Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #5,741
Mashabiki Corinthias wamtisha Roberto Carlos
Friday, 11 February 2011 20:33
SAO PAULO, Brazil
BEKI mkongwe Roberto Carlos anaweza kuiacha klabu yake ya Corinthians ya Brazil kwa sababu mashabiki wa timu hiyo wamekuwa wakiitishia familia yake.
Carlos ameuambia mtandao wa Lancenet kwamba hata yeye amekuwa akipokea ujumbe mfupi wa vitisho katika simu yake, pia watu asiowafahamu wamekuwa wakimfuatilia mitaani tangu klabu yao (Corinthians_ ilipotolewa katika michuano ya Copa Libertadores wiki iliyopita.
Carlos ambaye ni beki nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil, Selecao na klabu ya Real Madrid alisema,"Naona mambo yananishinda hapa Brazil, bado kuna mambo nayatafakari."
Beki huyo mwenye umri wa miaka 37, anayeweza kurudi barani Ulaya na kucheza soka.
"Nimekuwa nikitishwa kila mara kwenye simu na familia yangu imekuwa ikitishwa, pia zipo pikipiki huwa zinanifuata nikiwa na gari langu mitaaani,"alisema.
Baada ya Corinthians kufungwa mabao 2-0 na Deportes Tolima ya Colombia wiki iliyopita, mashabiki wa Corinthians walilitumia mawe basi lililokuwa limebeba wachezaji wa Corinthians, waliharibu magari ya wachezaji na kuchorachora kwa rangi kuta za ofisi za makao makuu ya klabu ya Corinthians kwa kuandika maneno amabayo siyo mazuri kwa beki huyo na mshambuliaji mkongwe, Ronaldo de Lima.
Zipo taarifa kutoka shirika moja la Habari la Estado kwamba klabu ya Los Angeles Galaxy inaweza ikamsajili Carlos kwa sababu mchezaji huyo alikuwa ni rafiki mkubwa wa David Beckham waliyekuwa wakicheza wote Real Madrid.
Pia, Beckham amekuwa nyota mkubwa wakati akiichezea Galaxy, hivyo anaweza kumshawishi Carlos kusaini kuchezea klabu hiyo.
Carlos alisema hivi sasa anamsubiri wakala wake, Fabiano Farah ili kuweza kufanya mazungumzo na kufahamu hatma yake katika klabu ya Corinthians.
Uongozi wa klabu hiyo ukizungumzia suala hilo umesema haujapata taarifa yoyote kama ipo klabu inataka kumsajili, lakini mkurugenzi wa timu hiyo alisema yeye hajapata taarifa kutoka klabu yoyote inayomtaka.
Alieleza kuwa Carlos alilalamika kwao kuhusu usalama wake na ana mpango wa kuihama klabu hiyo .
Kwa upande wa Ronaldo ambaye amekuwa mchezaji bora wa dunia, pia alikuwa maarufu kabla hajaanza mashindano ya Copa Libertadores alisema,"Nilikuwa nikifikiria kustaafu kucheza soka lakini kwa sababu ya hizi vurugu zilizotokea kwenye timu yetu siwezi kustaafu ili niwape wafanya vurugu nafasi ya kutamba."
Ronaldo ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa alikuwa amepanga kustaafu soka mwaka huu.
Corinthians imekuwa ikiandamwa na mashabiki wake tokea mwaka jana baada ya kushindwa kutwaa taji lolote, huku kombe la Copa Libertadores likiwa ndilo kombe kubwa ambalo hawajawahi kulitwaa.