Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Mourinho downbeat after loss


RivalsDM



PRINT RSS



Updated Jan 31, 2011 6:07 AM ET
Jose Mourinho could not fault Real Madrid as they lost to Osasuna - but admits it makes their pursuit of Barcelona "much more difficult".
A second-half strike from Javier Camunas earned 17th-place Osasuna the spoils in a hard-fought came at the Reyno de Navarra stadium and consigned Madrid to only a second league defeat of the season.

Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats

The defeat means Mourinho's men are now seven points adrift of in-form Barca - who have won 15 successive matches in La Liga - at the top of the table, and was a major blow to the capital club's hopes of winning a first league title since 2008.
Mourinho said after the game: "My players have done their jobs with dignity and I have nothing to reproach them for, they fought to the end. We lost three points that we didn't deserve to lose.
"Osasuna are a tough team and the crowd was fantastic. I don't think many teams win here. We had opportunities to score in both halves, but we haven't done it. And if the opponents score first it is very difficult. Congratulations to Osasuna."
The Portuguese added: "This is our second defeat in La Liga and we are in a much more difficult situation with respect to first place.
"I always tell my teams that I don't like to gift games to the opposition, by not playing, not fighting or because we were relaxed...that wasn't the case. We lost against a team who gave it everything, and who had a week to prepare for the match."
Madrid, who were held to a 1-1 draw by then-bottom club Almeria in their previous away game, do not have long to dwell on their defeat as they have an important match on Wednesday when they host Sevilla in the second leg of their Copa del Rey semi-final.
Madrid lead 1-0 from last week's first leg as they look to win the cup for the first time since 1993.
Mourinho said: "Tomorrow is another day. We will be thinking about the game on Wednesday."
Madrid midfielder Xabi Alonso, who started the match on the bench as he was struggling with illness, added: "With this defeat the distance to Barcelona has grown, but there's a long way to go and we need to continue fighting until the end.
"We know that it won't be easy, but we need to look ahead and continue with the good work we have been doing. We cannot give up.
"We need to look ahead and think first about the cup game against Sevilla and then the next league game (at home to Real Sociedad)."
 
Valencia's Mata to miss Monday's match at Racing


storypage_APlogo_01.png




PRINT RSS

0 comments »

Updated Jan 30, 2011 10:00 AM ET
Valencia's Juanma Mata will miss Monday's match at Racing Santander due to injury.
The Spain international hurt his left ankle in training on Friday and has been left out of the squad.
Valencia is fourth in the Spanish league after winning its last five games. During that run, Mata has scored three goals, including two late winners.
The 22-year-old forward recently agreed to a two-year contract extension that will keep him at the Spanish club until 2014.
 
Papic: Nasubiri nipewe haki zangu Yanga Monday, 31 January 2011 21:04

Clara Alphonce
PAMOJA na Mwenyekiti wa Yanga Lloyd Nchunga kumuandikia barua Kocha Mkuu Costadin Papic ya kumtaka kuendelea kuinoa klabu hiyo kwa mwezi mmoja tena kocha huyo amesema hataki tena biashara ya Yanga na anaondoka kesho.

Papic aliyebwaga manyanga wiki iliyopita kwa sababu mbalimbali, amekuwa akitajwa kuwa na mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo, lakini jana alisema kuwa anaondoka, na hana maamuzi ya kurudi nyuma.

Nchunga alimuandikia barua ya kumtaka Papic aendelee kuinoa timu hiyo kwa mwezi mmoja kabla ya kuondoka kwa madai kuwa hajamaliza mkataba wake, pia hajakamilisha baadhi ya mambo waliokubaliana.

Akizungumza na Mwananchi, kocha huyo alisema kuwa kwa sasa hataki tena kubaki Yanga pamoja na Mwenyekiti kumtaka kuendelea kuinoa timu hiyo kwa sasa hayupo tayari tena.

''Naondoka Yanga ila sio leo (jana) kwani bado nasubiri fedha zangu kutoka kwa Yanga na sasa ninavyoongea na wewe niko klabu nasaiti kupata fedha zangu ndio niondoke Yanga siwezi kuacha hela zangu'' alisema Papic.

Alisema pamoja na kungojea fedha zake pia anafuatilia tiketi yake kutoka kwa Uongozi kwani mpaka sasa bado hawajampa hivyo itakuwa ngumu yeye kuondoka.

Hata hivyo habari zilizopatikana jana kuwa kucha huyo huenda akaondoka kesho kwenda nchini Serbia na kusisitiza kuwa maisha popote sio Yanga peke yake.

Pamoja na kusisitiza kuondoka, habari zilizopatikana baadaye jana zilisema kuwa Nchunga amemwandikia Papic aeleze kama kuna kitu anachokidai Yanga au wao wanachokidai kutoka kwake ili waweze kuagana vema bila ya kuwa na utata wowote.

ìLengo letu tuwe na maelezo ya kina kuhusiana na matumizi ya fedha hasa wakati huu wa uhakiki wa mahesabu, unatakiwa kusema umechukua kiasi fulani na umekitumia kwa lengo fulani huku ukionyesha vithibitisho, huo ndiyo ukweli wa suala hili,î alisema Nchunga kwa simu.

Mbali na hilo, Nchunga pia alisema uongozi unamtaka Papic kuwapa maelezo ya kina kuhusiana na usajili wa kipa Ivan Knezevic ambaye amedhihirisha kuwa hana uwezo wa kucheza mashindano kama ya Ligi Kuu. Mchezaji huyo hajacheza hata mechi moja ya ligi.

Pia mwenyekiti huyo amemtaka Papic kutoa maelezo ya kina kuhusiana na utata wa usajili wa mchezaji, Kenneth Asamoah ambaye mbali ya kusaini mkataba na Yanga, hakuwahi kuichezea timu hiyo.

Imebainika kuwa Asamoah alisajiliwa Yanga kwa kulipwa si chini ya dola 15,000 wakati Knezevic alisajiliwa kwa dola 10,000 kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Wakati huo huo, baadhi ya wachezaji wa Yanga wamesema hawana taarifa za kupigwa kwa Nsa Job mara baada ya mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya Yanga na Dedebit ya Ethiopia kumalizika kwenye Uwanja wa Taifa na timu hizo kutoka sare ya mabao 4-4.

Mmoja wa wachezaji mkongwe alisema kuwa yeye binafsi hajaona tukio la kupigwa kwa Nsa na mabashabiki ikiwa nje na ndani ya gari kama ilivyodaiwa.

ìHizo ni habari mpya kwangu, tulimaliza mechi na kuingia kwenye vyumba, mara baada ya kutoka kwenye vyumba, tukaingia kwenye basi na kuondoka, sasa kama mtu alipigwa kwenye basi aliingiaje na kama ilikuwa nje ni wakati gani, maana hakukuwa na fujo siku hiyo,î alisema mchezaji huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Nahodha wa Yanga, Fred Mbuna naye alisema kuwa hajaona Nsa akipigwa siku hiyo zaidi ya kusikia maneno kutoka kwa watu wa Yanga kuwa ametuhumiwa akipewa pesa za kuwahonga wao ili wacheze chini ya kiwango huku akikanusha tukio la kuhongwa.

ìMimi nilikuwa naye uwanjani, tukatoka, sasa alipigwa wapi, baada ya kuondoka uwanjani, tulirudi majumbani kwetu, jana (juzi Jumapili), nikasikia wamepelekana polisi kupitia kwa mshikaji (rafiki) yangu,î alisema Mbuna.

Nsa mwenyewe alisema kuwa alipigwa na chupa uwanja wa Taifa wakati akienda kwenye gari lake, lenye namba za usajili T112 BKU aina ya Vitz, na waliompiga walimwambia kuwa wametumwa na Matokeo.

ìMimi siwajui hao watu, jina ambalo wamelitaja lilikuwa la Kibwana ambaye namfahamu, nikaenda kutoa taarifa kituo cha Polisi Msimbazi na kupewa jalada namba MS/RB/1112/2011,î alisema Nsa.

Alisema kuwa amechukua tahadhari hiyo ili kuhofia maisha yake na ameumia sehemu ya juu ya pua, japo ni kidogo.

Wakati Nsa anasema hayo, Kibwana Matokeo alikanusha taarifa hizo ambazo zilikuja baada ya yeye kupigwa na kwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi, Oysterbay.

Matokeo alisema kuwa baada ya kupigwa majira ya saa 5.00 alikwenda kufungua jalada namba OB/RB/1860/2011/shambulio, ambalo lilifanyika kwenye Baa ya Rose Garden.

Aliendelea kusema kuwa alikwenda kwenye baa hiyo baada ya mazoezi ya timu yake ya Rose Garden na alibaki kuduwaa wakati akiwa anashambuliwa na Mosha ambaye ni makamu mwenyekiti wa Yanga.
 
Phiri: Tatizo tuliwadharau Elan
Monday, 31 January 2011 20:56

Sweetbert Lukonge
KOCHA mkuu wa Simba, Patrick Phiri amesema kuwa historia ya zamani timu za Tanzania kuzifunga za Comoro ndiyo hasa iliyosabibisha washindwe kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliofanyika mwishoni mwa wiki.

Simba ilianza safari yake Jumamosi iliyopita dhidi ya Elan Club de Mistsoudje ya nchini Comoro na kushindwa kufanya vizuri katika mchezo huo baada ya kutoka suluhu.

Akizungumza na Mwananchi jana, Phiri alisema kuwa kujiamini na kuamini historia ya zamani ya soka la Comoro kuwa chini ndiyo iliyosabibisha wachezaji wake waliingia uwanjani wakijua kuwa tayari wameshinda mechi hiyo.

"Historia ya zamani ya Comoro katika soka ndiyo hasa iliyosabisha tutoke suluhu katika mechi hiyo kwa sababu vijana pamoja na watu wote tuliamini tutashinda mechi hiyo.

"Baada ya kuingia uwanjani, ndipo tulipogundua kuwa kumbe mambo yalikuwa ni tofauti na tulivyofikiria na ndipo vijana ikabidi wapambane ili kuhakikisha hawapotezi mechi hiyo.

"Namshukuru Mungu kwa kutuwezesha kutoka sale kwani hatua hiyo ni faida kwetu, hivyo jambo kubwa na la msingi ni kuhakiksha tunajipanga kwa ajili ya mechi ijayo ya marudiano ili tuweze kushinda mchezo huo na kusonga mbele katika hatua inayofuata," alisema Phiri.

Alisema Comoro ya sasa ni tofauti na miaka iliyopita ambayo timu zake zilikuwa zikichezea kichapo cha maana kila zilipokutana na timu za Tanzania, lakini kwa sasa soka la nchi hiyo lipo juu na kuongeza kuwa hii ni kutokana na wachezaji wa nchi hiyo kuwa na tabia ya kwenda kucheza soka nchini Ufaransa," alisema Phiri.

Kwa upande wake mshambuliaji wa timu hiyo Mussa Mgosi alisema kuwa tatizo lililosababisha washindwe kuibuka na ushindi katika mchezo huo ni kuamini kuwa soka la Comoro lipo chini na timu za nchi hiyo hazina historia ya kuzifunga wala kutoka sale na zile za Tanzania.

"Kujiamini zaidi na kujua kuwa tutashinda mechi hiyo ndiyo hasa kulisabisha mambo kuwa magumu zaidi kuliko tulivyofikiri, mbali na hilo pia wenzetu tayari walikuwa wanatujua tofauti na sisi ," alisema Mgosi.

Naye mkuu wa msafara wa timu hiyo, aliyekuwa akiliwakilisha Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Shaibu Nampunde amelitaka benchi zima la ufundi la Simba kuhakikisha wanazifanyia kazi kasoro zote zilizojitokeza katika mechi hiyo.

Simba iliwasili jana ikitokea Visiwa vya Comoro kujiandaa na mechi yake ya marudiano na ikishinda mchezo huo itapambana na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

 
Aliyeshindwa ZFA amdai Ferej Sh100mil Monday, 31 January 2011 20:55

Salma Said, Zanzibar
RAIS wa Kamati ya Muda ya Chama cha Soka Zanzibar, ZFA, Ali Ferej Tamim ameingia katika wakati mgumu baada ya waliokuwa wagombea nafasi ya urais na makamu wa ZFA kumpa wiki moja na awalipe fidia ya sh100mil kwa madai ya kuwakashifu .

Hatua hiyo inakuja wakati Fereji na wenzake kurudishwa madarakani kwa muda wa miezi mitatu ili warekebishe katiba ya chama hicho na kuandaa uchaguzi mkuu mwingine baada ya ule wa awali kubatilishwa

Walalamikaji ni pamoja na aliyekuwa mgombea urais, Suleiman Mahmoud Jabir na makamu wake, Aman Ibrahim Makungu ambao walidai Ferej aliwakashifu mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu uliofanyika Desemba 31 mwaka jana.

Barua ya kampuni ya mawakili AJM Solicitors of Advocate Chamber yenye kumbukumbu namba KK.NO.AJM/MJD/019/2011 ya Januari 20 mwaka huu na kusainiwa na wakili Rajab Abdalla Rajab na kutumwa kwa Ferej, ilidai kashfa hizo zilitolewa wakati kiongozi huyo akitoa hutuba ya mkutano mkuu.

Amedai kauli za Ferej mbele ya wajumbe zimepelekea wateja wake ziwashushie hadhi mbele ya jamii na kuwajengea dhana kuwa ni watu wasiofaa katika jamii kwa tuhuma nzito ambazo hakuwa na uhakika nazo.

Katika tuhuma zilizoelekezwa kwa Makungu imedaiwa Ferej aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa ni mtoa rushwa na mara zote amekuwa akiwahonga viongozi wa ZFA ili timu yake iweze kushinda na hivyo ni mchangiaji mkuwa wa kuuwa soka la Zanzibar

ìTuhuma hizo nzito zisizokuwa na uthibitisho mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu na waalikwa zimemuumiza mteja wangu na kumshushia hadhi yake mbele ya jamii na hivyo kusababaisha athari kubwa,î ilisomeka sehemu ya barua hiyo.

ìWateja wangu ni watu maarufu san a na wanaheshima kubwa katika jamii kupitia vyombo vya Habari nakutaka uwaombe radhi wateja wangu dhidi ya tuhuma ulizozitoa zilizokosa chembe za ukweli îInasomeka barua hiyo ya kurasa mbili

Madai hayo kwa Rais huyo yamekuja zikiwa zimepita siku chache tangu iliyokuwa kamati ya uchaguzi wa chama hicho ibatilishe matokeo ya uchaguzi kutokana na kujitokeza mapungufu mengi ya Fereji kushindwa kuthibitsha elimu ya kidato cha nne

Hata hivyo, habari nyengine zinadai kesi inayohusu wadau wa soka iliyowasiliswa mahaka kuu dhidi ya Ferej na wenziwe huenda ikaanza kutajwa wiki ijayo baada ya kupangiwa Jaji Abraham Mwampashe aisikilize

Wamaolalamikiwa ni Ferej , Makamo wa Rais Haji Ameir ,Mrajis wa vyama vya michezo Mustafa Omar ,Katibu mkuu wa ZFA, Mzee Zam Ali na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa, Sherry Khamis

Madai makuu ya shauri hilo ni kwamba kwa nyadhifa zao walishindwa kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa ZFA huku wakijuwa umejaa mapumgufu mengi ya kikatiba na kwamba Rais na Makamo wake hawana uhalali wa kuongoza chama hicho kwa vile muda wao ulimalizika tangu Septemba 30 mwaka jana.

 
Migogoro Yanga yamsononesha 'SMG'
Monday, 31 January 2011 20:53

Imani Makongoro
MSHAMBULIAJI wa zamani wa klabu ya Yanga, Said Maulid ìSMGî anaondoka nchini leo kwenda Angola na baadaye Brazil huku akiacha ujumbe kuwa ìYanga iachane na migogoroî na timu ya Taifa inaweza kufanya vyema endapo maandalizi ya kina yatafanyika katika mechi zilizobaki.

Mchezaji huyo anayechezea timu ya Bravo de Marquiz amesema kuwa tofauti za viongozi zinatakiwa ziepukwe kwani klabu inakabiliwa na mashindano makubwa ambayo utulivu na amani ndio nguzo pekee.

Alisema kuwa hali iliyopo ndani ya klabu hiyo inawachanganya wachezaji kwani viongozi (nguzo ya timu) inayumba.

ìYanga kuna tatizo ambalo dawa yake ni kutatatuliwa mapema kabla ya mechi ya marudiano na timu ya Dedebit SC ya Ethiopia, wachezaji wanachanganywa na taarifa za mgongano ndani ya klabu, watafanya nini,î alisema Maulid.

Alisema kuwa wachezaji wamesajiliwa na viongozi na anadhani kama wangekuwa wanajua ìkutatokea mgogoroî, hakuna mchezaji ambaye angesajili.

ìDawa hapa ni kuondoa tofauti kwa kukaa pamoja na kugundua nini chanzo, hali hii siyo nzuri kabisa,î alisema Maulid ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili zaidi kuichezea timu hiyo ya Angola.

Kuhusiana na timu ya Taifa, Maulid amesema kuwa amefarijika na nidhamu ya hali ya juu na kuwataka wachezaji kucheza kwa kujituma zaidi na kuleta mafanikio makubwa.

Alisema kuwa mechi dhidi ya Afrika ya Kati, Algeria na Morocco si za kuzibeza, lakini maandalizi ya kina ndiyo njia pekee ya kufanya vyema.

ìNi timu ngumu, lakini mpira ni mmoja, lazima tukubali kuwa tunahitaji timu ya ushindani na maandalizi ya kina vile vile, kwani hata wao wanasaka ushindi,î alisema.
Alisema kuwa akifika Angola, atakaa siku moja na kwenda Brazil kujiunga na wenzake ambao wako kambini.
 
Ukanda wa CECAFA wachemsha Afrika Monday, 31 January 2011 20:52

Ibrahim Bakari na Mashirika
BAADHI ya klabu za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati chini ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na kati, CECAFA, zimeshindwa kuwika katika michuano ya klabu Afrika, kwa mechi za mwishoni mwa wiki.

Klabu kadhaa zimeambulia zaidi sare huku nyingine zikipoteza mechi zake, ikiwa ni za hatua ya awali ya michuano hiyo. Mechi za marudiano zitachezwa wiki mbili baadaye.

Mabingwa wa Kenya, Ulinzi, walishindwa kutumia uwanja wake wa nyumbani baada ya kutandikwa mabao 4-0 na Zamalek ya Misri ikiwa ni mchezo wa kwanza hivyo kuweka nafasi finyu ya timu hiyo kusonga mbele.

Timu nyingine ya ukanda huo ni APR FC ya Rwanda iliyotoka sare ya 2-2 na Club Africain ya Tunisia. Mechi ya marudiano itakuwa mjini Tunis na kuipa nafasui kubwa timu hiyo ya afrika Kaskazini.

Mabingwa wa Burundi, VitalíO FC, ikiwa nyumbani, nayo ililazimishwa sare ya 2-2 na Coton Sport ya Cameroon na kutoa nafasi kubwa kwa timu hiyo ya Cameroon kujiweka katika mazingira mazuri zaidi.

Mabingwa wa Angola, Club Recreativo Caala waliichakaza mabao 2-0 Saint George ya Ethiopia mechi iliyopigwa kwenye mji wa Luanda huku Elan Club de MitsoudjÈ ya Comoro ikitoka suluhu na mabingwa wa Tanzania, Simba mchezo uliofanyika Moroni.

Mbali na timu hizo, pia mabingwa wa Zanzibar, Ocean View wakicheza nyumbani, walilazimishwa sare ya 1-1 na mabingwa wa DR Congo, AS V. Club mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Amaan.

Katika Kombe la Shirikisho, klabu za CECAFA hazikuonyesha makeke yake kwani KMKM ya Zanzibar ilisaklimu amri kwa kufungwa mabao 4-0 na DC Motema Pembe ya Congo DR huku Yanga ikilazimisha sare ya 4-4 na Dedebit ya Ethiopia. Timu zote hizo ziko chini ya CECAFA.

AC Leopards Dolisie (Congo) ilitoka sare ya 1-1 na wawakilishi wa Rwanda, Etincelles wakati Mbabane Highlanders ya Swaziland ikiwa nyumbani, ilitoka sare ya 1-1 na Victors ya Uganda.

Wawakilishi wa Gabon, Missisle walitumia vema uwanja wao wa nyumbani kwa kuichakaza Interstars ya Burundi mabao 4-0 wakati wawakilishi wa Kenya, Sofapaka walitoka suluhu na AS AviaÁao ya Angola.

Matokeo ya Ligi ya Mabingwa Afrika, yalikuwa mabaya zaidi kwa Tourbillon ya Chad iliyomiminiwa mabao 10-1 na Raja Club AthlÈtic ya Morocco. Timu hiyo inatakiwa kufunga mabao 10-0 iweze kufuzu raundi ya kwanza huku ikijivunia bao la ugenini.

Mabingwa wa Zambia, Zesco United iliifunga Liga Desportiva M. ya Msumbiji mabao 3-0 huku AS Forces ArmÈes Nigeriennes ya Niger ikitoka suluhu na JCAT ya Cote díIvoire.
 
Ji-sung astaafu rasmi timu taifa Monday, 31 January 2011 20:53

SEOUL, Korea Kusini
MSHAMBULIAJI wa Manchester United na Korea Kusini, Park Ji-sung ametangaza rasmi kustaafu soka ya kimataifa mbele ya waandishi wa habari.

Nahodha huyo wa Korea aliyecheza mechi 100 za timu ya taifa zilizokamilika katika michuano ya Asian Cup na timu yake kuishia robo fainali, michuan o iliyomalizika kwa Japan kutwaa ubingwa huko Doha, alisema matatizo ya goti ndiyo yanayomsukuma kufanya hivyo.

ìNi heshima na fahari kubwa kuchezea timu ya taifa,î Park aliwaambia wandishi wa habari kwenye mji wa Seoul.

ìJuu ya yote, vilevile napenda kuwaambia wachezaji wenzangu waliosalia kuwa wajitume na kufanya kweli katika timu,î alisema. ìKama nisingekuwa majeruhi, ningeendelea kuitumikia timu yangu ya taifa. Hata hivyo, sina jinsi zaidi ya kustaafu soka."

Park alimtaja Son Heung-min wa Hamburg SV na Kim Bo-kyung wa Cerezo Osaka ni kati ya wachezaji anaowaamini kuwa wanaweza kuziba nafasi yake.

Mchezaji huyo ambaye ni kati ya wachezaji wenye mafanikio makubwa, amkuwa mchezaji wa kwanza wa Korea kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Manchester United na ilifungwa katika fainali na Barcelona. Aliisaidia timu yake kutwaa ubingwa na mara tatu Kombe la Ligi akiwa na klabu hiyo ya England.

Park ni kati ya wachezaji makini, aliisaidia timu yake ya Korea Kusini kucheza nusu fainali ya Fainali za Kombe la Dunia 2002 na pia alikuwa kwenye fainali za Kombe la Dunia 2006 na 2010.
 
Kostadin Papic akwama kuondoka


*Anadai mpaka kieleweke

Na Elizabeth Mayemba

KOCHA Mkuu wa Yanga Kostadin Papic jana amekwama kuondoka nchini kwenda kwao Serbia kwa madai kwamba
hadi uongozi wa klabu hiyo, utakapomlipa fedha zake.

Papic amelazimika kuachana na Yanga ghafla, baada ya kusigana na viongozi wa klabu hiyo kwa madai ya kutoshirikishwa kwa baadhi ya vitu vya kiufundi ikiwemo kumteua, Felix Minziro kuwa msaidizi wake kitu ambacho hakuafikiana nacho.

Kocha huyo awali aliutaka uongozi wa Yanga, kumtafutia msaidizi ambaye atakuwa hajatoka kwenye timu zinazocheza Ligi Kuu kama ilivyo kwa Minziro ambaye kabla ya kuteuliwa alikuwa Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting.

Habari zilizopatikana Dar es Salaam jana kutoka kwa mtu wa karibu na kocha huyo zilidai kwamba, Papic alikuwa aondoke nchini jana lakini ameshindwa kwa kuwa kuna vitu vinamkwamisha ikiwemo malipo yake kutoka kwa viongozi wa Yanga.

"Jamaa amekuwa mgumu kubaki nchini ameng'ang'ania kurudi kwao na uongozi umeshindwa lakufanya na kumuacha aamue analolitaka, kwani kama kumbembeleza wamefanya hivyo sana, lakini amekuwa mgumu kuelewa," alidai rafiki wa karibu na kocha huyo.

Alidai kwamba kocha huyo kuna fedha za nyumba, ambazo anaidai klabu hiyo hivyo wakimalizana wakati wowote anarudi kwao Serbia.

Habari hizo zinadai kuwa kocha huyo ameweka msimamo wake wa kuondoka kwa madai kwamba hawezi kufanya kazi na Minziro wala Meneja wake Salvatory Edward.

Alipotafutwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Lloyd Nchunga ili kupata ufafanuzi zaidi kuhusu madai ya Papic, hakuweza kupatikana baada ya simu yake ya mkononi kuwa imezimwa.




1 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... papic inatosha,,ondoka zako kwani kuwepo hapo tena,,utaigawa yanga yetu,,waserbia hamna jipya zaidi ya 50% za kusajili wachezaji hewa kina mba,,boakye...wa tz wengi wanajua mpira,,tumwache mzawa,,akiwezeshwa ataweza,..
January 31, 2011 8:44 PM
 
Ufanisi unahitajika kamati za TFF
Monday, 31 January 2011 07:19

tenga1.jpg
Rais wa TFF,Leodgar Tenga

WIKI iliyopita Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF lilitangaza majina ya wajumbe waliopendekezwa kuunda kamati ndogondogo za Shirikisho hilo.

Kamati hizo ndogondogo ambazo zitakaa madarakani kwa kipindi cha miaka miwili zitakuwa zinafanya kazi kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya TFF.

Kwa ujumla TFF haijafanya mabadiliko makubwa katika kamati hizo kulinganisha na kipindi kilichopita hivyo tunaamini wenyeviti wa kamati hizo na wajumbe wao hivi sasa wana uzoefu wa kutosha kuziongoza kamati hizo na kutoa uamuzi sahihi.

Tunasema hivyo kwa sababu kamati hizo zina majukumu makubwa katika kuhakikisha ubora wa soka la Tanzania kupitia Shirikisho la soka.

Pia tunasema hivyo kwa sababu tunafahamu kamati hizo zinashughulikia masuala ya fedha na mipango,kuandaa mashindano,kushghulikia masuala ya ufundi na maendeleo ya soka, kusimamia soka la vijana, kusimamia waamuzi, kushughulikia masuala ya habari na masoko, kusimamia masuala ya katiba,sheria na hadhi za wachezaji, kusimamia masuala ya matibabu kwa wachezaji,kusimamia ukaguzi wa akaunti za Shirikisho, kusimamia uchaguzi wa Shirikisho, kushughulikia masuala ya nidhamu na kushughulikia rufaa.

Tunatarajia wale wote waliopendekezwa kuwa katika kamati hizo ndogondogo ndogo watafanya kazi kwa ufanisi ili kuleta maendeleo ya kweli ya soka Tanzania.

 
Zanzibar Ocean View yabanwa mbavu


Na Mwajuma Juma, Zanzibar

WAWAKILISHI wa Zanzibar kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika, Zanzibar Ocean View wameshindwa kuutumia vyema
uwanja wao wa nyumbani, baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na AS Vital Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), katika mechi iliyochezwa juzi Uwanja wa Amaan saa 2 usiku.

Katika mechi hiyo, tizo zilikianza kipindi cha kwanza kwa nguvu huku kila moja ikitaka kupata mabao lakini hata hivyo mabeki wa pande zote walikaa imara kuondoa hatari.

Mabao yote yaliingia kipindi cha pili, baada ya miamba hiyo kwenda mapimziko wakiwa hawajafungana.

Wageni Vital, ndiyo iliyoanza kutangulia kupata bao la kuongoza katika dakika ya 72, kupitia kwa mchezaji Mfungungu Afred ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukuwa nafasi ya Ibara Franchee, baada ya
kupokea pasi safi kutoka kwa Romarik Rogombe.

Kuinga kwa bao hilo kulizidisha kasi ya mashambulizi kwa pande zote
mbili, ambapo dakika ya 82 Othman Tamim wa Zanzibar Ocean aliikosesha timu yake bao la wazi.

Jitihada za Zanzibar Ocean View kutaka kusawazisha bao hilo zilizaa matunda dakika moja kabla ya mwamuzi kupuliza kipyenga cha kumaliza mpira ambapo Kheir Salum alitumbukiza mpira kimiani na kuzifanya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.

Kutokana na matokeo hayo Zanzibar Ocean sasa inatakiwa kutoka na ushindi wa bao 1-0 au zaidi katika mchezo wa marudiano utakaofanyika nchini Congo wiki mbili zijazo.

 
Wasanii watakiwa kujifunza kingereza


Na Addolph Bruno

WASANII wa sanaa za maonesho na filamu nchini wametakiwa kuongeza bidii kujifunza lugha ya kiingereza, waweze kupanua wigo wa soko la kazi zao
kimataifa.

Mwito huo ulitolewa Dar es Salaam jana na msanii maarufu wa maigizo nchini Christina Inocent 'Mama Bishanga', alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya sanaa hapa nchini.

Mama Bishanga ambaye kwa sasa anasomea shahada ya shughuli za kijamii nchini Marekani, alisema kazi za sanaa za Tanzania hazionekani katika nchi za nje hususani Marekani ikilinganishwa na kazi za nchi nyingine ambazo kutokana na tatizo la lugha.

"Kazi za wasanii wa nchi zote duniani zinatumika sana nchini Marekani, watu wananunua lakini nimefanya utafiti nimeona kazi za hapa kwetu nazo zipo kule lakini hazina soko," alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo wasanii hawana budi kukubali kuingia darasani kujifunza lugha ya kiingereza, bila kupoteza nafasi ya lugha ya kiswahili katika sanaa.

Mbali na hilo Mama Bishanga ambaye ni msanii wa zamani wa kundi la Kaole, alisema anaipongeza Serikali ya awamu ya nne kwa kusaidia michezo na kuomba iongeze juhudi iwasaidie wasanii wa sanaa za maonesho, ambao kazi zao zina soko kubwa kimataifa.

Hata hivyo Mama Bishanga alisema hali ya sanaa hapa nchini imefikia hatua nzuri, amewapongeza wasanii kwa juhudi wanazozionesha na kuwataka kuzingatia maadili.

 
Vyama vya michezo andaeni bajeti Monday, 31 January 2011 07:14

MICHEZO ya 10 ya Afrika 2011 inatarajiwa kufanyika mjini Maputo, Msumbiji kuanzia Septemba 3 mpaka 18, ambapo wanamichezo watashindana katika michezo 23 tofauti.

Katika michezo hiyo 23 tofauti mchezo mmojawapo ni mchezo wa soka ambao utashirikisha timu za vijana chini ya miaka 23 kwa wanaume na wanawake.

Hivi sasa mechi za awali za kufuzu kushiriki mashindano hayo kwa upande wa soka kwa baadhi ya timu zimeshaanza na zinatarajiwa kuisha mwishoni mwa mwezi huu kabla ya kuanza raundi ya kwanza mwezi April.

Ni timu nane tu kwa wanaume na nane kwa wanawake zinatakiwa kufuzu kushiriki katika mashindano ya Afrika mjini Maputo Septemba 3 ili kuungana na mwenyeji Msumbiji ambao wamefuzu moja kwa moja.

Kwa upande wa wanaume Tanzania itaanza harakati zake katika raundi ya kwanza kati ya Aprili 15-17 kwa kucheza na Uganda na kurudiana nao kati ya April 29 na Mei 1.

Kama Tanzania itaifunga Uganda itaingia raundi ya pili na kucheza na mshindi wa mechi ya Kenya na Eritrea kati ya Juni 24-26 na kurudiana Julai 8 mpaka 10 na kama ikishinda itapata tiketi ya kucheza michezo ya Afrika mwezi Septemba huko Maputo.

Hata kwa wanawake Tanzania itaanza harakati za kufuzu katika raundi ya kwanza April 29 mpaka Mei 1 na kurudiana kati ya Mei 13-15 kwa kucheza na mshindi wa mechi kati ya Sudan na Kenya.

Nchi mbalimbali za Afrika katika kipindi hiki zipo katika maandalizi ya michezo tofauti kwa ajili ya kuhakikisha zinatwaa medali nyingi katika mashindano hayo, na zingine zinashiriki hivi sasa mashindano ya awali,lakini katika hali inayoshangaza Tanzania bado haijaingiza timu kambini kwa ajili ya maandalizi na wala hakuna dalili ya kufanya hivyo katika siku za hivi karibuni.

Wiki iliyopita Serikali ilesema ipo tayari kugharamia maandalizi ya wanamichezo wetu kutoka vyama mbalimbali watakaoshiriki katika mashindano hayo ya Afrika ila vyama viandae bajeti zao ili serikali ijue inagharamia vipi.

Tunapenda kuvikumbusha vyama vyote vya michezo nchini kuandaa bajeti zao mapema kwa sababu tunaamini michezo hii ipo katika kalenda zao kwa hiyo suala la kuandaa bajeti siyo jambo geni kwao.

Tunasema hivyo kwa sababu mara kwa mara tumekuwa tukishuhudia maandalizi ya zimamoto wanayofanyiwa wanamichezo wetu kila mwaka inapobaki mwezi mmoja au wiki mbili kabla ya mashindano kuanza wakati tulikuwa na muda mrefu wa kuwafanyia maandalizi mazuri vijana wetu wanaoenda kuiwakilisha Tanzania.

Tunaamini vyama vya michezo visipowasilisha bajeti zao mapema serikalini hata fedha kwa ajili ya maandalizi ya vijana wetu watakaoliwakisha taifa yatachelewa na hivyo kufanya vibaya katika mashindano hayo ya Afrika.

 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom