Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Tanzania yatupwa tena kwa Uganda Tuesday, 14 December 2010 21:18

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Sunday Kayuni.

Allan Goshashy
WAKATI Shirikisho la Soka Afrika CAF) limetoa ratiba ya mechi ya kufuzu kushiriki michezo ya 10, ya Afrika mwakani ambapo Tanzania imepangwa dhidi ya Uganda, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema halina taarifa ya ratiba hiyo.

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Sunday Kayuni, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ufundi alisema jana alipoulizwa kuhusu ratiba hiyo kwamba shirikisho lake bado halijapata taarifa za ratiba hiyo na akakisisitiza kwamba wakiipata wataitolea tamko rasmi lakini baada ya kuijadili.

Lakini, kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jana na CAF, Tanzania kwa upande wa wanaume katika soka ambapo hushiriki timu ya vijana chini ya miaka 23, Ngorongoro Heroes, imepangiwa kucheza na Uganda katika raundi ya kwanza kati ya Aprili 15 na 17, 2011.

Michezo ya Afrika inatarajiwa kufanyika mjini Maputo, Msumbiji kuanzia Septemba 3-18, mwakani, ambapo hatua ya kutafuta timu nane zitakazoshiriki michezo hiyo inaanza Januari kwa hatua za awali na itaendelea hadi Julai.

Ratiba hiyo ambayo Mwananchi imepata nakala yake inaonyesha kuwa vijana wa Tanzania na Uganda watacheza mchezo wa marudiano kati ya Aprili 29 na Mei Mosi na mshindi atacheza na mshindi wa mechi baina ya Kenya na Eritrea katika raundi ya pili, kati ya Juni 22-26 na marudiano kuwa 08-10, Julai, 2010.

Ili kupata timu nane zitakazoshiriki michuano ya soka katika michezo hiyo ya Afrika, CAF imetenga kanda saba ambazo zitawakilishwa na timu moja moja ambazo zitaungana na mwenyeji, Msumbiji katika fainali ya michezo hiyo.

Kanda hizo ni:

Kanda I: Algeria, Libya.
Kanda II: Guinea, Guinea Bissau, Mali na Senegal.
Kanda III: Benin, Ghana, Liberia na Nigeria.
Kanda IV: Cameroon, Congo RD na Gabon.
Kanda V: Eritrea, Kenya, Uganda na Tanzania.
Kanda VI: Angola, Botswana, Lesotho, Malawi, Namibia, Swaziland, Zambia, Zimbabwe
Kanda VII: Madagascar, Seychelles

Kwa upande wa wanawake, Tanzania imepangiwa kucheza raundi ya kwanza kati ya Aprili 29-Mei 1 na mshindi wa mechi ya awali kati ya Kenya dhidi ya Sudan.

Ratiba hiyo ya CAF inaonyesha kuwa timu ya Tanzania ya wanawake itacheza mechi ya marudiano kati ya Mei 13-15, 2011.

Michezo hiyo ya Afrika kwa mara ya kwanza ilifanyika mwaka 1965 mjini Brazzaville,Congo, ambapo hufanyika kila baada ya miaka minne.

Katika michezo hiyo ya Afrika, michezo 30 hushindaniwa huku Misri ikiwa inaongoza kwa kutwaa medali nyingi tangu kuanza kwa michezo hiyo wakati Tanzania inashika nafasi ya 21 kwa kutwaa medali kati ya nchi 47.

 
Simba, Yanga zaunganisha nguvu Afrika
Tuesday, 14 December 2010 21:11

Clara Alphonce

HATIMAYE klabu kongwe za Simba na Yanga zimeamua kuunganisha nguvu ili kuhakikisha zinafanya vizuri katika michezo ya kimataifa na kuondoa aibu ya kufungwa mara kwa mara.

Makubaliano hayo yalifikiwa wakati viongozi hao walipokutana juzi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kula chakula cha mchana.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Simba, Cliford Ndimbo, alisema baada ya kuona timu hizo zinashindwa kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho wameona ni vema wakaungana ili waweze kupeana ushauri na mawazo.

"Tumeona ni vema tukianzisha undugu katika michuano hii ya kimataifa lengo letu ni kuhakikisha tunafanya vizuri, Simba wakiwakilisha nchi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na Yanga Kombe la Shirikisho (CAF)," alisema Ndimbo.

Alisema pia wanawataka na mashabiki wote wa Simba na Yanga kuwa na ushirikiano pale kila timu itakapokuwa ikicheza, ili kuwapa sapoti wachezaji na tabia ya kuzomeana isiwepo.

Ndimbo alisema katika mechi za Ligi Kuu Usimba na Uyanga utaendelea kama kawaida kutokana na upinzani mkali uliopo kwa timu hizo.

Pia klabu hizo mbili zimewapongeza viongozi wapya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Katibu Mkuu Angetile Oseah na Afisa habari wa shirikisho hilo Boniface Wambura.

"Tunaimani viongozi hawa watatoa ushirikiano kwenye klabu zetu hasa katika suala zima la mapato ambalo limekuwa likilalamikiwa sana," alisema Ndimbo.

Wakati huo huo viongozi wa Simba na Yanga wameendelea kuhangaikia Uwanja wa taifa au Uhuru ili waweze kutumia kwenye mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara mzunguko wa pili.

Sendeu alisema wanapokuwa wanachezea mikoani huwa wanatumia gharama nyingi tofauti na wanavyokuwa hapa Dar es Salaam.
 
Kikwete aelekea RT
Tuesday, 14 December 2010 21:09

Imani Makongoro
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kukutana na viongozi wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) mapema Januari kuzungumza nao juu ya rekodi mbaya ya wanaridha wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa.

Akizungumza Ikulu, Rais Kikwete alisema kuwa rekodi ya mchezo huo hapa nchini iko chini na haionyeshi kiwango kizuri kama ilivyokuwa miaka ya 1970 hadi1980 enzi za Filbert Bayi, Juma Ikangaa na Suleiman Nyambui walifanya vema katika mashindano ya kimataifa.

Wengine walioiwakilisha vema Tanzania na kuiweka katika ramani ya Dunia kupitia michezo miaka hiyo ni Girdamis Shahanga, Mosi Ali, Nzael Kyomo, Cleva Kamanya na Simon Robert Naali

"Kwa nini tunashindwa kung'ara katika mashindano ya kimataifa na kuishia kuwa wasindikizaji kila siku, nitakutana nao na kujadiliana kwa undani juu ya jambo hili", alisema Rais.

Kikwete alisema kuwa Serikali inahakikisha rekodi ya michezo hapa nchini inakwenda kama ilivyopangwa na kuiweka Tanzania katika kiwango kinachotakiwa ambapo tayari imeleta makocha kutoka Cuba kwa ajili ya kuwafundisha wanamichezo hao, lakini wanashindwa kufanya vema katika mashindano ya kimataifa.

Michezo mingine ambayo serikali imeiunga mkono kwa kulipia makocha ni Mpira wa Miguu, Netiboli, Ngumi za Ridhaa na Judo.

Tanzania haikupata medali hata moja katika mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyomalizika Oktoba mjini New Delhi, India, kama ilivyokuwa kwa nchi za Kenya na Uganda
 
Wenger aponda hali ya dimba la Old Trafford Tuesday, 14 December 2010 21:06

MANCHESTER, Uingereza
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger ameuponda Uwanja wa Old Trafford kwamba si mzuri na haufai kuchezea soka ya kuvutia.

Kauli hiyo ilitolewa mufa mfupi baada ya kuishuhudia timu yake ikifungwa 1-0 juzi usiku na Manchester United na kuondolewa kileleni mwa Ligi Kuu ya England.

Katika mchezo huo, klabu hiyo ya London ilishindwa kuonyesha cheche na soka yake ya kitabuni ya kushambulia zaidi na kwa muda mrefu.

"Tumeona makosa ya kiufundi kwenye timu zote mbili, lakini hayo ni matokeo ya uduni wa uwanja ambao umetuzuia kucheza soka ya kuvutia," alieleza Wenger baada ya mchezo huo . " Umejaa mabonde, yanaufanya mpira usitulie na pia ulikuwa na utelezi."

Wenger, ambaye mara kadhaa ameshindwa kuonana uso kwa uso na mpinzani wake wa Man United, Alex Ferguson, alikataa kuingia katika vita ya maneno kabla ya mchezo huo, ingawa alieleza kuwa matokeo hayo hayakuwa ya kukatisha tamaa.

"Kiufundi, uchezaji wa timu zote mbili ulikuwa wa wastani kwa sababu ya hali ya dimba ambayo kwa mtazamo wangu si nzuri, kiasi kwamba imeathiri mchezo kwa kiasi kikubwa," alisema.

"Kama nitaulizwa kama dimba ni mzuri au mbaya, unataka niseme nini?"

Alisema watumishi wa uwanja huo waliumwagia maji kabla ya mchezo na wachezaji kadhaa walianguka, ingawa ukuta na sehemu imara ya kiungo ya Man United iliyoundwa na watu watano na wepesi wa chipukizi Rafael aliyezuia krosi zetu wamechangia kushindwa kwetu.

Kabla ya kuanza kwa mchezo huo, beki wa United Patrice Evra aliwaita wachezaji wa Arsenal kuwa ni "kituo cha mafunzo", akieleza kuwa wanachezea mpira kwa kiasi kikubwa, lakini si miongoni mwa timu zinazowania taji la ubingwa.

Kwa jumla, mchezo wa kuvutia uliozoeleka wa Arsenal ulikosekana juzi usiku, lakini Wenger alieleza kuwa hana hakika matokeo hayo yana maana gani kwa timu yake ambayo haijashinda taji tangu mwaka 2004.

"Ni matokeo ya kukatisha tamaa, tumekata tamaa sana, lakini kitu muhimu kwetu ni kwenye mchezo ujao tupate matokeo mazuri ," alisema kocha huyo Mfaransa. "Kwa jumla, kutokana na hiki nilichokiona leo, hakuna sababu ya kutojiamini . Tumeonyesha kuwa imara kwa jumla."

Naye Ferguson alieleza kuwa walistahili kushinda kwa mabao zaidi, kama si kukosa nafasi nyingi za kufanya hivyo.

Alisifu safu yake ya ulinzi kwa kuweza kuwazima washambuliaji wa Arsenal na sehemu ya kiungo kwa kuwazuia kucheza mchezo wao wa kawaida wa pasi za haraka, kasi.

Wakati huohuo, beki chipukizi wa England, Kerrea Gilbert amefuata nyayo za David Beckham kwa kujiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS), Portland Timbers.

Gilbert, 23, ambaye ameichezea Arsenal kwa miaka mitano amekulia England akiwa katika shule ya soka ya klabu hiyo.
Alicheza kwa mkopo kwenye klabu kadhaa za madaraja tofauti nchini mwake.

Klabu hiyo ya Timbers, ambayo itacheza MLS msimu ujao, imemsajili beki huyo kwa lengo la kujiimarisha na kumpa mkataba wa miaka minne.
 
Blater asema hakutakuwa na ubaguzi Qatar 2022
Tuesday, 14 December 2010 21:05

JO'BURG, Afrika Kusini
RAIS wa Shirikisho la Soka la Kimataifa, Fifa, Sepp Blatter ameeleza imani yake kwa nchi ya Qatar kwamba haitakuwa na tatizo la ubaguzi wa kidini na kijamii wakati wa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022.


Blatter, ambaye alikuwa akizungumza mjini Johannesburg, Afrika Kusini wakati wa mkutano wa kupitia fainali za mwaka huu za Kombe la Dunia amekuwa akikosolewa kwa uamuzi wake kuipa nchi hiyo ndogo ya Kiarabu fainali hizo kubwa za soka duniani.

Lakini, yeye amekuwa akieleza kuwa ni uamuzi sahihi kuandaa fainali hizo Mashariki ya Kati kwa mara ya kwanza katika historia ya soka duniani.

Mbali ya joto kali katika eneo hilo wakati wa kiangazi ambako fainali hizo hufanyika, kumekuwa na hisia kwamba kufanyika kwa fainali hizo katika nchi ya Kiislamu kunaweza kusababiasha matatizo.

Sheria za nchi hiyo zinazuia unywaji wa pombe hadharani, huku baa na klabu za usiku hazipo katika nchi hiyo. Suala jingine ni lile la jamii ambako makundi ya mashoga yanahofu kuwa wanachaa wake watazuiwa kuingia katika nchi ambako ngono za jinsi moja pia haziruhusiwi.

Alipoulizwa kuhusu masuala kama hayo, Blatter alijibu kwanza kwa utani: "Nitafurahi kuona watu wakiacha vitendo vyote vya ngono.''

Lakini, akaongeza: "Kwa jumla, tunaishi katika ulimwengu huru na nina hakika kwamba wakati wa fainali hizo za Qatar 2022, hakutakuwa na matatizo.

"Unaona, ukiwa Mashariki ya Kati, mila nyingine kama hizi za unywaji pombe, ushoga ni ngeni, ni kinyume na imani yao, lakini, katika soka hakuna mipaka.

"Tupo wazi kwa kila kitu na kila mtu, ninaamini hakutakuwa na ubaguzi wowote kwa binadamu , iwe kushoto au kulia, mambo yatakuwa safi.

"Kama watu watapenda kuona mechi za soka za Qatar 2022, nina hakika wataruhusiwa kufanya hivyo .''
 
Serengeti Boys yaenda Rwanda Tuesday, 14 December 2010 21:03

Sweetbert Lukonge na Calvin Kiwia
TIMU ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti Boys inatarajia kuondoka jijini Dar es Salaam kesho kuelekea nchini Rwanda kushiriki mashindano Maalumu ya Vijana yaliyoandaliwa na shirikisho la soka la nchi ya Rwanda yatakayoanza kutimua vumbi keshokutwa Jumamosi mjini Kigali.

Akizungumza na Mwananchi jana jijini Dar es Salaam kocha mkuu wa timu hiyo Jamhuri Kihwelo alisema kuwa maandalizi ya michuano hiyo inayofahamika kama Mashindano Maalum ya vijana U-17 yanaendelea vizuri na anamshukuru Mungu kwani vijana aliwachagua ni wazuri na wenye vipaji.

"Vijana tuliowachagua ni wazuri na wenye vipaji, suala la umri tumelizingatia sana tunaamini hakuna aliyedanyanga umri wake," alisema Julio.

Alisema kikosi hicho wamekichagua kutoka kwenye timu za vijana za Simba, Yanga, Mtibwa, Azam na kituo cha kulea vipaji cha Tanzania Soccer Academy (TSA).

Aliongeza kuwa timu hiyo itaondoka nchini kwesho na msafara wa idadi ya watu 25 ukiwa na wachezaji 18 na viongozi saba kuelekea mjini Kigali.

Alitaja timu ambazo zimealikwa kwenye mashindano hayo katika ukanda huu wa Afrika mashariki kuwa ni Kenya, Uganda, Burundi naTanzania.
 
Pazia la Umitashumta lafunguliwa Tuesday, 14 December 2010 21:04

Julieth Ngarabali,Kibaha.
MICHUANO ya umoja wa michezo na taaluma kwa shule za msingi nchini(UMITASHUMTA) yamefunguliwa rasmi jana wilaya Kibaha mkoani Pwani na Serikali kutoa wito wa kuimarishwa kwa vyuo vya Malya na Butimba.

Lengo la kuimarisha elimu hiyo hapa nchini ili kupata wakufunzi bora wa michezo ya aina mbalimbali ambao wataweza kusambazwa katika shule na kuwafundisha vijana wakiwa na umri mdogo.

Wito huo umetolewa jana wilayani hapa na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na Serikali za mitaa Kapteni mstaafu George Mkuchika wakati akifungua mashindano ya UMITASHUMTA katika viwanja vya shirika la elimu Kibaha.

Mkuchika alisema ili kuboresha na kuinua viwango vya michezo nchini hakuna budi kuwepo na walimu wengi ambao wana taaluma za michezo wanaokwenda na wakati uliopo.

"Natumia fursa hii kutoa wito kwa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi pamoja na wizara ya habari,utamaduni na maendeleo ya vijana kuhakikisha kuwa inaimarisha elimu na taaluma ya michezo ambayo imekuwa ikitolewa katika vyuo viwili vya Malya na Butimba lengo likiwa ni kuliwezesha taifa kuwa na walimu na wataalamu mahiri wa michezo," alisema na kuongeza

"Na pia ningependa kupata taarifa mwaka ujao juu ya idadi ya wataalamu waliofuzu kozi mbalimbali kutoka kwenye vyuo hivyo nilivyovitaja."

Katika ufunguzi huo pia Mkuchika alizitaka halmashauri za wilaya na viongozi wa mikoa kupeleka walimu wa michezo katika mafunzo mbalimbali ya michezo ili kuwezesha mashindano hayo kushirikisha michezo mingi zaidi na taaluma kadri itakavyowezekana.

Alisema si vema taaluma hii ya michezo ikawa inatolewa na kila mtu tu ili mradi ni mwalimu katika shule fulani kwani michezo ni fani ambayo ina ubunifu wake, inakwenda na wakati na pia ni sehemu ya ajira.

Awali Katibu mkuu TAMISEMI, Maimuna Tarishi alisema lengo kuu la mashindano hayo ya UMITASHUMTA ni kuibua na kujenga vipaji ambavyo vitawawezesha kuboresha elimu ya msingi na kuondoa vikwazo vinavyoathiri uendeshaji wa elimu kwa ujumla.

Mashindano yatafanyika kwa siku saba na kwamba imeshirikisha wanamichezo 620 kutoka katika mikoa 11 ya Arusha, Singida,Tabora,Tanga, Iringa, Kilimanjaro, Mbeya, Morogoro, Dodoma, Dar esalaam na wenyeji Pwani.

Kati ya wanamichezo hao wavulana ni 355 na wasichana 265 huku wana michezo wenye mahitaji maalumu (wenye ulemavu) ni 47 kutoka mikoa ya Tabora na Dar es Salaam, viongozi wa wana michezo 113 wanaume wakiwa ni 69 na wana wake 45 na wametoka katika mikoa hiyo 11.

Michezo hiyo ya wiki moja ni ya majaribio baada ya aliyekuwa Waziri wa Elimu Joseph Mungai kuifutilie mwaka 2000 kwa madai ya kushusha kiwango cha elimu.
 
Simba, Yanga zafunga 'ndoa'


na Dina Ismail


KLABU za soka za Simba na Yanga zimeazimia kushirikiana katika michuano ya kimataifa wakati timu hizo zitakapoanza kampeni ya kushiriki michuano hiyo. Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana na wasemaji wa klabu hizo, Clifford Ndimbo (Simba), na Louis Sendeu (Yanga), walipozungumza na waandishi wa habari.
Walisema, wakati umefika kwa wadau wa klabu hizo kushirikiana na hasa ikizingatiwa hivi karibuni wadau hao waliweza kuzihamashisha timu za Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars' na Zanzibar ‘Zanzibar Heroes' katika michuano ya Chalenji.
Katika michuano hiyo iliyomalizika hivi karibuni, Kilimanjaro Stars ilitwaa ubingwa, ambapo wasemaji hao walisema hatua hiyo ni fundisho katika michuano ya kimataifa kwa kujenga umoja na ushirikiano.
"Wakati umefika wa kuleta mapinduzi ya soka hapa nchini wakati timu zetu zitakapopeperusha bendera ya nchi katika michuaano mbalimbali ya kimataifa. Ule wakati wa kuzisaidia timu pinzani kutoka nje ya nchi wakati wa michuano ya kimataifa uwe umemalizika, kwani mabadiliko yaliyopo hivi sasa timu inayowakilisha nchi inapoingia raundi ya tatu uwezekano wa kuongeza timu nyingine katika uwakilikishi umeongezwa," alisema Ndimbo.
Aidha, wasemaji hao walisema ni lazima kuweka uzalendo mbele, badala ya kuwekeana fitina katika michuano ya kimataifa huku suala la upinzani katika ligi za ndani na michuano ya ndani libaki kama lililivyo.
Ikumbukwe kuwa timu hizo zina uhasimu wa jadi hapa nchini, ambapo pindi mojawapo ikishiriki michuano ya kimataifa mashabiki huamua kushangilia timu za kigeni!
 
Kimeeleweka Chalenji 2011 Dar


na Juma Kasesa


HATIMAYE Baraza la Vyama vya Soka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), limeipa baraka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuandaa michuano ya Tusker Chalenji jijini Dar es Salaam mwakani. Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye, alisema, baada ya kushauriana na wadhamini wa mashindano hayo, wamekubaliana kuwa michuano hiyo ifanyike tena jijini.
Alisema, hamasa kubwa iliyoonyeshwa na mashabiki wa soka wa Tanzania katika michuano hiyo mwaka huu, imechangia kwa Tanzania kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo ambayo ilimalizika hivi karibuni kwa Kilimanjaro Stars kutwaa kombe hilo baada ya kulikosa kwa miaka 16.
Alisema, wanatarajia kuwa michuano ya mwakani itakuwa bora kushinda ya mwaka huu na kuwashukuru Watanzania kwa namna walivyoweza kujitokeza kwa wingi jambo lililoipa msisimko.
 
Togo waitaka Zanzibar Heroes


na Makuburi Ally


CHAMA cha Soka cha Togo (TFF), kimetuma maombi ya mechi ya kimataifa ya kirafiki na Zanzibar Heroes kwa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA). Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu kutoka Zanzibar jana, Katibu Mwenezi wa ZFA, Maulid Hamad Maulid, alisema, Kamati ya Utendaji ya ZFA imeketi na kujadili taratibu za mchezo huo, ambapo watawasilisha taarifa zaidi kwa TFF.
Maulid alisema, mbali ya Togo pia timu ya Taifa ya Ivory Coast imetuma maombi ya kucheza na Zanzibar, huku pia wakijipanga kucheza mchezo wa tatu dhidi ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars' ikiwa ni kwa ajili ya kuiweka sawa timu hiyo.
Aidha, Maulid aliongeza, kampuni ya Vannedrick, ambayo kati ya viongozi wake ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela, na Future Century Limited, zimetangaza kudhamini michuano ya kuwania Kombe la Kagame inayotarajia kuanza Mei mwakani.
Alisema, sambamba na kudhamini mashindano hayo pia kampuni hizo zimetangaza kudhamini Ligi Kuu ya Zanzibar kwa ahadi ya kutoa vifaa, nauli na zawadi za washindi wa mashindano hayo ambapo wameiomba ZFA kuandaa bajeti yake ya mashindano hayo.
Kuhusu suala la kocha wao mkuu wa Zanzibar Heroes, Hall Stewart, alisema kwamba hadi sasa hajawasilisha taarifa za kuvunja mkataba kwamba anakwenda Azam FC.
 
JK kuwaweka kikaangoni riadha Tanzania


na Juma Kasesa


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwaweka kiti moto viongozi wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), kutokana na kushindwa kwao kuzalisha vipaji vya wanariadha wenye uwezo kama walivyokuwa navyo kina Filbert Bayi, Juma Ikangaa na wengineo. Rais Kikwete alitoa kauli hiyo juzi jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchana na kukabidhiwa kombe na wachezaji wa timu ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars' iliyofanyika Ikulu.
Rais Kikwete alisema, ameshangazwa na RT kushindwa kuzalisha wachezaji wenye vipaji, wakati serikali ilikwishatatua kilio chao cha kukosa kocha wa kigeni ambaye atawasaidia katika kufanikisha azma hiyo, huku serikali yake ikiwa imeisharudisha michezo mashuleni kwa ajili ya kusaidia kupatikana kwa wachezaji hao.
"Nataka nikutane nao ili waniambie tatizo nini mpaka wanashindwa kutuibulia wachezaji wenye vipaji kama kina Juma Ikangaa na Filbert Bayi, ambao waliweza kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia mchezo wa riadha," alisema Rais Kikwete.
Kauli ya Kikwete imekuja siku chache baada ya Kilimanjaro Stars inayofundishwa na Mdenish Jan Poulsen kutwaa Kombe la Tusker Chalenji Cup ambalo Tanzania ilikuwa inalisaka kwa miaka 16 bila mafanikio mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kuifunga Ivory Coast ‘Tembo wa Pwani' bao 1-0.
Aliongeza kuwa serikali yake itaendelea kuwekeza katika kutoa walimu wa michezo mbalimbali ili Tanzania iweze kuondokana na dhana ya kuwa kichwa cha mwendazimu na kuwataka viongozi wa vyama mbalimbali kujipanga ili kutimiza malengo ya kupata mafanikio.
 
'Mtifuano' ZFA kuanza leo


na Makuburi Ally


ZOEZI la uchukuaji fomu za kuwania uongozi wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), unatarajia kuanza leo huku mwenyekiti na makamu wake wakionyesha nia ya kutetea nafasi zao. Akizungumza na Tanzania Daima jana, Katibu Mwenezi wa ZFA, Maulid Hamad Maulid, alisema, uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Desemba 31 kwenye ukumbi wa Uwanja wa Gombani ulioko Pemba.
Aliwataja baadhi ya wadau watakaojitokeza kuwania nafasi ya mwenyekiti kuwa ni pamoja na Ali Ferej Tamim anayetetea, Suleiman Mahmoud Jabir, Mahmoud Thabit Kombo na Amani Makungu, wakati Makamu Mwenyekiti ni Hajj Ameir ‘Bosi Mpakia', Mkurugenzi wa Kituo cha Radio Tanzania Zanzibar, Yusufu Omar Chunda na Ibrahim Raza.
 
Makocha kunolewa Brazil


na Mwandishi wetu


CHAMA cha Makocha wa Soka Tanzania (TAFCA), kimepata mwaliko wa kushiriki kozi ya wiki ya masomo nchini Brazil inayotarajiwa kuanza Januari 10-25 mwakani. Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TAFCA, Eugene Mwasamaki, alisema washiriki wa kozi hiyo wanatakiwa kujigharamia kila kitu katika mafunzo hayo.
Mwasamaki alisema, gharama za kozi hiyo ni dola 2,500 za Marekani, ambapo pia washiriki wanatakiwa kujigharamia nauli na gharama nyingine wawapo huko.
Aidha Mwasamaki alisema, sambamba na kozi hiyo, kozi nyingine kama hiyo itafanyika kuanzia Julai 5-20 mwakani.
Alisema, washiriki watajifunza masuala mbalimbali ya ualimu wa soka, ambapo wanaostahili kushiriki kozi hizo ni wenye sifa kuanzia ngazi ya cheti na ngazi ya kati.
 
Dk. Remmy kuzikwa Sinza kesho


na Dina Ismail


NGULI wa muziki wa dansi nchini Ramazani Mtoro Ongala maarufu kama Dk. Remmy anatarajiwa kuzikwa kesho katika makaburi ya Sinza. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana mjomba wa marehemu Kitenzogu Makassy 'Mzee Makassy' alisema kabla ya maziko hayo, mwili wa marehemu utaagwa na viongozi wa kiserikali kisha baadaye watu wa kawaida.
Alisema viongozi wa kiserikali watauaga mwili huo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kabla ya kupelekwa nyumbani Sinza ambako watu wengine watapata fursa ya kumuaga na kisha kuanza safari ya kupelekwa katika nyumba ya milele.
"Tulikuwa tunasubiri ujio wa ndugu na baadhi ya watoto wa marehemu waliokuwa nje ya nchi, baadhi yao wameanza kuwasili leo (jana) na wengine watawasili kesho (leo)," alisema Mzee Makassy.
Marehemu alikutwa na umauti Jumapili ya Desemba 12 alipokwenda kupata matibabu katika Hospitali ya Regency ambapo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa figo, moyo na shinikizo la damu kwa muda mrefu.
Dk. Remmy alizaliwa mwaka 1947 huko Kivu nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na enzi za uhai wake alipata kutunga nyimbo mbalimbali zilizompatia umaarufu mkubwa, huku nyimbo zake nyingi na za kusisimua zikizungumzia kifo.
Baadhi ya nyimbo hizo ni "Siku ya Kufa", "Kwa Nini Nife Dunia", " Kifo Hakina Huruma", "Narudi Nyumbani Matimila" "Ndumilakuwili', "Mnyonge Hana Haki", "Kipenda Roho," "No Money, No Life," and "One World.", "Mambo Kwa Soksi", "Asili ya Muziki", "Athuman Vipi Mambo Valuvalu", "Namolema", "Mariamu Wangu" , "Mwanza", "Mola Nalilia Mtoto" na nyinginezo.
Remmy ni msanii ambaye awali alikuwa akiimba muziki wa kidunia kabla ya mwaka 2003 kuoka; alikuwa ni msanii mwenye vituko huku akijiita majina ya kustaajabisha ikiwemo 'Nabii wa Kifo'.
Alikuja nchini kwa wito wa Mzee Makassy mwaka 1977 kuziba pengo la wasanii wa iliyokuwa bendi ya Makassy Orchetra aliyodumu nayo hadi mwaka 1981 alipojiunga na Orchestre Super Matimila.
 
Cindy, TMK kupamba fainali BSS


na Juma Kasesa


MWANAMUZIKI nyota kutoka Uganda Cindy anatarajiwa kupamba fainali za kumsaka bingwa wa shindano la kusaka na kuinua vipaji linalojulikana ‘Bongo Star Search’ (BSS), litakalofanyika Desemba 17 kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Production, Rita Paulsen, alisema wanamuziki wengine watakaopamba fainali hizo ni Diamond, Mh. Temba, Chege, TMK Wanaume Family, Mwasiti, Joh Makini, Imani na Kibonde.
Alisema, maandalizi ya fainali hizo ambazo mdhamini wake mkuu ni Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager yamekamilika.
Aliwataja washiriki watano waliotinga fainali hizo kuwa ni Joseph Payne, Bella Kombo, Mariam Mohamed, James Martin, na Waziri Salum, ambapo bingwa atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 30, huku wa pili akipata milioni 10 na wa tatu milioni 5.
Alitaja viingilio vya onyesho hilo kwa viti maaalumu (VIP) kuwa ni shilingi 45,000, viti vya kawaida (20,000) ambapo fainali hizo zitarushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV.
Kwa upande wake, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe, alisema, Kilimanjaro imedhamiria kuwafikisha katika kilele cha mafanikio wasanii wa muziki nchini.
 
Bozi Boziana, Twanga wakamilisha kazi


na Khadija Kalili


BAADA ya kukamilisha kazi iliyomleta nchini, msanii nyota barani Afrika Aboubakar Benz ‘Bozi Boziana' anatarajiwa kuondoka nchini leo kurejea kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati wowote kuanzia sasa. Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Asha Baraka ambaye ndiye aliyemleta nchini kwa minajili ya kurekodi naye nyimbo katika video na audio, alisema kazi hiyo imekamilika.
"Kazi aliyokuja kuifanya Boziana imekamilika, hivyo mashabiki wakae mkao wa kuona mambo mazuri na ya kimataifa zaidi, alisema Asha.
Alisema kuwa tayari wadau walionjeshwa ladha ya nyimbo hizo Jumapili iliyopita kwenye Ukumbi wa TCC Chang'ombe, ambako Boziana aliimba sambamba na bendi ya Twanga Pepeta International nyimbo mbili walizorekodi pamoja.
Asha, alizitaja nyimbo hizo kuwa ni ‘Mapenzi Hayana Kiapo' uliotungwa na mwimbaji Saleh Kupaza na ‘Kauli' ikiwa ni kazi ya Roggert Hegga ‘Caterpillar'.
Mbali ya kurekodi na bendi hiyo, pia Boziana alifanya nayo maonyesho yaliyofana katika Ukumbi wa Club Bilicanas, Club Sunciro, Mango Garden na Leaders Club jijini Dar es Salaam na Uwanja wa Mkwawani, jijini Tanga.
 
Blackburn confirm they want Maradona

Published 23:00 14/12/10 By Alan Nixon




Blackburn's new owners have admitted they want Diego Maradona as manager
The move for Maradona was first revealed in Mirror Sport yesterday.
And after appointing Steve Kean as caretaker, Venky's chairwoman Anuradha Desai said last night: "We thought about Maradona as a coach after we took over.
"Talks were at the initial stage then, but there is no development on that front yet.

"For now, the current coach will be the manager till the end of the season.
"There is no question of signing anyone for such a short time."
Maradona is keen to take on a Premier League job and the Rao family, who run Venky's, the company that owns Blackburn, are desperate for an iconic *worldwide name and will try to get the Argentine involved in any capacity.
Maradona would not even have to be at Ewood Park on a regular basis in the new-look set-up.
The respect for Kean is great – and he is also a client of Kentaro, the agents who advise Venky's.
Desai said: "Kean is well connected with the game and the players as well. We have full faith that he will do the best job and keep the team motivated.
"He works long hours and is talented at his job.
"He also works well with our very skillful young players – and that is important."
Desai also claimed her family was right to sack Allardyce and hoped that chairman John Williams would stay.
She said: "We have not taken any hasty decision in replacing the manager with the coach. It was a long, pending issue and it's a calculated risk.
"I don't want to get into why we were unhappy with Allardyce, or any kind of negative remarks.
"John Williams is close to Allardyce but he is very much with us and he has not expressed any willingness to quit. His position in the team is safe."
 
Blackburn owners target 'marquee' manager

Published 23:00 14/12/10 By Alan Nixon




Blackburn Rovers's new Indian owners want to chase the Champions League - and with a revolutionary new management team.
The millionaire Rao family who own the Venky's chicken firm are ready to flap their wings and reach for the skies, but their plans and statements are more like One Flew Over the Cuckoo's Nest at the moment.
Venkatesh Rao, one of the close-knit group that now runs Rovers, admitted yesterday that they have their managerial target and hope to have someone in charge soon as they look to stamp their mark on the club.
Rao and the rest of the VH Group, who made their millions in the poultry industry, now want a marquee appointment to help raise their profile. Argentinian legend Diego Maradona has been discussed by the Rao family - as Mirror Sport revealed - and he fits the bill. They would love him as manager, technical director or just an ambassador.

The Rao family are considering having a 'figurehead' boss, a first-team coach and a director of football who seems likely to be leading agent Jerome Anderson.
If the Maradona move fails the Indians will go for another mega-star name as they look to replace Sam Allardyce and make the big-time in the Premier League and also put their company in the spotlight.
Pune-based businessman Venkatesh revealed their 'mystery' man was being lined up and said: "We have got a target in mind. It is in the pipeline. The whole management team is talking and we will come back as soon as possible.
"I can't say when, give us some time. We are looking forward and for the best for the club. We are thinking of the fans - we are looking for a better team. We want to give them a gift.
"We have been talking to the chairman and other people also. It is just about improving the management and improving the club.
"It's about being a better football club, it is nothing against anybody. It's nothing against Mister Sam. All the best to him."
Venkatesh Rao, who has watched Rovers along with his brother Balaji, has taken a crash course on football recently - and also relied heavily on his advisers Kentaro, the football agency.
However their ambitious aims to make the 'top five' will take some inspired appointments and signings and their lack of knowledge is putting them under immediate pressure.
But the Raos put in their money and want something from their next investment - in the management team and the signings they will make - as Venkatesh explained the reasons for the change.
He said: "Everything is a combination here. We want better results and better entertainment."
Allardyce and assistant Neil McDonald are the first of the casualties. But chairman John Williams is on the brink of leaving too - he was 'in tears' about the way the manager was sacked.
Honorable statesman Williams did not want Allardyce to go so soon after the takeover and his position looks untenable. However, the Raos were trying to talk him into staying yesterday.
The Indians hope to have their new-look team in place shortly, but the repercussions will be great if they fail. The pressure is on caretaker Kean, starting with West Ham on Saturday.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…