Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #1,421
Real Madrid yapiga 8-0 Kombe la Mfalme
Thursday, 23 December 2010 20:52
BARCELONA, Hispania
MABAO matatu (hat-trick) ya Cristiano Ronaldo na Karim Benzema yameiwezesha Real Madrid kuilaza Levante mabao 8-0 kwenye mchezo wa awali wa Kombe la Mfalme juzi.
Kwa mabao hayo, Ronaldo amefikisha 25 msimu huu katika mechi 24 alizocheza kwa klabu yake msimu huu.
Mabao mengine yalifungwa na Mesut Oezil na Pedro Leon huku vijana hao wa Jose Mourinho wakitawala mchezo huo wa kwanza kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu na kuonyesha mchezo tofauti na ule wa ligi waliohangaika kuilaza Sevilla 1-0.
"Matokeo haya ni mazuri kwetu na mashabiki wote kwani walihitaji kuona mchezo wa kuvutia wa soka, naamini tumewaonyesha," alisema Benzema, ambaye amefikisha mabao tisa msimu huu.
Benzema alifungua milango ya mabao dakika ya sita kwa kuichachafya ngome ya Levante na kumtungua kipa Gustavo Munua.
Oezil aliongeza jingine dakika nne baadaye baada ya Ronaldo kuuwahi mpira karibu na msitari wa katikati ya uwanja na kumpa pasi kiungo huyo wa Kijerumani.
Benzema aliongeza la tatu dakika ya 32 kwa pasi ya Angel Di Maria. Kisha, Benzema alimlisha Ronaldo ambaye alifunga la nne.
Kisha Benzema alikamilisha mabao yake matatu kwa kumchungulia kipa Munua, tena kwa pasi ya Di Maria, dakika ya 70 kabla ya Ronaldo kuongeza mengine dakika ya 72 na 74. Leon alikamilisha karamu kwa bao la dakika ya 90.
Mourinho alieleza kufurahishwa na mchezo wa Benzema na jinsi alivyochangia kwenye mabao yaliyofungwa.
Nao Atletico Madrid waliifunga Espanyol kwa bao 1-0 la Simao Sabrosa, huku kila timu ikipoteza mchezaji mmoja.
Bao la Simao la penalti dakika ya 33 lilitokana na beki wa Espanyol, Jordi Amat ambaye aliuchezea mpira kwa mkono.
Winga wa Atletico, Jose Antonio Reyes alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 42 kwa kumpiga kichwa mshambuliaji wa Espanyol, Jesus Datolo, huku Victor Ruiz akitolewa pia dakika ya 68.
Rais wa Atletico, Enrique Cerezo alisema karibuni kuwa Simao atahamia Besiktas ya Uturuki na winga huyo wa Ureno alishangiliwa na ashabiki kwenye Uwanja wa Vicente Calderon.
Naye Koffi Romaric alifunga mawili kwa Sevilla iliyoshinda 5-3 dhidi ya Malaga, hukuJose Ulloa kufunga matatu, hat kwa Almeria iliyoshinda 4-3 dhidi ya Mallorca na Getafe iliilaza Real Betis 2-1.
Jumanne, ilikuwa ya sare baada ya Atletico Bilbao kuikamata Barcelona kwa suluhu 0-0. Pia, Valencia na Villarreal zilimaliza 0-0 huku Cordoba ikitoka 1-1 Deportivo La Coruna. Mechi za marudiano zitakuwa Januari 4 na 5.