na kamisheni ya michezo selikani kuwachukulia hatua madhubuti za kinidhamu makocha hao wawili, baada ya kuonekana kutaka kusababisha ghasia na kuvuruga mchezo.

Kamisheni hiyo ilieleza kuwa, hatua ya Preciado kuja juu kufuatia kauli ya Mourinho kwamba, timu yake haikufanya jitihada kubwa kuwafunga Barcelona, ilikuwa ni ya hatari na ya kujenga mazingira ya uadui wakati wa mechi baina ya timu hizo mbili.

Klabu hiyo ya Gijon ilieleza kupitia tovuti yake kuwa, kamati ya mashindano ya RFEF ilieleza juzi kuwa, taarifa iliyotolewa kuhusu taarifa za makocha hao, haikulingana na hatua ya kupewa adhabu.Hata hivyo, shirikisho hilo liliongeza kuwa, kamati hiyo imeagiza wadau wote wa soka kupitia taarifa hiyo.


Katika mvutano huo, Preciado anamshutumu Mourinho kwa kukosa heshima na alitoa matamshi ya Kireno katika mkutano wa vyombo vya habari, jambo ambalo liliifanya timu ya Real Madrid kutoa taarifa kabla ya mechi kulaani kitendo hicho.

Hatua hiyo inaungwa mkono na makocha kadhaa wa La Liga, akiwemo kocha wa timu ya Villarreal, Juan Carlos Garrido na kocha wa Espanyol, Mauricio Pochettino ambao wanamuunga mkono Preciado.

 
Kanumba, Jeniffer watuzwa kung'ara ZIFF


na Khadija Kalili


amka2.gif
KAMPUNI ya Steps Entertainment jana iliwakabidhi tuzo wasanii wawili ambao inasimamia kazi zao waliofanya vizuri katika tamasha la filamu la Majahazi ‘ZIFF' lililomalizika wiki iliyopita visiwani Zanzibar.
Wasanii waliokabidhiwa tuzo zao ni Steven Kanumba na Hanifa Daudi Kibavu maarufu kwa jina la ‘Jeniffer' waliotunikiwa kupitia filamu yao ya ‘This Is It'.
Katika tamasha hilo, Jennifer alishinda nafasi ya msanii bora katika filamu hiyo hivyo, ambako filamu hiyo imeingia kwenye shindano la ‘Panafrican Film and Television Festival' (FESPACO) Ouagadougou – Burkina Faso mwezi ujao.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana, Meneja Masoko, Simbiso Machine, alisema kwamba mbali ya ‘This Is It' filamu nyingine zilizowania tuzo hiyo ni ‘Briefcase', na ‘Best Wife Divorce'.
Filamu hizo zote zinasambazwa na Kampuni ya Steps Entertainment.
Katika hatua nyingine, kampuni hiyo inatarajia kufungua tawi la kuuza filamu za kibongo nchini Rwanda, ambazo pia zitauzwa kwa bei nafuu ikiwa ni katika mpango wa kujipanua kimasoko na kukidhi haja ya wapenzi wa filamu za Kitanzania.
 
Matokeo ya Uchaguzi ZFA yafutwa Thursday, 06 January 2011 20:14

Vicky Kimaro

MATOKEO ya uchaguzi wa Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA), uliofanyika mapema wiki iliyopita yamefutwa na badala yake chama hicho kimetakiwa kuitisha uchaguzi mwingine ndani ya wiki mbili.

Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Gombani mjini Pemba, rais wa chama hicho aliyedumu kwa miaka 22, Ali Fereji Tamim, alichaguliwa tena kuiongoza ZFA kwa miaka mingine minne baada ya kumshinda mpinzani wake wa karibu Suleiman Mahmoud Jabir.

Katika uchaguzi huo, Tamim alipata kura 32, Jabir kura 20 na Munir Zakaria kura 2.

Baada ya uchaguzi huo Suleiman Jabri alikata rufaa kwenye kamati ya uchaguzi ya ZFA kupinga matokeo hayo akidai kuwa Tamim hakuwa na sifa inayotakiwa ambayo ni ya elimu ya kidato cha nne na pia kamati tano za ZFA zilizopiga kura hazikuwa na sifa za kufanya hivyo kwa vile hazikufanya chaguzi zake kwa muda mrefu.

Kamati hiyo ya uchaguzi iliyokaa jana chini ya mwenyekiti wake, Ally Suleiman Shehata na katibu wake, Mustapha Omary ambaye pia ni msajili wa vyama vya michezo visiwani Zanzibar ilibaini kuwa Tamimu hakuwa na sifa hiyo baada ya kushindwa kuwasilisha vyeti vyake vya kidato cha nne na badala yake alimpeleka mtu ambaye alisoma naye na kumaliza naye kidato cha nne.

Akitangaza uamuzi huo, mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya ZFA ambaye aliendesha mchakato mzima wa uchaguzi huo jana, Shihata alisema, "Kamati imepitia rufaa iliyokatwa na tumebaini Tamim hana sifa za elimu kwa vile ameshindwa kuthibitisha kwa kuleta vyeti vyake.

Kwa mantiki hiyo matokeo ya uchaguzi uliofanyika tumeyabatilisha, na naiagiza ZFA kwa gharama zake itishe uchaguzi haraka iwezekanavyo ndaniya wiki mbili."alisema Shehata"

"Pia, namuagiza Katibu Mkuu wa ZFA aitishe uchaguzi haraka wa vyama vya waamuzi, ufundi, wanawake, walemavu na soka ya vijana ambavyo havijafanya uchaguzi wake kwa muda mrefu vifanye hivyo ndani ya wiki moja ili viwe na sifa ya kupiga kura kwenye uchaguzi ujao utakaofanyika wiki mbili zijazo,"alisisitiza Shehata

Hata hivyo, Tamim aliomba apewe muda hadi Jumanne ijayo ili aweze kuwasilisha vielelezo vyake, kamati hiyo imekubali maombi yake kwa sharti kuwa maamuzi yake ya kufuta uchaguzi yatabaki pale pale.

Shehata, pia amewataka wadau wa soka Zanzibar kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo ujao ili aweze kupatikana kiongozi mwenye sifa na si kuachia watu wachache kufanya hivyo, jambo ambalo linapunguza ushindani na mantiki ya kufanyika kwa uchaguzi huo.


 
Sputanza yajitosa kumtibu Mtagwa
Thursday, 06 January 2011 20:11

Sweetbert Lukonge
UONGOZI wa Chama cha Wachezaji Soka Tanzania (Sputanza) upo katika mchakato wa kumpeleka nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Jellah Mtagwa mkoani Iringa kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya ugonjwa wa kiharusi unaomsumbua tangu mwaka 2006.

Kauli hiyo ya Sputanza inafuatia kujitokeza kwa wasamaria wema watakaogharimia matibabu yake.

Hatua hiyo imechukuliwa siku chache baada ya gazeti hili kuandika habari kuhusu matatizo ya kiafya yanayomkabili kiungo huyo wa zaman wa Stars kiasi cha kumsababishia kushindwa kumudu gharama za matibabu ikiwa ni pamoja na kujikimu kimaisha na familia yake.

Akizungumza na Mwananchi jana, Katibu Msaidizi wa Sputanza, Abeid Kasabalala alisema kuwa kufuatia habari hiyo iliyochapishwa Jumatatu na gazeti hili, wadau mbalimbali wameguswa na tatizo hilo na baadhi yao wamejitokeza kumsaidia.

Wengi wao, Kasabalala alisema wamenuia kuhakikisha anarudia hali yake ya zamani.

"Tunamshukuru Mungu kwa mchango mkubwa uliotolewa na gazeti la Mwananchi kwani baada ya habari hiyo kuchapishwa wadau pamoja na wapenzi mbalimbali wamejitokeza kumsaidia kwa kile wanachoweza, lakini pia wapo wengine ambao tumewasiliana nao kuwa wapo tayari kumsaidia kwa matibabu.

"Ukiacha na hao pia hivi sasa tunamsubiri mdau mwingine kutoka mkoani Iringa ambaye yupo njiani anakuja Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya mazungumzo naye (Mtagwa) na kama ikiwezekana ataondoka naye kwenda mkoani humo kwa ajili ya matibabu zaidi ambayo yatamsaidia aweze kurudi katika hali yake ya kawaida kama alivyokuwa zamani,'' alisema Kasabalala.

Katika hatua nyingine, Kasabalala amewata ka wapenzi na wadau wote michezo nchini kuendelea kumsaidia mchezaji huyo pamoja na wengine wote wanaokabiliwa na matatizo makubwa ili waweze kurudi katika hali zao za kawaida ambazo zitawawezesha kushiriki kikamilifu katika harakati zao za kawaida.

 
Afande Sele kukomalia filamu 2011


na Mwandishi wetu


amka2.gif
MSANII mahiri katika medani ya muziki wa kizazi kipya nchini, Selemani Msindi ‘Afande Sele' wa Morogoro, amesema mkakati wake mwaka 2011 ni kujikita zaidi katika filamu na mambo ya kijamii.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Morogoro jana, Afande Sele alisema, kwa kuanza anakamilisha kazi ya filamu iitwayo ‘Haki iko Wapi', ambayo itaingia sokoni hivi karibuni.
Alisema kuwa, anaamini filamu atakazozitoa zitakuwa zenye kuvutia na kuelimisha kwa kiasi kikubwa, zikielezea maisha halisi ya wasanii wa hapa


h.sep3.gif

 
Sababu tano kipigo cha Stars


na Mwandishi wetu, Cairo


amka2.gif
KIPIGO cha mabao 5-1 ilichokipata timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars' juzi kutoka kwa Misri ‘Pharaos' kimetokana na sababu tano za msingi, huku kikiwa kimemchanganya Kocha Mkuu, Mdenish Jan Poulsen.
Moja ya sababu iliyotajwa na Kocha Poulsen ni kwamba Stars ilifungwa na timu bora Afrika.
"Tumecheza na timu bora, huwezi ukalinganisha nafasi ya 116 tuliyopo Tanzania na wao wapo katika 20 bora za dunia, pia ndiyo namba moja Afrika. Misri ni timu nzuri, imecheza vizuri, ni mabingwa mara tatu mfululizo Afrika, vijana wangu walipambana vilivyo, lakini walikutana na timu bora, naamini michezo ijayo tutaimarika," alisema Poulsen.
Kocha huyo alisema, makosa machache waliyoyafanya wachezaji wake, yalitumiwa vizuri na wapinzani wao kufunga na hiyo ilitokana na kucheza bila kuelewana dakika 20 za mwanzo.
Sababu ya pili inayoelezwa na wadau wa soka nchini ni pamoja na ushindi wa Stars kwenye michuano ya Chalenji iliyomalizika nchini mwezi uliopita.
"Ushindi wao kwenye Kombe la Chalenje, nao umewachongea Stars, hivyo Misri ilikamia kwa kuweka wachezaji wake wote maarufu, wakijua inacheza na bingwa wa CECAFA mwaka huu," alisema mmoja wa wadau wa soka nchini.
Sababu ya tatu ni kutoelewana kwa timu nzima, hasa safu ya ulinzi pamoja na kipa namba moja nchini, Juma Kaseja, ambao juzi walicheza chini ya kiwango.
Kuna wakati Kaseja alitaka kupigana na Nadir Haroub ‘Canavaro' baada ya beki huyo kujifunga bao la tatu akiwa katika harakati za kuokoa, jambo lililopunguza kuelewana zaidi.
Kaseja mwenyewe ambaye umaarufu wake nchini uliongezeka wakati wa michuano ya Chalenji, alishindwa kucheza mipira kadhaa ya krosi iliyochangia kipigo hicho, kutokana na kupungua kwa umakini wa mabeki wa pembeni.
Sababu ya nne ni washambuliaji wa kati na pembeni, ambao walizidiwa ujanja na wachezaji wa Misri walioonekana kuwa na miili mikubwa ikilinganishwa na wa Stars
Sababu ya tano ya kichapo cha Stars, imetolewa na Nahodha wa Stars, Shadrack Nsajigwa, ambaye alisema kuwa hali ya baridi kali ya Misri, iliwachanganya kiasi Fulani, hasa kipindi cha kwanza, lakini baadaye walichangamka wakati tayari mambo yameharibika.

Aliwaomba Watanzania wasikatishwe tamaa na matokeo hayo na kukumbusha kuwa, hata michuano ya Chalenji iliyomalizika mwezi uliopita jijini Dar es Salaam timu ya taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars' ilianza kwa kufungwa bao 1-0 na Zambia, lakini ikaja kuibuka bingwa.
Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Misri, Hassan Shehata, aliisifu Stars na kusema inahitaji marekebisho kidogo, lakini itakuwa nzuri.
Alisema, mpira ambao Stars ilicheza kipindi cha pili, kama ingecheza hivyo kipindi cha kwanza, mchezo ungekuwa mgumu kwao na kusisitiza kuwa timu yake licha ya kupata ushindi mnono, lakini ilikabiliana na upinzani mkubwa.
Naye nahodha wa Misri, Wael Goma alisema michuano hiyo ya soka kwa nchi za Bonde la Mto Nile ni migumu na kwamba Tanzania si timu ya kubezwa, kwani ina wachezaji wenye miili midogo, lakini wana vipaji.
Stars juzi ilikubali kipigo hicho, ambapo bao la kwanza lilifungwa na Said Khamdi, dakika ya nne, kisha dakika 10 baadaye Mohammed Aboutrika alifunga la pili na dakika tisa baadaye beki Nadir Haroub ‘Cannavaro' akajifunga.
Bao la nne lilifungwa na Said Khamdi dakika ya 57, wakati lile la mwisho lilifungwa na Ahmed Ally dakika ya 74 na la Stars lilifungwa na mchezaji aliyetokea benchi Rashid Gumbo dakika ya 77.
Kesho Stars itacheza na Burundi ambayo nayo juzi ilifungwa mabao 3-1 na Uganda, hivyo ili Stars iweke hai matumaini ya kufuzu nusu fainali italazimika kushinda na kusubiri mchezo wa mwisho dhidi ya Uganda.
 
Uchaguzi ZFA ‘ulichakachuliwa'


na Mohamed Said Abdullah, Zanzibar


amka2.gif
KAMATI ya uchaguzi mkuu ya Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), imesema kuwa uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika Desemba 31 mwaka jana kisiwani Pemba ni batili na kutaka urejewe ndani ya wiki mbili kutokana na kujitokeza kwa kasoro mbalimbali ikiwemo kuruhusiwa kwa wajumbe wasiopungua watano bila ya kuwa na sifa.
Hatua ya kutengua matokeo ya uchaguzi huo, yanatokana na rufaa iliyowasilishwa na aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais, Suleiman Mahmoud Jabir ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo, katika kile alichodai kuwa uchaguzi huo haukuwa halali kwa vile wajumbe wasiokuwa na sifa waliruhusiwa kushiriki na kupiga kura.
Pia alipinga mpinzani wake aliyekuwa Rais mteule Ali Ferej Tamim, kushindwa kuwasilisha cheti cha kidato cha nne alipokwenda kuchukua na kurejesha fomu za kutetea nafasi yake.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ), zilizopo Mwanakwerekwe, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Ali Suleiman Ali alisema, baada ya kupitia rufaa hiyo, kamati inaunga mkono hoja zote zilizotolewa, ikiwemo ya Ali Ferej Tamim baada ya kushindwa kupeleka mbele ya kamati ushahidi wa cheti cha kidato cha nne, kama ambavyo kanuni ya uchaguzi inavyoelezea sifa za wagombea wa nafasi za juu za uongozi wa chama hicho.
Mwenyekiti huyo alisema kwamba kamati ilikutana jana na Tamim ikimtaka kuwasilisha cheti chake cha kidato cha nne, badala yake alikuja katika kikao akiwa na majina ya watu aliosoma nao, pamoja na hati za kiapo cha mahakama, hivyo kamati imempatia muda kuanzia jana awasilishe vielelezo vyake ikiwemo cheti cha kidato cha nne.
"Kwa vile leo ameshindwa kuwasilisha cheti chake, kamati imemtaka siku ya Jumanne Januri 11, mwaka huu, awasilishe cheti chake cha kidato cha nne, kwa vile kamati haiwezi kujitosheleza kwa ushahidi wa maneno, hivyo tumempatia muda wa siku sita atuletee cheti chake cha kidato cha nne," alisema Ali Suleiman Ali maarufu kwa jina la ‘Shihata'.
"Kamati inatangaza rasmi imetengua maamuzi ya nafasi zote za ushindi za uchaguzi mkuu wa ZFA taifa, kuanzia Rais na Makamu wa Rais Unguja na Pemba, uchaguzi umekuwa batili," alisema mwenyekiti huyo.
Aidha, alizitaja kamati zilizowakilishwa na wajumbe ambao hawakuwa na sifa ya kushiriki katika mkutano mkuu kuwa ni pamoja na kamati ya waamuzi iliyowakilishwa na Hafidh Ali Tahir, kamati ya vijana ya Central iliyowakilishwa na Abdulnabil Tesso, kamati ya wanawake iliyowakilishwa na Nasra Juma, kamati ya ufundi na uendelezaji iliyowakilishwa na Abdallah Ali, pamoja na kamati ya watu wenye ulemavu.
Maamuzi hayo yamemtaka Katibu Mtendaji wa chama hicho, Mzee Zam Ali, aandae uchaguzi wa kamati hizo ndani ya wiki moja kuanzia jana ili kuweza kupata wajumbe halali watakaoziwakilisha kamati hizo za kudumu katika mkutano mkuu wa kuchagua viongozi wa kitaifa wa ZFA.
Kwa uamuzi huo, mwenyekiti huyo wa uchaguzi ametoa wito kwa wapenda michezo, wadau wa soka na Wazanzibari kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi hizo za juu za uongozi.
Kwa upande wake, aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo ya urais, mwandishi wa habari wa Channel Ten, Munir Zakaria alisema uamuzi huo ni ushindi wa Wazanzibari wote wapenda maendeleo wa michezo na si ushindi wa mgombea aliyekata rufaa na kutoa wito kwa wajumbe wa mkutano mkuu kutorudia tena makosa ya kuchagua bora viongozi na badala yake wawatazame wagombea makini watakaokuwa viongozi bora na watakaoleta maendeleo na mabadiliko makubwa ya mfumo mzima wa uendeshaji wa soka.
 
Minziro amfuata Papic Zenji


na Juma Kasesa


amka2.gif
KOCHA Msaidizi wa timu ya Yanga, Fred Felix Minziro ‘Majeshi', ametua mjini Zanzibar tayari kumsaidia Mserbia Kostadin Papic kuinoa timu hiyo inayoshiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea mjini Zanzibar.
Minziro alitangazwa kujiunga na timu hiyo juzi jijini Dar es Salaam na kusainishwa mkataba kuchukua nafasi iliyoachwa na aliyekuwa Kocha Msaidizi, Salvatory Edward, ambaye amepigwa ‘Stop' na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa kile kilichoelezwa vyeti vyake havikidhi vigezo vya kuzinoa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu hiyo, Louis Sendeu, Minziro aliyetua mjini Zanzibar jana alitarajiwa kukaa katika benchi la timu hiyo katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC uliotarajiwa kupigwa usiku.
Aidha, Sendeu alisema, Minziro ameongozana na jopo la viongozi wa juu wa klabu hiyo kwa ajili ya kuiongezea nguvu ili iweze kunyakua kombe hilo ikiwamo kujinoa vya kutosha kwa ajili ya Ligi Kuu inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 15 mwaka huu wakati katika michuano ya kimataifa Yanga itaanza kutupa karata yake kwa kuvaana na Dedebits ya Ethiopia.
Katika hatua nyingine, Sendeu alisema uongozi wa klabu hiyo, umeipa shavu Kampuni ya Hari Singh & Sons LTD kwa ajili ya kukarabati ukuta wa Uwanja wa Kaunda ambao ulibomoka hivi karibuni.
Alisema ujenzi wa ukuta huo unatarajiwa kuanza leo kwa kampuni hiyo kukarabati eneo lote lililobomoka tayari kwa Uwanja huo kutumika kwa michezo ya kirafiki na mazoezi.
mwisho
 
Vyama vyatakiwa kuacha kulalamika


na Samia Mussa


amka2.gif
VYAMA vya michezo mbalimbali nchini vimetakiwa kutolalamika kuhusu kutosaidiwa na serikali, kampuni, taasisi au wadau pale mashindano ya kitaifa na kimataifa yanapotokea.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Rachel Khowoya, alisema kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwenye vyama kuwa hawasaidiwi na serikali na hakuna wafadhili wanaojitokeza kudhamini katika vyama vyao, wakati jambo hilo linasababishwa na wenyewe.
Khowoya, alivitaka vyama hivyo kuacha lawama kwa serikali, kwa kuwa haiwezi kusaidia michezo yote nchi nzima, labda itumie bajeti za wizara zote.
Alitaka vyama hivyo, badala yake viandae mikakati endelevu na yenye dalili ya mafanikio, ili iweze kuwavutia wadhamini kuwekeza katika michezo yao.
Alisema kuwa mipango mibovu ndio inayofanya wafadhili washindwe kufadhili michezo mingine mbali na soka, ambapo aliwataka kubadili mwenendo wao wa sasa na kuwa na mipango endelevu ambayo itawafanya wafike mbali kimaendeleo.
Aidha, alizitaka kampuni nyingine kujitokeza kusaidia vyama vya michezo ambavyo vina mwelekeo mzuri, ili kuzisaidia kampuni kama TBL, NMB, zile za simu na nyinginezo ambazo zimekuwa mstari wa mbele katika kudhamini mashindano mbalimbali hususan soka
 
Simba yafungishwa virago Uhai Cup


na Juma Kasesa


amka2.gif
BAO la dakika ya 51 likipachikwa wavuni na Frank Ndomayo wa JKT Ruvu U 20 jana liliiwezesha timu hiyo kutinga nusu fainali ya Uhai Cup na kuifungisha virago Simba katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani kwa timu zote kushambuliana kwa zamu, Simba ndio walikuwa kwanza kulisogelea lango la maafande watoto hao dakika ya 5, kupitia Kelvin Chale lakini shuti lake likadakwa na kipa wa JKT Philimon Ramadhani.
Maafande watoto hao walijibu shambulizi hilo dakika ya 16 kupitia mfungaji wa bao lao pekee Ndomayo, lakini akiwa katika eneo la hatari akanyang'anywa mpira na mabeki.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu hizo zilitoka uwanjani zikiwa sare ya bila kufungana.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa Simba kutawala dakika zote 45 za mchezo, lakini kosa lililofanywa na mabeki wa timu hiyo dakika 51 kushindwa kuokoa mpira langoni mwao lililotosha kumpa mwanya Ndomayo kuachia shuti lililotinga moja kwa moja nyavuni na kuiondosha Simba mashindanoni.
Mwisho.
 
h.sep7.gif
master.gif

BASATA toeni mrejesho wa majukwaa

ban_tahariri.jpg

amka2.gif
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) na Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa Tanzania (CAJA) Juni mwaka jana walianzisha jukwaa linalowakutanisha wasanii na wanahabari za sanaa ambao kila Jumatatu hukutana katika ukumbi wa mikutano wa baraza hilo.
Jukwaa hilo lilianzishwa kwa lengo la kukutanisha wadau wa sanaa na habari, baada ya kuonekana kwamba ukaribu kati ya wadau hao ulikuwa si wa kuridhisha, ikaonekana njia pekee ya kuwakutanisha pamoja ni kupitia jukwaa la sanaa.
Awali jukwaa hilo lilijulikana kama ‘Sanaa Press Talk', ambapo kutokana na kujali lugha adhimu ya Kiswahili jina hilo lilibadilika kutoka jina hilo hadi Jukwaa la Sanaa, ikiwa na maana sawa.
Uanzishwaji wa jukwaa hilo ni jambo jema kutokana na umuhimu wa pande hizo mbili na unyeti wa Basata kwa jamii.
Tanzania Daima tunapongeza uanzishwaji wa majukwaa hayo kwa sababu yanafanikisha mawasiliano baina ya pande mbili, ingawa uhudhuriaji wake ni mdogo kutokana na idadi ndogo ya wadau wanaohudhuria majukwaa hayo.
Wasanii na wanahabari inatakiwa wayaone majukwaa hayo kuwa ni chachu ya mawasiliano na maendeleo yao kutokana na kufikishiana salamu zao ambazo zinahitaji mwendelezaji, lakini wengi hawataki kuhudhuria.
Mara kadhaa ambapo yamefanyika majukwaa hayo, kuna wasomi ambao walihudhuria na kutoa elimu bora kwa wasanii na wana habari, ambao baadhi yao hawafahamu mojawapo ya masuala ya maendeleo kati yao.
Wito pekee kwa pande hizo mbili ni kujitokeza kila Jumatatu katika majukwaa hayo kwa ajili ya kujipatia elimu ambayo itaondoa ufinyu wa mawazo tuliyozoea ambayo si mwendo mwema wa maendeleo husika.
Pamoja na matokeo bora ya majukwaa ya sanaa, lakini Basata wanatakiwa kuwasilisha mrejesho wa yaliyowasilishwa kwao na baadhi ya wadau waliokuwa wakihudhuria makujwaa hayo, ambayo yaliitaka Basata kutoa ufafanuzi wa baadhi ya matukio.
Sambamba na mrejesho, pia Basata wazingatie mapendekezo yaliyowasilishwa na wadau katika majukwaa hayo, mojawapo ikiwa ni kuhifadhi baadhi ya matukio muhimu katika hali mbalimbali kama katika mifumo ya sauti na picha ambazo baadaye itakuwa ni kumbukumbu bora kwa vizazi vijavyo.
Mfano mojawapo wa matukio ambayo yanatakiwa kupewa kipaumbele ni pamoja na jukwaa lililokutanisha Mkurugenzi wa Utamaduni, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, sambamba na msaidizi wa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, ambao kwa pamoja walihudhuria jukwaa moja na kutoa tamko ambalo lilikemea matatizo ya kumbi za burudani kutokana na matatizo yake.
Basata inatakiwa kuyatolea ufafanuzi baadhi ya matukio ambayo yalionekana dhahiri kwamba yanaweza kukwamisha maendeleo ya sanaa.
 
TDMA rudisheni mashindano ya disco taifa
ban..jpg


amka2.gif
AKHLAN wasaalan msomaji wangu wa Jamvi la Kulonga, nianze kwa kukutakia heri ya mwaka 2011, kwa kuweza kuingia kwa kishindo lakini zote zikiwa ni neema zake Muumba wa mbingu na ardhi.
Hili ni Jamvi la Kulonga la kwanza katika mwaka huu mpya ambao nakuahidi kukupa habari motomoto zitakazokuwezesha kufahamu mambo mengi yanayohusu tasnia ya habari za burudani na sanaa kwa ujumla.
Leo katika Jamvi hili nataka nizungumzie kupotea kwa mashindano ya taifa ya disco na uwepo wanenguaji wasiokidhi umri wa miaka 18 kushiriki katika shughuli za unenguaji huku chama cha muziki wa disco Tanzania (TDMA) chenye dhamana ya kuyaandaa kikiwa kimekaa kimya jambo ambalo ni kutowatendea haki wadau wa muziki wa huo.
Katikati ya miaka ya 1980 hadi mwanzoni mwa mwaka 2000 kulikuwa na msisimko wa mashindano ya disco nchini yaliyokuwa yakiandaliwa na Chama cha muziki huo ambayo yaliweza kuibua vipaji vya madansa mbalimbali ambao waliing'arisha Tanzania kimataifa, ingawa wengine waliipa kisogo fani hiyo na kujikita katika uimbaji.
Jamvi la Kulonga linakumbuka mashindano kuwa yaliweza kutengeneza ajira kwa vijana waliokuwa wakishiriki katika mashindano hayo ikiwamo kuitangaza Tanzania kupitia mashindano ambayo yalikuwa yakizihusisha nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Miongoni mwa madansa ambao waling'ara katika mashindano hayo ambao Jamvi hili lilipata bahati ya kuwashudia ni hayati Mussa Simba ‘Black Moses', Athumani Digadiga, Ally Baucha, Sabah A. Jackson, Super Ngedere, Askof Pompiduu, Bob Rich, Sammy Cool, Maganga Michael Jackson, Cadet Bongoman na Coco Rico ‘Bileku Mpasi'.
Hao ni baadhi tu ya madansa ambao waliweza kuleta ushindani na msisimko katika mashindano mbalimbali yaliyokuwa yakiandaliwa na TDMA chini ya usimamizi madhubuti wa Baraza la Taifa Sanaa Tanzania (BASATA).
Hoja ya Jamvi hili ni kuona tangu mashindano hayo yalipofanyika mara ya mwisho mwaka 2000, hakujawahi kutokea kitu kingine ambacho kinafanana na mashindano hayo zaidi ya kushuhudia kumbi mbalimbali za burudani na baa zikiendesha shoo kwa wanenguaji hao kiholela wakiwa utupu na bila baraka za TDMA na BASATA.
Swali ambalo Jamvi hili linajiuliza, TDMA ipo hai kweli? Na kama jibu ni ndiyo wanafanya nini kuturejeshea mashindano hayo ambayo yalikuwa ni sehemu ya burudani kwa wananchi mbalimbali lakini pia yakiwa ni sehemu ya njia ya kuitangaza Tanzania katika nyanja ya sanaa.
Kubwa la kushangaza ni kuona uongozi wa chama hicho ulio chini ya Mwenyekiti Ibra Radi Washokera, Katibu Mkuu wake, Samwel Semkuruto na Naibu wake, Selemani Mchovu ‘Cisco' tangu umeingia madarakani kushindwa kuandaa mashindano ya Disco au kusimamia uchezeshwaji holela wa mabinti walio chini ya umri wa miaka 18 katika kumbi na baa mbalimbali nchini.
Pengine tuwaulize wa TDMA tuambieni mmekwama wapi kuturejeshea mashindano yetu ambayo yalikuwa yakijaza mamia ya watu katika kumbi za Lang'ata, Kinondoni, Magomeni kwa Macheni, Sweet Corner, Madoto na Vijana Social Hall jijini Dar es Salaam, wakati Morogoro ilikuwa ni Mango Garden na Kaumba wakati Mwanza ni Deluxe.
Mashindano ya disco nchini yalikuwa yakifanyika kuanzia mikoani na hatimaye fainali zake kufanyika jijini na kupatikana bingwa ambaye alikuwa akiiwakilisha Tanzania katika mashindano ya ukanda wa Afrika Mashariki ambapo kwa miaka kadhaa nchi iliweza kutangazika nje ya mipaka kupitia madansa hao.
Jamvi la Kulonga linahoji, nini kinakwamisha mashindano hayo yasifanyike ikiwa viongozi hao wapo madarakani muda mrefu na wameshindwa kutangaza mipango waliyonayo katika kurudisha hadhi ya mashindano hayo na chama kwa ujumla.
Lakini pia TDMA imekuwa kimya ikipuuzia madisco yanayopigwa mitaani kiholela na shoo zinazofanywa na wanenguaji walio chini ya umri huo ingawa bado suala hili linaigusa pia na BASATA katika kusimamia maadili.
Katika siku za hivi karibuni kumeibuka uyoga wa madisco mitaani ambayo yanapiga muziki na kutumia wanenguaji wasiokidhi umri husika, jambo ambalo ni kwenda kinyume na taratibu zinazokiongoza chama hicho na BASATA kwa ujumla.
Jamvi hili linakumbuka miaka ya nyuma maofisa wa TDMA walikuwa wakihangaika huku na kule hadi usiku wa manane kuingia katika kumbi za burudani kukagua vibali vya kupiga disco, jambo lililokisaidia chama hicho kujiongezea kipato na pia kusimamia maadili ya shoo hizo ili kuepuka vijana walio chini ya umri huo kujiingiza katika unenguaji.
Lakini hali imekuwa tofauti hakuna kinachofanyika ndani ya TDMA kutokana na viongozi wake kukaa kimya bila kuanika mipango waliyonayo katika kukiendeleza chama na kurudisha hadhi ya muziki wa disco.
Jamvi hili linapata wasiwasi pengine chama hiki hakipo katika orodha ya vyama wanachama wa BASATA ambao wanapaswa kuwasilisha kalenda yao inayoonyesha mipango yao ya mwaka mzima ili wadau na wapenzi mbalimbali wa mashindano ya gisco waweze kujitolea kuyaandaa iwapo chama kinakabiliwa na ukata.
Ni wakati wa BASATA kuanza kuvikagua vyama vyake kuona vinatekeleza vipi majukumu kwa wanachama wao ambao wanahitaji kuona wanatekeleza kile ambacho wametumwa na watu waliowachagua, lakini pia ikiwezekana kuvifutia uanachama kwa kushindwa kuwajibika kwa wanachama wao.
Kwa leo nalikunja Jamvi nikikusihi tuwasiliane Ijumaa ijayo kwa habari zaidi za burudani na sanaa.
 
SAID MABERA ‘DOKTA': Miaka 38 Msondo Ngoma bila kuhama
ban.blank.jpg

Abdallah Menssah

amka2.gif
NINA hakika, kama kutatokea tuzo ya mwanamuziki aliyedumu katika bendi kwa muda mrefu, basi bila shaka tuzo hiyo itakwenda kwa mkongwe wa gitaa la solo, Said Mabera ‘Dokta'.
Hiyo inatokana na ukweli kwamba, kihistoria Mabera ndiye mwanamuziki pekee aliyedumu kukaa katika bendi moja kwa muda mrefu zaidi kuliko wanamuziki wote waliowahi kutokea hapa nchini.
Alijiunga na Msondo Ngoma wakati huo ilipokuwa ikijulikana kama ‘NUTA Jazz', mnamo mwaka 1972, baada ya kuombwa na marehemu Mnenge Ramadhani, aliyekuwa kiongozi wa bendi hiyo.
Mnenge na Mabera walikutana Kigoma nyumbani kwao ambako Mabera alikuwa amerudi mapumzikoni kupiga muziki baada ya kuitumikia Musoma Jazz kwa miaka mitatu, huku Mnenge akiwa likizoni.
Katika mazungumzo na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Mabera anasema kuwa, Mnenge alitumia fursa hiyo kumbembeleza waende naye jijini Dar es Salaam na kujiunga na NUTA.
"Nilivyokwenda jijini Dar es Salaam na Mnenge, kabla sijaajiriwa na NUTA, nilisafiri jijini Arusha nilipojiunga na Orchestra International iliyokuwa chini ya Amini Mussa," anasema Mabera.
Aidha, Mabera anasema kuwa miezi miwili baadaye alipata telegram kutoka katika uongozi wa NUTA, iliyokuwa ikimtaka arejee jijini Dar es Salaam kujiunga nao mara moja.
Anakumbuka siku yake ya kwanza kupanda katika jukwaa la Msondo ilikuwa ni Jumamosi, kwenye ukumbi wa Amana Social Club, Ilala alikokabidhiwa gitaa na kurindimisha vibao kadhaa.
Juni 3, mwaka 1973, aliajiriwa rasmi NUTA na kuanza kupakua vibao kadha wa kadha vikiwamo vile maarufu mno vya ‘Nisingekukimbia' pamoja na ‘Maisha ya Taabu'.
"NUTA ilivyobadili jina na kuwa JUWATA, nikatunga vibao viwili moto wa kuoteambali; ‘Uzuri si Shani' na Mwana Acha Wizi'," anafafanua Mabera.
Hata bendi hiyo ilipobadili tena jina na kuitwa OTTU, bado Mabera alionyesha cheche zake katika utunzi kwa kuipua kibao ‘Kifo cha Baba' kinachopatikana kwenye albamu ya ‘Binti Maringo'.
Hivi sasa, mkongwe huyo anatamba na kibao ‘Huna Shukrani', kikiwa ndicho kilichobeba albamu yao iliyoko sokoni hivi sasa, yenye nyimbo saba.
Je, kuna uhusiano wowote kati ya vibao vya Mabera na matukio ya kweli ya kimaisha yaliyowahi kumtokea yeye mwenyewe ama mtu mwingine anayemfahamu?
"Kusema kweli, ukiondoa kibao ‘Nisingekukimbia', nyimbo zangu nyingine zote ni matukio ya kubuni na hisia tu zinazonijia ninapokuwa nimetulia," anaweka wazi Mabera.
Kadhalika, Mabera anasema, katika vibao vyote alivyoshiriki kupiga, ni ‘Faurata' pekee kilichotungwa na Joseph Lusungu ndicho anachoona amejitahidi vilivyo kucharaza gitaa.
Akizungumzia mafanikio na tija aliyokwishaipata katika kazi ya muziki, hususan tangu alipokuwa na Msondo Ngoma, Mabera anasema kuwa amefaidika vya kutosha.
Anasema, muziki umemfanya kuishi maisha aliyokuwa akiyataka tangu alipokuwa mdogo, kumiliki nyumba, bendi maeneo ya Mburahati, jijini Dar es Salaam na kusomesha watoto wake.
"Mcharaza gitaa la solo mwenzangu pekee anayenivutia hapa nchini ni kijana Miraji Shakashia wa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta Sugu'," anasema Mabera.
Mabera anasema, kwa namna anavyovutiwa na Shakashia anayemtaja kuwa mwepesi katika upigaji na anayecharaza vema gitaa, yuko radhi amrithi nafasi yake Msondo Ngoma pindi atakapofariki dunia.
Anapotakiwa atoe maoni yake kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya, mwimbaji huyo aliwataka wasanii hao wajifunze zaidi kutumia ala badala ya wengi kutumbuiza kwa kutumia CD.
Mabera anasema kuwa msanii wa kweli ni yule anayeweza kupanda jukwaani na kutumbuiza laivu kwa ala za kupiga mwenyewe na si kutumia CD kwani alikufananisha na kuwaibia mashabiki.
Huyo ndiye Said Mabera aliyedumu Msondo Ngoma kwa zaidi ya miaka 38 bila kuhamia kwingine, na anayemudu kutumia ala zote za muziki wa dansi zikiwamo Tarumbeta na Saxophone.
Kihistoria amezaliwa mwaka 1949 mjini Kigoma na kupata elimu ya msingi katika Shule ya Government, hukohuko Kigoma katika Wilaya ya Ujiji, kuanzia mwaka 1958.
Alianza muziki mwaka 1961, kwa kujifunza gitaa maeneo ya Gungu, Kigoma ambako mwalimu aliyemfundisha alikuwa akipiga gitaa la solo kwenye bendi ya Lake Jazz iliyokuwa Ujiji Kigoma.
"Miaka miwili baadaye nilishajua kucharaza gitaa, mwaka 1967 nikajiunga na Lake Jazz kabla ya mwaka 1969 kutua Tabora Jazz Band iliyokuwa chini ya Mzee Mlekwa wakati huo," anasema.
Mwaka 1970 akaingia Musoma Jazz Band iliyokuwa ikiongozwa na mzee Matiku, na ambayo maskani yake yalikuwa Musoma, Mara, akaitumikia kwa takriban miezi 18.
Wakati akichengua katika dansi hapo Musoma Jazz, alikuwa pia akicheza mpira wa miguu katika timu ya Mara Spurs, ambako nafasi yake ilikuwa ni winga wa kushoto.
Mwaka 1972, aliamua kuacha muziki na kurejea nyumbani kwao Kigoma kabla hajakutana na Mnenge aliyemrudisha tena jukwaani kwa kusafiri naye hadi jijini Dar es Salaam na kumuunganishia NUTA Jazz.
 
Tunataka wasanii makini 2011
ban.blank.jpg

Khadija Kalili

amka2.gif
MU hali gani wapenzi wasomaji wangu wa safu hii adimu na adhimu kabisa ya ‘Busari la Wikiendi' iwajiayo kila wiki katika siku kama ya leo.
Ni matarajio yangu kuwa nyote ni wazima wa afya na siha, mkiwa mnaendelea vema na shughuli zenu za kila siku za kujitafutia riziki
kwa ajili yenu na familia zenu kwa ujumla.

Ama kwa wale ambao kwa namna hii ama ile, hawakubahatika kuamka salama usalimini, nawaombea kwa Mungu Mpate ahueni ili tuendelee kulisukuma gurudumu la maendeleo tukiwa wote.
Ndugu zangu, leo ni siku ya nane baada ya kutinga mwaka 2011 baada ya kuukaribisha Jumamosi iliyopita.
Kisanii, mwaka 2010 ulikuwa na changamoto nyingi na kemkemu, huku ukikabiliwa na vikwazo vya hapa na pale katika fani zote za muziki na maigizo.
Kiukweli, wasanii wetu walijitahidi kwa hali na mali kuhakikisha wanafanya kile kinachotarajiwa na jamii inayowazunguka ambacho si kingine bali ni elimu na burudani.
Na bila shaka wenye macho tuliweza kushuhudia kila kizuri ambacho ni matunda ya jitihada za wasanii wetu mbalimbali hapa nchini.
Nyimbo pamoja na filamu nyingi zenye ujumbe, elimu pamoja na burudani maridhawa zilipakuliwa na kuwekwa mbele ya walaji ambao ni hadhira.
Bila kuficha kitu, mwaka jana ulijaa kashikashi na hekaheka za kiburudani, hasa kwetu sisi wadau, mashabiki na wapenzi wa fani ya muziki pamoja na filamu.
Labda nichukue fursa hii kuwapongeza wale wote ambao hata wenyewe wanajijua kuwa wamejitahidi vya kutosha katika kuwaletea raha na msisimko mashabiki wao.
Kuwataja hapa itakuwa ni sawa na kuwavunja moyo wengine ambao kwa namna moja ama nyingine hawakufanikiwa kutimiza malengo yao katika kukata kiu ya mashabiki.
Ila sina shaka wenyewe wanajijua na hata mashabiki nao pia wanawatambua kupitia ‘utamu' wa kazi zao walizozipakua na kufanikiwa kukonga nyoyo zao.
Hata hivyo, nachukua fursa hii kuwataka wasanii ambao hawakufanya vema katika mwaka huu uliomalizika siku nane zilizopita, kukaza buti na kuzidisha juhudi katika mwaka huu.
Kwa sababu, nia yetu Watanzania wote wapenda burudani ni kuhakikisha sanaa hapa Bongo inasonga mbele haraka na kila uchao.
tusipofanya hivyo hatuwezi kusonga mbele na kupiga hatua kama kuna baadhi yetu katika kundi la sanaa bado wana kasi dhaifu katika kusaka mafanikio.
Tujitahidi jamani mwaka huu ulioanza hivi karibuni kwa sababu pamoja na kuwa sanaa ni burudani na starehe, kadhalika pia ni kazi inayotegemewa na wengi katika kukimu majukumu waliyonayo.
Tunachokingoja wengi wetu mwaka 2011 ni kuona wasanii wetu mnapiga hatua zaidi na kazi zenu kuonekana hadi nje ya taifa na Bara la Afrika.
Ndiyo maana nikaeleza na kusisitiza zaidi kuwa mwaka mpya 2011 tunahitaji wasanii makini zaidi watakaotusaidia kujenga jamii makini ya sanaa.
 
Kukata tamaa katika sanaa ni udhaifu
ban.blank.jpg

Abdallah Menssah

amka2.gif
MAMBO vipi msomaji wangu wa safu hii murua na maridadi kabisa ya ‘Kijiwe cha Burudani?' Sina shaka u - mzima wa afya Ijumaa hii unapolikamata gazeti la Tanzania Daima ukitaradadi nalo taratibu.
Kwa upande wangu, nachukua fursa hii kumshukuru Mtukufu Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha mimi pamoja na ninyi wenzangu kumaliza mwaka 2010 na kuuona mwaka mpya 2011 kwa furaha na faraja ya hali ya juu, tukiwa salama salimini.
Leo ikiwa ni siku ya saba tangu tuuanze mwaka huu mpya, nimepanga kuzungumzia namna ya umuhimu wa wasanii pamoja na wanamuziki wetu wote hapa nchini kuwa ngangari katika kusaka kwa nguvu zote mafanikio ya kimuziki.
Unajua, kuna baadhi ya watu hapa ulimwenguni wanamfananisha msanii na mwanamuziki na askari, huku pia wakiilinganisha sanaa na jeshi kakamavu kutokana na namna mazingira yake na jinsi yanavyopatikana mafanikio katika fani hiyo kwa wasanii husika.
Kwasababu hadi kufikia mafanikio, wasanii wengi huanzia taabu na mashaka tele, ambako kwa wale wenye mioyo laini isiyoweza kustaamili taabu na mashaka hayo, hujikuta wakikata tamaa mapema na kugeukia shughuli nyingine.
Tunayo mifano mingi ya wasanii na wanamuziki ambao kutokana na kutaabika na kusota mno katika sanaa kwa muda mrefu bila mafanikio, wameamua kuachana nayo na aidha kuwa wajasiriamali ama waajiriwa katika kazi nyingine kwenye sekta tofauti.
Lakini kuna wengine wale ambao kwa namna hii ama ile, waliyachukulia mataabiko pamoja na misoto ya kisanaa kuwa ni sawa na mafunzo ya kijeshi msituni, ambako hatimaye sasa wamejikuta wakianza kula matunda ya uvumilivu wao huo.
Wapo wasanii wengi mno, ila mmojawapo anayeweza kuwa kielelezo cha wasanii wastaamilivu ni yule anayejulikana kama Hamis Mohammed Tambiko ‘Unyayo' anayetamba sasa kwenye vituo mbalimbali vya radio na kibao chake kipya kiitwacho ‘Enemy'.
Unyayo aliyeanza sanaa mwanzoni mwa miaka 2000, alishasota sana kutafuta kutoka bila mafanikio, ambako hatimaye hivi sasa ameanza kujikuta akifuta jasho la faraja kwa baadhi ya vibao vyake kukubalika kwa mashabiki pamoja na wapenzi wa muziki.
Kibao cha kwanza cha mkali huyu kilikuwa kinakwenda kwa jina la ‘Nieleze' alichomshirikisha Chelea Man, ambacho alikuwa amekirekodia Studio ya Tip Top Records chini ya Mtayarishaji anayefahamika zaidi kwa jina moja tu la Kaju.
Baada ya hapo akaibuka na rekodi nyingi ambazo nyingine hakuwahi hata kuzisambaza katika vituo vya radio kwa utambulisho kutokana na sababu mbalimbali huku kubwa ikiwa ni ukosefu wa fedha za kutosha kuendeshea shughuli hizo.
Kibao chake hiki kipya cha ‘Enemy' kilichobeba ujumbe mzito kwa jamii, ndicho hasa kilichoanza kufufua matumaini yake ya kukubalika kwa mashabiki wa muziki kutokana na kufikia hatua ya kushika nafasi za juu katika chati mbalimbali kwenye vituo kadhaa vya radio.
Mwenyewe, Unyayo baada ya kuona mashabiki pamoja na wapenzi wameanza kumuitika, ameanza mikakati ya kuandaa albamu yake ya kwanza ambayo amepanga kuifyatua baadaye mwaka huu ikiwa na vibao tisa, vyote vikiwa moto wa kuoteambali.
Hii inafundisha jambo moja zuri kwa wasanii na wanamuziki wetu wote hapa nchini. Nalo ni kuwa, hakuna ajuaye siku ambayo nyota yake ya kisanii itachomoza na kung'aa zaidi kiasi cha kutokea kuwa gumzo kwa watu mbalimbali.
Kwasababu kama rafiki yangu Unyayo aliyekuwa akijiita Zidi huko nyuma, angelikata tamaa mapema, saa hizi asingekuwa na kibao kinachopigwa radioni ama kama mwenyewe anavyopenda kusema, asingekuwa akishobokewa na masista duu.
Unajua Mungu ndiye ajuae na apangaye yote kwa wote. Hii ina maana kuwa, pengine wewe mwenyewe hufahamu kama nyimbo zako ni mbaya ndiyo maana hazipati fursa ya kuteka ndewe za masikio ya mashabiki pamoja na wapenzi wa muziki.
Uvumilivu ndiyo ngao, nguzo na mhimili pekee unaostahili katika sanaa, ama pengine kwenye sekta nyingine zote za kikazi pamoja na majukumu mbalimbali ya kijamii, si katika sanaa tu pekee kwasababu asiye mvumilivu hawezi kula mbivu.
Lazima kila msanii na mwanamuziki akaze buti ili kuyafikia mafanikio ya kweli katika sanaa kwani bila ya hivyo hatutapiga hatua kamwe. Kwa leo naishia hapo, tukutane tena Ijumaa ijayo na kwavile hatujaonana tangu mwaka huu mpya uanze, basi nawatakia kila la heri katika mwaka 2011.
Wadau wangu wa Kijiweni leo hii ni Said Makorokoto, Shaaban Salum ‘Shebby Shiner', ‘Abdul Latino ‘LN', Amir Ally ‘Cool Boy', Noel Nole, Juma Kipanya, Ikota Mhamila, Dogo Baraka ‘Jembe', Bilsan Hemed, Asha Salum na Ben Mtwanga.
Wengine ni Yahya Rajab ‘Westi', Mohammed Mtwale, George Nelson, Super Shomy, Mariam Said, Jastin Isaya, Big Raja, Ahmed Balozi, Azizi Gumgum, Mohmmed Imonje, Mussa Yunus, Mkubwa Mameke, Sina Mohammed, Omary Tambiko.
Kadhalika kuna Seif Kitambulilo, Martin Huruma, Mwarami Yahya, Mbwana Twaha, Dullah Chiki, Idd Omary, Suleiman Tupa, Mbaraka Ramadhan, Amir Babu na Ubaya Said pamoja na Super D Mnyamwezi anayetujengea heshima mimi na wewe kwa kutuuzia dawa kabambe ya Inzoy.
 
Shindano la kuibua nyota wapya wa muziki laja
Monday, 06 December 2010 21:27

Zaina Malongo
SHINDANO maarufu la kusaka wanamuziki nyota wapya wa muziki wa dansi linatarajiwa kufanyika mwakani nchini kote.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa shindano hilo, Suleiman Matthew ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Makukwe Entertaiment alisema lengo lao ni kusaka vijana wapya wenye uwezo wa kuimba muziki wa dansi.

Kama walivyokuwa Dk Remmy Ongala (ambaye kwa sasa anaumwa), Hassan Rehani 'Bitchuka', Mzee Makassy, Muhidin Gurumo (pia ni mgonjwa) au kina Marijani Shaaban, John Kijiko na Mbaraka Mwinshehe (marehemu).

"Kuna vijana wengi wanapenda kuwa wanamuziki, lakini ni wachache wanaotambua aina ya muziki ambao wanaufanya kwa amaani hiyo tumeamua kuwakutanisha vijana kwa njia ya shindano la kusaka vipaji,"alisema Matthew

Matthew, ambaye ni mwanamichezo mstaafu nchini alisema kuimba muziki ni jambo dogo, lakini ugumu wake unakuja kuwa pale ni muziki gani unaoimbwa na kama unakubalika kwa watu.

Alisema shindano hilo litafanyika katika hatua ya kwanza au mchujo Desemba 21 na itawahusisha vijana wa Dar es Salaam pekee.

Alisema wameamua kuanzia Dar es Salaam ambapo kwa hatua ya pili kama tutapata wadhamini wataenda mikoani.
 
Rare Abidal goal puts Barcelona into last eight of Spanish Cup

January 5, 2011 -- Updated 2332 GMT (0732 HKT)

t1larg.abi.gi.jpg

Eric Abidal, right, celebrates after coming on to score Barcelona's crucial away goal against Athletic Bilbao.

STORY HIGHLIGHTS

  • Barcelona reach Spanish Cup quarterfinals on away goals after 1-1 draw at Athletic Bilbao
  • Substitute Eric Abidal scores the second goal of his career to put visitors ahead
  • Holders Sevilla go through 8-3 on aggregate after beating Malaga 3-0
  • Deportivo La Coruna beat second division Cordoba 3-1 in extra-time


RELATED TOPICS



(CNN) -- Barcelona battled into the quarterfinals of the Copa Del Rey on Wednesday night as veteran French defender Eric Abidal scored his first goal for the Spanish champions in a 1-1 draw at Athletic Bilbao.
Pep Guardiola's team set up a clash with either La Liga rivals Getafe or second division Real Betis after winning on away goals following the 0-0 draw at the Camp Nou last month.
The 31-year-old Abidal, who was brought on as a second-half substitute, netted only the second goal of his career in the 75th minute to leave Bilbao needing two goals to go through.
The left-back sidefooted home after Xavi marked his record-breaking 550th appearance for Barcelona with a trademark pass to the feet of the recalled Lionel Messi, who guided the ball into Abidal's path.
Xavi equals record as Pedro double puts Barcelona further ahead
The Basques threatened to take the match into extra-time when Spain striker Fernando Llorente continued his fine scoring run with an 85th-minute equalizer, but Barcelona held on.
"When I get a chance like that, I shoot. Now I hope to score more this season," Abidal told AFP.
Defending champions Sevilla cruised into the last eight with an 8-3 aggregate victory over La Liga rivals Malaga, winning 3-0 in the away leg.
Ivory Coast midfielder Ndri Romaric scored the opener with a deflected freekick six minutes after halftime, then substitute Diego Perotti made it 2-0 before Malaga defender Weligton was sent off for a second booking and Brazil striker Luis Fabiano netted late with another setpiece.
What were the top sporting moments of 2010?
Sevilla will next play either Villarreal or Valencia, who meet on Thursday following a 0-0 first-leg draw.
Top-flight team Deportivo La Coruna needed extra-time before ending the hopes of second division Cordoba as Adrian scored a hat-trick in a 3-1 win.
The Spain under-21 international's treble ultimately gave the Galicians a 4-2 aggregate victory, but he needed to convert a penalty late in regulation time to stop his side crashing out after David Arteaga struck in the 86th minute.
Cordoba collapsed after Miguel Angel Tena was sent off in extra-time as Deportivo set up a clash with either Mallorca or Almeria, who lead 4-3.
Real Madrid also play on Thursday, holding an 8-0 advantage over Levante, while last season's runners-up Atletico Madrid take a 1-0 lead to Espanyol.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom