Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Top C kuzindua Bilicanas Valentine's Day


na Dina Ismail


amka2.gif
WASANII mbalimbali wa muziki wa bongo fleva wanatarajiwa kusindikiza uzinduzi wa albamu ya msanii mwenzao anayekwenda kwa jina la Top C inayojulikana kama ‘Lofa'.
Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Club Bilicanas katika Sikukuu ya Wapendanao ‘Valentines Day.
Msanii huyo anayetoka katika kundi la Masharobaro linaloongozwa na Mr. Chocolate msanii na mtayarishaji wa Sharobaro Records.
Wasanii wanaotarajiwa kupamba uzinduzi huo ni pamoja na Mr.Chocolate, H-Baba, Diamond, Sam wa Ukweli na Q-Chillah.
 
Sabodo: Niko tayari kuzisaidia Simba, Yanga


na Dina Ismail


amka2.gif
PAMOJA na kukiri kuwa ni Jangwani dam dam, mfanyabiashara maarufu nchini Mustafa Sabodo amesema yuko tayari kuzisaidia klabu za Simba na Yanga iwapo zitahitaji msaada wake.
Sabodo aliyasema hayo nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam jana, wakati wanafunzi wa shule ya Tanzania Sports Catalyst (TASCA), iliyopo Kigamboni, jijini Dar es Salaam walipokwenda kumzawadia kutokana na mchango wake kwa shule hiyo.
Alisema, amekuwa akiyasikia matatizo mbalimbali yanayozikabili timu hizo kubwa na zenye mashabiki lukuki nchini, lakini hakuna kiongozi wa timu yoyote kati ya hizo aliyefika kwake kuomba msaada.
“Nimekuwa nikisikia tu matatizo ya Simba na Yanga na hata hiyo migogoro yao, lakini siwezi kuingilia kwa namna yoyote kwa kuwa hakuna kiongozi yeyote wa timu hizo aliyekuja kwangu,” alisema Sabodo.
Sabodo aliongeza kuwa yeye yuko katika kuisadia jamii yote ya Tanzania bila kubagua imani ya mtu, itikadi, kabila, rangi, hivyo hata Simba na Yanga zinakaribishwa kuwasilisha matatizo yao kama watapenda.
Katika hatua nyingine, wanafunzi wa TASCA walimzawadia Sabodo picha maalum kama shukrani ya mchango wake katika shule hiyo inayolea watoto yatima wenye vipaji vya michezo.
Akisoma risala maalum, mmoja ya wanafunzi alisema: “Tunakushukuru kwa moyo wako wa upendo uliojaa utu na kuipenda nchi yako ya Tanzania kwa kuona kwamba elimu na mahitaji ya jamii maskini za Kitanzania zinanufaika na maisha bora.”
Naye Sabodo ambaye aliahidi kuwajengea ukuta, bweni moja na kuwachimbia visima, aliwashukuru watoto hao na kuahidi kuendelea kuisaidia shule hiyo kadiri ya uwezo wake hivyo ni kuomba uzima na afya njema.
 
Sudan yaanza vema CHAN


na Mwandishi wetu, KHARTOUM, Sudan


amka2.gif
WENYEJI Sudan juzi waliaza vema michuano ya kuwania ubingwa wa Afrika 2011, kwa wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN), baada ya kuwachapa Gabon kwa bao 1-0, ikiwa ni michuano ya pili tangu kuanzishwa.
Alikuwa ni Mudather Eltaib aliyewafungia wenyeji bao hilo pekee katika kipindi cha kwanza, likiwapa wenyeji pointi tatu na matumaini ya kufika mbali kutoka kundi lao.
Katika mechi ya pili Algeria nayo ilianza vizuri kampeni hizo baada ya kuilaza Uganda kwa mabao 2-0, bao la kwanza la Algeria lilipachikwa wavuni na Abdelmounem Djabou katika dakika ya 17, ikiwa ni mechi ya kwanza ya kundi A iliyopigwa mjini Khartoum.
Bao la pili la Algeria liliwekwa wavuni na Hilal Soudani, katika dakika ya 78.
Washindi wa pili katika mashindano ya mwaka 2009 Ghana, pia wanaanza kampeni ya mashindano hayo katika kundi B siku ya Jumamosi, wanapokumbana na Afrika Kusini, huku Niger wakipepetana na Zimbabwe.
Haya ni mashindano ya kwanza kuandaliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika- Caf kufanyika nchini Sudan tangu mwaka 1970, walipoutumia vizuri uwanja wa nyumbani na kutwaa Kombe la Mataifa huru ya Afrika.
 
Palestina waifagilia Taifa Stars


na Makuburi Ally


amka2.gif
TIMU ya Taifa ya Palestina jana iliwasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Taifa Stars unaotarajiwa kuchezwa keshokutwa kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana, kocha mkuu wa Palestina, Mousa Bezaz, alisema, mchezo huo utasaidia timu yake kujiweka vizuri katika mpangilio wa soka.
Bezaz alisema, timu yake ina wachezaji sita wa kulipwa wanaocheza nchini Ujerumani, Misri, Jordan, Algeria na Poland ambako kati ya hao wanne ndio wameambatana na timu hiyo.
Bezaz alisema, awali waliwahi kuishuhudia Tanzania kupitia televisheni na CD katika michezo yake mbalimbali iliyowahi kucheza, hivyo wakavutiwa nayo hadi kufikia hatua ya kuiomba kucheza nayo mchezo wa kirafiki.
Aidha Bezaz alisema, sababu za Palestina kuwa katika kiwango cha chini katika viwango vya Shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA), ni kutoshiriki michezo ya kimataifa ya kirafiki na mashindano mengine ya kimataifa.
Naye Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga, alisema Tanzania na Palestina ni nchi ambazo zina historia bora ya maendeleo ya jamii ingawa katika soka ni mara ya kwanza kucheza pamoja.



h.sep3.gif

 
Coastal yawashukuru wadau


na Neema Kishebuka


amka2.gif
TIMU ya Coastal Union ya jijini hapa imeshukuru jitihada zinazoendelea kufanywa na viongozi wa mkoa wa Tanga katika kuisaidia timu hiyo iendelee kufanya vema katika Ligi Daraja la Kwanza hatua ya tisa bora inayoendelea katika Uwanja wa Mkwawani. Kwa sasa Coastal Union ndio inayoongoza katika msimamo wa ligi hiyo kwa kuwa na pointi 7 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Morani iliyochezwa mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Mkwawani.
Akizungumza na Tanzania Daima, Ofisa Habari wa Coastal Union, Benedict Kaguo alisema juhudi hizo za viongozi wa mkoa wa Tanga zimesaidia kuwapa hamasa wachezaji wa timu hiyo na kufanikiwa kuendelea kuongoza katika msimamo wa ligi hiyo.
Kaguo alisema juhudi hizo zinaongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Meja Jenerali Mstaafu, Saidi Kalembo, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Steven "Ngonyani Profesa Maji Marefu", Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, ambao wamekuwa bega kwa bega kuisaidia timu hiyo.
Alisema juhudi za viongozi hao zinapaswa kuungwa mkono na wananchi wote wa Tanga katika jitihada za kuendelea kuisaidia timu hiyo ili izidi kung'ara katika mashindano hayo.
Katika hatua nyingine, kocha mkuu wa Morani FC Musa Rashidi ametuma salamu za kujiweka mkao wa kupokea kipigo kwa timu ya Rhino Rangers ya Tabora katika mchezo unaotarajiwa kupigwa kesho katika uwanja wa CCM Mkwakwani.
Kocha huyo alituma salamu hizo mapema jana wakati alipokuwa akizungumza na Tanzania Daima kuhusu mandalizi ya mchezo wao huo.
Alisema kuwa licha ya kupoteza michezo kadhaa iliyopita katika ligi hiyo kuwa ni kawaida yao kufanya hivyo ili kuweza kuangalia uelekeo wa upepo upo vipi katika ligi.
Akijitapa kuhusu mchezo uliopigwa juzi dhidi ya Coatal Union ambapo walitoka sare ya kufungana bao moja kwa moja, kocha huyo alisema walitumia udhaifu wa Coastal kwani walikuwa wanajiamini kupita kawaida.
Morani Fc iliyocheza jumla ya michezo mitatu imepoteza miwili na imedroo moja.
 
Simba yaishusha kileleni Yanga
• Yawapigisha kwata Polisi Tanzania 2-0

na Happiness Mtweve


amka2.gif
WEKUNDU wa Msimbazi Simba ya jijini Dar es Salaam jana waliwaengua kileleni mwa Ligi Kuu bara mahasimu wao Yanga baada ya kuwapigisha kwata maafande wa Polisi Tanzania kwa kuwalaza mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Katika mechi hiyo iliyoanza kwa timu zote kukamiana, ili kuhakikisha kila moja inaibuka na ushindi na kujitwalia pointi tatu muhimu hasa Simba ambao walikuwa wakitaka kulipa kisasi cha kupoteza mechi ya awali kwenye Uwanja wa CCM Kirumba ambapo ilikubali bao 1-0. Lakini hadi dakika 45 zinamalizika nyavu za pande zote zilikuwa hazijatikisika.
Kipindi cha pili, Simba ilianza kwa kasi na dakika ya 53 Musa Hassan Mgosi alipachika bao la kwanza kwa mpira wa adhabu, baada ya Haruna Shamte kufanyiwa madhambi, kabla ya dakika ya 63 Juma Semsua wa Polisi kulambwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Mgosi.
Pengo hilo liliwagharimu maafande hao na kujikutwa wakilishindwa ligwaride na kulegeza hivyo kupachikwa la pili dakika ya 84 na Mgosi tena kwa kichwa akimalizia vema kazi nzuri ya Shamte. Hadi filimbi ya mwisho Simba 2, Polisi 0.
Kwa ushindi huo Simba imejikita kileleni ikiwa na pointi 33 baada ya kushuka dimbani mara 14 na kuishusha Yanga yenye pointi 32 ikiwa imecheza mechi 15 ambao walikuwa wamepumzika kwenye uongozi kwa muda.
Akizungumzia mechi hiyo, Kocha wa Simba Patrick Phiri alisema ushindi huo unampa matumaini ya kufanya vema katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Elan, huku msaidizi wake Amri Said alikiwamwagia sifa lukuki wachezaji wake na kutamba kuwa kuanzia sasa kila baada ya mechi tatu watakuwa wakitoa taarifa kuelekea kutwaa taji.
Kocha Polisi, John Simkoko, alisema mpira ulikuwa ‘fair' na kwamba wameshindwa kutokana na makosa, pia kadi nyekundu iliwamaliza hivyo kuwataka wapenzi wa timu hiyo wasife moyo waendelee kuisaidia timu yao.
Simba iliwakilishwa na Juma Kaseja, Haruna Shamte, Amir Maftah, Juma Nyosso, Kelvin Yondan, Jerry Santo, Nico Nyagawa, Patrick Ochan, Mussa Mgosi, Mbwana Samatta, Amri Kiemba/ Mohammed Banka.
Polisi: Said Kombo, Nahodha Haji, Noel Msawa, Elias Mafutaa, Salmin Kissi, Ismail Nkulo, Sihaba Mkude, Khalid Ally, Juma Semsua, Seif Muhando na Delta Thomas.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom