Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
FIFA kuendesha semina ya siku nne


Na Zahoro Mlanzi

SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), linatarajia kuendesha semina ya siku nne nchini kwa Wenyeviti, Makatibu Wakuu na Maofisa Habari wa
Klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara itakayohusu mapitio ya awali waliyokubaliana katika Azimio la Bagamoyo.

Azimio hilo lilifanyika Bagamoyo Desemba, 2007 ambapo FIFA ilizitaka klabu hizo kutekeleza na kutafuta ufumbuzi wa muundo wa utawala, mfumo wa idara ya ufundi, vitendea kazi na utawala bora ambapo klabu ziliazimia kutimiza hayo ndani ya miaka mitatu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema semina hiyo itafanyika Februari 14 mpaka 18, mwaka huu jijini Dar es Salaam ikiwa na lengo la kupitia waliyokubaliana katika azimio la Bagamoyo.

"FIFA ilikubaliana na klabu yafanyike mapitio ya kile kilichoazimiwa Bagamoyo, baada ya miaka mitatu ili kuona kama utekelezaji wake umefanyika ambapo wenyeviti, makatibu na maofisa habari ndiyo watakaohusika na semina hiyo," alisema Wambura.

Alisema wenyeviti watapata fursa ya kufanya mapitio kwa pamoja na viongozi wengine, ambapo baada ya mapitio hayo viongozi watakaobaki watapata semina kwa siku zitakazofuata.

Wakati huohuo, Wambura alisema Machi 31, mwaka huu kutakuwa na mtihani kwa watakaokuwa wanataka uwakala wa FIFA ambapo mtihani huo, utafanyika jijini siku hiyo kuanzia saa nne asubuhi.

"Tumekuwa tukipata maswali mengi juu ya huo mtihani, sasa kila kitu kimekamilika na utafanyika siku hiyo, hivyo wale waliokuwa wakihitaji sasa ni wakati muafaka kuja kuchukua fomu na kuzijaza," alisema Wambura.
 
TBL yazindua 'Safari Nyama Choma 2011'


Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Safari jana imezindua mashindano ya kuchoma nyama 'Safari Lager Nyama Choma 2011' na kutangaza
zawadi za washindi ambapo bar itakayoibuka bingwa itanyakua sh. milioni.

Baa itakayokuwa ya pili katika mashindano hayo itapewa sh. 800,000, wa tatu sh. 600,000, wa nne sh. 400,000 na wa tano sh. 200,000. Zawadi hizo zimegawanywa katika kila mkoa.

Akizungumza Dar es Salaam jana Meneja wa bia ya Safari Lager, Fimbo Butallah alisema mashindano ya mwaka huu yatafanyika katika mikoa minne ya Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro na Mbeya ambao umeongezwa mwaka huu.

Butallah alisema utaratibu wa mashindano hayo, yataendeshwa kwa njia ya simu ambapo wananchi watatakiwa kutuma ujumbe wa maneno 'Safari kisha mkoa ikifuatiwa na jina la baa' kwenda namba 15540.

"Mashindano haya hushirikisha majiko ya baa mbalimbali katika umahiri wa kuchoma nyama na hatimaye zawadi hutolewa kwa washindi,' alisema Butallah.

Alisema madhumuni makubwa ya bia ya Safari ni kuendesha mashindano hayo, ambayo yamekuwa kivutio kwa walaji wa nyama na watumiaji wa bia hiyo ni kuleta changamoto kwa majiko yanayochoma nyama ili kuhakikisha walaji wanapata kilichobora.

Meneja huyo alisema vigezo vitakavyotumiwa na majaji wa mashindano hayo ni usafi wa eneo, vifaa na muhusika, nyama inavyosafishwa na maji, uchaguzi wa nyama, maandalizi, uchomaji, muda, ladha na nyama inavyopelekwa kwa mlaji.

"Baa zitakazofanikiwa kuingia katika kinyang'anyiro hicho zitapewa semina elekezi juu ya vigezo hivi kabla ya mpambano," alisema Butallah.

 
Torres anza kwa mkosi Chelsea


LONDON, Uingereza

MSHAMBULIAJI Fernando Torres, juzi alinza na mkosi kuichezea timu yake mpya ya Chelsea, dhidi ya klabu yake ya zamani Liverpool baada
kuchapwa bao 1-0.

Torres aliyesainiwa kwa pauni milioni 50, alitolewa katika dakika ya 65 na kubezwa na mashabiki wa Liverpool.

Raul Meireles, ndiye aliyeiletea furaha Liverpool kwa kufunga bao pekee na kumfanya kocha Kenny Dalglish kutoa kijembe kwa Torres.

Alisema: "Sifikiri kama kati ya washmabuliaji wao walikuwa na siku ya furaha.

"Kipa wetu hakuwa na kazi kubwa sana ya kufanya, kwa kuwa wachezaji waliokuwa mbele yake walikuwa wakilinda vizuri sana."

Torres alipokuwa akitoka uwanjani mashabiki wa Liverpool, walipaza sauti wakiimba, "ungebakia na timu kubwa'.Dalglish aliongeza: "Mashabiki wetu walitoa mawazo yao na wanajua utii wa wachezaji. Wanatakiwa kuonesha kuiheshimu klabu hii.

"Watu wa muhimu sana ni watu waliopo katika Liverpool na kila wakati itakuwa hivyo. Mtu anapoamua kufanya kitu sehemu nyingine aatakuwa akifanya hivyo kwa maisha yake, hilo ni chaguo lao.

"Watu waliopo katika timu pinzani si kitu muhimu kwangu. Kama Carlo Ancelotti angecheza sehemu ya mbele kwa Chelsea, bado ningetaka pointi tatu."

Mlinzi Jamie Carragher alisema: "Wachezaji wazuri wanakuja na kuondoka. Nimeshacheza dhidi ya wachezaji wengi wa zamani wa Liverpool kuanzia Robbie Fowler.

"Torres ni mmoja wa washambuliaji wazuri duniani, lakini kwa sasa hatuko pamoja na sisi. Tuna kazi yetu ya kufanya na hicho ndicho tunataka kufanya."
 
Simba, Yanga zageukia soka ya Afrika
Monday, 07 February 2011 20:50

patrick%20phiri.jpg
Kocha wa Simba,Patrick Phiri

Jessca Nangawe na Clara Alphonce

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba na watani zao, Yanga tayari zimeingia kambini kwa maandalizi ya mechi zao za marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho zitakazochezwa mwishoni mwa wiki.

Simba watakuwa nyumbani kuikaribisha Elan Club de Mitsoudje ya Comoro baada ya kulazimishwa suluhu 0-0 ugenini, huku Yanga wakiwa safarini kuelekea Ethiopia kuivaa Dedebit iliyopata mabao manne kwenye Uwanja wa Taifa katika mchezo wa kwanza.

Mabingwa hao wa Tanzania Bara, Simba wanaingia kambini leo katika hoteli ya Lamada tayari kwa maandalizi ya mchezo huo wa marudiano dhidi ya Wacomoro hao wakiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania na kufanikiwa kuiondoa kileleni Yanga.

Akizungumza na Mwananchi jana, ofisa habari wa klabu hiyo, Clifford Ndimbo alisema timu hiyo inatarajiwa kuingia kambini leo na itaendelea na mazoezi yake hadi hapo itakapokutana na Elan, Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa.

Alisema kiufundi timu ipo katika hali nzuri na wachezaji wote wanaendelea vyema huku kocha Patrick Phiri akikiri kuwa mechi walizocheza zimewapa mwanga mzuri wa kujiwinda vyema dhidi ya wapinzani wao.

"Timu yetu ipo vizuri kabisa na na wachezaji wote wapo katika hali nzuri kila mmoja akielekeza akili yake katika mchezo wetu wa kimataifa ambao kwa sasa tunaupa umuhimu mkubwa,tunajiandaa kikamilifu kupambana na wageni wetu na tunaamini tutafanya vizuri,"alisema Ndimbo.

Endapo Simba itashinda, raundi ya kwanza itakutana na timu ya TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika raundi ya pili.

Kwa upande wao, Yanga itapanda ndege Alhamisi kuelekea Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano dhidi ya Dedebit.

Katika mchezo wa awali uliofanyika Dar es Salaam timu hizo zilitoka sare ya mabao 4-4 katika mchezo uliofanyika karibu wiki mbili zilizopita.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Lloyd Nchunga alisema kuwa wao walipanga timu hiyo kuondoka kesho Jumatano, lakini mpaka sasa wenzao hawajawatumia tarehe ya mechi hiyo.

''Unajua wale wenzetu bado hawajatutumia tarehe ya mchezo wa marudiano kitu ambacho kinatupa ugumu sana sisi kwani tulipanga kwenda mapema kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa ya huko kwani kule ni baridi sana,'' alisema Nchunga.

Pia, alisema katika msafara huo kutakuwa na kocha wao mpya, Sam Timbe raia wa Uganda aliyechukua mikoba ya Kostadin Papic aliyejiuzulu hivi karibuni baada ya kudai kuwa uongozi haukumshirikisha katika masuala ya kumchagua msaidizi wake, Ferd Felix Minziro.

Alisema kocha huyo ameanza kazi rasmi jana ya kuinoa timu hiyo ambayo imerejea jana kutoka Songea kucheza mchezo wao wa ligi dhdi ya Majimaji na kutoa suluhu 0-0.

Naye Minziro alisema kuwa bado ana amini kuwa timu yake inauwezo wa kufanya makubwa katika mchezo wao wa marudiano dhidi ya Dedebit na kuwatupa nje ya michuano hiyo.

Alisema anajua mechi hiyo ni ngumu sana, lakini tayari wamekwishafahamu upungufu wao uko wapi, hivyo watajitaidi kuhakikisha wanashinda katika mchezo huo.

Comments




0 #1 ay 2011-02-08 06:51 Upungufu wenu Yanga unatokana na kutomtendea haki Papic, kutokulipa madeni yenu na pia kuwalipa wachezaji kama inavostahaki.
Quote

 
Simba, Yanga kazeni buti CAF

ban_tahariri.jpg

amka2.gif
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya kimataifa barani Afrika, Simba na Yanga, zinakabiliwa na mechi za marudiano za hatua ya awali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Hizi ni mechi zitakazopigwa kati ya Februari 12 hadi 14, baada ya kutanguliwa na mechi za awali zilizopigwa huko Moroni na jijini Dar es Salaam.
Katika mechi hizo za awali, tofauti na Watanzania walivyokuwa wakitegemea matokeo yake yaliwashangaza na kuwaacha wamepigwa bumbuwazi, baada ya wawakilishi wao wote kupata matokeo ya sare.
Yanga ambayo ilikuwa nyumbani jijini Dar es Salaam ililazimishwa sare ya 4-4 na Dedebit huku Simba nayo ikienda sare ugenini ya bila kufungana.
Wakati Yanga wakiwa ugenini Ethiopia, Simba watakuwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam kuwakabili Elan Club ya mjini Mitsoudje, Comoro.
Kulingana na umuhimu wa mashindano haya na matokeo ya wawakilishi wetu katika mechi za awali, sisi wa Tanzania Daima tukiwa kama wadau wa michezo na burudani, tumesukumwa kuzipa tahadhari timu zetu kuwa ziko mguu ndani mguu nje kuendelea katika kinyang'anyiro hicho.
Kutokana na matokeo hayo, wawakilishi wetu wanapaswa kutambua kuwa bado wana kibarua kigumu kusonga mbele kwani lolote linaweza kutokea na kujikuta wakitupwa nje ya michuano hiyo.
Kwenda katika mechi hizo kwa fikra ya wapinzani wetu si mahiri sana au faida ya uwanja wa nyumbani ni mambo ya kuepukwa kwani yanaweza kusababisha maafa.
Kikubwa kwa Simba na Yanga zihesabu kama zimepoteza mechi zao za awali na hivyo kuwa na deni kubwa la kusaka ushindi wa mabao mengi ili kujihakikishia kusonga mbele.
Simba ambayo itakuwa uwanja wa nyumbani jijini Dar es Salaam inapaswa kuhakikisha inautumia vema kuwaondosha Wacomoro ili iweze kuingia raundi ya kwanza na kuwavaa mabingwa watetezi TP Mazembe wa DRC.
Nayo Yanga ambayo itakuwa na kibarua kigumu ugenini, sare ya nyumbani isiwatie hofu bali waingie uwanjani kwa kujiamini na kujituma ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi ugenini.
Timu hizo zote ambazo zimetoka katika mechi zao za Ligi Kuu bara, zinapaswa kutumia muda huu mchache uliobaki kujiandaa vema na kurekebisha kasoro zilizojitokeza ili kuhakikisha zinaibuka na ushindi katika mechi hizo na kuipeperusha vema bendera ya Tanzania.
Kwa upande wa mashabiki na wadau wa soka hapa nchini ni wakati wao kuimarisha mshikamano na kuondoa tofauti zao angalau kwa muda ili kuunganisha nguvu na kuhakikisha ushindi unapatikana kwa manufaa ya taifa.
Lakini tunaonya, kinyume cha hapo, yaani klabu zikaridhika na wadau kujitenga, tusishangae kushuhudia wawakilishi wetu wote wakiaga huku tukibaki kuchagua timu za wenzetu za kuzishangilia.
Shime Simba na Yanga, jipangeni mkafanye kweli katika michezo yenu ya marudio na kuwapa raha Watanzania, kwani wahenga walinena penye nia pana njia, hivyo hapo inachotakiwa ni kutia nia na yote yanawezekana.
Mungu zibariki Simba na Yanga, Mungu Ibariki Tanzania.
 
Tanzania yaingia mtego wa Fifa Monday, 07 February 2011 20:50

Sweetbert Lukonge

HUKU Tanzania ikiwa imejitega kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kwa kukubali kucheza na Palestina kesho, hukuShirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo huo kuwa ni kati ya Shilingi 10,000 na 1000.

Tanzania ambayo inashika nafasi ya 123 katika viwango vya sasa vya Fifa inaweza kuporomoka zaidi endapo itashindwa wa wageni hao walioko chini yao katika viwango vijavyo vya Fifa.

Mchezo huo wa kirafiki utafanyika kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na unatarajiwa kuwa na historia yakutokana na Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kucheza na Palestina.

Akizungumza na Mwananchi jana, ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kuwa wameamua kuweka viingilio hivyo ili kutoa nafasi kwa Watanzania wengi kujitokeza na kuishangilia timu yao katika mchezo huo.

"Tumeamua kufanya hivyo ili kila mtu mpenda soka aje kuiunga mkono timu yetu na viingilo katika viti vya kijani mzunguko itakuwa ni Sh1000, Sh 2000 viti vya rangi ya bluu na Sh 3000 kwa viti vya rangi ya chungwa.

"Kwa upende wa VIP C, Wambura alisema kiingilio itakuwa ni Sh 5000, VIP B ni Sh 7,000 na VIP A kingilio ni Sh 10000," alisema Wambura.

Alisema tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zinaanza kuuzwa leo katika vituo vya Big Bon Kariakoo, Uwanja wa Taifa, Benjamini Mkapa pamoja na mgahawa wa Steers.

Katika hatua nyingine, Wambura alisema kuwa mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi kutoka hapa nchini ambao tayari wameteuliwa na Fifa ambao ni Oden Mbaga atakayesaidiwa na Hamis Chang'walu na Hamis Kisiwa.

Mbali na hilo, pia TFF kwa kushirikiana na Fifa wanatarajia kufanya mapitio ya azimio la Bagamoyo lilitokana na semina ya iliyoandaliwa na mashirikisho hayo mawili kwa klabu za Ligi Kuu iliyofanyika Desemba 2007.

Wambura alisema kuwa mapitio hayo yataanza kufanyika Februari 14-18 kwemye hoteli ya Whitesands, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Alisema Fifa ilikubaliana na klabu husika kuwa yafanyike mapitio ya kile kilichoazimiwa baada ya miaka mitatu ili kuona utekelezaji wake na kutafutia ufumbuzi upungufu utakokuwa umejitokeza.

Maeneo ambayo klabu hizo zilipendekeza yafanyiwe mapitio ni pamoja na muundo wa utawala katika klabu, mfumo wa idara ya ufundi, vitendea kazi pamoja na utawala bora.
 
Simba, Tanzania Polisi ilikuwa mshikemshike Monday, 07 February 2011 20:47

Masoud Masasi, Dodoma
MECHI ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Polisi Tanzania na Simba ya Dar es salaam imeingiza zaidi ya milioni19 katika mapato ya mlangoni kwenye mchezo huo uliojaza mashabiki wengi uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa.

Katika mchezo huo ambao timu ya Simba ilishinda mabao 2-0 yaliyofungwa na mshambuliaji wake Mussa Hassan Mgosi na uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dodoma.

Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Dodoma (DOREFA) Abobakar Ibrahim alisema katika mchezo huo mashabiki 8,161 waliingia kushuhudia pambano hilo na sh.19,322,000 zilipatikana katika mchezo huo.

Saa chache kabla ya mchezo, Mwananchi ilishuhudia baadhi ya mashabiki wakigombania tiketi hatua iliyofanya wakanyagane licha ya tiketi kuanza kuuzwa kuanzia saa 4:00 asubuhi hatua iliyofanya baadhi kuibiwa simu na fedha na kundi la vibaka waliokuwepo uwanjani hapo.

Hata hivyo katika mchezo huo mashabiki wengi walikosa ustarabu kwa kuvamia uwanja mara baada ya mechi kumalizika na kwenda kuwapongeza wachezaji wa Simba hali iliyowapa wakati mgumu wachezaji hao hasa na kulazimika kukimbilia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kuwakepa mashabiki hao waliokuwa wengi kushinda askari waliopo uwanjani hapo.

Wakati huo huo, ligi ngazi ya mkoa inatarajia kuanza kutimua vumbi leo katika viwanja mbalimbali mkoani hapa.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa DOREFA, Abobakar alisema maandalizi ya ligi hiyo tayari yamekamilika na timu zote zimeshawasili katika vituo vyao walivyopangiwa.
 
Hiki ndio chanzo cha chokochoko TEFA
ban.blank.jpg

Abdallah Menssah

amka2.gif
MARA nyingi unapofikia wakati wa uchaguzi mkuu wa chama cha soka wilayani Temeke huzuka migogoro ambayo husababisha mivutano ambayo haileti tija katika maendeleo ya soka.
Kuzuka kwa migogoro na vurugu kila unapofanyika uchaguzi wa viongozi wa TEFA, limekuwa ni jambo la kawaida hivi sasa.
Katika miaka ya hivi karibuni, chaguzi za TEFA zimekosa kuwa za amani, kiasi cha kufikia kusimamiwa na maofisa wa usalama wakiwa na silaha kwa ajili ya kujihami na ghasia zinazoweza kuzuka.
Hali hiyo iko tofauti kabisa na chaguzi katika vyama vingine vya wilaya kama Ilala (IDFA) pamoja na Kinondoni (KIFA), jijini Dar es Salaam, ambako chaguzi zake mara zote huwa ni shwari kabisa.
Kupigania mabadiliko kwa kuung'oa utawala wa TEFA ulio madarakani ni kati ya madai makubwa ya baadhi ya wanaojiita wanachama wa chama hicho, wanaotokea kuibua migogoro na vurugu katika vipindi vya uchaguzi.
Ajabu ni kuwa kinachotokea kila baada ya chaguzi hizo huwa tofauti kabisa, kwani viongozi wanaopita tena kwa kishindo, huwa ni walewale waliokuwa wakipigiwa kelele za kupingwa kipindi cha kampeni.
Kutokana na hali ambayo hivi sasa inazidi kuota mizizi kama si kutaka kuwa utamaduni, Mwandishi wa makala hii alilazimika kumtafuta Mwenyekiti wa TEFA, Peter Mhinzi, ili kuzungumzia hili kwa mapana zaidi.
Mhinzi anaanza kwa kubainisha kuwa unapotangazwa uchaguzi wa TEFA kila mmoja huwa huru kugombea.
"Unajua, uchaguzi wa TEFA unapotangazwa kila mtu huwa huru kugombea hata kama si mwanachama na hicho ndio huwa chanzo cha vurugu kwani wengi hupigana vikumbo ili wapate kula na umaarufu," alisema Mhinzi.
Aidha, Mhinzi anasema utajiri uliopo TEFA pia ni sababu kubwa za kutokea kwa vurugu wakati wa uchaguzi, kwani hivi sasa chama hicho kina miundombinu, mitaji na njia za kupatia fedha, huku ikivuta hisia za hadi matajiri wanaotaka kujitangaza kibinafsi.
Anasema, hali hiyo ndio inayofanya uchaguzi wa chama hicho utofautiane na chaguzi katika vyama vyote vingine jijini Dar es Salaam, kama IDFA ambako uchaguzi wao wa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2003.
"Mara ya kwanza kuingia madarakani mwaka 1974, hakukuwa na mikikimikiki tena, niliombwa kugombea kwa sababu uongozi ulikuwa ni mzigo," anasema Mhinzi.
Anasema, wakati huo klabu zilikuwa si zaidi ya 20, TEFA haikuwa na ofisi na nyaraka kama mafaili yalikuwa yanawekwa nyumbani kwa kiongozi husika.
Mhinzi anawakumbuka baadhi ya viongozi wa TEFA wa wakati huo, kuwa ni pamoja na Shaaban Mchumila na Tido Mhando waliokuwa wakijichangisha wenyewe katika masuala mbalimbali yahusuyo chama hicho.
Kadhalika, Mhinzi anasema, utatuzi pekee wa hali hii ya migogoro na vurugu kwenye chaguzi ni kuwa na katiba nzuri na wanachama kuiheshimu katiba hiyo.
"Vilevile, asasi za habari na zinazotoa haki, ziheshimu maamuzi ya wanachama wa TEFA," anasema Mhinzi huku akisisitiza kuwa, maoni ya watu barabarani yasichukuliwe na kugeuzwa tuhuma.
Anawaomba wanahabari kutoshabikia migogoro inayoanzishwa kwa makusudi na wenye tamaa ya kuwa viongozi, kwa manufaa yao binafsi ya umaarufu na utajiri zaidi.
Anatoa mfano kampeni za uchaguzi zilizomalizika hivi karibuni, ambako anadai vyombo vya habari vilimpa kipaumbele Abdulrahman Kipenga asiyekuwa mwanachama wa TEFA.
Anasema, katika vipindi vya uchaguzi, wanaopiga kelele kutaka mabadiliko katika uongozi, wakidai waliokuwapo madarakani ni wabovu, si wanachama ndio maana kila mara orodha inayorejea kutawala huwa ni ile ile.
"Kama ni kweli kuwa kelele za kutaka mabadiliko ndani ya TEFA zinapigwa na wanachama, sisi tusingechaguliwa tena, ama kama tungepita, basi wangejitokeza watu kukata rufaa," anasema Mhinzi.
Mhinzi anasema, hivi sasa wamepata dawa ya kudhibiti vurugu hizo anazoziita za kutengezwa kwa makusudi, kwa kuwapatia vitambulisho maalum wanachama wao wote.
Anasema, kuanzia sasa anayetaka kulalamika kuhusu jambo lolote kwenye uongozi wa TEFA ni lazima awe na kielelezo, ambacho ni kitambulisho cha uanachama.
Mhinzi anasema, kama TEFA wanajivunia kulifikisha soka la Temeke hatua ya kuzungumzwa kimataifa, kwani ni matunda yao, huku akijisifu kuwa wako juu kimichezo na kiuchumi pia.
"Kingine cha kujivunia ni kuwa chama chetu ndiyo pekee chenye uwanja, kilichotoa Makamu wa kwanza wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), ambaye ni Athuman Nyamlani," anasema Mhinzi, kati ya waasisi wa TEFA.
Anasema, vile vile wameiondoa TEFA kutoka katika ofisi iliyokuwa mifukoni na majumbani kwa viongozi na kuwa yenye ofisi rasmi na inayoheshimika zaidi.
Mhinzi anasema hivi sasa wako katika mkakati wa utekelezaji wa uwanja wa kisasa kwa kufumua sehemu ya kucheza na pia kuongeza maduka kutoka 131 hadi kufikia 371.
Uongozi wa TEFA ulioingia madarakani hivi karibuni unaongozwa na mwenyekiti Peter Mhinzi, makamu wa kwanza Saleh Mohammed, makamu wa pili, Bakili Makere, mweka hazina, Yusufu Kinega, mweka hazina msaidizi, Henry Kaiza, na mwakilishi mkoa, Francis Mdenda ‘Waya'.
Mwakilishi wa klabu ni Said Akida, wakati wajumbe ni Fikiri Magoso, Ally Kulita na Obby Steleck.

Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa simu namba 0718 102050, au baruapepe abmenssah@yahoo.com



h.sep3.gif


Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa simu namba 0718 102050, au baruapepe abmenssah@yahoo.com
 
Tanzania yaingia mtego wa Fifa
Monday, 07 February 2011 20:50

Sweetbert Lukonge

HUKU Tanzania ikiwa imejitega kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kwa kukubali kucheza na Palestina kesho, hukuShirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo huo kuwa ni kati ya Shilingi 10,000 na 1000.

Tanzania ambayo inashika nafasi ya 123 katika viwango vya sasa vya Fifa inaweza kuporomoka zaidi endapo itashindwa wa wageni hao walioko chini yao katika viwango vijavyo vya Fifa.

Mchezo huo wa kirafiki utafanyika kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na unatarajiwa kuwa na historia yakutokana na Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kucheza na Palestina.

Akizungumza na Mwananchi jana, ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kuwa wameamua kuweka viingilio hivyo ili kutoa nafasi kwa Watanzania wengi kujitokeza na kuishangilia timu yao katika mchezo huo.

"Tumeamua kufanya hivyo ili kila mtu mpenda soka aje kuiunga mkono timu yetu na viingilo katika viti vya kijani mzunguko itakuwa ni Sh1000, Sh 2000 viti vya rangi ya bluu na Sh 3000 kwa viti vya rangi ya chungwa.

"Kwa upende wa VIP C, Wambura alisema kiingilio itakuwa ni Sh 5000, VIP B ni Sh 7,000 na VIP A kingilio ni Sh 10000," alisema Wambura.

Alisema tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zinaanza kuuzwa leo katika vituo vya Big Bon Kariakoo, Uwanja wa Taifa, Benjamini Mkapa pamoja na mgahawa wa Steers.

Katika hatua nyingine, Wambura alisema kuwa mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi kutoka hapa nchini ambao tayari wameteuliwa na Fifa ambao ni Oden Mbaga atakayesaidiwa na Hamis Chang'walu na Hamis Kisiwa.

Mbali na hilo, pia TFF kwa kushirikiana na Fifa wanatarajia kufanya mapitio ya azimio la Bagamoyo lilitokana na semina ya iliyoandaliwa na mashirikisho hayo mawili kwa klabu za Ligi Kuu iliyofanyika Desemba 2007.

Wambura alisema kuwa mapitio hayo yataanza kufanyika Februari 14-18 kwemye hoteli ya Whitesands, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Alisema Fifa ilikubaliana na klabu husika kuwa yafanyike mapitio ya kile kilichoazimiwa baada ya miaka mitatu ili kuona utekelezaji wake na kutafutia ufumbuzi upungufu utakokuwa umejitokeza.

Maeneo ambayo klabu hizo zilipendekeza yafanyiwe mapitio ni pamoja na muundo wa utawala katika klabu, mfumo wa idara ya ufundi, vitendea kazi pamoja na utawala bora.
 
Azam yageuka tishio Ligi Kuu Monday, 07 February 2011 20:50

Doris Maliyaga

MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu Bara, ukiwa kwenye mapumziko kwa ajili ya kupisha mechi za kimataifa za klabu kwa michuano ya Shirikisho na Ligi ya Mabingwa pamoja na timu ya Taifa ‘Taifa Stars' na itaendelea tena Jumapili, Febuari13.

African Lyon ilifunga pazia hilo kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Ruvu kwenye mchezo pekee uliochezwa jana. Lyon ilipata bao lake la kuongoza dakika 20, kupitia kwa Haji Dudu aliyepokea pasi ya Idrisa Rashid.

JKT walisawazisha dakika ya 44, kupitia kwa Kess Mapande kwa shuti akiwa nje ya eneo la18, baada ya kipa Noel Lucas kutoka golini, Lyon ilipata bao la ushindi dakika ya 90 kupitia Samwel Ngasa aliyeunganisha mpira wa kona uliopigwa na Bakari Omary.

Wakati hilo likiendelea, Azam ndiyo inaongoza kwa ubora, hukuPolisi Tanzania ndiyo kibonde na imevurunda baada ya kufungwa mechi zote nne walizocheza.

Katika mechi hizo, mabao 56, yamefungwa katika michezo 24 iliyochezwa mzunguko wa pili sawa na wastani wa mabao 2.3 ambapo ndani ya mabao hayo Azam inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo, imefunga mabao mengi zaidi 11, ikifuatiwa na Yanga nane na Simba saba.

Timu hiyo imefanya mabadiliko na kuwa tishio baada ya kuzinduka hatua ya pili ikiwa chini ya kocha Mwingereza, Stewart Hall ambaye ameiwezesha kushinda kila mechi.

Mshambuliaji wake, John Boko aliyefunga mabao sita katika mechi tatu kila moja akifunga mawili amempiku kwa ubora Mzambia Davies Mwape wa Yanga aliyefunga matano, yakiwamo mawili katika mechi moja na nyingine matatu pamoja na Gaudence Mwaikimba wa Kagera Sugar aliyefunga matano katika mechi nne alizocheza mawili mechi moja na yaliyobaki alifunga moja kila mchezo.

Mrisho Ngassa ndiye anayeongoza kuwa na mabao 10, akiwa amefunga manne katika mchezo mmoja na moja moja kwenye mechi nyingine anafuatiwa Mussa Hassan ‘Mgosi' wa Simba ambaye kasi yake ilizinduka na kung'aa mechi yao dhidi ya Polisi Tanzania baada ya kufunga mabao mawili peke yake na kufanya safu hiyo kuongozwa na Ngassa,Mwaikimba mabao tisa, Boko nane, Mgosi na Tegete wakifungana kwa mabao sita.

Simba ndio kinara wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 32, ikiizidi Yanga kwa pointi moja, Azam ni ya tatu pointi 29, Mtibwa Sugar ya nne pointi 26, inafuatiwa na Kagera Sugar ya tano pointi 25 na JKT Ruvu ya sita pointi 21.

Toto Africa ya Mwanza ni ya saba ikiwa na pointi 16, nyuma ya ya JKT Ruvu huku Afican Lyon ikishika ya nane, Ruvu Shooting ikiwa ya tisa ikiwa na pointi 13 sawa na Polisi Tanzania yenye 10, ikifuatiwa na Majimaji yenye 11 na AFC Arusha nane.
 
Katika hili Yanga mueleweni Davis Mosha
ban.nachonga.jpg

Tullo Chambo

amka2.gif
KARIBUNI tena wapenzi wa safu hii ya Uwanja wa Kuchonga iwajiayo kila siku kama ya leo, lengo lilikiwa kujadiliana na kupeana changamoto kwa ajili ya kuongeza ufanisi.
Bila shaka mu wazima wa afya na mnaendelea vema na majukumu ya ujenzi wa Taifa, kwa wale ambao hali zao si shwari tunawaombea nafuu waweze kurejea kwenye hali zao za kawaida.
Kabla hatujajikita katika mada yetu ya leo, tukumbushane kwa ufupi kile kilichojiri Uwanjani wiki iliyopita.
Wiki iliyopita tuliwastua washika dau wote wa mchezo wa riadha, katika mustakabali mzima wa kuelekea katika tukio kubwa na muhimu, nalo si jingine bali uchaguzi mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu.
Katika mada hiyo tuliwaeleza RT jinsi wanavyojiandalia mazingira ya kuongozwa na viongozi vimeo.
Tulizungumzia jinsi uchaguzi ambao tuliuita ni wa kihistoria uliofanyika mwaka 2006 jijini Mwanza, ambao ndio ulizaa RT kutoka iliyokuwa ikiitwa TAAA.
Ni uchaguzi uliofanyika baada ya chama hicho enzi hizo kikijulikana kama TAAA kukaa miaka tisa bila kuchaguana hivyo kudumisha ufanisi na maendeleo ya mchezo huo, achilia migogoro ya kila kukicha.
Lakini katika hili, tulizungumzia mazingira ya uchaguzi wa Mwanza yalivyokuwa na matatizo na fitna zilizotumika na ile iliyokuwa Kamati ya Uchaguzi kufanikisha uchaguzi huo huku katiba ikifinyangwa katika namna ya kuogopa mabadiliko na kuwalinda baadhi ya wahusika, hivyo kwa namna moja ama nyingine kushindwa kuchagua viongozi muafaka.
Kutokana na makosa yaliyofanyika 2006, madhara yake ndio haya tunayashuhudia sasa ndani ya RT, ambako viongozi wachapakazi wameonekana na vimeo vimeonekana, ambako wahusika walioshiriki kuwaweka madarakani viongozi hao wanalia na kusaga meno wakitaka uchaguzi hata leo ili waweze kurekebisha makosa yao ya awali, lakini ndio hivyo walishachelewa.
Lakini wakati makovu ya 2006 yakiwa bado hayajapona, RT imetangaza mchakato kuelekea uchaguzi wa Novemba ili hali ikiwa kama ile ile ya 2006, jambo ambalo mashabiki wa Uwanja wa Kuchonga hatukusita kulipigia kelele hilo na kutoa maono jinsi chama hicho kinavyojiandaa tena kuongozwa na vimeo.
Bila shaka wahusika ujumbe ulifika na kwa nia njema ya mchezo huu wenye historia iliyotukuka hapa nchinini, wahusika watayafanyia kazi mapungufu hayo ili twende uchaguzi wa Novemba tukiwa hatuna mianya ambayo itaruhusu au kuwezesha watu wasi na uzalendo na uchungu na mchezo hii jumlisha uwezo kupata nafasi ya kuingia na kuzidi kuudidimiza.
Baada ya dondoo hizo, turejee katika mada yetu ya leo. Kwa takriban mwezi sasa, hali ndani ya klabu kongwe ya Yanga si shwari.
Yameshuhudiwa mengi katika klabu hiyo ndani ya muda huop mfupi wa misigano, ikiwamo baadhi ya viongozi kuachia ngazi na sasa kinachojiri ni vurugu za kuwapiga viongozi na wachezaji pale matokeo ya uwanjani yanapokuwa sio mazuri.
Kimsingi mitafaruku hii ndani ya Yanga ilianza na kugawanyika katika makundi makuu mawili, moja likiwa la mfadhili na mjumbe wa bodi ya wadhamini, Yussuf Manji, akiwa na mwenyekiti wa klabu hiyo Lloyd Nchunga huku mwingine ukiwa wa viongozi wengine wa Kamati ya Utendaji wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti, Davis Mosha.
Ndani ya muda huo mfupi wa mtafaruku ndani ya Yanga, madhara mengi yamejitokeza kama nilivyodokeza hapo awali na kutokana na kutotafutiwa ufumbuzi, ule usemi wa vita ya panzi......... unazidi kujidhihirisha. Hivi sasa wanaothirika Yanga tumeshuhudia ni Wanayanga wenyewe.
Yanga hivi sasa ufanisi wake ndani ya dimba ni hafifu, tena ukizingatia kipindi hiki ikiwa kwenye michuano ya kimataifa.
Kugawanyika kwa uongozi wa Yanga hivi sasa, kumetokana na kupishana misimamo kati ya makundi hayo mawili niliyoyaainisha hapo juu, wakati Mwenyekiti na Manji wakituhumiwa kufanya maamuzi makubwa ndani ya klabu hiyo bila kushirikisha vikao husika, Mosha na wenzake nao wanageuziwa kibao eti kuwa wametumwa kuihujumu klabu hiyo na mfadhili huyo.
Inashangaza, lakini ukweli ulio wazi kitendo cha Mosha na wenzake, hata viongozi wa matawi ya Mkoa wa Dar es Salaam ambao waliitisha mkutano makao makuu ya klabu na kung'amua mambo mengi ya kimsingi ambayo yalikuwa yakipindishwa ndani ya klabu, wote walikuwa na nia moja ya kuiona Yanga inabaki kuwa Yanga.
Lakini kwa makusudi kabisa, wanaoitwa wanachama wakereketwa ambao baadhi yao wanajiita Jeshi la Manji, wanapotosha maana na hoja za Mosha na wenzake, kisa tu Manji kaguswa, bila kuangalia maslahi ya klabu. Kwa lugha nyepesi wanachama hao wako Yanga kuangalia maslahi ya watu wachache na wala si klabu yao.
Kuthibitisha hilo, ndio haya yanayotokea hivi sasa viwanjani Yanga inapocheza, ambako matokeo yanakuwa si mazuri na wanachama hao kuanzisha vurugu za kuwapiga na kuwajeruhi viongozi ambao hawaungi mkono maamuzi binafsi ya Manji na Nchunga, hali ambayo inazidi kuichafua na kuhatarisha amani ndani ya klabu hiyo kongwe.
Hivi karibuni limeshuhudiwa tukio la hatari ambalo si la kianamichezo, ambako baadhi ya wachezaji walinusurika kula kibano kutoka kwa wanachama hao, huku Makamu Mwenyekiti Mosha akiponea chupuchupu kujeruhiwa kwa mawe ambayo yaliishia kuvunja kio cha gari lake.
Kutokana na hali hiyo, Mosha alifungua jalada kituo cha Polisi Chang'ombe kuhusiana na tukio hilo, akiwatuhumu watu kadhaa kuhusiana na hali hiyo, ambako baadhi yao walokamatwa na kushikiliwa na Jeshi la Polisi.
Lakini wakati hali ikiwa hivyo, juzi Mosha kwa moyo wa kiungwana na kiuna michezo kwa maslahi ya klabu ya Yanga, alifikia uamuzi wa kumsamehe kijana aliyeongoza uharibifu wa gari lake, baada ya mtuhumiwa kukiri na kuomba msamaha.
Pili Mosha alifanya kazi ya ziada, lengo likiwa ni kuiona Yanga moja yenye amani, kwenda kukutana na kundi hilo la Wanachama ambalo limekuwa likiendesha kampeni za kumchafua na kumpinga, kuzungumza nao kwa kina kuhusiana na hayo wanayomtuhumu.
Kutokana na hali ilivyo hivi sasa ndani ya Yanga, hakika Mosha amejipambanua ni kiongozi wa namna gani ndani ya klabu hiyo na atakayeshindwa kumwelewa basi ana matatizo.
Mosha ameonyesha ukomavu kwa kutaka kuyamaliza matatizo haya kiungwana na kiuna michezo, tofauti na baadhi ya wanachama ambao wanajidanganya kuwapiga ama kuwafanyia vurugu viongozi na wachezaji ndio ukereketwa wa kuisaidia Yanga.
Wanachama hao ambao wanashindwa kujenga nguvu ya hoja katika vikao halali na kukimbilia kufanya vurugu, wanapaswa kutambua kuwa hilo haliwezi kuwa suluhisho la amani na mafanikio ndani ya klabu hiyo, bali ni kuididimiza kama ambavyo hivi sasa hali inatokea.
Kwani endapo Mosha na wenzake ambao wanaandamwa na kundi hilo la Wanachama, nao wangejipanga na kuwaandaa wanachama wao wanaowainga mkono, sijui kama Yanga pangekalika.
Hivyo kwa uamuzi alioufanya Mosha juzi, hakika kwa kila Mwana Yanga wa kweli na si Yanga maslahi, anapaswa kuukubali, kuuelewa na kuunga mkono kwa manufaa ya Yanga na wala si ya mtu binafsi, vinginevyo kinyume cha hapo, basi huyo haitkakii mema klabu hiyo. Hivyo wito kwa wana Yanga, muelewi Davis Mosha kwa maslahi ya klabu.
Ni imani yetu amani itarejea na kudumu Yanga kwa manufaa ya klabu hiyo na maendeleo ya soka la Tanzania kwa ujumla. Kila la heri tukutane wiki ijayo.
 
Azam yageuka tishio Ligi Kuu Monday, 07 February 2011 20:50

Doris Maliyaga

MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu Bara, ukiwa kwenye mapumziko kwa ajili ya kupisha mechi za kimataifa za klabu kwa michuano ya Shirikisho na Ligi ya Mabingwa pamoja na timu ya Taifa ‘Taifa Stars' na itaendelea tena Jumapili, Febuari13.

African Lyon ilifunga pazia hilo kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Ruvu kwenye mchezo pekee uliochezwa jana. Lyon ilipata bao lake la kuongoza dakika 20, kupitia kwa Haji Dudu aliyepokea pasi ya Idrisa Rashid.

JKT walisawazisha dakika ya 44, kupitia kwa Kess Mapande kwa shuti akiwa nje ya eneo la18, baada ya kipa Noel Lucas kutoka golini, Lyon ilipata bao la ushindi dakika ya 90 kupitia Samwel Ngasa aliyeunganisha mpira wa kona uliopigwa na Bakari Omary.

Wakati hilo likiendelea, Azam ndiyo inaongoza kwa ubora, hukuPolisi Tanzania ndiyo kibonde na imevurunda baada ya kufungwa mechi zote nne walizocheza.

Katika mechi hizo, mabao 56, yamefungwa katika michezo 24 iliyochezwa mzunguko wa pili sawa na wastani wa mabao 2.3 ambapo ndani ya mabao hayo Azam inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo, imefunga mabao mengi zaidi 11, ikifuatiwa na Yanga nane na Simba saba.

Timu hiyo imefanya mabadiliko na kuwa tishio baada ya kuzinduka hatua ya pili ikiwa chini ya kocha Mwingereza, Stewart Hall ambaye ameiwezesha kushinda kila mechi.

Mshambuliaji wake, John Boko aliyefunga mabao sita katika mechi tatu kila moja akifunga mawili amempiku kwa ubora Mzambia Davies Mwape wa Yanga aliyefunga matano, yakiwamo mawili katika mechi moja na nyingine matatu pamoja na Gaudence Mwaikimba wa Kagera Sugar aliyefunga matano katika mechi nne alizocheza mawili mechi moja na yaliyobaki alifunga moja kila mchezo.

Mrisho Ngassa ndiye anayeongoza kuwa na mabao 10, akiwa amefunga manne katika mchezo mmoja na moja moja kwenye mechi nyingine anafuatiwa Mussa Hassan ‘Mgosi' wa Simba ambaye kasi yake ilizinduka na kung'aa mechi yao dhidi ya Polisi Tanzania baada ya kufunga mabao mawili peke yake na kufanya safu hiyo kuongozwa na Ngassa,Mwaikimba mabao tisa, Boko nane, Mgosi na Tegete wakifungana kwa mabao sita.

Simba ndio kinara wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 32, ikiizidi Yanga kwa pointi moja, Azam ni ya tatu pointi 29, Mtibwa Sugar ya nne pointi 26, inafuatiwa na Kagera Sugar ya tano pointi 25 na JKT Ruvu ya sita pointi 21.

Toto Africa ya Mwanza ni ya saba ikiwa na pointi 16, nyuma ya ya JKT Ruvu huku Afican Lyon ikishika ya nane, Ruvu Shooting ikiwa ya tisa ikiwa na pointi 13 sawa na Polisi Tanzania yenye 10, ikifuatiwa na Majimaji yenye 11 na AFC Arusha nane.
 
Ligi 9Bora yapamba moto Tanga
Monday, 07 February 2011 20:46

Calvin Kiwia
IKIWA imechezwa jumla ya michezo 12 kwenye Fainali za ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara zinazoendelea kutimua vumbi lake kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga, mabao 19 yamefungwa kwenye ligi hiyo mpaka sasa.

Maafande wa Oljoro JKT Arusha wanaongoza kwa idadi kubwa ya mabao ya kufunga kwenye fainali hizo wakiwa wamekwishafunga mabao matano kwa michezo yao miwili waliyocheza tangu kuanza kwa ligi hiyo.

Huku Morani FC Manyara ikiwa inaongoza kwa idadi kubwa ya mabao ya kufungwa ikiwa imekwishafungwa mabao saba mpaka sasa kwa michezo yake mitatu iliyocheza.

Mshambuliaji wa Oljoro JKT, Nasoro Said ndiye anayeongoza kwa kupachika mabao akiwa amepachika mabao mawili mpaka sasa.

Rhino Rangers ya Tabora ndiyo timu pekee ambayo haijaruhusu nyavu zake kuguswa kwa michezo yake yote mitatu iliyocheza kwenye fainali hizo zinazoendelea kutimua vumbi lake kituo cha Mkwakwani Tanga.

Hata hivyo, Polisi Morogoro ni timu ambayo haijaweza kufunga bao lolote kwenye Fainali hizo mpaka sasa kwa michezo yote mitatu iliyocheza, imefungwa mabao matatu lakini yenyewe haijafunga bao hata moja wala ladha ya kufunga bao bado hawajaionja.

Timu za Tanzania Prisons Mbeya na Oljoro JKT Arusha ndizo ambazo zimecheza michezo miwili wakati nyingine zote zikiwa zimecheza michezo mitatu kila moja.
 
Cameroon , Ivory Coast zaanza vyema CHAN 2011
Monday, 07 February 2011 20:44

KHARTOUM, Sudan

CAMEROON na Ivory Coast zimeanza vyema michuano ya mwaka huu ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN), mechi zilizochezwa mwisho wa wiki.

Cameroon, maarufu kama The Indomitable Lions waliwalaza watetezi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa mabao 2-0.

Nao Ivory Coast, The Elephants, wenyeji wa fainali za mwaka 2009 waliilaza Mali 1-0 , mchezo wa Kundi C kwenye Uwanja wa Al Merrikh mjini Omdurman.

Bao moja la kila kipindi kupitia kwao, Joseph Mamosso na Ousmaila Baba yalitosha kuipa ushindi Indomitable Lions dhidi ya DR Congo ambayo ilionekana timu ya kawaida.

Chipukizi Kone Zoumana aliipa bao Ivory Coast katika mchezo mwingine wa michuano hiyo dhidi ya Mali.

DRC waliwatumia wachezaji saba kutoka klabu bingwa ya Afrika, TP Mazembe,, ambao ni kipa Muteba Kidiaba, nahodha Mihayo Kazembe, Kabangu Mulota, Bedi Mbenza, Joel Kimwaki, Kasusula Kiritsho na Alain Kaluyituka Dioko.

Cameroon ambao wanashiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza walianza vibaya kabla ya kujirekebisha licha ya kumpoteza mshambuliaji Valentine Atem aliyeumia dakika 10 za kwanza na nafasi yake kuchukuliwa na Monkam Arnaud.

Hata hivyo, kuondoka kwa Atem, ambaye amerejea kwao baada ya kucheza soka Ulaya hakukuiathiri Cameroon na kuwakabili The Leopards wa DRC ambao walionekana kukosa mbinu za kuwakabili wapinzai wao.


Walikosa nafasi ya kupachika bao la penalti baada ya Abouna Patrick kukosa mkwaju huo dakika ya 30 ya mchezo huo.

Sehemu ya kiungo ya DRC ikiwa chini ya Nkanu Mbiyavanga, Salakiaku Matondona Mbenza ilionekana kupwaya kwa kiasi kikubwa huku Kaluyituka akizuiwa na mabeki wa Cameroon.

Kipa Kidiaba aliwazuia Cameroon dakika ya 36 ya mchezo kwa kuzuia mkwaju wa Joel Babanda. Dakika ya 41, Joseph Momasso alipachika bao la kwanza kwa juhudi zake boinafsi kisha kumchambua kipa Kidiaba.

Kipindi cha pili, DRC walibadili mchezo na kupiga pasi ndefu kuwadhibiti Cameroon na kushambulia kwa kushtukiza.

Mchezaji aliyeingia kipindi cha pili, Kasongo Ngandu alikaribia kuziona nyavu, lakini mpira wake uligonga mwamba na kurejea uwanjani baada ya pasi murua ya Kasusula.

Baba aliiipa bao la pili Cameroon dakika ya 78 baada ya kutoelewana kwa kwa beki Gladys Bokese na Kidiaba.
Bokese alimrejeshea pasi ya nyuma kipa wake Kidiaba ambaye alikuwa ametoka langoni kwa kasi, akimwacha Baba akimalizia mpira wavu uliokuwa wazi.

Baadaye, Kone aliifungia Ivory Coast kwa kichwa dakika ya 21 kutokana na krosi ya Kouame Konan.

Mali, ambao pia wanashiriki kwa mara ya kwanza walionekana kukosa mbinu mbele ya lango la wapinzani wao na kushinda kutumia nafasi walizozipata.

Kwa matokeo hayo, Kundi C limeipa uongozi Cameroon na kufuatiwa na Ivory Coast huku DRC na Mali zikiwa hazina pointi.

Afrika Kusini na Niger, pia zilianza vyema michuano hiyo kwa ushindi Jumamosi. Afrika Kusini iliilaza Ghana iliyokuwa ya pili mwaka 2009 kwa bao 1-0. Niger, ambayo pia ni mshiriki kwa mara ya kwanza iliilaza Zimbabwe 1-0.
 
Kwetu Liverpool tulishamsahau Torres, atamba kocha Dalglish Monday, 07 February 2011 20:45

LONDON, Uingereza

KOCHA wa Liverpool, Kenny Dalglish amesema kuwa kikosi chake kilimsahau mshambuliaji wao wa zamani, Fernando Torres kabla ya kucheza na kuilaza Chelsea kwa bao 1-0 Jumapili.

Juzi, Torres aliishuhudia Chelsea ikilala 1-0 katika mchezo wake wa kwanza tangu alipouzwa kwa pauni 50 milioni siku ya mwisho ya dirisha dogo la usajili wa wachezaji Ulaya.

Dalglish ambaye bado ni kocha wa muda wa Livepool alikana kwamba kuwapo kwa Torres katika kikosi cha Chelsea hakukuwa kichocheo kwao kuibuka na ushindi na kumpongeza Raul Mereiles kwa bao safi la kipindi cha pili.

"Raul na wenzake wote walionyesha kuwa ni wachezaji wa kulipwa," alisema Dalglish mzaliwa wa Scotland. "Sidhani kama kuwapo kwa Torres kulikuwa kivutio.

"Kivutio kwetu kilikuwa ni kupata pointi tatu na tumefanikiwa. Kile tulichokitaka ni kupata pointi tatu dhidi ya Chelsea na kuzidi kusonga mbele.

"Nilikwenda Stamford Brigde nikihitaji pointi tatu, nimefanikiwa, sidhani kama mwenzangu Carlo Ancelotti alikuwa mmoja wa wachezaji, nilifuata pointi tu."

"Ninatambua kuwa Ancelotti hakuwa sehemu ya washambuliaji wa Chelsea, bali alikuwa kwenye benchi lao akishuhudia Torres aliyegharimu pauni 50m akicheza kwa dakika 65.

"Tatizo halikuwa jinsi alivyocheza Torres – alijitahidi na kufanya kazi nzuri. Tulifanya mazoezi ya pamoja ya kuikabili Liverpool yenye wachezaji wengi na hiki ni kitu cha kawaida kwetu," alisema Ancelotti.

"Nimeshasahau kila kitu kwani baada ya dakika 60 za harakati nyingi, ilikuwa vyema kwangu kumpumzisha."

Beki mkongwe Jamie Carragher, ambaye alirejea dimbani baada ya miezi miwili akiwa majeruhi alikuwa mtu muhimu kwenye safu ya ulinzi ya Liverpool na kumzima Torres, akieleza pia kuwa kila mmoja alikuwa tayari amemsahau Torres.
"Fernando ni mmoja wa wachezaji muhimu, washambuliaji hatari duniani, nina hakika kwamba akizoea atakuwa msaada mkubwa kwao, Chelsea lakini si kwa sasa," alisema beki huyo wa zamani wa kimtaifa wa England. "Tumebadili mwelekeo wetu na sasa tunatazama mbali zaidi kuliko tulivyocheza na Chelsea."
 
Tunawataka Mazembe, Al Hadood wakati 'sisimizi' wanatutoa jasho
ban.blank.jpg

Kenny Mwaisabula

amka2.gif
KARIBUNI tena wapenzi wasomaji wa safu hii ya ‘Kona ya Mwaisabula', ikujiayo kila siku kama ya leo katika gazeti lako ulipendalo la Tanzania Daima.
Tunakutana tena katika kona hii, baada ya kushuhudia wawakilishi wetu wa michuano mikubwa kabisa barani Afrika, wakimaliza ngwe ya dakika 90 kwa kuambulia sare na sasa kindumbwendumbwe kilichobaki ni kukamilisha dakika nyingine kama hizo, ili kumpata mshindi wa kwenda kuumana na Harass El-Hodood ya Misri na mabingwa wa soka barani Afrika, TP Mazembe ya DRC.
Ilipotangazwa ratiba ya michuano ya ligi ya soka ya klabu barani Afrika mapema Desemba, tayari ule mshawasha wa ligi ukaanza.
Kila timu katika bara hili, ikawa inajipanga kivyake ili mradi tu ifike hapo ilipopakusudia, yaani kuchukua ubingwa au ngazi yoyote ya juu, lakini sio kutolewa mapema.
Kama vile wenzetu waliomo katika sayari hii na sisi tukajipanga kutokana na ratiba ilivyokuwa, bahati mbaya yetu wadau, viongozi, wapenzi na baadhi ya waandishi wa habari, tayari wakawa wamezipitisha Simba na Yanga katika raundi ya awali, kuwa wameishawafunga Elan Club de Mitsoudje ya Comoro na Dedebit ya Ethiopia, bila kufanya tathimini ya kutosha.
Tunatukana mamba na mto bado hatujavuka ni balaa! Leo yametukuta ya kutukuta.
Katika moja ya makala zangu zilizopita, niliwatahadharisha Yanga na Simba wasifikirie mechi za mzunguko wa pili kabla hawajavuka ule wa kwanza, ni kosa kubwa tena la jinai kuwafikiria TP Mazembe na Harass El-Hodood kabla ya kuwatoa Wacomoro na Wahabeshi.
Kwani timu hizo si za kubeza kama tunavyofikiri na kwa kuzingatia wengi wetu tuliwaona Wahabeshi katika michuano ya Kombe la Chalenji Desemba mwaka jana jijini Dar es Salaam.
Wiki iliyopita, tumeshuhudia wawakilishi wetu wote wakitoka sare na ukijumlisha na ndugu zetu Wazanzibar ndio hatari, kwani moja imetoka sare na nyingine imeambulia kichapo, tena cha mbwa mwizi, yaani 4-0.
Ni ukweli, katika soka chochote huweza kutokea, lakini dalili ya mvua mara nyingi huwa ni mawingu na sasa tayari taa ya kijani imewaka kwa wawakilishi wetu kuonyesha dalili zote za kuyaaga mashindano hayo makubwa kabisa barani Afrika.
Wakati CAF ilipotoa ratiba, Simba hawakutilia maanani kuwa kuna kikwazo watapata kutoka kwa Wacomoro na badala yake walielekeza nguvu zote kwa TP Mazembe, lakini matokeo ya wiki iliyopita yamewastua.
Sasa badala ya kuangalia uwezekano wa kuibuka washindi mechi yetu ya marudiano na kufanya tathmini ya mechi iliyopita, tayari kuna mizengwe imeanza, wachezaji na viongozi wameanza kumtolea mimacho kocha wao mkuu, Mzambia Patrick Phiri, kuwa sasa ameanza Uswahili wa kupanga timu kwa mizengwe ingawa mi' siamini.
Lakini kama ni hivyo basi, namshauri Phiri aachane na suala hilo, bado Simba wana nafasi ya kurudisha matumaini yao ya kukutana na wale vigogo wakuu kabisa barani Afrika, TP Mazembe.
Watani wao Yanga, nao baada ya ratiba yao kutoka tu, wakaanza kuiwaza Harass El-Hodood badala ya kuwafikiria Dedebit, jambo ambalo ni hatari kweli kweli, matokeo yake ndio kama tulivyoona, wametoka 4-4 na kuifanya mechi ya marudiano kuwa ngumu mno, kwani sare ya aina yoyote ya pungufu mabao manne imewatoa Yanga katika ndoto zao za kukutana Hodood.
Ni ukweli usipingika, kwa watu tulioshuhudia soka siku ile, wale Dedebit ni wazuri mno kwa kutandaza soka chini, tena la kisasa, walimiliki mpira kwa sehemu kubwa na mabao yote waliyofunga, waliingia hadi ndani ya eneo la hatari na kupasia nyavuni.
Hiyo inadhihirisha jinsi wanavyoweza kuingia katika eneo letu bila hofu, tofauti na mabao tuliyoyafunga sisi, yote yakiwa ni mbali na ya kumshtukiza kipa wao wa pili.
Ni lazima tukiri kuwa, tuna kazi kubwa ya kuvuka ili kuwavaa hao Mafarao, ndio maana nasema sasa soka limefika patamu.
Kwa kuwa soka ni mchezo unaochezwa kiwanjani na kila mtu anauona, kila mtu ni kocha, nami kama hao wengine nitumie kalamu kumshauri kaimu kocha mkuu wa Yanga, Fred Felix ‘Minziro', Dedebit ni wazuri sana wakiwa na mpira na wanatumia muda wote pasi fupi fupi na mfumo wao ni 3-5-2, na upande wao wa kulia ndiko kuzuri mno, wanakotengenezea mabao kuanzia kwa beki wao wa kulia, upande wao wa kushoto ambako wachezaji karibu wote wa upande ule wanatumia miguu ya kushoto, hawafanyi kazi kubwa sana zaidi ya kuutoa mpira katika eneo lao na kuwapelekea wale mafundi wa upande wa kulia.
Wachezaji wa Dedebit, hawana nguvu za kugombea mpira wala kupiga mashuti na mabao yao yote ni lazima wafunge wakiwa ndani ya eneo letu la 18.
Kwa kifupi, mazuri na mabaya yao binafsi ndio niliyoyaona, sasa tatizo lipo katika tiba, kila mtu anaweza kuwa na dawa yake.
Ni kweli mie sitagi yai, lakini yai viza nalijua, ushauri wangu kwa benchi la ufundi linaloongozwa kwa sasa na Fred Felix Minziro maarufu kwa Majeshi au Baba Isaya:
La kwanza, tusiwaruhusu waingie katika eneo letu la hatari mara kwa mara, la pili nguvu yetu ya timu iwe upande wa Mwasika ili kushindana kwa hali na mali na watu wao wa upande huo.

(Ingawa pia unaweza kuweka nguvu upande wa kulia, kule ambako wenyewe ni dhaifu). Hilo la kwenye mabano mie silipendi, kwa sababu huwezi kumfukuza mwizi huku mlango umeacha wazi, la tatu Baba Isaya weka viungo imara watano wenye uwezo, nimefarijika kusikia Athuman Idd Chuji naye karudi kundini.
Ili tutawale lile eneo la kati, kamwe usimtumie Jerryson Tegete kama kiungo, mweke eneo la kumalizia na usimpe majukumu mengi zaidi ya kutupia mpira nyavuni tu, nyuma yake kidogo akiwa huyo Mwape au Mbaga.
La nne, kwa kuwa Wahabeshi hawana nguvu ya kukabana, ni lazima watakuwa hawapendi kukabwa, hivyo tulazimishe kuwakaba kwa asilimia 100 ili wasicheze mpira wao.
Yapo mengi ya kuyasemea ya kiufundi, lakini yote hayo yametukuta kwa kudharau mechi za awali, kutofanya maandalizi ya kutosha na wengine kujikita katika migogoro ya mara kwa mara isiyokwisha na kuiweka timu katika misukosuko isiyokuwa na faida yoyote.
Tunataka tukutane na Mazembe na Hodood wakati hao wadogo wametutoa jasho? inasikitisha mno! Tutaendelea kupangwa awali na CAF mpaka lini?
Tukutane tena wiki ijayo, nikupe taarifa ya timu yenye historia ya pekee Afrika, ndani ya miaka 10 imefundishwa na makocha 10! Naombeni msininyang'anye kalamu ili niandike yote na kwa uzuri. Alamsiki.


h.sep3.gif

Mwandishi wa makala hii ni Mwanafunzi wa Chuo cha Bandari, anasomea Diploma ya Maintenance, pia ni kocha mzoefu nchini anapatikana kwa simu, 0713 243 711 au Email kennymwaisabula@yahoo.com
 
Kupiga wachezaji kudhibitiwe haraka
ban.blank.jpg

Mwandishi wetu

amka2.gif
KITENDO cha baadhi ya wahuni, kuanza kujichukulia sheria mikononi na kuwapiga wachezaji baada ya mechi kumalizika, kimevuka mipaka na kinastahili kidhibitiwe na wahusika wachukuliwe hatua kali na vyombo vya sheria.
Umefika wakati Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), linapaswa kuchomoza makucha yake kama ilivyo kwa vyama au mashirikisho ya soka katika nchi nyingine duniani, zilizoweza kuwadhibiti wahuni katika medani hiyo.
England na Italia ni kati ya mataifa yaliyoendelea kisoka ambayo yalikuwa yakikabiliwa na matukio ya uhuni wa aina hii katika viwanja mbalimbali lakini wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kudhibiti kutokana na kuwabana wahuni walioendesha matukio hayo.
Kile kilichofanywa na wahuni kwenye dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa mechi ya Ligi ya Kombe la Shirikisho (CAF), kati ya Yanga na Dedebit ya Ethiopia na kurudiwa katika mechi ya Yanga na Mtibwa Sugar, hakipaswi kuachwa kiendelee.
Wahuni waliojifanya manazi wa Yanga walimpiga mshambuliaji Nsa Job, baada ya mechi ya Yanga na Dedebit kwa madai ya kucheza chini ya kiwango na kutumiwa kuihujumu timu.
Kama hiyo haitoshi wahuni hao wanaoonekana kufurahia ujinga huo wanaoufanya, walirudia tena tukio kama hilo kwa kumpiga kiungo mkongwe wa Yanga, Godfrey Bonny, na wachezaji wengine baada ya kumalizika mechi ya Yanga na Mtibwa Sugar.
Katika kuonyesha kuwa wahuni hao walikuwa na dhamira mbaya na wachezaji hao hata baada ya kiongozi wao, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Davis Mosha, kujaribu kuwaonya wasiwapige wachezaji walimgeuzia kibao kwa kulipopoa mawe gari lake na kupasua kioo cha nyuma.
Binafsi ninalaani vikali upuuzi wa wahuni hawa na ninaamini kama hatua za haraka hazitachukuliwa basi siku moja watakuja kuwaua wachezaji wasio na hatia yoyote.
Nadhani imefika haja TFF, kwa kushirikiana na vyombo vya usalama na viongozi wa timu kuwasaka wahusika ambao ninaamini wanajulikana na wanaweza kupatikana iwapo watasakwa.
Nasema hivyo kwa kuwa wahuni hao wanaishi katika maeneo ambayo wanachama, wapenzi na mashabiki wengine wa soka wanatokea, hivyo watakuwa wanajulikana aidha kwa sura kama sio majina.
Ninaamini kuwa, wahuni hawa hawana nia ya kuwapiga wachezaji tu bali wana nia nyingine kabisa na hii inachukuliwa kama kisingizio tu cha kutaka kufanikisha uhuni wao huo.
Laiti kama wahuni hawa wangekuwa wanachama wa kweli, wapenzi au mashabiki wa soka, wasingethubutu kuwatukana wachezaji wao achilia mbali kuwapiga baada ya mechi, bali wangeomba kukutana na viongozi wa klabu kujadili jinsi ya kuepuka matokeo wasiyoyataka.
Kwa hili TFF haipaswi kuendelea kusubiri bali inapaswa kuchukua hatua za haraka na za makusudi, ambazo zitalenga kuwapa fundisho sio wahuni hawa tu bali hata kwa wahuni ambao wangejitokeza katika kizazi kijacho.
Watu hawa ni hatari na hawapaswi kuachwa waendelee kuwepo katika jamii ya wanasoka, jamii ambayo duniani kote huonekana ni ya watu wastaarabu wenye kupendana na kuheshimiana wasio na chembe ya ubaguzi wa rangi, dini wala kabila.
Iwapo TFF haitawakomesha wahuni waliojitokeza katika siku za hivi karibuni jijini Dar es Salaam, basi wataweza kueneza tabia hii katika viwanja mbali mbali vya soka hapa nchini, hivyo kuondoa hadhi ya mchezo husika.
Wachezaji watashindwa kucheza kwa kufikiria dhahama watakayokutana nayo baada ya kumalizika kwa mechi, huku pia baadhi ya wapenzi na mashabiki wema wa soka nao wakiogopa kwenda viwanjani kwa kuhofia usalama wao na mali zao baada ya mechi.
Aidha nao viongozi wa klabu zote za Ligi Kuu na zile zisizoshiriki ligi yoyote wanapaswa kuanzisha utaratibu maalumu wa kuwajua na kuwadhibiti wanachama wao, jambo litakalowafanya wawadhibiti kirahisi wahuni wanaotaka kujipenyeza na kutumia migongo ya klabu kufanya uhalifu.
Bila ya kufanya hivyo siku moja tutashuhudia klabu zikikutana na adhabu kubwa kutoka CAF na FIFA kwa sababu ya wahuni hawa ambao huenda wasiwe hata wanachama au mashabiki wa klabu husika.



 
Ni mitihani Simba, Yanga CAF
ban.blank.jpg

Mwandishi wetu

amka2.gif
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya kimataifa barani Afrika, Simba na Yanga, zinakabiliwa na mechi za marudiano za hatua ya awali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Hizi ni mechi zitakazopigwa kati ya Februari 12 hadi 14, ambapo Yanga itakuwa mjini Addis Ababa Ethiopia kukabiliana na Dedebit.
Wakati Yanga wakiwa ugenini, Simba watakuwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, kuwakabili Elan Club ya mjini Mitsoudje, Comoro.
Yanga chini ya kocha wake mpya, Mganda Sam Time, itakwenda Ethiopia ikiwa na deni la kushinda mechi hiyo kama inataka kusonga mbele.
Hiyo inatokana na kulazimishwa sare ya mabao 4-4 katika mechi ya nyumbani iliyochezwa Januari 29, ambapo Yanga ilishindwa kuutumia vizuri uwenyeji.
Kama Yanga inataka kuwang'oa Dedebit ambao ni mara ya kwanza kwao kucheza michuano ya kimataifa na msimu wa pili tangu wapande Ligi Kuu, wanapaswa kujipanga vizuri.
Hiyo inatokana na ugumu wa mechi hiyo kwani kupitia mechi ya kwanza, Dedebit chini ya kocha wake, Gebremedhin Haile, aliyepewa mikoba ya timu hiyo tangu Januari 14, itakuwa imewajenga.
Mbali ya kuwajenga kwa maana ya kuondokewa na wingu la hofu ya mechi za kimataifa, kwenye mechi ijayo watakuwa wakicheza mbele ya mashabiki wao.
Kama Dedebit na ugeni wao Tanzania na michuano ya kimataifa kwa ujumla bado walicheza kwa kiwango kile, itakuwa vipi wakiwa nyumbani?
Kwa kuonyesha kiwango bora katika mechi hiyo ya kwanza dhidi ya Yanga, uongozi wa Dedebit uliwazawadia kila mchezaji kiasi cha birr 5,000 (fedha za Ethiopia), kama pongezi kwa kazi nzuri.
Unaweza kuona ni kama kiasi kidogo cha fedha, lakini kina maana kubwa katika kuwajenga kisaikolojia wachezaji kuelekea mechi ya marudiano.
Kiasi hicho ambacho ni nusu ya fedha iliyokuwa imeahidiwa na uongozi wao kama wangeshinda mechi hiyo ya kwanza, ni sawa na dola 300 za Marekani, karibu sh 400,000 za Tanzania.
Hivi kwa mazingira hayo, unatarajia nini kutoka kwa Getaneh Kebede, Berhanu Bogale, Dawit Fekadu na Tadele Mengesha ambao walikuwa mwiba hadi kufunga katika mechi ya kwanza?
Kikosi kamili cha Dedebit ambacho kilicheza mechi ya kwanza, ni kipa Biniam Habtamu.
Mabeki: Mengistu Assefa, Adamu Mohamud, Daniel Gebre-Michael, and Mesfin Wondimu/Tadele Zerihun.
Viungo: Ephrem Zeru/Mulugetta Mehret, Shehabe Jibril, Behailu Assefa na Berhanu Bogale
Washambuliaji: Getaneh Kebede/Temesgen Tekle na Dawit Fekadu.
Aidha, kwa umuhimu wa mechi ya marudiano, Dedebit iliahirishiwa mechi yake ya Ligi Kuu dhidi ya Ethiopian Coffee kwa kuepuka majeruhi.
Mbali ya Dedebit, pia timu ya St. George inayoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa nayo iliweka kiporo mechi yake dhidi ya Hawassa City.
Wakati Dedebit wakikusanya nguvu kuwasubiri Yanga mjini Addis Ababa, St. George wao watawakaribisha Recreativo da Caála ya Angola.
Aidha, wakati Dedebid wakiwa na kazi ya kusaka ushindi wowote ili kusonga mbele
kuwakabili Haras El Hadoud ya Misri, St. George wapo nyuma kwa mabao 2-0.

Wakati Dedebit wakiwa nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu kwa kujikusanyia pointi 18 katika mechi 10, Yanga ya pili.
Yanga itakabiliana na Dedebit wakitoka kucheza mechi mbili tangu walipocheza na Dedebit, wakichapwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar kabla ya kutoka sare ya bila kufungana na Majimamaji ya Songea.
Kwa upande wa benchi la ufundi, wakati Kocha wa Dedebit akikabiliana na wachezaji aliowaona katika mechi ya kwanza, kwa upande wa Timbe itakuwa mara ya kwanza.
Timbe kwa kiasi kikubwa itabidi apate maelekezo kutoka kwa msaidizi wake, Fred Felix Minziro, aliyekuwepo Yanga tangu mechi ya kwanza dhidi ya Waethiopia hao.
Kitu muhimu kwa benchi la ufundi la Yanga, ni kufanyia kazi dosari zote zilizojitokeza katika mechi ya kwanza kiasi cha kutoa nafasi kwa Dedebit kupata mabao manne.
Licha ya Dedebit kuwa nyumbani, kama Yanga watajipanga vizuri, wanaweza kuvuna ushindi katika uwanja wa ugenini kwa sababu katika soka hakuna kisichowezekana.
Ukija kwa Simba ambao wao walianza kwa sare ya bila kufungana mjini Mitsoudje, wao watakuwa na kazi kupambana kushinda kitu ambacho kinawezekana
hasa ikizingatiwa watakuwa nyumbani.

Hata hivyo, Kocha Mkuu wa Simba, Mzambia Patrick Phiri, anapaswa kuwajenga vizuri vijana wake kukabiliana na ugumu ambao haukutarajiwa katika mechi ya kwanza.
Wakati mshindi kati ya Yanga na Dedebit akikwaana na Haras El Hadoud ya Misri, mshindi kati ya Simba na Elan Club, atakutana na mabingwa ma
 
Sioni mantiki waimbaji Injili kushindania tuzo
ban.mtazamo.jpg

Abdallah Menssah

amka2.gif
KIPAJI au kipawa chochote, hata kile cha uimbaji wa nyimbo za Injili ni tunu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Lakini, hata kwa mtu anayejiona hawezi kuimba vizuri kama mwingine, bado anaweza kufanya hivyo kwa kiwango chake na bado Mungu akamsikia na kubariki.
Kwa sababu Mungu ndiye mwenye kugawa hivyo vipawa na karama mbalimbali, hakuna wa kuhoji kwa nini huyu anamzidi yule au vipi yule hajui kuimba.
Imeandikwa, kama mwanadamu asipoinuka kumsifu na kumtukuza Mungu kwa nyimbo, yeye anao uwezo wa kuyainua mawe yakafanya hivyo.
Kwa mtazamo wangu, kitu kikubwa ambacho tunapaswa kujifunza hapa ni kwamba mbele ya Mungu, hakuna mjuvi na asiyejua kuimba vizuri, maadamu wote wanamwimbia yeye.
Katika hili, kunaweza kuwa na waimbaji kwa mfano 10 unaoweza kuwaweka kwenye kundi bora, lakini bado si rahisi wakalingana.
Hii inatokana na ukweli kuwa kila mtu ana namna alivyojaaliwa na Mungu kwa mfano uimbaji wa huyu ukawa tofauti na yule.
Ukija kwenye muziki wa kidunia, kwa mfano bongo fleva, dansi, mchiriku, taarabu ni rahisi kuwashindanisha jukwaani na kupata mshindi na mshindwa miongoni mwao.
Mshindi au mshindwa katika muziki wa aina hiyo, anaweza kupatikana kwa mujibu wa vigezo vilivyopo kama mpangilio wa sauti, ala, ujumbe, umahiri wa kutawala jukwaa
na kadhalika, lakini kwa nyimbo za Injili, binafsi ninapata taabu wa kumpa tuzo.

Ukakasi wa ushindani miongoni mwa waimbaji wa muziki wa injili unatokana na ukweli kwamba, kitu muhimu kwa Mungu, si sauti wala midundo ya ngoma, bali usafi wa moyo.
Ndio maana hata uimbaji wenyewe wa muziki wa Injili, huwa wenye maana kama utaendana na matendo yao, kwa sababu imani bila matendo imekufa.
Jiulize, hao waimbaji wa Injili wanaoshindanishwa jukwaani, wanamshindania nani, Mungu au fedha, kwa sababu Mungu kamwe hashindaniwi.
Utukufu wa Mungu haushindaniwi kwa vigezo vya ubora wa sauti nzuri jukwaani, kusali sana, bali kwa usafi roho ambao husadifiwa na matendo.
Nimeamua kuliweka wazi hili kwa maslahi ya huduma ya muziki wa Injili, kwa sababu kitendo cha kuwashindanisha waimbaji au kwaya na kutoa tuzo, kinaweza kuleta mgawanyiko na mitafaruku kwao na hata katika madhehebu husika.
Katika hali ya kawaida, ushindani una mambo yake, hivyo matokeo ya ushindani wao, unaweza kuwa mwanzo wa kuibua misigano na matabaka miongoni mwao.
Nayasema haya kutokana na uzoefu wa mazingira ya ushindani ambapo kumekuwa kukizua malalamiko mengi yakiwemo huyu amependelewa na yule ameonewa.
Hivyo, ukija kwenye muziki wa Injili, sidhani kitu kama hicho kitakuwa na tija kwa maendeleo ya huduma hiyo ya uimbaji ambayo kwa mtazamo wangu, imezidi kukua kila siku.
Sina haja ya kumnyooshea kidole mtu wala kampuni fulani, kwa sababu pia haina tija kwangu, bali ni kuangalia faida na hasara za waimbaji wa Injili kushindanishwa katika kuwania tuzo za kidunia.
Tumesikia habari za kuwepo kwa tamasha lenye nia ya kupongeza na kufanya tathmini ya jumla kwa wasanii binafsi wa muziki wa Injili na kwaya mbalimbali ambapo kutakuwa na tuzo kadha wa kadha kwa waimbaji wataoonekana wamefanya vizuri kwenye mwaka uliotangulia.
Binafsi napata ugumu kuafiki kitu kama hiki kwa waimbaji wa muziki wa injili kwa maana kuwa ushindani wao katika kuwania tuzo unaweza kuwa wenye athari nyingi kuliko
faida.

Unaweza kuzua manung'uniko, hivyo kuzaa matabaka miongoni mwao, kitu ambacho ni hatari kwa mustakabali wa huduma ya uimbaji ambayo bado inahitajika na tungependa izidi kukua.
Narejea tena, Mungu hashindaniwi kwa misingi ya umahiri wa kuimba na kucheza jukwaani au kupiga vyombo bali kwa usafi wa kweli wa roho.
Pili majaji wa kupima vigezo vya Mungu anavyohitaji katika kumtumikia watatoka wapi?
Wako waandaaji wa tuzo ambao walijaribu kuingiza muziki wa Injili na Kaswida ili kuzitolea tuzo, lakini kilichojiri wafuatiliaji wanayajua na mwisho wake zoezi hilo lilikufa kwa aibu hadi leo hii.
Kwa mtazamo wangu, sioni tija yoyote waimbaji wa Injili kushindania tuzo jukwaani kwa sababu inaweza kuzua mengi yanayoweza kuharibu huduma yenyewe.
Wito wangu kwa wahusika ni kwamba naamini lengo lao si baya, lakini wakae chini na kutumia
namna bora ya kufikia lengo bila kuharibu huduma yenyewe.



h.sep3.gif

Kwa maoni na ushauri; simu namba 0718 102050, au baruapepe abmenssah@yahoo.com
 
Waimbaji Kenya, Rwanda wathibitisha Tamasha la Pasaka


na Dennis Fussi


amka2.gif
WAJUMBE wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Msama Promotions, wanakwenda nchini Afrika Kusini kukutana na waimbaji wa muziki wa Injili watakaokuja kutumbuiza tamasha hilo la kimataifa.
Waimbaji hao watakaoteuliwa, wanakuja nchini kwa ajili ya kutumbuiza kwenye tamasha hilo la kumsifu na kumtukuza Mungu litakalofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka Aprili 24 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti Kamati ya Msama Promotions, Alex Msama, lengo la kwenda Afrika Kusini ni kuangalia waimbaji wa muziki wa Injili wenye majina makubwa ambao watakuwa na sifa ya kutumbuiza katika tamasha hilo.
Msama alisema waimbaji nane wa muziki wa Injili kutoka Kenya na wengine saba wa Rwanda wamethibitisha kushiriki.
Aidha, Msama alisema kutafanyika mchujo kwa waimbaji 15 wa Rwanda na Kenya ili kuwapata wawili wakali watakaotumbuiza katika tamasha la Pasaka.
Msama alisisitiza kwamba tamasha la mwaka huu litakuwa na utofauti mkubwa ikilinganishwa na matamasha mengine yaliyopita, kwani limeboreshwa zaidi.
Msama alisema tamasha la mwaka huu limekuwa na maboresha makubwa kwa ajili ya kukidhi matakwa ya wapendwa wengi.
Msama alisema baada ya tamasha hilo pia matamasha mengine yatafanyika katika mikoa ya Shinyanga Jumatatu ya Pasaka Aprili 25 na Mwanza Aprili 26 ambayo itakuwa ni sikukuu ya Muungano.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom