Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #5,401
Wataka sanaa iingizwe katika mtaala
Tuesday, 08 February 2011 19:54
Vicky Kimaro
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imeshauriwa kuliingiza somo la sanaa kwenye mitaala ya elimu kutoka ngazi ya awali ili kujenga vipaji vya vijana katika tasnia hiyo ili hatimaye waweze kujiajiri.
Maombi hayo yalitolewa jana na wadau wa sanaa wakati wakichangia mada kwenye Jukwaa la Sanaa linaloandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata ).
Mada hiyo ilihusu Mchango wa Majeshi Katika Kukuza Ajira za Sanaa nchini iliyowasilishwa na Mkufunzi wa Bendi ya Polisi, Damas Mpepo.
Katika semina hiyo wadau wengi walikunwa na jinsi majeshi nchini yanavyoenzi sanaa na kuwa mstari wa mbele kuiimarisha tasnia hiyo.
"Majeshi yetu yamekuwa yakifanya vizuri katika tasnia ya sanaa kwa kuwa kuna elimu wanayoipata katika tasnia hii, ni lazima Wizara ya Elimu iamke sasa na itambue kwamba tasnia ya sanaa ni kimbilio la vijana wengi kwa sasa hivyo lazima uwekwe utaratibu wa kujenga vipaji vya sanaa toka ngazi ya awali ili kukuza tasnia hii inayoajiri vijana wengi kwa sasa," alisema Mpepo
Mpepo aliweka wazi kwamba, wizara haina jinsi kwa sasa zaidi ya kuliingiza somo la sanaa kwenye mitaala ya elimu badala ya ilivyo sasa ambapo limekuwa halitahiniwi na vijana wengi katika shule nchini wamekuwa wanalikuta mitaani baada ya kumaliza shule.
"Sanaa inaajiri watu wengi sana, hata Jeshi la Polisi limeajiri wasanii karibu 500, tatizo lililopo sasa ni kwamba somo la sanaa halifundishwi na hivyo ujuzi katika tasnia hii ni tatizo.
Wizara ya Elimu lazima sasa ione haja ya kuliingiza somo la sanaa kwenye mitaala ya elimu toka ngazi ya awali na litahiniwe kwenye mitihani ya shule na taifa" alisisitiza Mpepo.
Kwa upande wake, Mratibu wa Jukwaa la Sanaa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mfuko na Uwezeshaji Basata, Ruyembe Mulimba alisema kwamba, hoja ya somo la sanaa kufundishwa toka ngazi ya awali ya elimu ilichukua muda mwingi kwenye kikao cha nane cha sekta ya Utamaduni kilichomalizika hivi karibuni jijini Mwanza.
Alisema wadau walitoka na azimio la kushawishi somo hili kuanza kufundishwa na kutahiniwa kama masomo mengine.
"Kaulimbiu ya kikao cha nane cha sekta ya utamaduni ilikuwa ni Sanaa ni Ajira Tuithamini, lakini wadau wengi walisikitishwa na somo la sanaa kutokufundishwa toka ngazi ya awali na walitaka serikali kusikia kilio hicho kwani tasnia hii kwa sasa inaajiri vijana wengi sana wanaokadiriwa kufika milioni sita.
Jeshi la Polisi kupitia bendi yake limetoa taratibu za kuajiri wasanii na sifa zinazohitajika ambapo jumla ya wadau 157 waliohudhuria walipata wasaa wa kuelimishwa kazi mbalimbali za Bendi ya Polisi.

PRINT