Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #4,501
Phiri: Kuiondoa Elan Mitsoudje ipo kazi
Monday, 31 January 2011 19:26 newsroom
* Asema wakizembea tu Simba itatolewa
NA SOPHIA ASHERY
KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Patrick Phiri, amesema ili timu yake isonge mbele katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika, ni lazima ifanye jitihada kubwa. Akizungumza Dar es Salaam, jana, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, akitokea Comoro, alisema kuna haja ya kikosi chake kufanya jitihada ya kushinda mchezo wa marudiano dhidi ya Elan Mitsoudje.
Phiri alisema wapinzani wao si wale ambao alidhani hawajui soka, na ndio maana walipocheza mchezo wa awali hawakutarajia kupata upinzani hali ambayo iliwalazimu kutoka suluhu.
Alisema wachezaji wa timu hiyo wanatumia nguvu na wanacheza kwa kufuata mafunzo ambayo yanaonekana kuwa katika mfumo wa kiwango cha juu, na ndio maana waliwasumbua.
Alisema soka la Comoro kwa sasa limebadilika kwani wachezaji wake wengi wanacheza soka nje ya nchi yao, hasa Ufaransa ambako wanakwenda kusoma, na kuifanya nchi hiyo pamoja na timu zake kuwa na wachezaji wazuri.
Phiri alisema kutokana hali hiyo, kikosi chake kitajipanga kikamilifu kutoa upinzani mkali na kushinda mchezo wa marudiano utakaochezwa Dar es Salaam, baada ya wiki mbili zijazo, ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele.
"Tunajua tutashinda mchezo wa marudiano, lakini hatuwezi kushinda bila kujipanga kuwakabili wapinzani wetu na wala hatutawadharau," alisema.
Simba inatarajia kuingia kambini leo jioni kujiandaa kwa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, pamoja na mchezo huo wa marudiano.
Timu hiyo ilirejea nyumbani jana baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita kuivaa timu hiyo ya Comoro, mjini Moroni, na kutoka suluhu, matokeo ambayo yameishitua Simba, iliyotarajia mchezo wake huo ungekuwa mteremko.
Ili kuitoa Elan Mitsoudje na kusonga mbele kwenye michuano hiyo, Simba inahitaji ushindi wowote nyumbani, kwani sare
ya magoli itaiondoa katika michuano hiyo.