Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #3,181
Kuwaona Wabrazil leo 5,000/-
na Dina Ismail
WAKATI timu inayoshiriki Ligi Kuu ya soka nchini Brazil, Atletico Paranaense, leo inashuka katika dimba la Uwanja wa Taifa kukipiga na Yanga, kiingilio cha juu katika mechi hiyo kimepangwa kuwa sh 200,000 kwa watakaokaa jukwaa la VIP A huku cha chini kikiwa sh 5,000 kwa watakaokaa jukwaa la kijani.
Atletico iko nchini kwa ziara maalumu ya kimichezo chini ya uratibu wa kampuni ya RBP Oil &Industrial Technology inayomiliki timu ya African Lyon inayoshiriki Ligi Kuu Bara, ambako ujio huo ni mahsusi kwa uzinduzi wa timu hiyo.
Pamoja na kucheza na Yanga leo, timu hiyo Alhamis itacheza na mabingwa wa Ligi Kuu Bara Simba ambako pamoja na viingilio hivyo vya juu na vya chini, watakaokaa VIP B watalipa sh 100,000, VIP C sh 50,000 na wayakaokaa viti vya rangi ya chungwa watalipa sh 10,000.
Wakizungumzia mechi zao mbele ya waandishi wa habari, makocha wa Yanga Kostadin Papic na Patrick Phiri wa Simba, wamesema zina manufaa sana kwao na hasa ikizingatiwa wako katika maandalizi ya michuano ya kimataifa.
Papic alisema, pamoja na umuhimu wa mechi hiyo, lakini hawezi kupata picha halisi ya kikosi chake na hasa ikizingatiwa kuwa baadhi ya wachezaji wake wanaandamwa na majeruhi, huku wengine wakiwa katika timu ya Taifa iliyokuwa nchini Misri kushiriki michuano ya Nile Basin.
Naye Phiri alisema, mechi hiyo itawapa mafunzo tosha wachezaji wake katika kuelekea kwenye michuano ya kimataifa, pia kufahamu hatua waliyofikia wachezaji wake kabla ya kushiriki michuano hiyo.

PRINT