Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #1,401
Mgosi, Humud wafyekwa mshahara Simba
Wednesday, 22 December 2010 19:41
Ofisa habari wa klabu hiyo, Clifford Ndimbo
Clara Alphonce
UTOVU wa nidhamu ulioonyeshwa na wachezaji wawili wa Simba, Mussa Hassan ' Mgosi na Abdulhalim Humud umewasababishia kukatwa asilimia tano ya mshahara wao wa mwezi.
Ofisa habari wa klabu hiyo, Clifford Ndimbo alisema jana kuwa wachezaji hao wameonyesha utovu wa nidhamu kwa kutokuhudhuria mazoezi bila taarifa yoyote kwa uongozi au kocha wao, Patrick Phiri.Alisema kuwa kuanzia sasa Simba imeamua kudhibiti utovu wa nidhamu kwa wachezaji wake ili kila mmoja aweze kutimiza wajibu wake kulingana na programu ya kocha.
Aliongeza kuwa hatua hiyo dhidi ya nyota hao wawili inalenga kuondoa dhana ya baadhi ya wachezaji kujiona nyota katika timu hiyo na kutambua kwamba kila mchezaji anapaswa kuwa mazoezini na anapokosa mazoezini lazima aadhibiwe kwa kukatwa mshahara.
Alisema wachezaji karibu wote wameshawasili katika mazoezi yanayofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam wakati wa asubuhi na jioni kwenye viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe.
Aliongeza kuwa wachezaji wawili, Patrick Ochan na Joseph Owino ndio hawajaripoti na uongozi unazo taarifa zao na wanatarajia kuwasili wiki hii ili kujiunga na wenzao katika programu ya mazoezi ya uwanjani.
Alisema timu hiyo itaingia kambini rasmi baada ya sikukuu ya Krismasi kisiwani Zanzibar ikijiwekwa tayari kwa michuano ya Kombe la Mapinduzi, pia mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.
Kuhusu maandalizi ya mechi zao za kimataifa, Ndimbo alisema kuwa uongozi unasubiri programu kutoka benchi la ufundi ndipo waanze kuifanyia kazi.
Alisema lakini tayari kocha ameshaomba uongozi umwandalie mechi za kirafiki na wameshawasiliana na AFC Leopards ya Kenya na timu moja kutoka Brazil, ambazo watacheza nazo kabla ya michuano ya Kombe la Mapinduzi.