Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Kikwete mgeni rasmi Tamasha la Nyerere


Na Nayla Abdulla

RAIS Jakaya Kikwete anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la The Mwalimu Nyerere Film Festival, lililoandaliwa na Shirikiasho la Filamu
Tanzania (TAFF) ambalo litakalofanyika Februari 14 hadi 19 mwaka huu.

Tamasha hilo ambalo linafanyika kwa mara ya kwanza, litaenda sambamba na uzinduzi wa shirikisho hilo ambalo litafanyika katika viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam.

Akizungumza Dares Salaam jana, Rais wa shirikisho hilo, Simon Mwakifwambwa alisema lengo kuu la kuanzishwa kwa tamasha hilo ni kukuza soko la kazi za filamu nchini na kukuza mahusiano ya kisekta kati ya wasanii na taasisi ya kibiashara za ndani na nje ya nchi.

Alisema tamasha hilo litafanyika sambamba na kumuenzi Hayati Mwalimu Nyerere, kutokana na mchango wake mkubwa katika tasnia ya filamu hapa nchini enzi za uhai wake.

Mwakifwamba alisema tamasha hilo litahudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiwemo nyota wa filamu wa Afrika Kusini na Hollywood wakiwemo Diamond Eliot wa Nigeria, Marwa na Mama Kayayi wa Kenya.

Alisema zaidi ya filamu ishirini zilizofanya vizuri za ndani na nje ya Tanzania, zitaoneshwa katika tamasha hilo ambalo litasindikizwa na burudani mbalimbali zikiwemo ngoma za asili, vichekesho, muziki wa dansi, taarabu, bongo fleva, pamoja na michezo ya asili.

Mwakifambwa alisema tamasha hilo litatanguliwa na mafunzo ambapo mada mbalimbali zinazohusu shughuli za filamu na maigizo zitatolewa na wakufunzi waliobobea kwenye fani za utunzi, uongozaji, uhariri na ufundishaji.
 
BFT yaziangukia kampuni kudhamini ngumi


Na Mwali Ibrahim

SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), limetoa wito kwa kampuni mbalimbali kudhamini mashindano ya wazi ya ngumi hizo, yaliyopangwa
kufanyika Dar es Salaam Februari 26 hadi Machi 5, mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Msemaji wa BFT, Eckland Mwaffisi alisema mashindano hayo yanatarajia kushirikisha zaidi ya mikoa 20 ya Tanzania.

Alisema lengo la mashindano hayo ni kutafuta timu ya taifa, ambayo itaiwakilisha Tanzania katika mashindano mbalimbali ya kimataifa ikiwemo michezo ya Mataifa ya Afrika 'All African Game' iliyopangwa kufanyikia Maputo, Msumbiji Septemba 2011.

"Mbali ya mashindano hayo, timu hii ambayo itachaguliwa na Kocha Mkuu Hurtado Pimenter, itaiwakilisha Tanzania katika michezo ya Olympic, ambayo itafanyika London, Uingereza Julai 2012," alisema Mwaffisi.

Aliongeza kuwa, gharama za mashindano hayo ni zaidi ya sh. milioni 25 ambazo hadi sasa hakuna kampuni, taasisi au shirika ambalo limethibitisha kutoa udhamini wao.

Mwaffisi alisema, umefika wakati wa kampuni mbalimbali kutoa udhamini katika mchezo huo wenye historia ya kuitangaza Tanzania kimataifa, ili uweze kufika mbali zaidi.

"Leo hii mchezo wa soka ndiyo unaopewa kipaumbele zaidi kuliko michezo mingine, ambayo kama itapewa udhamini na wachezaji kuandaliwa vizuri, wataiwezesha Tanzania kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa na kuondoa dhana iliyojengeka kwa wachezaji wetu kuitwa watalii," alisema.
 
Chelsea, Man Utd, Arsenal zafanya kweli England


LONDON, England

TIMU za Chelsea, Manchester United na Arsenal zimeendelea kufukuzana katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu wa England, baada ya kuibuka na
ushindi dhidi ya wapinzani wao katika michuano hiyo ya ligi.

Katika mechi hizo za usiku wa kuamkia jana, Chelsea iliibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Sunderland, Manchester United ikiwa kwenye Uwanja, Old Trafford ikailaza Aston Villa kwa mabao 3-1 huku Arsenal, ikitoka nyuma na kuondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Everton

Katika mchezo kati ya Chelsea na Sunderland, Nicolas Anelka alijibu mapigo ya ujio wa mchezaji mpya aliyesainishwa na klabu hiyo, Fernando Torres kwa kupachika bao moja na kutengeneza mengine yaliyoipa ushindi huo wa mabao 4-2.

Mshambulijai huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa, ambaye namba yake ipo shakani kutokana na usajili uliovunja rekodi ya usajili nchini Uingereza, alipachika bao lake dakika za majeruhi na kuipa Chelsea ushindi wa tatu mfululizo kwenye michuano ya ligi.

Hata hivyo kabla ya bao hilo alikuwa ni kiungo wa Chelsea, Frank Lampard ambaye alisawazisha bao la dakika ya nne lililowekwa kimiani na Phil Bardsley kabla ya Salomon Kalou, kuifanya Blues iongoze dakika ya 23 baada ya kukimbia na mpira wa pasi aliyotengewa na Anelka.

Mchezaji Kieran Richardson ndiye aliyewasawazishia bao wenyeji hao dakika ya 26, lakini mabao waliyowekwa kimiani kipindi cha pili na wachezaji John Terry na Anelka, ndiyo yakaihakikishia Chelsea kuondoka na pointi za kutosha.

Matokeo hayo yanakifanya kikosi hicho cha Carlo Ancelotti, kubaki nyuma kwa pointi 10 dhidi ya vinara wa ligi hiyo ambao hadi sasa hawajafungwa, Manchester United.

Wakati Chelsea ikijitambia ushindi huo, Manchester United nao waliifunga Aston Villa mabao 3-1 katika Uwanja wao wa nyumbani Old Traford.

Katika mchezo Wayne Rooney alipachika mabao mawili kipindi cha kwanza na lingine likiwekwa kimiani na Nemenja Vidic kipindi cha pili na kuifanya timu yake kujikita kileleni ikiwa inaizidi Arsenal kwa pointi tano zaidi katika msimamo wa ligi.

Kwa upande wak Arsenal walifanikiwa kupata ushindi wao kwa mabao mawili ya kichwa yaliyofungwa na Laurent Koscielny, kipindi cha pili ndani ya dakika sita na kuifanya timu hiyo iweze kuondoka uwanjani na ushindi huo wa mabao 2-1 dhidi ya Everton.

Mshambuliaji wa Everton, Louis Saha ndiye alikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Arsenal dakika ya 24 kwa bao la utata lililopatikana baada ya Seamus Coleman, kupenyeza mpira kwenye ukuta wa Arsenal.

Hata hivyo bao hilo liliruhusiwa baada ya mpira huo kumfikia, Saha wakati mabeki wakijaribu kuokoa mpira huo.
 
Yanga mwereka!

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 2nd February 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 299; Jumla ya maoni: 0


02_11_zvu2vn.jpg

Kipa wa timu ya Mtibwa, Shaban Kado (kushoto) akiokoa moja ya hatari iliyoelekezwa kwenye lango lake na mshambuliaji wa Yanga, Nurdin Bakari (kulia) huku beki wake Obadia Mungusa akiwa tayari kusaidia wakati wa mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Mtibwa ilishinda kwa goli 1-0. (Picha na Fadhili Akida).





YANGA imekula mwereka baada ya kuchapwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Ushindi huo wa Mtibwa Sugar umeitia doa Yanga kwani imefungwa mechi ya kwanza tangu kuanza kwa Ligi mwaka jana.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga iendelee kuongoza ligi kwa pointi nne lakini ikiwa imecheza mechi nyingi zaidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 27.

Mtibwa Sugar imefikisha pointi 26 sawa na Azam lakini ikiwa nafasi ya nne kwani Azam ina uwiano mzuri wa mabao.

Bao pekee la Mtibwa Sugar lilifungwa na Hussein Java katika dakika ya 70 baada ya
kuunganisha krosi ya Juma Abdul.

Java aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Yusuf Mgwao. Kwa ujumla katika mechi ya jana timu zote zilionekana kutocheza vizuri na hasa safu za ushambuliaji ambapo umaliziaji ulikuwa mbovu.

Tangu kuanza kwa mchezo, wachezaji wa pande zote walikuwa wakishambuliana kwa zamu na Yanga ilianza kufanya shambulizi katika dakika ya kwanza ya mchezo lakini Davis Mwape aliikosesha Yanga bao baada ya kuchelewa kuunganisha pasi ya Jerryson Tegete akiwa jirani na kipa wa Mtibwa Sugar Shaaban Kado.

Dakika ya 38 Kigi Makasi alikosa tena nafasi nzuri ya kufunga baada ya kupewa pasi safi na Godfrey Bonny lakini akapiga mpira juu na kupoteza nafasi hiyo.

Akizungumza baada ya mechi hiyo kocha wa Yanga Fredy Minziro alisema wachezaji wake walipata nafasi nyingi za kufunga lakini walishindwa kuzitumia.

"Lakini kufungwa pia ni sehemu ya mchezo na ligi ya sasa ina ushindani mkubwa,"alisema.
 
Azan ampa pole Mzee Yussuf


na Abdallah Menssah


amka2.gif
MBUNGE wa Kinondoni, Idd Azan amemtumia salamu za pole, Mfalme wa mipasho na Mkurugenzi Mkuu wa kundi la Jahazi Modern Taarab, Mzee Yussuf, kutokana na kuugua kwake.
Azan alitoa salamu hizo za pole ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana katika mazungumzo maalumu na mwandishi wa habari hizi.
Alisema kuwa amelazimika kumtumia Yussuf salamu za pole kwa sababu yeye ni Mbunge wa Kinondoni anakoishi msanii huyo na anathamini pia mchango wake katika muziki na sanaa kwa ujumla.
"Unajua, muziki ni kati ya vyanzo vya maendeleo hapa nchini, hivyo hatuna budi kuwafariji wanamuziki wetu na kuwa nao bega kwa bega wanapopatwa na matatizo kwa kuwa wao ndio wanaofanya muziki uwepo," alisema Azan.
Aidha, Azan alisema kuwa pia anawaomba wapenzi, mashabiki pamoja na wadau wengine wote wa muziki kuzidi kumuombea Yussuf apate nafuu haraka.
Alisema kwa kuonyesha anawajali na kuthamini mchango wa wasanii wilayani Kinondoni, amepanga kuhudhuria onyesho la kwanza kwa Yussuf kupanda jukwaani akiwa na kundi lake la Jahazi.
"Kadhalika, kama siku mbili hizi kama nitapata nafasi, basi nitakwenda kumjulia hali huko kisiwani Zanzibar alikopumzika kabla hajaanza kazi," alisema Azan.
Onyesho la kwanza kwa Yussuf kupanda jukwaani ni lile lililopangwa kurindima katika mkesha wa Siku ya Wapendanao ‘Valentine's Day', kwenye ukumbi wa Travertine Hotel, Magomeni, jijini Dar es Salaam.
 
Waziri afagilia Tamasha la Pasaka kusaidia yatima


na Mwandishi wetu


amka2.gif
NAIBU Waziri wa Uchukuzi, Dk. Athuman Mfutakamba, amelisifia tamasha la Pasaka kwa kusema kwa kitendo cha sehemu ya fedha hizo kusomesha yatima na kuwasaidia yatima, hilo ni zaidi ya tamasha.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Mfutakamba alisema amepata faraja kubwa na Msama Promotions inayoratibu tamasha hilo kuyajali makundi hayo maalumu kwenye jamii.
"Nimefarijika mno na muamko huu, kwakweli huu ni mfano wa kuigwa kwani ni watu wachache mno wanaoweza kuandaa matamasha kama haya na fedha zinazopatikana kuwasaidia watoto yatima na wajane," alisema Mfutakamba.
Aidha, Mtufakamba amesema kwamba kwa kiasi kikubwa, tamasha hilo pia litasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, kwani wengi hivi sasa wameamua kujikita katika muziki wa injili kwa ajili ya kumuimbia Mungu na kujipatia kipato.
"Unapokuwa na watu wenye uzalendo kama Msama Promotions kwa hakika kabisa vijana wengi watajitokeza na watahamasika kujiingiza katika muziki huu, kwani watakuwa na uhakika wa kujipatia kipato," alisema Mfutakamba.
Tamasha kubwa la Pasaka linatarajiwa kufanyika Aprili 24 mwaka huu siku ya Sikuu ya Pasaka katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na baadaye kufanyika mjini Shinyanga Jumatatu ya Pasaka, Aprili 25 na jijini Mwanza Aprili 26, lengo lake kubwa mwaka huu ni kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidi mtaji wa biashara wanawake wajane.
Msama Promotions chini ya Mkurugenzi wake, Alex Msama, ndiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa injili nchini kupitia matamasha mbalimbali kama ya Krismasi na Pasaka, achilia mbali yale ya uzinduzi wa albamu mbalimbali.



h.sep3.gif

 
TOT yamnyakua Paka Mapepe


na Abdallah Menssah


amka2.gif
KUNDI mahiri la mipasho hapa nchini, TOT Taarab, limemnyakua mwimbaji mahiri wa kike wa fani hiyo, Mariam Khamis ‘Paka Mapepe' aliyekuwa katika kundi jingine la Five Stars Modern Taarab.
Akithibitisha habari hizo, Katibu wa TOT, Gasper Tumaini, alimweleza mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana kuwa, wamemnyakua Paka Mapepe kama moja ya mikakati yao kabambe ya kulirejesha kundi hilo katika chati.
Aidha, Tumaini alisema kuwa tayari Paka Mapepe ameishaanza kushiriki mazoezi na wasanii wenzie wa TOT walioko kambini hivi sasa wakijiandaa kwa albamu yao ijayo wanayoitarajia kuifyatua baadaye mwaka huu.
Paka Mapepe ambaye mbali ya Five Stars, pia amewahi kupitia makundi ya East African Melody na Zanzibar Stars, ni kati ya waimbaji wa kike wa mipasho aliyetokea kuvuta mashabiki wengi, hasa kutokana na uimbaji wake uliojaa hisia kali.
Baadhi ya vibao alivyoimba na kuchangia kumpa mashabiki wengi zaidi ni pamoja na kile alichokiimba awali kabisa akiwa na kundi la Melody, kilichompa jina hilo, ‘Paka Mapepe', ‘Huliwezi Bifu', ‘Raha ya Mapenzi' na ‘Ndo Basi Tena'.


h.sep3.gif

 
Miwa yailewesha Yanga
• Mashabiki wawashukia viongozi, wachezaji

na Ruhazi Ruhazi


amka2.gif
WAKATA miwa wa Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani, Morogoro jana walitibua rekodi ya Yanga ya kutopoteza mechi katika Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Bao pekee lililoizamisha Yanga lilifungwa na mtokea benchi, Juma Javu, dakika ya 70, akiunganisha krosi ya Juma Abdu, aliyeambaa na mpira wingi ya kulia na kumimina krosi iliyowapita walinzi wa Yanga na kumkuta mfungaji.
Kuingia kwa bao hilo kuliwafanya Yanga kuzinduka na kupeleka mashambulizi mengi langoni mwa Mtibwa, lakini kukosa umakini na mbinu kwa washambuliaji wao kukawagharimu kushindwa kusawazisha.
Vincent Barnabas aliyeingia badala ya Ally Mohammed nusura aipigie Mtibwa bao la pili dakika ya 80 lakini shuti lake likambabatiza mlinzi wa Yanga, Chacha Marwa.
Mlinzi chipukizi wa Yanga anayecheza pembeni kushoto Zuberi Ubwa, nusura aipatie Yanga bao la kusawazisha dakika za lala salama lakini shuti lake la mita 30 lilipanguliwa na kipa Shaban Kado na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.
Hadi mwamuzi Alex Mahagi kutoka Mwanza anamaliza pambano hilo, ni Mtibwa Sugar waliotoka kidedea wakijikusanyia pointi zote tatu, huku mashabiki wa Yanga wakirusha maneno makali nje ya uwanja huo.
Huu ni mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu kwa Yanga kucheza chini ya Fred Minziro, baada ya Kocha aliyeifikisha hapo Kostadin Papic kuiacha timu hiyo wiki iliyopita.
Baada ya mechi hiyo kumalizika, mashabiki waliokuwa na hasira walitaka kumshusha kwenye gari la wachezaji, kiungo wao Godfey Bonny ‘Ndanje', kwa madai kuwa alikuwa akimnyima pasi za kufunga mshambuliaji Mzambia Davies Mwape, kabla ya Jerry Tegete kuokoa jahazi kwa kuwaambia kuwa watakwenda kuyamaliza wenyewe mambo hayo.
Baada ya kumkosa Bonny, mashabiki hao walimvaa Makamu Mwenyekiti, Davis Mosha ambaye alijifungia ndani ya gari lake aina ya Noah, ingawaje mashabiki hao walifanikiwa kuvunja kioo cha nyuma na kumtwanga jiwe akiwa ndani kabla ya gari hilo kuondolewa kwa kasi na kutoweka eneo hilo la uwanja.
Mashabiki hao, ambao walikuwa wamegawanyika makundi kila moja likilaumu baadhi ya viongozi, pia walimweka kati mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Mohammed Bhinda kwa madai hayo hayo ya kuwashawishi wachezaji kucheza chini ya kiwango, lakini alijitetea na kupona kupokea kibano.
Mosha akizungumzia hali hiyo, alisema itafika wakati wataachia Yanga hao, kwani anaona hakuna kitu kinachoendelea, ingawa yeye yuko hapo kwa ajili ya kutetea masilahi ya wanachama ambao ndio waliomchagua.
Vikosi Yanga, Nelson Kimathi, Fred Mbuna, Abuu Ubwa, Chacha Marwa, Nadir Haroub ‘Cannavaro', Godfrey Bonny, Juma Seif, Jerryson Tegete, Davies Mwape na Kigi Makasi/Nsa Job.
Mtibwa Sugar, Shaban Kado, Juma Abdu, Yussuf Nguya, Obadia Mungusa, Salum Swedi, Julius Mrope, Faustin Lukoo, Omari Matuta, Ally Mohammed/Vincent Barnabas na Lameck Dayton/Yussuf Mgwao/ Hussein Javu.
Leo Simba inashuka katika dimba hilo kuvaana na African Lyon katika mfululizo wa ligi hiyo.
 
Yanga: Papic katoroka


na Dina Ismail


amka2.gif
UONGOZI wa Yanga umesema kuwa aliyekuwa Kocha wake Mkuu, Mserbia Kostadin Papic, ametoroka na mamilioni ya fedha za klabu hiyo hivyo wanafanya taratibu za kisheria ili kumnasa.
Papic inadaiwa alitoroka nchini juzi usiku kwenda kwao Serbia, huku uongozi wa timu hiyo ukisema kwamba hatAweza kuondoka mpaka pale atakapojibu shutuma mbalimbali zinazomkabili.
Mwenyekiti wa Yanga, Wakili Lloyd Nchunga, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kwamba Papic aliamua kujiuzulu na kutoroka baada ya kuona huenda aliyoyafanya yataweza kumletea matatizo.
Alisema, Papic alifanya usajili wenye utata kwa kuwalipa wachezaji fedha pungufu za usajili, wakati hela zote zilitolewa, huku akimtolea mfano Omega Seme, ambaye alimpa sh milioni 10 badala ya 15 zilizotolewa.
Nchunga pia alisema, kocha huyo alichakachua fedha za usajili wa Mghana Kenneth Assamoh kwa kuidanganya klabu aliyotoka kuwa Yanga imemsajili kwa mkopo, wakati fedha za usajili wake zilitolewa.
Kama hiyo haitoshi, Papic alitumia fedha za kumsajili kipa kutoka Serbia, Ivan Knezevic, huku pia akiondoka na dola 3,000 alizokopa Agosti mwaka jana.
"Tutamfuatilia kwa namna moja ama nyingine yeye pamoja na wengine wanaohusika katika sakata hili, tutawachukulia hatua za kisheria," alisema Nchunga.
Hata hivyo, habari zilizopatikana jana zinadai kuwa mmoja wa viongozi wa Yanga anahusika katika mchakato wa kumtorosha Papic.
Katika hatua nyingine, makocha wanne kutoka nchi mbalimbali wamejitokeza kuomba kibarua cha kumrithi Papic.
Nchunga alisema tayari wameishafanya mazungumzo na mmoja kati ya hao, Sam Timbe, ambayo yanakwenda vizuri lakini hatima yake itajulikana katika kikao hicho.
Aliwataja makocha wengine ambao wametuma wasifu wao (cv), kuwa ni Roy Barego wa Uingereza anayeishi nchini Afrika Kusini, ambaye aliwahi kuinoa timu ya taifa ya Zimbambwe, wengine wanatoka Yugoslavia na Serbia.
Pia Nchunga alimtangaza Mwesigwa John Selestine kuwa kaimu katibu mkuu wa klabu hiyo mpaka pale mchakato wa kumpata katibu wa kudumu utakapokamilika, ajira hiyo imeanza Februari mosi.


h.sep3.gif


juu
 
Wagosi wazidi kutakata Ligi Daraja la Kwanza


na Safari Chuwa, Tanga


amka2.gif
WENYEJI wa Ligi Daraja la Kwanza hatua ya tisa bora, Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya' wa hapa, jana walizidi kupalilia njia ya kurejea Ligi Kuu Bara msimu ujao baada ya kuwafumua Moro United mabao 2-1.
Kwa matokeo ya mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Coastal Union wamefikisha pointi sita baada ya kushinda mechi zote mbili.
Kabla ya kukutana na Moro United, Coastal Union waliwafunga Villa Squad ya Kinondoni bao 1-0.
Katika mechi ya jana ambayo ilichezwa mapema, wenyeji Moro United walikuwa wa kwanza kuziona nyavu za Coastal Union dakika ya 16 mfungaji akiwa Henry Ngonye, baada ya beki wa Coastal Union, Mohamed Danstan, kukawia kuokoa mpira katika eneo la lango lake.
Hata hivyo, Coastal Union walicharuka na kufanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 20, likifungwa na Daniel Lyanga akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa Moro United, Lucheke Mussa, kutokana na shuti la Kibabu Chandiga.
Bao hilo liliwapa nguvu Coastal Union ambao waliongeza kasi ya mchezo na dakika ya 35, walifunga bao la pili, likiwekwa wavuni na Shafii Kaluwani kwa pasi ya Mohamed Issa.
Licha ya timu hizo kushambuliana kwa nguvu, lakini hadi mapumziko, Coastal Union walikuwa mbele kwa mabao hayo 2-1.
Kipindi cha pili kiliendelea kuwa cha mashambulizi makali, lakini hadi filimbi ya mwisho, matokeo yalibaki kuwa 2-1.
Coastal Union: Godson Mmasa, Said Nassor, Paul John, Konji Mayega, Jamal Machelenga, Mohamed Danstan, Mohamed Issa, Daniel Lianga, Moses Lutandika na Ally Hassan.
Moro Union: Lucheke Mussa, Musiba Selemani, Jeofrey Isdori, Said Fundikira, Hassan Kibweni, Adam Simba, George Mkoba, Henry Ngonye, Benedict Ngassa, Erick Mawala, Bakar Mpakala.
Katika mechi ya pili, Villa Squad walifanikiwa kuvuna pointi zote tatu kwa kuwafunga Morani FC mabao 2-0.
Villa walipata bao la kwanza dakika ya 29, likiwekwa wavuni na Stahimili Kebe kwa mkwaju wa penalti ambalo lilidumu hadi mapumziko.
Dakika ya 52, Villa Squad walipata bao la pili likiwekwa wavuni na Yahya Daruweshi aliyeambaa na mpira kabla ya kupiga shuti na kutinga wavuni.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa mechi kati ya maafande wa Prisons ya Mbeya dhidi ya wenzao wa JKT Oljoro katika mechi ya kwanza kabla ya wavaa buti wengine Rhino Rangers ya Tabora kupigishana kwata na Polisi Moro.
 
Kagasheki ahimiza ushiriki kongamano la michezo


na Asha Bani, Bukoba


amka2.gif
MBUNGE wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki, amewataka wadau mbalimbali wa michezo kujitokeza kwa wingi katika kongamano la michezo litakalofanyika katika ukumbi wa Linas mjini hapa Februari 6 mwaka huu. Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi mchango wake wa sh milioni moja kwa timu ya maveterani ambao ndio waandaji wa kongamano hilo, Balozi Kagasheki alisema ni vema wadau wakajitokeza kwa wingi ili kutoa maoni yao katika nyanja mbalimbali za michezo.
Alisema, Mkoa wa Kagera kwa sasa uko nyuma katika michezo kwa ujumla, ukilinganisha na hali ilivyokuwa zamani, hivyo aliwataka wadau kujitokeza ili waweze kuelezea kinachotakiwa kufanyika ili kuhakikisha sekta hiyo mkoani hapa inapanda chati kama zamani.
"Viwango vya michezo vimeshuka chini sana katika mkoa huu, hivyo kuna haja wananchi wapenda michezo wakakusanyika na kujadili nini kifanyike na kwa nini tumefikia hapa tulipo, hakuna riadha, mpira wa kikapu, michezo yote viwango vyake viko chini kabisa," alisema Balozi Kagasheki.
Naye Kocha wa timu hiyo, Benny Kampambe, alimshukuru Balozi Kagasheki ambaye pia ni mlezi wa timu hiyo kwa kuwasaidia na kumtaka kutokata tamaa kuendelea kufufua michezo mjini hapa kwa njia yoyote ile.
Alisema, wao kama maveterani wana malengo makubwa ya kuhakikisha kuwa soka inasonga mbele sambamba na michezo mingine na kwa kuanza wameweza pia kununua sehemu ya kiwanja kwa ajili ya kujenga miradi mbalimbali ikiwa kama ni kitega uchumi katika michezo yao.
Aliongeza kuwa, kwa sasa wana mafanikio makubwa kutokana na kuwa na ongezeko la wanachama 82, ambao wako katika michezo mbalimbali.
 
Simba Silaha wahimizwa mshikamano


na Chile Kasoga


amka2.gif
WANACHAMA wa tawi la Simba la Silaha lililopo Mtoni Manispaa ya Temeke wametakiwa kujenga ushirikiano na mshikamano kwa lengo la kuiletea ushindi klabu yao.
Mwenyekiti wa tawi hilo, Mathias Nyanda, alitoa wito huo juzi wakati wa mkutano wake na wanachama wa tawi hilo.
"Endapo wanachama wenyewe ndani ya tawi tutakuwa hatuna umoja na ushirikiano, hatutaweza kuwa na muda wa kuweza kujadili maendeleo ya klabu," alisema Nyanda.
Aliwataka wanachama hao, kujiepusha na migogoro na badala yake wapange mikakati ya kuweza kuisaidia klabu ya Simba ili iweze kutetea ubingwa wa Ligi Kuu.
Hata hivyo alibainisha kuwa, tawi hilo lina mpango wa kuongeza wanachama wapya watakaokuwa na kadi halali za uanachama mara baada ya kuwafanyia upya uhakiki.
Wanachama wa tawi hilo, walikutana mwishoni mwa wiki kujadili jinsi ya kuweza kupata jengo la kudumu la tawi lao, ambako kila mwanachama ameombwa kuchangia sh 7,000.
 
Kostadin Papic katoroka- Nchunga

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 2nd February 2011 @ 23:55 Imesomwa na watu: 194; Jumla ya maoni: 0


02_11_cahsb4.jpg

Aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga, Kostadin Papic.





MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Llyod Nchunga amesema aliyekuwa kocha wa timu hiyo Kostadin Papic ametoroka nchini bila kukabidhi baadhi ya ripoti ya taarifa za wachezaji.

Vyombo vya habari mbalimbali jana viliripoti kuwa uongozi wa Yanga ulimpa masharti matatu Papic na kwamba ulitaka atoe ufafanuzi wa baadhi ya mambo ndio aondoke.

Lakini badala yake saa nne usiku wa kuamkia jana, kocha huyo aliripotiwa kuondoka na Nchunga jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa Papic alitoroka kwani yeye kama Mwenyekiti hakuwa na taarifa za kuondoka kwake licha ya kuwepo kwa madai kuwa kocha huyo alimuaga Makamu wake Davis Mosha.

Baadhi ya masharti ambayo uongozi wa Yanga ulimtaka Papic kutoa ufafanuzi kwa mfadhili wao Yusuf Manji ni kwanini aliitia hasara klabu kwa kumsajili mchezaji Keneth Asamoah na badala yake asiweze kuichezea timu hiyo, mchakato wa fedha za usajili wa wachezaji na pia kutoa maelezo ya fedha za usajili za kipa Ivan Knezevic Sh milioni 3.7.

Inadaiwa kuwa Papic alikopa Sh milioni nne kwa uongozi wa Yanga na ilipofika wakati wa kuzirudisha alisema kwamba atampa Knezevic lakini mpaka siku mbili kabla ya kocha huyo kutoroka kipa huyo alikuwa hajapewa fedha zake.

"Kuna ufisadi zaidi uliofanyika kwenye sakata la usajili kwa kuwa kuna baadhi ya wachezaji walioripotiwa kuwa wamepewa fedha za usajili Sh milioni 15 lakini wachezaji hao wamepewa sh milioni kumi," alisema.

Alisema kuwa kwa sasa uongozi wa klabu hiyo unaendelea na hatua zake za kawaida za kufuatilia ukaguzi wa hesabu za klabu.

Akizungumzia hatua ambayo klabu inachukua kutafuta kocha, Nchunga alisema kuwa uongozi wake ulikuwa na mazungumzo na Sam Timbe ili kuangalia kama anaweza kupewa mikoba ya Papic.

Pia aliongeza kuwa makocha kutoka nchi mbalimbali walioomba kuinoa Yanga na tayari wametuma CV zao kwenye mtandao.

Makocha hao ni Roy Barreto wa Uingereza, Simeon Afremov wa Yugoslavia na Ivo Von wa Slovenia.

Wakati huohuo, Nchunga jana alimtangaza Mwesigwa Selestine kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Lawrance Mwalusako.

Alisema uteuzi wa Mwesigwa ulifanyika juzi na kwamba Kaimu Katibu huyo ni mwanachama wa Yanga mwenye kadi namba 004010 na ana uhusiano na mitandao mingi duniani ijishugulishayo na mchezo wa soka ikiwa pamoja na kuendeleza soka la vijana.
 
Kostadin Papic katoroka- Nchunga

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 2nd February 2011 @ 23:55 Imesomwa na watu: 194; Jumla ya maoni: 0


02_11_cahsb4.jpg

Aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga, Kostadin Papic.





MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Llyod Nchunga amesema aliyekuwa kocha wa timu hiyo Kostadin Papic ametoroka nchini bila kukabidhi baadhi ya ripoti ya taarifa za wachezaji.

Vyombo vya habari mbalimbali jana viliripoti kuwa uongozi wa Yanga ulimpa masharti matatu Papic na kwamba ulitaka atoe ufafanuzi wa baadhi ya mambo ndio aondoke.

Lakini badala yake saa nne usiku wa kuamkia jana, kocha huyo aliripotiwa kuondoka na Nchunga jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa Papic alitoroka kwani yeye kama Mwenyekiti hakuwa na taarifa za kuondoka kwake licha ya kuwepo kwa madai kuwa kocha huyo alimuaga Makamu wake Davis Mosha.

Baadhi ya masharti ambayo uongozi wa Yanga ulimtaka Papic kutoa ufafanuzi kwa mfadhili wao Yusuf Manji ni kwanini aliitia hasara klabu kwa kumsajili mchezaji Keneth Asamoah na badala yake asiweze kuichezea timu hiyo, mchakato wa fedha za usajili wa wachezaji na pia kutoa maelezo ya fedha za usajili za kipa Ivan Knezevic Sh milioni 3.7.

Inadaiwa kuwa Papic alikopa Sh milioni nne kwa uongozi wa Yanga na ilipofika wakati wa kuzirudisha alisema kwamba atampa Knezevic lakini mpaka siku mbili kabla ya kocha huyo kutoroka kipa huyo alikuwa hajapewa fedha zake.

“Kuna ufisadi zaidi uliofanyika kwenye sakata la usajili kwa kuwa kuna baadhi ya wachezaji walioripotiwa kuwa wamepewa fedha za usajili Sh milioni 15 lakini wachezaji hao wamepewa sh milioni kumi,” alisema.

Alisema kuwa kwa sasa uongozi wa klabu hiyo unaendelea na hatua zake za kawaida za kufuatilia ukaguzi wa hesabu za klabu.

Akizungumzia hatua ambayo klabu inachukua kutafuta kocha, Nchunga alisema kuwa uongozi wake ulikuwa na mazungumzo na Sam Timbe ili kuangalia kama anaweza kupewa mikoba ya Papic.

Pia aliongeza kuwa makocha kutoka nchi mbalimbali walioomba kuinoa Yanga na tayari wametuma CV zao kwenye mtandao.

Makocha hao ni Roy Barreto wa Uingereza, Simeon Afremov wa Yugoslavia na Ivo Von wa Slovenia.

Wakati huohuo, Nchunga jana alimtangaza Mwesigwa Selestine kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Lawrance Mwalusako.

Alisema uteuzi wa Mwesigwa ulifanyika juzi na kwamba Kaimu Katibu huyo ni mwanachama wa Yanga mwenye kadi namba 004010 na ana uhusiano na mitandao mingi duniani ijishugulishayo na mchezo wa soka ikiwa pamoja na kuendeleza soka la vijana.
 

Coastal, Villa zachanua ligi daraja la kwanza


Imeandikwa na Anna Makange, Tanga; Tarehe: 2nd February 2011 @ 23:50
TIMU za soka za Coastal Union ya Tanga na Villa Squard ya Dar es Salaam zimeibuka na ushindi katika mechi zake za Ligi Daraja la Kwanza zinazoendelea kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini hapa.

Coastal Union ndio iliyokuwa ya kwanza kumaliza siku kwa furaha jana baada ya kuichapa Moro United mabao 2-1.

Bao la kwanza la Coastal lilifungwa katika dakika ya 20 kupitia kwa Daniel Iyanga kabla ya Shafii Kaluwani hajaifungia bao la pili katika dakika ya 35.

Bao la Moro United lilifungwa katika dakika ya 16 kupitia kwa Henry Ngonye. Kwa upande wa Villa Squard ilipata ushindi wake kwa mabao yaliyofungwa na Stamili Kebe kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 29 na Yahaya Darueshi alifunga bao la pili katika dakika ya 52.

Timu zinazoshiriki zipo tisa ambapo timu nne zitakazoshika nafasi za juu zitapanda kucheza Ligi Kuu msimu wa 2011/2012.


 
Kamati ya gofu kukutana Feb.23

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 2nd February 2011 @ 23:45

MKUTANO Mkuu wa Kamati ya gofu Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam (DGC) umepangwa
kufanyika Februari 23 kwenye klabu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa gofu Lawrence Pangani aliyoitoa Dar es Salaam jana mbali na kupokea taarifa ya kamati ya mwaka mkutano huo mkuu pia utachagua viongozi wapya.

Pangani pia alisema fomu za nafasi mbalimbali zitakazowaniwa kwenye uchaguzi huo mkuu tayari zimetoka hivyo, kila mwanachama yupo huru kupendekezwa.

Alitaja nafasi hizo kuwa ni nahodha na makamu wake, katibu katibu wa mashindano, msimamizi wa uwanja na nahodha wa wachezaji wa daraja C.

Uongozi utakaochaguliwa utakaa madarakani kwa kipindi cha mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mwingine utakaofanyika Februari mwakani.

Joseph Tango ndiye kiongozi anayemaliza muda wake baada ya kutumika kwa mwaka mmoja. Nahodha huyo katika kipindi chake amefanikiwa kuboresha viwanja hivyo ambavyo viko katika hali nzuri kwa sasa ukilinganisha na alivyoingia madarakani.

Hata hivyo, changamoto kubwa bado inakabili viongozi watakaoingia madarakani katika kuhakikisha DGC ambayo ni kati ya klabu mbili Tanzania zenye viwanja vya gofu vilivyo na mashimo 18 vinaboreshwa zaidi na kufikia viwango vya kimataifa.

Klabu nyingine yenye mashimo 18 ni ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo.

 
Wasanii kuwatuza Nyerere, Kawawa

Imeandikwa na Hellen Mlacky; Tarehe: 2nd February 2011 @ 23:40


SHIRIKISHO la Filamu Nchini (TAFF), linatarajia kuwakabidhi tuzo Maalumu Waasisi wa Taifa akiwemo hayati Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Rashidi Kawawa kwa mchango wao katika maendeleo ya Taifa na Tasnia ya Filamu nchini.

Rais wa TAFF, Simon Mwakifamba alisema jana kuwa tuzo hizo walizoziita "TAFF Special Awards" zitakabidhiwa siku ya kilele cha Tamasha la Filamu la Mwalimu Nyerere ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mama Maria Nyerere.

Alisema tamasha hilo la filamu litafanyika kwa siku sita kuanzia Februari 14 hadi 19 mwaka huu katika viwanja vya Leaders Club ambapo siku ya mwisho Mama Nyerere atafunga na kutoa zawadi mbalimbali.

Alisema siku ya kwanza ya tamasha hilo itakuwa ni ufunguzi na burudani ya ngoma za asili, siku ya pili yatatolewa mafunzo yanayohusu uandishi bora wa "script" na umuhimu wa hakimiliki na hakishiriki kwa wasanii mbalimbali na baadaye burudani.

"Siku ya tatu tamasha litaanza na mafunzo yanayohusu athari ya HIV kwa maendeleo ya
wasanii, uongozi katika vikundi na taasisi za sanaa pamoja na umuhimu wa maadili katika tasnia ya filamu na baadaye yatakuwepo maonesho ya kazi mbalimbali za wasanii," alisema.

Alisema siku ya nne yatatolewa mafunzo kuhusu utafutaji wa masoko na soko la pamoja la Afrika Mashariki, mbinu bora za uongozaji wa filamu na michezo ya kuigiza kwa wasanii mbalimbali ambapo baadaye yataendelea maonesho ya bidhaa na kazi mbalimbali za wasanii.

Mwakifamba alisema kuwa siku ya tano yatatolewa mafunzo ya utawala bora na haki za binadamu kwa wasanii na umuhimu wa kanuni na sheria ndogo ndogo za shirikisho kwa maendeleo ya tasnia na baadae yataendelea maonesho ya bidhaa na kazi za wasanii.

Alisema katika tamasha hilo kiingilio kwa watoto kitakuwa Sh 1,000 na kwa watu wazima ni kuanzia Sh 5,000.


 
Rooney aipaisha Man United England Wednesday, 02 February 2011 20:35

LONDON, England
MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Wayne Rooney ameisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Aston Villa na kuifanya timu yake kukalia kilele kwa pointi tano mbele huku Arsenal na Chelsea zikinyemelea baada ya mechi za juzi.

Rooney alifunga mabao kwa mashuti katika mechi hiyo iliyopigwa Old Trafford na kuisiadia United kuendeleza rekodi ya mechi 29 bila kupoteza.

Wanaoshikilia nafasi ya pili, Arsenal walifufuka na kuichapa Everton 2-1 wakiwa nyumbani kwa mabao ya Andrey Arshavin na Laurent Koscielny.

Chelsea iliyoingia uwanjani bila mshambuliaji wake iliyomsajili kwa makeke, Fernando Torres iliilaza Sunderland 4-2, na kuisogelea Manchester City kwa pointi moja, ambayo jana ilikuwa ikicheza na Birmingham.

Wigan iliendelea kusogezwa katika shimo la kushuka daraja baada ya kutoka sare ya 2-2 na West Bromwich Albion katika mchezo mwingine wa ligi hiyo.

Katika mechi za juzi, alikuwa Rooney ambaye kwa kipindi kirefu alikumbwa na ukame wa mabao kwa timu yake na taifa, aliklakini katika mchezo wa juzi, alikuwa mwenye furaha.

"Bao ndilo linalomjenga mshambuaji," alisema kocha wa United, Alex Ferguson alipokuwa akimzungumzia Rooney. "Kila wakati linamfanya kuwa na hamu ya kucheza … na amefanikiwa."

Rooney alipata mpira mrefu uliopigwa na kipa wake, Edwin van der Sar na kuutengeneza vizuri umbali wa mita 20 na kuachia fataki iliyokwenda moja kwa moja ndani ya kimia ikiwa ni sekunde 48 tangu kuanza mchezo.

Bao lake la pili alilifunga dakika chache kabla ya mapumziko, lilikuwa la umbali wa mita nane, baada ya kuunganisha krosi ya Nani ndani ya eneo la hatari na akaujaza mpira wavuni.

Mshambuliaji wa England, Darren Bent aliifungia Villa bao katika dakika ya 58, ikiwa ni bao lake la pili kwa timu hiyo tangu alipojiunga akitokea Sunderland, lakini Mserbia Nemanja Vidic aliipatia United alitikisa nyavu kwa kombora kali.

Naye beki wa kati wa Ufaransa, Koscielny alifufua uhai wa Arsenal katika pambano hilo kwenye Uwanja wa Emirates na kuandika bao la pili katika dakika ya 76.

Awali Arshavin aliisawazishia timu yake bao katika dakika ya 70, ikiwa ni dakika nane baada ya kuoingia kuchukua nafasi ya Tomas Rosicky, akifuta bao la mshambuliaji wa Everton, Louis Saha.

Licha ya kufunga bao hilo akiwa ameotea, Saha alipokea pasi ya Seamus Coleman na kumpita Koscielny na kufunga.

"Hatukuwa makini hata Everton wakafunga," alisema kocha wa Arsenal, Arsene Wenger na kuongeza. "Tulikuwa na kila hali na ari ya ushindi. Nimefurahi na hili ndilo linalotakiwa kwenye timu, wachezaji kucheza kwa jinsi hii."

Torres hakuweza kuvaa jezi ya Chelsea kwa kuwa hakuwa amesajiliwa kwa wakati na kujipanga kwa mchezo huo. Alivunja rekodi ya usajili kwa pauni 50 million kutoka Liverpool.

Hata hivyo, mabingwa hao watetezi, hawakuwa na kazi sana, kwani Frank Lampard alifunga kwa mkwaju wa penalti huku Salomon Kalou akifunga lingine dakika nne baadaye.

Frikiki ya Kieran Richardson ya dakika ya 26 ilifanya matokeo kusomeka 2-2 lakini mabao ya kipindi cha pili ya John Terry na Nicolas Anelka yaliifanya Chelsea kuibuka kidedea.

Kocha wa Chelsea, Carlo Ancelotti alisema kuwa timu yake imechukua muda mrefu kupata ushindi, na sasa mbio za ubingwa zinaanza rasmi.

"Kama Manchester United wataendeleza ushindi, itakuwa ngumu kuziba pengo la pointi," alisema Ancelotti, baada ya Chelsea kushika nafasi ya tatu.

Marc-Antoine Fortune aliyeingia kipindi cha pili, aliisawazishia West Brom dhidi ya Wigan katika dakika ya 79 akifuta bao la Charles N'Zogbia na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1.

 
Torres sasa kulianzisha kwa Liverpool
Wednesday, 02 February 2011 20:34

SUNDERLAND, England
MSHAMBULIAJI mpya wa Chelsea, Fernando Torres anajipanga kuitumikia Chelsea katika pambano dhidi ya Liverpool.

Liverrpool ilimuuza mchezaji huyo kwa pauni 50 milion na hata hivyo hakuwemo kwenye kikosi kilichocheza mchezo wa juzi na kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Sunderland.

Mshambuliaji huyo wa Hispania, alitimka Anfield dakika za mwisho kwani mapema alikuwa akiwekewa zengwe la kuondoka na klabu yake.

Lakini bilionea wa Chelsea, Roman Abramovich, ambaye timu yake iko nyuma kwa pointi 10 na vinara Manchester United licha ya kuifunga Sunderland, alisema ana matumaini makubwa kuona timu yake inafika mbali.

Juu ya kiwango cha Chelsea, kwa mchezo huo uliofanyika Stadium of Light, Carlo Ancelotti ambaye alimkalisha benchi Torres, alisema kuwa alifanya hivyo akiamini Didier Drogba na Nicolas Anelka wamezoeana na kila mmoja anatambua nafasi ya mwenzake.

Lakini kocha huyo Muitaliano alisema kuwa Torres ataanza mechi ijayo kwenye kikosi cha Stamford Bridge dhidi ya Liverpool.

"Torres na Drogba wakijipanga mbele na Anelka anafuatia nyuma yao, naamini mambo yatakuwa safi sana."

Mpango wa Ancelotti ni kumpa Torres nafasi ya kujitanua kama alivyokuwa akifanya alipokuwa Liverpool. Hata hivyo, imeelezwa pia kuwa Torres hajaonyesha makeke hasa baada ya kutoka Afrika Kusini katika Fainali za Kombe la Dunia.

"Fernando ni mzuri na mwenye uwezo," Ancelotti alisema. "Kwa sifa zake, hatakuwa na kikwazo wala kuona ugumu wa kucheza na sisi. Hatakuwa na tatizo, naamini akisimama na Didier Drogba au mshambuliaji mwingine, itajipa."
 
Waziri asifu waandaaji tamasha Wednesday, 02 February 2011 21:35

Priscar Malecela
NAIBU Waziri wa Uchukuzi, Dk. Athumani Mfutakamba amewataka mapromota wa kazi mbalimbali za sanaa kutumia sehemu ya mapato yao kusaidia watu yenye matatizo wakiwemo wajane na mayatima.

Mfutakamba aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumzia hatua ya waandaaji wa Tamasha la Pasaka baada ya kutangaza kutumia sehemu ya fedha za mapato ya tamasha hilo kusomeseshea watoto yatima, kuwasaidia mitaji ya biashara wanawake wajane.

"Nimefarijika mno na mwamko wa Kampuni ya Msama Promotions, waandaaji wa tamasha kuona jinsi gani wanaweza kuwasaidia watoto yatima na wanawake wajane."

Alisema kwamba kwa kiasi kikubwa tamasha hilo pia litasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, kwani wengi hivi sasa wameamua kujikita katika muziki wa injili kwa ajili ya kumuimbia Mungu na kujipatia kipato.

"Binafsi imenihamasisha, sasa naamini wengi watajitokeza na lengo ni kuona fedha zinapatikana na kuwafikia walengwa," alisema.

Tamasha la Pasaka limepangwa kufanyika Aprili 24 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na kufuatiwa na matamasha mengine Shinyanga Aprili 25 na Aprili 26 jijini Mwanza .
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom