Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #2,941
TanTrade: Wasanii fanyeni utafiti masoko ya sanaa
na Mwandishi wetu
SERIKALI imetoa wito kwa wasanii kufanya tafiti mbalimbali za mauzo ya kazi zao na kupanga bei stahili ili kukuza na kuendeleza soko la ndani na kupata soko bora la nje.
Akizungumza katika jukwaa la sanaa mwanzoni mwa wiki hii, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Masoko ya Ndani wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Edwin Rutageruka, alisema inatakiwa wasanii kukuza soko la ndani ili kufanikisha soko la nje.
Rutageruka alisema changamoto inayolikabili soko la ndani kwa wasanii ni kutothamini kazi zao, ambako sanaa ya Tanzania inapendwa nje kwa vitu kama mti wa mpingo, nguo za Tanzania zinazotengenezwa na malighafi mbalimbali na ufumaji wa vikapu.
Changamoto nyingine zinazoikabili tasnia ya sanaa ya Tanzania ni kupenda bidhaa za nje na kutokuwa wazelendo wa kupenda vya kwetu, mtandao wa usambazaji umekaa vibaya sambamba na tatizo la vituo vya kusambazia.
Aidha, Rutageruka alisema wasanii wa Tanzania hawako tayari kwa soko la nje kwa sababu ya bidhaa zao kutokuwa na ubora, ubinafsi wa wasanii wenyewe, uwezo mdogo wa uzalishaji, kutokuwa na biashara kwa njia ya mtandao, ufungaji wa bidhaa, kuitangaza na kuisambaza na tafiti za masoko.
Alitoa wito kwa wasanii na wasambazaji wa kazi za sanaa kuunganisha nguvu na TanTrade ili kufanikisha maendeleo stahili ya tasnia hiyo ambayo yakifanikishwa ipasavyo tasnia hiyo itapiga hatua ipsavyo.
Rutageruka alisema sababu nyingine inayoshusha maendeleo ya sanaa ni kubweteka kwa wasanii baada ya kupata mafanikio ya awali na baada ya mafanikio ya kwanza wasanii hubweteka.
Naye Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa, Ghonche Materego, alisema wamejipanga kuandaa banda la Basata katika maonyesho ya Sabasaba mwaka huu ambalo litashirikisha kazi mbalimbali za sanaa.
Materego alisema banda hilo litaonyesha kazi mbalimbali za sanaa ambalo litafanikisha kazi zaidi za wasanii sambamba na tamasha la Uhuru linalofanyika Desemba ya kila mwaka, ikiwa ni mojawapo ya changamoto ya kukuza na kuendeleza kazi za sanaa hapa nchini.

PRINT