Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Monday December 06, 2010 Sports
Dar es Salaam designer for Mozambique Fashion Week

By LUDOVICK KAZOKA, 5th December 2010 @ 12:00, Total Comments: 0, Hits: 36

UPCOMING fashion designer Manju Msita is expected to represent the country in the Mozambique Fashion Week set to be staged in Maputo from Monday to Saturday.

The Swahili Fashion Week Media and Public Relation Manager, Saphia Ngalapi said in the city on Sunday that Manju was selected due to the quality of his work, saying he was selected by the international designer Jan Malan from South Africa during the Swahili Fashion Week.

"The relations between Swahili Fashion Week and Mozambique Fashion Week
started when Mozambique sent its representative in the Swahili Fashion Week, which took place in the city last year," she said.

Marinella Rodriguez represented Mozambique in this year's Swahili Fashion.

On his part, Manju expressed his delight following the appointment, saying "I am glad to represent the country and the Swahili Fashion Week in the event. Hopefully I will fly the Tanzanian flag well."
 
Kuziona Kili Stars, Z'bar Heroes 1,000/-


Na Zahoro Mlanzi

MASHABIKI wa soka nchini watalazimika kulipa sh. 1,000 kiingilio cha chini na sh. 5,000 kiingilio cha juu kuzishuhudia timu zao za Tanzania bara 'Kilimanjaro Stars' na Zanzibar'Zanzibar Heroes' zitakapocheza robo fainali ya michuano ya Chalenji.Timu hizo
zitashuka uwanjani kesho kwa nyakati tofauti ambapo Zanzibar Heroes itakuwa ya kwanza itakapoumana na mabingwa watetezi Uganda 'The cranes' na Kili Stars itaoneshana kazi na Rwanda katika michezo itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Sunday Kayuni alisema baada ya kuona mashabiki wana moyo wa kuipa sapoti timu zao za Tanzania ndio maana wameamua kupunguza viingilio.

"Tumeamua kupunguza kabisa viingilio ambapo kwa viti vya kijani na bluu kiingilio kitakuwa sh. 1,000, viti vya mchungwa sh. 2,000, viti maalum C (VIP C) ni sh. 3,000, VIP B sh. 4,000 na VIP A sh. 5,000)", alisema Kayuni.

Alisema kati ya viti vyote vilivyopo VIP B, viti 400 vitatengwa kwa ajili ya waandishi wa habari, wachezaji ambao timu zao hazichezi, makamisaa na viongozi wengine, hivyo mashabiki watakaokaa eneo hilo wanaombwa kuwa watulivu zaidi.

Mbali na hilo, Kayuni alizungumzia pia michezo ya nusu fainali ambapo alisema itapigwa siku moja ya Ijumaa ambapo wa kwanza utaanza saa tisa na wa pili saa 11 na mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu utapigwa Jumamosi saa saba mchana ukifuatiwa na fainali.

Kayuni anawaomba mashabiki wa soka nchi kujitokeza kwa wingi katika michezo hiyo kwani muda waliowapa kudunbduliza fedha za kuingiliwa uwanjani hapo ni mwingi, hivyo wajitokeze kwa wingi.
 
Taifa Queens uwanjani leo Singapore


Na Amina Athumani

TIMU ya taifa ya Tanzania ya netiboli 'Taifa Queens' leo saa 8 mchana itarusha karata yake ya kwanza katika michuano ya ufunguzi ya Kimataifa, inayofanyika nchini Singapore dhidi ya Scotland.Akizungumza kwa njia ya simu, Kaimu katibu Mkuu wa Chama cha
Netiboli Tanzania (CHANETA), Rose Mkisi alisema timu hiyo iliwasili juzi nchini Singapore, ikiwa salama na wachezaji wote wana morali ya kufanya vizuri.

Alisema timu hiyo pia itaingia uwanjani kesho, kuchuana na wenyeji wa michuano hiyo Singapore ambapo pia itachuana na India katika mchezo utakaofuata, kabla ya kumenyana na Namibia.

"Kwa kweli timu yetu ipo katika hali nzuri ya kiushindani na tunaimani itafanya vizuri, kutokana na maandalizi mazuri waliyopewa na Kocha Mkuu wa timu yetu, Simone Macknis," alisema Mkisi.

Timu hiyo iliondoka Ijumaa iliyopita ikiwa na jumla ya wachezaji 12, katika michuano hiyo itakayopandisha timu viwango vya kimataifa vinavyotambulika na Shirikisho la Kimataifa la Netiboli (IFNA).

Tanzania ni ya 22 kwa ubora wa viwango vya kimataifa, na kwa nchi za ukanda wa Afrika, Malawi ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na Afrika Kusini huku Newsland ni ya kwanza kwa ubora duniani.

 
Ni robo fainali ya ushindani, mvuto mkubwa Chalenji
Monday, 06 December 2010 21:41 0diggsdigg

mzee-heroes.jpg
Mshambualiaji wa timu ya taifa ya Zanzibar Heroes, Sabri Ramadhan Mzee akiwania mpira wa juu na beki wa Rwanda, Eric Gasana pamoja na kipa Jaen Luc Nayishimiye wakati wa mechi ya makundi ya Kombe la Tusker Chalenji kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Sosthenes Nyoni
ROBO fainali ya michuano ya Kombe la Tusker Chalenji inaanza leo kwa michezo miwili ambapo katika mpambano wa awali, vigogo wa soka kutoka kusini mwa Afrika, Zambia au Chipolopolo watakabiliana na Swala wa Ethiopia.

Mpambano unaotarajiwa kuwa mkali wenye ushindani utafanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam saa 8 mchana, ukifuatiwa na ule ambao utaikutanisha timu ngumu ya Ivory Coast (Elephants) dhidi ya Malawi, maarufu Flames, ambayo pia imeonyesha mchezo wa kuvutia.

Kikubwa zaidi, ni mchezo huo baina ya timu hizo ambazo zote zimealikwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), unaorejesha kumbukumbu ya mechi ya mjini Abidjan mwaka juzi, ambapo Ivory Coast iliichakaza Malawi 5-0.

Katika mchezo huo wa kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika na Kombe la Dunia mwaka 2010, mashabiki 20 walikufa na wengine kadhaa kujeruhiwa kwa kukanyagana kwenye Uwanja wa Felix Houphouet Boigny.

Ikiwa na nyota wake, Didier Drogba, Salomon Kalou na wengineo wengi, ambao hata hivyo hawashiriki fainali hizi za Chalenji, Ivory Coast ilitoka jasho katika mchezo wa marudiano mjini Blantyre kwa ushindi wa bao 1-0 ambao uliikatia tiketi ya fainali hizo zilizochezwa Angola na Afrika Kusini.

Kwa vyovyote vile, mchezo huo wa leo utakuwa wenye ushindani mkubwa kutokana na kasi ambayo Malawi inacheza, dhidi ya ubabe, nguvu za vijana wa Ivory Coast.

Chipolopolo imefanikiwa kuingia robo fainali baada ya kujikusanyia pointi saba zilizotokana na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji, Kilimanjaro Stars, sare ya bao 1-1 ilipocheza na Burundi pamoja na kipigo cha 6-0 kutoka kwa timu dhaifu ya Somalia.

Ikiwa na mpachika mabao kinara wa michuano hiyo, Felix Sunzu(21)ambaye pia aliyewahi kuichezea Konkola Blades ya nchini humo, Chipolopolo imeonyesha nia yake ya kutwaa ubingwa wa michuano na dola 30,000 baada ya kuongoza Kundi A lililokuwa na Kilimanjaro Stars, Burundi na Somalia.

Kocha wake, Mario Bonetti ambaye ni raia wa Italia alisema juzi kuwa ni vigumu kutabiri mwelekeo wa kikosi chake kwa sasa, lakini ameapa kupigana kufa au kupona ili waweze kuvuka hatua hiyo.

"Hii ni soka bwana unakuwa na malengo, lakini huwezi kumhakikishia mtu kwamba utafanya kile, lakini tumejiandaa kuikabili Ethiopia ili tuvuke hatua hii na hili ndilo muhimu kwa wakati huu,"alisema Bonetti.

Ikitokea Kundi C, Ethiopia ' swala' ilibebwa na idadi kubwa ya mabao matatu na kuitupa nje Burundi iliyokuwa na mabao mawili licha ya timu hizo kulingana kwa pointi, nne.Wahabeshi hao ambao wameonyesha kuwavutia mashabiki wengi kwa kandanda yao ya pasi nyingi walianza kwa kuadhibiwa na Uganda mabao 2-1 kisha ikaitungua Kenya, Harambee Stars, mabao 2-1 na kufuatia na suluhu ya 0-0 dhidi ya Malawi.

Ivory Coast iliyokuwa kundi B na inayoonekana kuwa na chipukizi wengi pengine kuliko timu nyingine yoyote inayoshiriki michuano hii imefikia hatua hiyo baada ya kujikusanyia pointi sita ikiwa imezisulubu Zanzibar Heroes 1-0, Sudan 3-0 na kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Rwanda.

Kocha wa Ivory Coast, Kouadio Georges ambaye kikosi chake kitaikabili Malawi alisema mpaka kuwa hadi wakati huu vijana wake wameimarika kiasi cha kutosha tayari kwa mpambano huo ambao ameuita ni vita isiyotabirika.

Malawi,'The Flames' itashuka katika kipute hicho ikijivunia rekodi ya kutopoteza mchezo ambapo ikitokea Kundi C ilikoibanjua Kenya 3-2 na kufuatia na sare mbili ikiwa ni ile ya bao 1-1 na Uganda sambamba na bao 1-1 dhidi ya Ethiopia.
 
...Kuiona Chalenji buku tu! Monday, 06 December 2010 21:28 0diggsdigg

Clara Alphonce

BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati
(Cecafa) limepunguza kiingilio cha michuano ya Chalenji huku cha juu kikiwa ni Sh 5,000 na chini Sh1,000.

Awali, Cecafa ilitangaza viingilio vya kati ya Sh20,000 kwa kile cha juu na chini cha Sh2,000, kwa ajili ya michuano hiyo.

Lakini, baada ya kuanza kwa michuano hiyo mashabiki waliadimika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa kumudu kiingilio hicho na kuifanya Cecafa, kuamua kuondoa viingilio kwa mechi za makundi ili mashabiki waingie na kushangilia timu zao.
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Sunday Kayuni alitangaza viingilio hivyo kuanzia mechi za leo za robo fainali kuwa Sh1000 kwa jukwaa la kijani na bluu, Sh2,000 k wa lile la rangi ya machungwa, VIP C Sh3,000 huku VIP B itakuwa Sh4,000 na VIP A itakuwa Sh5,000.

Alisema kuwa katika VIP B kutakuwa na viti 400 ambavyo vitakuwa wazi kwa ajili ya wachezaji, waamuzi na waandishi wa habari, hivyo amewataka Watanzania kutofanya fujo pindi wanapoambiwa kuwa hawatakiwi kukaa sehemu hizo.

Alisema wao na Cecafa wameamua kupunguza viingilio hivyo ili kila mmoja aweze kushuhudia michuano hiyo ambayo kwa sasa hipo katika hatua ya robo fainali. Leo, Zambia itacheza na Ethiopia saa 8.00 mchana na saa 10.00 itakuwa zamu Ivory Coast na Malawi.

Hata hivyo, Kayuni alisema kuwa viingilio hivyo ni vya robo fainali na nusu fainali na hapo baadaye vitatangazwa vile vya fainali.

Pia, Kayuni alisema kuwa kutakuwa na mabadiliko katika michezo ya nusu fainali ambayo ilitakiwa kuchezwa Alhamisi hivyo imepelekwa mbele mpaka Ijumaa.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye alisema kuwa kama mchezaji alikuwa amepata kadi mbili za njano katika mechi za makundi ataendelea na adhabu yake kwenye robo fainali na kama alikuwa na kadi moja katika robo fainali inafutwa.

Alisema kuwa kwa wale ambao wametolewa katika michuano hiyo na walikuwa na adhabu ya kadi zitaendelea tena katika michuano ijayo katika mwaka ujao.

Musonye aliongeza kuwa katika robo fainali na nusu fainali hakutakuwa na muda wa nyongeza, hivyo kama timu itatoka dakika 90 haijafungana, basi wataingia moja kwa moja katika mikwaju ya penalti.
 
Msechu ashika nafasi ya wa pili TFP, akuna wengi Monday, 06 December 2010 21:24 0diggsdigg

Henry Mdimu, Nairobi

LICHA ya Mganda Davis Ntare kutwaa taji la Tusker Project Fame 2010, jopo la majaji kwa pamoja na uongozi wa chuo cha mafunzo cha shindano hilo wamekiri kwamba mshiriki wa Tanzania, Peter Msechu, ana kila sababu ya kuwa ndiye mshindi wa shindano.
Kila mtu kwa wakati wake, majaji Ian, Hermes Joachim na Juliana Kanyomozi, walimtaja Msechu kuwa ni mwanamuzikii maarufu anayejiamini sana na kujiweza jukwaani, na pia mbunifu.

Sifa hizo ndizo zinazotakiwa kwa mwanamuziki wa karne hii iliyojaa utandawazi, walieleza majaji.

Msechu ambaye kete yake ya mwisho aliitupa kwa kutumia kwa kibao cha Kilwa Jazz aliudhihirishia tena umma wa wengi katika Afrika Mashariki kwamba anaweza kuwainua kwenye viti na kuwaimbisha muda wowote anaotaka.

Msechu, huku akionyesha kujiamini kwamba muziki ni njia pekee ya kueleza hisia zake kwa jaji huyu kwani, angepata wapi nafasi nyingine ya kumwambia.

"Ningemuita nikamwambia nina maongezi naye angekuja?", alisema Msechu katika mkutano na waandishi wa habari mara baada ya onyesho hilo kwisha na washindi kutajwa katika maeneo ya Ruaraka, jijini Nairobi, eneo ambapopia yapo makao makuu ya East African Breweries, watengenezaji wa bia ya Tusker.

Akizungumza na Mwananchi, Msechu ambaye ameshinda mkataba wa mwaka mmoja wa wa kurekodi na Kampuni ya Africa Sound yenye makao makuu nchini Kenya alisema anaamini kuwa yeye ni mshindi, ila zawadi kubwa amechukua Davis, na atalithibitisha hilo atakapoanza rasmi kazi yake ya muziki, mashabiki wataendelea kufurahi kumsikiliza na kumuona jukwaani.

Davis Ntare, alipata tiketi ya kuingia katika msimu wa nne kupitia nchini Kenya, huku sababu ya msingi ikiwa ni kwamba, wakati usaili wa mashindano haya unapita Uganda, yeye alikuwa shamba ambako alienda kumtembelea bibi yake.

Ndipo alipoambiwa na rafiki zake kwamba usaili umepita, akakimbilia Kenya kujaribu bahati yake na juzi kufanikiwa kutawazwa rasmi kuwa mshindi wa Tusker Projact Fame kwa msimu wa nne ambao umeisha.

Tangu nusu fainali ambazo zilifanyika Jumamosi, majina mawili tu yalikuwa yakitajwa sana miongoni mwa mashabiki waliokuwa wakifurika kushuhudia shindano hilo. Peter Msechu na Steve kutoka Kenya.

Ushindi wa Davis ni wa pili kwa Uganda kuchukutaji hilo ambapo baada ya Esther Nabassa kulichukua taji hilo mwaka jana akafuatiwa na Alpha kutoka Rwanda.
 
Ubingwa Chalenji bado waumiza vichwa
Monday, 06 December 2010 21:23 0diggsdigg

Waandishi Wetu

WAKATI hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Chalenji ikiwa imemalizika na kusubiriwa robo fainali itakayoanza kupigwa leo,utabiri wa nani atakuwa mfalme mpya umekuwa ni kitendawili kisichokuwa na majibu.

Ugumu huo unatokana takribani timu zote ukiiondoa Sudan na Somalia ambayo kwa miaka mingi imekuwa kibonde zimeonyesha uhai mkubwa tofauti na michuano iliyopita.
Tayari, Sudan ambayo haikushinda mchezo hata mmoja zaidi ya sare, Somalia iliyopoteza mechi zote na Burundi iliyoshinda mchezo mmoja, zimeondolewa mashindanoni.

Wenyeji Kilimanjaro Stars licha ya kuanza kwa kusuasua na kipigo cha bao 1-0 kutoka Zambia, bado ilionyesha kuwa ni timu isiyotabirika kwani kiwango chake kimeonekana kupanda mchezo baada ya mchezo.

Zambia imeonyesha kuwa haitaki kurudia makosa kama yale iliyoyafanya mwaka jana pale ilipotolewa na Zanzibar Heroes kwa penati 4-3.

Uganda Cranes, inatetea taji lake na imekuwa ni tishio pengine kutokana rekodi yake katika michuano hiyo ikiwa imetwaa kombe la Chalenji mara 12.

Baada ya mwaka uliopita kulinyakua kombe hilo nchini Kenya kwa kuifunga Rwanda 2-0, sasa inasaka kulibeba moja kwa moja.

Kocha wake mzoefu, Bob Wiliamson na nahodha wao Andrew Mwesigwa wameifanya The Cranes ionekane timu iliyokamilika zaidi pengine kutokana na wachezaji wake kukaa pamoja kwa muda mrefu.

Vijana mchanganyiko, wenye pumzi wa Ivory Coast wakiwa na staili yao ya kucheza pasi nyingi wameonekana kuwa wanaweza kufanya lolote.

Pia, Ivovy Coast ina mshambuliaji hatari, Kipre Tchetche ambaye ameonyesha si mtu wa masihara.

Rwanda au Amavubi, nayo ni timu inayoundwa na vijana wengi wa umri mdogo ukiwaondoa wakongwe wachache kama Mbuyi Twite na Haruna Niyonzima, imeonyesha ukomavu hasa kwa kuwa iliitungua Ivory Coast kwa mabao 2-1 wakati mfumo wa kushambulia kwa kushtukiza ambao umekuwa ukitumiwa na Malawi umenyesha unaweza kulifikisha taifa hilo mbali.

Ukuta mzuri wa Zanzibar Heroes chini ya nahodha wao Nadir Haroub na Agrrey Morris umekuwa ukileta hofu kwa timu zinazoshiriki michuano hiyo, lakini pia uwezo wa kukimbia na mpira kwa kasi na kufumania nyavu wa mshambuliaji wa timu hiyo, Ally Ahmed Shiboli ambaye alianza michuano hiyo kwa mabao mawili, lakini akapoteza dira katika mechi zilizofuata.
 
Nafasi nne zasakwa Ligi ya Mabingwa Monday, 06 December 2010 21:16 0diggsdigg

ZURICH, Uswisi
NAFASI nne pekee za kucheza hatua ya 16 bora ndizo zinasakwa kwenye mechi zaLigi ya Mabingwa Ulaya zinazochezwa leo na kesho.

Mbali ya nafasi hizo nne, pia zinatafutwa nafasi tano za kushiriki michuano ya Europa League, hatua ya 32 bora.

Arsenal na Shakhtar, ni timu mbili ambazo zinaweza kujaza nafasi hiyo kutokea Kundi H kwenye mechi za Jumatano, Desemba 8.

Mechi hizo za kukamilisha hatua hiyo ya kucheza 16 bora itaendelea leo huku timu12 zikiwa tayari zimefuzu.

Kundi H ndilo kivutio, ambako Shakhtar Donetsk, Arsenal na Braga hakuna ambayo imejihakikishia nafasi ya kufuzu.

Lakini, katika makundi mengine matano, kinachosakwa ni timu zipi zitacheza michuano ya Europa League kwa kushika nafasi ya tatu.

Mechi za Makundi A-D zinamalizika leo wakati zile za Makundi E-H zitachezwa kesho, huku ratiba ya mtoano, maarufu 16 bora itapangwa Desemba 17.

Kundi A

Swali ambalo halijajibiwa ni iwapo wageni wa michuano hiyo,Tottenham Hotspur watamaliza kileleni mbele ya watetezi, Internazionale Milano. Zote, hata hivyo zimefuzu, ingawa Spurs inajivunia matokeo mazuri dhidi ya Inter. Twente na Dortmund zinasaka nafasi ya tatu.

Kundi B

Schalke 04 na Olympique Lyon zina hakika ya kufuzu , ingawa klabu hiyo ya Ujerumani (Schalke) ipo mbele kwa pointi moja. Lyon wanatakiwa kuilaza Hapoel Tel-Aviv, wakitumaini Schalke ishindwe na Benfica; lakini Lyon itashinda itakuwa na pointi 10, sawa na Schalke 04, huku Wajerumani wakiwa mbele kwa mechi iliyozikutanisha timu hizo. Benfica, yenye pointi tatu inasaka nafasi ya Europa au kuipiku Lyon .


Kundi C

Manchester United na Valencia zinasaka nafasi ya uongozi wa kundi hilo. Lakini, Valencia wapo nyuma ya wakali hao wa Old Trafford kwa pointi tatu, wataipiku kama wataifunga leo. Rangers inaikaribisha Bursapor, ikiwa na uhakika wa kumaliza ya tatu.

Kundi D

Barcelona imefuzu ikiwa kinara na Panathinaikos inashika nafasi ya nne, huku nafasi ya pili ikisakwa baina ya FC København ambao wanaikaribisha Rubin Kazan yenye pointi sita. Rubin, ambao waliilaza Barca 2-1 kwenye Uwanja wa Camp Nou, wanaweza kumaliza mbele ya FCK kwa tofauti ya mabao.
 
Wababe Ulaya wagomea kileleni mwa ligi zao
Monday, 06 December 2010 21:18 0diggsdigg

MADRID, Hispania

KLABU za Borussia Dortmund, Barcelona na AC Milan zimethibitisha dhamira zao za kutaka ubingwa wa ligi za nchi zao msimu huu, huku uongozi wa ligi za England na Ufaransa ukibadilika.

Borussia na Barcelona ziliendelea kutoa vipigo na kuongoza ligi za Ujerumani na Hispania. AC Milan, pia ilionja ushindi pia mwishoni mwa wiki.

Ujerumani
Dortmund imeendelea kusaka taji la ubingwa wa Ligi Kuu, Bundesliga baada ya ushindi wa mechi yake ya 13 katika mchezo wa Jumapili.
Kwa ushindi huo wa mabao 2-0 dhidi ya Nurnberg, Borussia inaongoza kwa tofauti ya pointi 10.

Mainz 05 ambayo ilishindwa 2-1 dhidi ya Eintracht Frankfurt ilipoteza mwelekeo. Bayer Leverkusen ilishika nafasi ya pili baada ya ushindi mnono wa mabao matano dhidi ya FC Koln, huku Schalke 04 ililipa kisasi cha mabao 5-0 ilichopata kutoka kwa Kaiserslautern wiki iliyopita kwa kushinda 2-0 dhidi ya Bayern Munich, ikishika nafasi ya saba.

Italia

Milan ilipata ushindi wa tisa wa Ligi Kuu, Serie A kwenye mechi 11 baada ya kuilaza 3-0 Brescia kwa mabao ya Kevin-Prince Boateng, Robinho na Zlatan Ibrahimovic.

Kwingineko, jirani zao, Internazionale Milano waliporomoka kwa kipigo cha tatu cha mabao 3-1 kwenye mechi nne za ligi baada ya kufungwa na Lazio, ambako mabao yaliwekwa kimiani na Giuseppe Biava, Mauro Zarate na Hernanes.

Lazio ipo nyuma ya AC Milan kwa pointi tatu na mbili mbele ya Juventus, ambayo iliiadhiri Catania 3-1. Inter inashika nafasi ya sita, ikiwa sawa kwa pointi na timu tatu, Palermo, ambayo jana iliikaribisha Napoli , Sampdoria na AS Roma, ambayo ilipoteza uongozi wa mabao mawili dhidi ya Chievo Verona na kutoka sare ya 2-2.

Hispania

Barcelona walijikuta wakiwa na wakati mgumu kwenda kuivaa Osasuna Jumamosi baada ya mgomo wa waongoza ndege uliowachelewesha kufika uwanjani.

Lakini, mechi hiyo iliyochelewa kuanza ilishuhudia Barca ikishinda kwa mabao 3-0 huku Lionel Messi akifunga mawili na kuwawezesha vijana hao waJosep Guardiola kuongoza kwa pointi mbili mbele ya Real Madrid , ambayo ilishuhudia Cristiano Ronaldo akifunga mawili dhidi ya Valencia ambayo ilifungwa 2-0.
"Kitu muhimu kwetu kilikuwa kuweka kando kipigo kutoka kwa Barca, ndiyo maana tulikuwa na mchezo mgumu mno," alisema kocha wa Madrid, Jose Mourinho,

Villarreal inaendelea kushika nafasi ya tatu iliilaza Sevilla 1-0, huku walioko katika nafasi ya nne Espanyol ikiilaza Real Sporting de Gijón 1-0.

England
 
Mufindi waibuka kidedea SHIMISEMITA Moro


na Samia Mussa


amka2.gif
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa imeibuka bingwa wa jumla katika mashindano ya taifa ya Shirikisho la Michezo la Serikali za Mitaa Tanzania ( SHIMISEMITA), yaliyomalizika juzi uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Mufindi ilinyakua ubingwa huo kwa kupata mataji manne katika mpira wa wavu kwa wanaume na wanawake, netiboli na soka.
Katika mpira wa wavu wanaume kwa upande wa Mufindi walishika nafasi ya tatu wakifuatiwa na wilaya ya Ilala ambapo Njombe walishika nafasi ya kwanza.
Wavu wanawake, Njombe walishika nafasi ya tatu, Iringa Manispaa ya pili na Mufindi nafasi ya kwanza.
Kwenye netiboli, Mufindi walishika nafasi ya tatu, huku Kinondoni ikiibuka ya pili na Mbeya ya kwanza.
Katika soka, Mbeya ilishika nafasi ya tatu ikiwa nyuma ya Mufindi iliyoibuka ya pili huku vinara wakiibuka Arusha.
Mashindano hayo yalifungwa na Ofisa Mwandamizi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), John Chamkulu ambaye katika hotuba yake, aliahidi baraza hilo litatoa ushirikiano kuhakikisha Shirikisho hilo linasimama na kuwa na mafanikio makubwa.
Chamkulu alizitaka halmashauri zilizoshiriki mashindano ya mwaka huu, kuwa mabalozi wa kuhamasisha nyingine ambazo hazijashiriki ili idadi iongezeke hapo mwakani.
Pia aliwataka viongozi wa muda wanaoendesha shirikisho hilo, kuhakikisha linasajiliwa.
 
Super D awezeshwa kozi ya ukocha ya BFT


na Mwandishi wetu


amka2.gif
KOCHA wa ngumi wa klabu ya Ashanti jijini Dar es Salaam ambaye pia hutoa mafunzo ya kujitegemea Rajabu Mhamila 'Super D' amekabidhiwa msaada wa sh 150,000 kumwezesha kushiriki kozi iliyoandaliwa na Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT). Msaada huo ambao ni wa pili kwa kocha huyo kupewa, ulitolewa na mdau wa michezo Zulfiqal Ali ili kumwezesha Super D kufanikisha malengo yake ya kuendeleza mchezo wa ngumi kwa vijana, baada ya kushiriki kozi hiyo itakayoanza Desemba 14 hadi 24 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, wakati akikabidhi fedha hizo, Zulfiqal alisema, ameamua kufanya hivyo ili kuungana na wadau wengine ikiwemo serikali katika kuendeleza michezo.
"Michezo siku hizi hapa nchini ni ajira kwa vijana wetu na ili tuweze kufanikisha zaidi, tunatakiwa kuwawezesha walimu kwanza ambao watatoa mwanga kwa wengine, ndio maana nimeguswa katika hili na kusaidia," alisema.
Hata hivyo, Zulfiqal amewaomba wadau wengine kujitokeza kuungana na jamii kusaidia kukuza michezo ili kuwawezesha vijana wasio na ajira waweze kujiajiri.
Naye Super D, alishukuru na kuahidi kuzingatia kozi hiyo siku zote, ili aweze kupanua ujuzi ambao utamwezesha kuwasaidia mabondia wanaochipukia hapa nchini.
Awali, kocha huyo alipewa msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani zaidi ya shilingi 300,000 kwa ajili ya mazoezi ya mabondia wanaohudhuria mafunzo yanayotolewa na kocha huyo.



h.sep3.gif
 
KUTOKA BSS KILI HOUSE: Milioni 30 zaanza kunukia


na Hellen Ngoromera


amka2.gif
FAINALI za shindano la kusaka vipaji vya kuimba nchini, ‘Bongo Star Search’ (BSS), litahitimishwa mwezi huu jijini Dar es Salaam, wakati ambao kutakuwa na shamra shamra za kuzifikia Sikukuu za X-Mass na mwaka mpya. Kuhitimishwa kwa shindano hilo, kulitangazwa juzi na mtangazaji wa shindano hilo, Godwin Gondwe ‘Double G’, wakati wa kipindi hicho kinachoonyeshwa kila Jumapili kutoka ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam.
Hata hivyo, mtangazaji huyo hakutaja siku ya fainali za mashindano hayo, ambayo kwa mwaka huu ni msimu wa nne tangu yaanzishwe, ambapo mwaka huu mshindi wake atajinyakulia kitita cha sh milioni 30.
Tayari shindano hilo limebaki na washiriki wanane, baada ya wawili Ruth Oscar na Pelucy Joctan kutolewa siku hiyo kutokana na kura zao kutotosha.
Katika kura hizo, anayeonyesha kushika nafasi ya kwanza ni Joseph Payne ‘Mzungu’ (07) ambaye hadi sasa amepata asilimia 25 ya kura alizopigiwa na wananchi.
Wengine walioingia katika 'danger zone' kwa wiki hii ni Chiby Dayo (04), James Martin (14) na Christabela Nzowa (20) ambao ikiwa hawatapigiwa kura za kutosha, wawili kati yao wataondoshwa katika mashindano hayo katika juma lijalo.
 
Mchujo 'Music Dance Competitions' Afri Centre


na Makuburi Ally


amka2.gif
MCHUJO wa kwanza wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba muziki wa dansi ‘Music Dance Competitions' unatarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 20 hadi 21 kwenye ukumbi wa Afri Centre Ilala jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), jijini Dar es Saalm jana, mkurugenzi wa kampuni ya Makukwe Entertainments, Suleiman Mathew, alisema katika mchujo huo yatapatikana makundi 12 yatakayoanza fainali za kwanza zitakazoanza Januari 16 mwakani.
Mathew alisema fainali za mwisho za kupata kundi bora la wanamuziki saba, zitafanyika Machi 6 kwenye ukumbi wa kimataifa wa Club Bilicanas jijini Dar es Salaam.
Mathew alisema, fomu za kushiriki shindano hilo zinapatikana ukumbi wa Afri Centre Ilala jijini Dar es Salaam kwa gharama ya sh 3,000.
Aidha, Mathew alitoa wito kwa vijana ambao wana vipaji vya kuimba na kutumia vyombo vya muziki, kujitokeza kushiriki shindano hilo ambalo nia yake ni kukuza na kuendeleza muziki wa dansi Tanzania.
Naye mmoja wa majaji watakaoteua washindi wa shindano hilo, mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choky, alisema, ni jambo bora lililoanzishwa na Makukwe Entertainment kwa kusaka warithi watakaoziba nafasi zao pindi watakapohamia katika ujasiriamali.
Naye Mkurugenzi wa bendi ya Hisia, Abdul Salvador ‘Father Kidevu', alisema asilimia kubwa ya Watanzania walizoea ladha ya muziki wa aina moja na kusahau kwamba kuna muziki wa dansi ambao upo tangu enzi za mababu.
Salvador alisema, muziki wa dansi kwa nchi zilizoendelea, ndio unaoshika kasi katika biashara ya muziki duniani, lakini wadau wenyewe hawauthamini.
 
Mchujo 'Music Dance Competitions' Afri Centre


na Makuburi Ally


amka2.gif
MCHUJO wa kwanza wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba muziki wa dansi ‘Music Dance Competitions’ unatarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 20 hadi 21 kwenye ukumbi wa Afri Centre Ilala jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), jijini Dar es Saalm jana, mkurugenzi wa kampuni ya Makukwe Entertainments, Suleiman Mathew, alisema katika mchujo huo yatapatikana makundi 12 yatakayoanza fainali za kwanza zitakazoanza Januari 16 mwakani.
Mathew alisema fainali za mwisho za kupata kundi bora la wanamuziki saba, zitafanyika Machi 6 kwenye ukumbi wa kimataifa wa Club Bilicanas jijini Dar es Salaam.
Mathew alisema, fomu za kushiriki shindano hilo zinapatikana ukumbi wa Afri Centre Ilala jijini Dar es Salaam kwa gharama ya sh 3,000.
Aidha, Mathew alitoa wito kwa vijana ambao wana vipaji vya kuimba na kutumia vyombo vya muziki, kujitokeza kushiriki shindano hilo ambalo nia yake ni kukuza na kuendeleza muziki wa dansi Tanzania.
Naye mmoja wa majaji watakaoteua washindi wa shindano hilo, mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choky, alisema, ni jambo bora lililoanzishwa na Makukwe Entertainment kwa kusaka warithi watakaoziba nafasi zao pindi watakapohamia katika ujasiriamali.
Naye Mkurugenzi wa bendi ya Hisia, Abdul Salvador ‘Father Kidevu’, alisema asilimia kubwa ya Watanzania walizoea ladha ya muziki wa aina moja na kusahau kwamba kuna muziki wa dansi ambao upo tangu enzi za mababu.
Salvador alisema, muziki wa dansi kwa nchi zilizoendelea, ndio unaoshika kasi katika biashara ya muziki duniani, lakini wadau wenyewe hawauthamini.
 
Sikinde, Msondo kumaliza ubishi


na Dina Ismail


amka2.gif
WAKONGWE wa muziki wa dansi nchini, Msondo Ngoma Music na Mlimani Park ‘Sikinde Ngoma ya Ukae' wanatarajiwa kufanya onyesho maalumu la mpambano kesho kwenye Ukumbi wa Millennium Tower, Makumbusho jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mratibu wa onyesho hilo lililoandaliwa na Chechi Advertising, John Momadi ‘Tall', mpambano huo ni mahsusi kwa kuzindua ‘Usiku wa Mwafrika' utakaokuwa ukirindima kila Jumatano.
Alisema, maandalizi kwa ajili ya onyesho hilo yamekamilika, hivyo mashabiki wajiandae kupata burudani ya aina yake kutoka kwa wakongwe hao.
Tall aliongeza kuwa kupitia mchuano huo watatambulisha baadhi ya nyimbo zao mpya zinazotarajiwa kuwemo kwenye albamu yao mpya itakayotoka hivi karibuni sambamba na kupigia nyimbo zao za zamani kama ‘Kicheko cha Jirani', ‘Huna Shukrani', ‘Mama Cosy', 'Kiapo', ‘Cheo ni Dhamana', ‘Haki yangu iko wapi', ‘Kimya kingi' na nyinginezo.
Aidha, Tall alisema, Sikinde itashuka na vibao kama ‘Hamnazo', ‘Sivyo Nilivyo', ‘Supu Umeitia Nazi', ‘Survive', ‘King Fish' na nyinginezo ambapo kiingilio katika onyesho hilo litakaloanza kurindima majira ya saa 3:00 usiku kitakuwa sh 10,000.
 
Mukubwa apata ajali Kenya


na Mwandishi wetu


amka2.gif
MWANAMUZIKI wa kimataifa wa Injili, Solomon Mukubwa, ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), anayefanya kazi zake nchini Kenya, amepata ajali ya gari akiwa mpakani mwa Kenya na Tanzania. Kwa mujibu wa Alex Msama ambaye ni mdau wa muziki wa Injili na promota wa mwimbaji huyo hapa nchini, ajali hiyo ilitokea Jumamosi.
Msama alisema, Mukubwa akiwa na Meneja wake, Rehema Lugore, walipata ajali hiyo mjini Nairobi wakiwa njiani kuelekea Silari, mpakani mwa Kenya na Tanzania.
Alisema, katika ajali hiyo meneja huyo ndiye ameumia sana sehemu za miguu kiasi cha kulazwa hospitalini nchini Kenya.
Akizungumzia zaidi tukio hilo, Msama alisema kuwa amepokea taarifa ya ajali hiyo kwa masikitiko makubwa, lakini akasema kitu cha kushukuru Mungu ni wahusika wote kuwa hai.
Mukubwa ni kati ya waimbaji waliojaaliwa kipaji cha utunzi na uimbaji aliyewahi kutamba na vibao kadha wa kadha vikiwamo vya ‘Mfalme wa Amani', ‘Mungu Mwenye Nguvu' na vinginevyo.
Msama kwa upande wake amesema anataraji kwenda nchini Kenya kumjulia hali Mukubwa, kwani ni mtu aliye karibu naye kwa kiasi kikubwa akiwa promota wake kwa upande wa Tanzania.
 
Tuesday December 07, 2010 Sports
Martina Navratilova ascends Kilimanjaro
By a Correspondent, 6th December 2010 @ 12:00, Total Comments: 0, Hits: 13

TENNIS legend Martina Navratilova on Monday embarked on her climb to the summit of Africa’s highest Mountain, Mt Kilimanjaro, in Moshi, to raise funds for the Laureus Sport for Good Foundation.

Martina is joined on the challenge by a team of 27, including German Paralympic cyclist Michael Teuber and British Olympic badminton star Gail Emms and a host of international fundraisers.

It will take the climbers six days to reach the summit. Martina, who battled breast cancer earlier this year, is raising funds for the Laureus Sport for Good Foundation, a charity which supports community sports projects around the world, which have helped to improve the lives of over one million young people.

Speaking as the team were about to depart on their expedition, Martina said: “I’ve been planning to climb Mt Kilimanjaro since early this year, even before my breast cancer diagnosis, so it feels really great to finally be underway.

I’m feeling well prepared for the challenge, and although I’m sure we’ll all be in for a tough few days of climbing, I am determined to reach the summit.

I am really pleased to be joined on the climb by a team of international fundraisers, and I hope everyone will support us by donating at www.laureus. com” Mt Kilimanjaro is the world’s highest freestanding mountain.

The expedition will ascend by the Rongai Route. The climb will take seven days. Before the climb Martina visited the Laureussupported Mathare Youth Sports Association (MYSA) project in Nairobi - the kind of project which will benefit from funds raised from the Kilimanjaro challenge.

Based in the largest and one of the poorest slums in Nairobi in which HIV/ AIDS and other diseases are widespread, the project has pioneered the use of football as a tool to encourage co-operation and raise selfesteem in the young people of the community.

Each year MYSA organises thousands of matches for around 20,000 young people, playing in over 1,000 leagues. Success is measured not just by the goals scored in matches, but by the work the young people do in cleaning up the slums.

MYSA has been supported by Laureus since 2000. It has been nominated for the Nobel Peace Prize for its work.
 
Tuesday December 07, 2010 Sports
Kili Stars face tough battle
By ABDALLAH MSUYA, 6th December 2010 @ 12:00, Total Comments: 0, Hits: 16

KILIMANJARO Stars assistant coach, Sylvester Marsh has said the Cecafa Tusker Challenge Cup quarter-final tie against Rwanda will be difficult, but he expects the home team will come out on top and eventually reach the semifinals.

Kilimanjaro Stars finished second in Group A, to set up the Amavubi clash in the last quarterfinal scheduled for tomorrow at the National Stadium in Dar es Salaam from 5:00pm.

Most of the players in the Kilimanjaro Stars still have bad memories of being dumped out of the African Nations Championship (CHAN) qualifiers by Rwanda mid this year.

The Amavubi secured their CHAN participation with a 2-1 aggregate win over Tanzania's Taifa Stars in June.

Marsh said: "The history of playing Rwanda in the past tells you it's going to be a very difficult tie for us. It is a fact that we're up against a good, experienced team, which will cause us problems. But we're a strong team too, and playing at home, we expect nothing but victory as we're determined to go through".

"We know there are a lot of expectations from our fans, the Tanzanians want us to win, and we promise that we'll work hard and fight for it and hopeful we won't let them down, there is a lot of improvement in the side," added Jan Poulsen's right hand man.

He is expecting for a huge home crowd that will stand behind them throughout, "Winning is what's important, but doing it in front of our fans is a bonus, the fans should rally behind their team, be patient and supportive.

"The coach (Poulsen) has done a good job to get the team where it is now despite having very little time to work with the players. He's a very good tactician and can take us forward. It's important that the fans put faith in their squad."

The former Kagera Sugar, Azam FC and national youth coach said his team is well prepared for tomorrow's match, "Hopeful we'll have everyone we need for the game and we've got a good chance."

Despite of a potential semi-final clash with defending champions Uganda cranes, Marsh believes that Stars can have great chance to end their 16-years wait for the coveted regional trophy, if they overcome Rwanda on Wednesday.

"The tournament is tough and it is going to be difficult but we have to do it because if we want to be the best we have to compete," he said.

After a false start to this year's regional championship losing 1-0 to Zambia, Stars bounced back to beat Somalia 3-0, and confirmed their place in the quarter-final with an outright 2-0 win over Burundi.

The performance won approval from thousands of local soccer fans, who however warned players not to be carried away by their recent wins, but keep their concentration and focus to win the tournament's silverware that has eluded the Mainland side for the past 16 years.
 
CHAMA cha Gofu Tanzania (TGU) kimeweka hadharani kalenda yake ya mashindano ya mwaka 2011.
Kalenda ya gofu 2011 hii hapa
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 6th December 2010 @ 23:20 Imesomwa na watu: 19

Kwa mujibu wa kalenda hiyo iliyotolewa na Ofisa Tawala wa TGU, Sophie Nyanjera Dar es Salaam jana na HABARI LEO kupata nakala yake, michuano ya wazi ya gofu ya Morogoro itakayofanyika kwenye Viwanja vya Klabu ya Gymkhana Morogoro ndio itakayofungua kalenda ya mwaka.

Hata hivyo, kwa mujibu wa kalenda hiyo michuano ya Kombe la Mwenyekiti na Bingwa wa Mabingwa ambayo ni kiporo cha mwaka 2010 itatangulia kabla ya michuano hiyo ya wazi ya Morogoro.

Michuano ya Kombe la Mwenyekiti ambayo awali ilikuwa ifanyike mwezi huu imesogezwa mbele kuanzia Januari 8 hadi 9 na Bingwa wa Mabingwa itakuwa Januari 11 hadi 12 yote kwenye viwanja vya Klabu ya Gymkhana, Moshi.

Katika kalenda hiyo inaonesha michuano ya Match Play ndio itakayofuata Februari 23 hadi 25 kwenye Viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam na kufuatiwa na Michuano ya Stroleplay ya Ridhaa Tanzania Machi 16 hadi 18 TPC, Moshi.

Mbali na michuano ya kitaifa pia michuano ya kimataifa ambayo TGU inakusudia kupeleka timu imeainishwa kwenye kalenda hiyo mpya.

Michuano ya kimataifa ni pamoja na ile ya Afrika ya vijana chini ya umri wa miaka 19 ambayo hata hivyo haijaonesha tarehe na mahali itakapofanyika, Kanda ya Sita Afrika imepangwa kufanyika Nairobi, Kenya lakini tarehe haijawekwa wazi na michuano ya Kombe la Challenge Afrika Mashariki ambayo itapigwa kwenye Viwanja vya Gymkhana Arusha Novemba 8 hadi 11.

Nyanjera alisema tarehe na miezi itakayofanyika michuano hiyo ya kimataifa zitajulikana baadaye. Kalenda hiyo inaonesha michuano 25 itafanyika ndani na nje chini ya usimamizi wa TGU ndani ya miezi 12 ijayo.
 
Nourdin aomba ushirikiano kuing'oa Rwanda
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 6th December 2010 @ 23:30 Imesomwa na watu: 110

MCHEZAJI wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars' Nourdin Bakari ametoa shukrani kwa mashabiki wa soka nchini na wachezaji wenzake kwa kufanikisha kufika hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Chalenji.

Stars ilifikia hatua hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuifunga Burundi mabao 2-0 yote yakifungwa na Bakari na sasa inatarajiwa kucheza na Rwanda katika robo fainali kesho.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Bakari alisema asingeweza kufunga mabao hayo kama si ushirikiano mzuri na wachezaji wenzake pamoja na mashabiki waliojaa uwanjani siku hiyo.

"Mashabiki walijaa sana uwanjani siku ile nilijisikia furaha kubwa kwani kelele zao zilikuwa zikinihamasisha kutafuta bao kwa vile tusingeshinda mechi ile mashabiki wetu wangerudi majumbani mwao wanyonge sana,"alisema.

"Lakini pia napenda kuwashukuru wachezaji wenzangu kwa ushirikiano mkubwa walionipa wote kwa pamoja tulicheza kwa ari kubwa kupata ushindi,"alisema.

Bakari alifunga bao la kwanza kwa krosi ya Mrisho Ngassa na bao la pili alifunga kwa juhudi zilizofanywa na Ngassa kabla mpira haujamfikia Shadrack Nsajigwa aliyempa pasi mfungaji.

"Sasa tusibweteke, najua kwamba tunatakiwa kukaza buti ili tufike nusu fainali na baadaye fainali hivyo nawaomba wachezaji wenzangu na mashabiki kwa ujumla waje kwa wingi katika mechi yetu na Rwanda kutupa hamasa ya ushindi zaidi," alisema.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom