Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Simba bajeti Shs1.5 bil, usajili 375m Send to a friend Monday, 02 May 2011 20:06

ragesimba.jpg
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage

Clara Alphonce
UONGOZI wa klabu ya Simba unaandaa bajeti ya shilingi 1.5 bilioni huku ikipanga kutumia sh.375 milioni kwa usajili msimu ujao, huku wakitoa saa 48 kwa wapangaji wao kusaini mkataba mpya.

Akizungumza na wanahabari jijini jana, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema kuwa kwa sasa wanataka klabu hiyo ijiendeshe yenyewe na majengo hayo ya mchango mkubwa katika kufikia bajeti hiyo ya mwaka na kufanikisha wa usajili wa wachezaji wapya ambao bajeti yake ni sh.375m.

Alisema kutokana na matatizo yalitokea mwanzoni ya kutoheshimu mkataba wa majengo yao uliofanywa na uongozi uliopita kwa kuchukua fedha kinyume na utaratibu. Simba imeshatoa saa 48 kuondoka kwa wapangaji hao.

''Nataka klabu ya Simba ijiendeshe yenyewe iweze kusajili wachezaji kwa fedha zao wenyewe siwezi kukubali kuona mali za Simba zinateketea kinyuma na utaratibu huo kama kuna mpangaji yoyote ataamua kuingia mkataba na uongozi wangu basi ndani ya saa 48 awe amefanya hivyo na wamepanga kwenda mahakamani ili waweze kupewa oda ya kuwatoa wapangaji hao,'' alisema Rage.

Rage alisema fedha hizo zinatosha kusajili wachezaji wazuri na wenye uwezo wa kuipa mafanikio Simba.

Juu ya uchaguzi mkuu wa klabu hiyo ambao utafanyika Mei 15, alisema kuwa mwanachama yeyote ambaye hajalipia kadi yake ya uanachama mpaka siku ya mkutano huo hataruhusiwa kuingia kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay.

Alisema wanachama wote wanatakiwa kulipia kadi zao katika benki ya CRDB na risiti wanatakiwa kuipeleka klabu kwa ajili ya kupata kadi ambayo ndiyo kibali cha kuingia katika mkutano huo, kwani hadi sasa wanachama waliolipia ni 45 tu na wanatakiwa kulipia 12,000 ya kadi na 20,000 ya uwanja kama walivyokubaliana katika mkutano uliopita.

Rage alisema katika mkutano huo, wakaguzi wa hesabu za Simba watakuwepo kwa ajili ya kutoa ripoti yao na wao kama uongozi utawasilisha bajeti yao ya mwaka kwa wanachama wao ambayo ni Sh 1.5 bilioni na wanachama na wao ndio wataamua kama inafaa au la.

Mwenyekiti huyo alizungumzia pia ujio wa mabingwa wa Kombe la Ligi Birmingham kwa ajili mechi mbili za kirafiki dhidi ya Simba na Yanga hapo Julai 7 na 12.

Alisema kuwa viongozi wawili wa timu hiyo ambao ni kocha msaidizi Andy Watson na daktari Johnlan MC Guinness watawasili nchini Mei 9 kwa ajili ya kukagua hoteli ya Kempinski na uwanja.

"Timu hiyo ikiwa na kikosi kipya walichokisaji pamoja na mashabiki wao 1,000 watatua nchini Julai 5 na kucheza dhidi ya Simba hapo Julai 7 na siku tano baadaye watacheza na Yanga.

Wakati huo huo, Rage ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini, alisema wameingia mkataba wa miaka miwili na kocha Moses Basena, lakini atakuwa chini ya uangalizi wa miezi sita.

"Basena ametia saini na amerudi Uganda, atarejea nchini Mei 9, na timu itaingia kambini siku moja baadaye kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Kagame itakayoanza kutimua vumbi Juni 21 nchini Sudan.

Rage pia, aliwataka wachezaji wao waliowasimamisha Kelvin Yondan na Mussa Hassan Mgosi kujieleza kwa maandishi kuwa wamekwisha tuma barua ya kuomba msamaha, lakini kamati bado hawajazipitia.
 
Real yajipanga kuimaliza Barca leo Send to a friend Monday, 02 May 2011 20:02

MADRID, Hispania
LICHA ya kukabiliwa na mtihani mgumu dhidi ya Barcelona leo kwenye Uwanja wa Nou Camp, Real Madrid inajipa matumaini kuwa ina mbinu sahihi za kupata ushindi na kukuta tiketi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Real imetangaza kuwa itatumia kumbukumbu zile zile za mafanikio ya miaka ya nyuma na kufuta matokeo ya mabao 2-0 na kuiondoa Barcelona.

Mtandao wa klabu hiyo, Jumapili ulichapisha picha ya wachezaji wa klabu hiyo wakishangilia ushindi wa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Nou Camp mwaka 2002 waliposonga mbele na kutwaa taji la tisa la michuano hiyo ya Ulaya.

Wachezaji wa zama hizo, Zinedine Zidane na Steve McManaman walifunga mabao usiku ule na timu hizo zikatoka sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Bernabeu, kisha Real wakailaza Bayer Leverkusen ya Ujerumani kwa mabao 2-1 katika fainali kwa mkwaju wa ajabu wa Zidane.

"Kila mmoja atakubali kuwa ni kazi ngumu, lakini matokeo hayo yanatupa matumaini," uliandika mtandao huo."Ni historia pekee ambayo tunatarajia kuitumia, lakini tuna imani kwamba tunaweza kuwashinda Barca ."

Kipa na nahodha wa Real, Iker Casillas aliongeza sauti katika hilo akieleza kuwa kila mmoja ana matumaini.

"Majina ya timu mbili ambazo zitacheza fainali baadaye mwezi huu bado hayajaandikwa," alieleza kipa huyo aliyeiwezesha Hispania kutwaa Kombe la Dunia mwaka jana.

Alisema: "Huwezi kujua katika soka, kitu kama hicho kinaweza kutokea. Tutaikabili Barcelona tukijua kwamba fainali ipo mbele yetu baadaye mwezi huu na timu nne zilizoingia nusu fainali zinaweza kufuzu."

Mchezo wa kwanza baina ya timu hizo ulitawaliwa zaidi na hasira, lakini mchezaji bora wa dunia, Lionel Messi alifunga mabao mawili na kuipa ushindi timu yake huku Real ikimpoteza beki wa kati, Pepe.

Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) limefungua malalamiko dhidi ya Real, Barca na kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho.Mourinho amelalamikiwa kwa kumdhalilisha mpinzani wake, Pep Guardiola akidai kuwa mafanikio yake ni ya kubahatisha huku Real ikiwatuhumu wachezaji wa Barca kwamba ni waongo.

Rais wa Barca, Sandro Rosell amejaribu kupunguza shinikizo la mchezo huo kwa kuwaomba mashabiki wa klabu yake wawe watulivu, wenye nidhamu katika mchezo huo wakitumia akili.

"Mashabiki wetu ni mfano wa kuigwa kwa tabia nzuri, nina hakika kwamba watafanya hivyo leo, Jumanne kwani macho yote ya walimwengu yatakuwa kwenye runinga.

"Ninawataka waiunge mkono timu yao, wasahau vitu vingine vyote, wajiepushe na uchokozi wa aina yoyote ."

Barca na Real ziliwapumzisha nyota wao na kufungwa katika mechi za Ligi Kuu, La Liga mwisho wa wiki. Barca walitangulia kufunga lakini wakalazwa 2-1 na Real Sociedad huku Real wakifungwa 3-2 na vibonde Real Zaragoza.

Lakini, kwa matokeo hayo Barca imeendelea kuongoza kwa tofauti ya pointi nane dhidi ya Real , zikiwa zimebakisha mechi nne.Ukuta wa Barca umeandamwa na majeruhi na Jumamosi walipata pigo jipya kwa kuwapoteza Gabriel Milito na Martin Montoya.

Lakini, kulikuw na habari njema kwa kiungo Andres Iniesta ambaye amekuwa majeruhi na kukosa mechi ya kwanza baina ya timu hizo baada ya Jumapili kufanya mazoezi.

Real itamkosa Pepe katika mchezo huo huku beki mwingine Sergio Ramos akiwa amefungiwa. Mourinho, ambaye alitolewa benchi kwa kadi nyekundu kwa kupinga kadi nyekundu ya Pepe atakuwa jukwaani akifuatilia mchezo huo.

"Madridismo inafahamika kwa upiganaji wake wa kutoka nyuma na kushinda," alieleza Mkurugenzi Mkuun wa Real, Jorge Valdano.

"Kama kuna timu inajivunia ushujaa , basi hakuna zaidi ya Real Madrid. Hakuna kitu kinachoweza kutuzuia kujiamini katika mchezo wa leo."

Katika mchezo wa Jumatano, Man United ambao wanaongoza Ligi Kuu England na waliofungwa 1-0 na Arsenal katika ligi, wataikaribisha Schalke 04 wakiwa na mabao 2-0 kibindoni. Fainali itachezwa Uwanja wa Wembley, London, Mei 28.
 
Matumla atwaa ubingwa UBO Send to a friend Monday, 02 May 2011 19:58

Sosthenes Nyoni
BONDIA Mtanzania Mbwana Matumla mwishoni mwa wiki alitetea taji lake la ubingwa wa dunia (UBO) baada ya kumtandika Gabriel Ochieng wa Kenya katika pambano la raundi 12 la uzani wa bantam lililofanyika kwenye Ukumbi wa PTA jijini Dar es Salaam.

Katika pambano hilo lililokuwa na upinzani mkali, jaji wa kwanza, Billy Kiremi alitoa pointi 120 – 117 , Hassan Mwingira pointi 120 – 114 na Jalus Ligongo 116 - 113.

Baada ya kutangazwa mshindi wa pambano hilo Matumla alisema: "Nilistahili kushinda, nilikuwa nimejiandaa vizuri na kwa muda mrefu kuhakikisha natetea taji langu, mpinzani wangu ni mzuri isipokuwa nilimzidi ufundi,"

Kabla ya pambano hilo kuu pia kulikuwa na mapambano mingine ya utangulizi, Issa Sewe alimpiga kwa pointi Omari Bayi kama ilivyokuwa kwa Ambukile Chusa aliyemchapa Emmanuel Kayala.

Naye, Fadhili Majia alimtandika Kijepa Omari Sadiki Momba alitoka sare na Jumanne Mapombe baada ya mwamuzi Billy Kiremi kumaliza pambano baada ya mabondia hao kugongana vichwa na Mapombe kuumia vibaya.

Aidha Shaaban Mtengela alimaliza shughuli hiyo kwa kumwadhibu Idrisa Issa kwa pointi katika pambano lako la uzani wa unyoya.
 
COSOTA mbioni kukamilisha marekebisho

na Makuburi Ally

amka2.gif
CHAMA cha Hakimiliki na Shiriki Tanzania (COSOTA), kimesema kiko kwenye mchakato wa kukamilisha matayarisho (draft), ya marekebisho ya sheria ya hakimiliki na shiriki kabla ya kuiwasilisha Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko ili yapelekwe bungeni.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji wa COSOTA, Yustus Mkinga alisema, kazi hiyo inafanywa na mwanasheria wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mkinga alisema, zoezi hilo linatarajiwa kufanyika zaidi ya miezi mitatu na baadaye watawasilisha wizarani ili kupitiwa kwa mara nyingine, ili kujionea mapendekezo ya sheria hiyo.
Sheria hizo ambazo zinatakiwa kufanyiwa marekebisho ni za mwaka 1999, ambazo zimeonekana zina upungufu.
 
Fatma Dogodogo azikwa Dar

na Abdallah Menssah

amka2.gif
MWIMBAJI mkongwe wa kundi la Tanzania One Theatre ‘TOT Taarab', Fatma Ally ‘Dogodogo' (49), amezikwa jana saa 7:00 kwenye makaburi ya
Mwananyamala kwa Kopa jijini Dar es Salaam.
Dogodogo, alifariki juzi majira ya saa 8:00 mchana kwenye Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na kansa ya kizazi.
Wakati wa uhai wake, Dogodogo aliyejiunga na TOT, Agosti 1993, alitamba vilivyo na vibao kadha wa kadha vikali kama vile ‘Tamtam', ‘Upinde', ‘Asojijiua', ‘Hujawa Mcheza' na ‘Utaniona Hivi Hivi'.
Aidha, aliweza kumudu kukonga nyoyo za mashabiki pamoja na wapenzi wa taarab na kutokea kuwa kivutio kwa wengi, kutokana na uimbaji wake, miondoko pamoja na uchezaji wa aina yake.
Akizungumza baada ya mazishi hayo, Mkurugenzi wa TOT, Kapteni mstaafu John Komba, alisema kundi lake limesimamisha shughuli zote za burudani kwa juma moja, ambapo watakuwa wanaomboleza.
Marehemu Dogodogo, ameacha mtoto mmoja, pamoja na wajukuu watatu: Sharifa, Fatma na Nasma.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amin.
 
Simba kuwaleta mabingwa wa Carling Dar

na Dina Ismail

amka2.gif
MABINGWA wa Kombe la Carling nchini England, Birmingham City, wanatarajiwa kutua nchini Julai mwaka huu kwa ziara maalumu ya kimichezo ambapo watakipiga na vigogo wa soka nchini, Simba na Yanga, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa baadhi ya maofisa wa juu wa timu hiyo, akiwemo kocha msaidizi, Andy Watson, pamoja na daktari Ian Mc Guinness, wanatarajiwa kuwasili nchini Mei 9 kwa ajili ya kukagua Uwanja na Hoteli.
Rage alisema, ujumbe huo utakagua Uwanja wa Taifa utakaotumika, pamoja na hoteli ya Kilimanjaro Kempinski ili kuona kama vinakidhi vigezo vya timu hiyo, ambayo itaambatana na mashabiki wasiopungua 1,000 ambao watajilipia gharama za hoteli na uwanjani.
Alisema, usiku wa Julai 7, Birmingham itakipiga na Simba kabla ya jioni ya Julai 12 kukipiga na mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2010/2011, Yanga.
"Tunafurahi kupata wasaa wa kuwa wenyeji wa timu kubwa kama hiyo, ujio wao huo utafungua mipaka ya kimataifa baina yetu na wao…tayari tumeshazungumza na watu wa Wizara ya Maliasili na Utalii juu ya ujio huo," alisema Rage.
Katika hatua nyingine, Rage alisema mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama wa klabu hiyo, unatarajiwa kufanyika Mei 15 katika Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam na wanachama watakaoruhusiwa kushiriki ni wale ambao watakuwa wamelipa ada ya mwaka ambayo ni sh 12,000 pamoja na ile ya uwanja sh 20,000 na kwamba malipo hayo yafanywe katika akaunti ya wanachama.
Pia Rage alisema, uongozi umetoa saa 48 kwa wapangaji wanaotaka kuendelea kupanga katika jengo lao kuwasiliana na uongozi, kinyume cha hapo watakwenda kuomba kibali chama mahakama kwa ajili ya kuwaondoa kwa nguvu.
Wakati huo huo, beki wa timu hiyo Kelvin Yondani amewasilisha barua ya kuomba msamaha kutokana na utovu wa nidhamu huku akisihi arudishwe kundini, wakati mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi ambaye naye aliadhibiwa kutokana na kukiuka mkataba kwa kuzungumza sana na vyombo vya habari, akitakiwa kusoma upya mkataba wake na kutoa maelezo.
 
Kindai kuanza Mazengo Kili Taifa Cup 2011
• Mchezaji wake afariki mazoezini

na Makuburi Ally

amka2.gif
MABINGWA watetezi wa mashindano ya Kili Taifa Cup, timu ya Mkoa wa Singida ‘Kindai Shooting Stars' inatarajiwa kuanza kampeni zake kwa kupepetana na jirani zao Dodoma ‘Mazengo Warriors' kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.
Akitangaza ratiba ya Kili Taifa Cup 2011 mara baada ya kumazikika kwa droo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Idd Mshangama alisema, baada ya mechi hiyo ya ufunguzi kundi A, siku hiyo hiyo pia wenyeji Tabora wataumana na Kigoma.
Mshangama alisema, kundi B lililoko mkoani Morogoro, Watoto wa Mjini Ilala, watamenyana na wenyeji Mount Uluguru na Manyara wataonyeshana kazi na Pwani kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Kundi C, Kagera ‘Lweru Eagles' itaonyeshana ubavu na wenyeji Mwanza huku Shinyanga ‘Igembensabo' ikivurumishana na Mara kwenye dimba la CCM Kirumba, wakati kule Kilimanjaro kwenye Uwanja wa MUCCoBS lililoko kundi D, Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 23 itafungua dimba na wenyeji huku Arusha ‘Mount Meru Warriors wakimenyana na Tanga.
Kundi E, wenyeji Mbeya ‘Mapinduzi Stars' itamenyana na Iringa ‘Ruaha Stars' huku Rukwa ‘Pinda Boys' wakipambana na Temeke uwanja wa Sokoine kundi F lililoko mkoani Lindi, Mtwara itaanza na Kinondoni na wenyeji Ilulu Stars watawakaribisha Ruvuma kwenye uwanja wa Ilulu.
Katika hatua nyingine, mabingwa hao watetezi wa Kili Taifa Cup, Kindai wamepata pigo baada ya mchezaji wake Nassoro Issa (19), kufariki dunia jana saa 9 alasiri akiwa mazoezini kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Mwenge mjini Singida.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Singida (SIREFA), Issa ambaye alikuwa mchezaji wa timu ya Aston Villa ya mjini humo, alijisikia vibaya wakati akiwa mazoezini na kumuomba kocha wake Abdallah Msamba apumzike, ambaye alimruhusu na kwenda chini ya mti nje ya uwanja.
Mwamba alisema, Issa ambaye aliuwakilisha mkoa huo kwenye michuano ya Copa Coca- Cola mwaka 2009, aliomba apewe maji ya kunywa na baada ya hapo alijipumzisha, baadaye daktari wa Kindai alikwenda kumuangalia ili kujua hali yake. Hata hivyo baada ya kujaribu kumuinua aligundua kuwa ameishafariki dunia.
TFF imepokea kwa masikitiko makubwa msiba huo na kutuma salamu za rambirambi SIREFA, hasa ikizingatiwa kuwa mchezaji huyo alikuwa bado kijana, hivyo kuwa na fursa pana ya kutoa mchango katika maendeleo ya mpira wa miguu nchini, hasa kupitia Mkoa wake wa Singida. Mungu aiweke roho ya marehemu Nassoro Issa mahali pema peponi. Amina.
 
Mtanzania ang'ara Moroni Send to a friend Monday, 02 May 2011 20:00

Elie Djouma, Moroni
MWANARIADHA wa kimataifa wa Tanzania, Stephan Huche ameshinda mbio za nyika za Comoro kwa kukimbia km 42.195 kwa saa 2:23:17 na kuvunja rekodi iliyoweka ya mbio hizo za Moroni ya saa 2:23:47.

Mkimbiaji huyo chipukizi mwenye miaka 21, alianza mbio hizo kwa kasi kwenye uwanja wa Mitsamihuli, karibu na pwani ya Maludja.

Kwa ushindi huo Stephane anaamini ataweza kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano mengine ya mbio za nyika za Berlin, Ujerumani baadaye Septemba. Mshindi wa mwaka jana, Mkenya Hillary Kericho aliyetumia muda wa saa 2:31 hakushiriki mwaka.

Huche aliyekuwa wa pili katika mbio za nyika za Kilimanjaro 2011, alitumia saa 2:18.

Akizungumzia ushindi wake Huche alisema: "Sikutarajia kufikia kiwango hiki. Nilijua nitakuwa miongoni mwa washindi watatu wa juu. Nilijua kutakuwa na upinzani mkubwa kutoka kwa majirani zetu wa Kenya.

"Naamini shirikisho langu litaichukulia kwa umakini rekodi yangu hii. Itanisaidia kupata mialiko sehemu mbalimbali ya mbio. Hii ni mara yangu ya tatu kushiriki katika mashindano ya kimataifa."

Huche aliwashukuru watu wote wa Comoro kwa kujitokeza kwa wingi kuangalia mbio hizo pamoja na kudhamini mchezo huo kabla ya kuanza safari ya kurejea Dar es Salaam leo.
 
Matumla atwaa ubingwa wa mabara UBO

na Dina Ismail

amka2.gif
BONDIA Mbwana Matumla wa Tanzania, juzi alifanikiwa kutwaa ubingwa wa mabara unaotambuliwa na UBO baada ya kumshinda kwa pointi, Mkenya Gabriel Ochieng katika pambano la uzito wa Bantam lililofanyika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Katika pambano hilo la raundi 12, Ochieng alijikuta akilamba sakafu raundi ya 11, lakini alinyanyuka na kuendelea hadi raundi ya mwisho.
Katika pambano hilo ambalo mwamuzi wake alikuwa Anthony Ruta, Jaji Billy Kiremi alitoa pointi kwa Mbwana 120 –117, huku Hassan Mwingira akitoa 120 –114 na Jalus Ligongo alitoa 116 -113.
Kwenye mapambano mengine, Issa Sewe alimshinda Omari Bayi kwa pointi katika pambano la raundi nne Light, huku Ambukile Chusa naye akimdunda Emmanuel Kayala kwa pointi katika Super Welter wakati Fadhili Majia alimshinda Kijepa Omari katika raundi ya pili kati ya nne Fly na Sadiki Momba alitoshana nguvu na Jumanne Mapombe uzito wa Feather, ambako Shabani Mtengela alimtambia Idrissa Issa katika uzito wa Feather. Mapambano hayo yote yalisimamiwa na Kampuni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST).
 
Tenga kubariki Muungano Mufindi

na Francis Godwin, Iringa

amka2.gif
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Muungano Mufindi mkoani Iringa.
Mratibu wa Kombe la Muungano wilayani Mufindi, Daudi Yassin, alisema kuwa kamati ya mashindano hayo, imemwalika Tenga kufungua mashindano hayo Mei 7 mwaka huu kwenye uwanja wa shule ya Msingi Igowole.
Yassin alisema kuwa mashindano hayo yameendelea kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi hao wa TFF na kuwa, ushiriki wao katika kuendeleza mashindano hayo umekuwa mkubwa zaidi.
Mbali ya rais huyo wa TFF kuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo, pia kutakuwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Iringa.
Mratibu huyo, alizitaja timu ambazo zitashiriki mashindano hayo kwa upande wa bara ni Foysa na Mbalari United za Mbeya, Holly Family ya Ruvuma na Vodacom FC ya Rukwa.
Nyingine ni Benki ya Wananchi Mufindi (Mucoba Fc), MPM Mgololo, Zamalek FC, VETA, Young Star na Nyabula Fc.
Yassin alisema, siku ya ufunguzi kutakuwa na mechi mbili, ambako Zamalek itavaana na VETA huku mchezo wa pili utakaochezwa jioni utakuwa kati ya Young Stars na Mucoba FC.
 
Temeke bado wanyonge kwa Ilala

na Lilian Lihame

amka2.gif
TIMU ya soka ya mkoa wa Temeke juzi ilishindwa kufurukuta mbele ya mahasimu wao Ilala baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kwenye uwanja wa Tandika Mabatini. Mechi hiyo ilikuwa ni maandalizi ya michuano ya Kili Taifa Cup 2011, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 7 katika vituo sita tofauti.
Katika mchezo huo uliovuta mashabiki kadhaa ambao walikuwa na hamu kuviona vikosi vyao, walikuwa ni wenyeji TMK walioanza kuliona lango la wapinzani wao kwa bao la Benedicto Jacob dakika ya 20.
Temeke ilizidi kutawala kipindi chote cha kwanza, ambako ilikosa nafasi nzuri za kufunga kupitia mshambuliaji wake Benedicto Jacob.
Kipindi cha pili, Ilala waliibuka na kuchomoa bao hilo dakika ya 50 mfungaji akiwa Adam Kingwande, baada ya kupokea pande safi la Mussa Hassan Mgosi.
Baada ya Ilala kusawazisha bao hilo, walianza kuliandama lango la Temeke na kufanikiwa kupachika bao la pili dakika ya 67 kupitia kwa Andrew Bundala aliyepoteza matumaini ya Temeke.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, kocha wa Temeke Habibu Kondo alisema kuwa, mchezo huo ni wa majaribio, hivyo wakazi wa manispaa hiyo wasikasirike na wasife moyo juu ya kikosi hicho.
Naye Meneja wa Ilala, Alhaji Kabunju, aliushukuru uongozi wa TEFA kwa kuandaa mchezo huo wa kirafiki na kuwa wameweza kuona udhaifu uliopo katika kikosi chao .
 
Ferguson amtupia lawama mwamuzi Send to a friend Monday, 02 May 2011 19:51

LONDON, Uingereza
KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amesisitiza kuwa ubingwaupo wazi kwao au Chelsea licha ya timu yake kuadhibiwa na maamuzi duni ya mwamuzi wa mchezo dhidi ya Arsenal juzi.

Alisema makosa ya mwamuzi Chris Foy katika mchezo huo yaliikosesha penalti Man United kipindi cha pili baada ya Gael Clichy kumkwatua Michael Owen.Ferguson alieleza imani yake kwamba Foy alikosea kwa kushindwa kuwapa penalti ya dakika ya 88 baada ya Clichy kumchezea vibaya Owen.

Pia, alieleza kuwa wapinzani wao (Arsenal) pia walinyimwa penalti kipindi cha kwanza baada ya Nemanja Vidic kucheza kwa mkono krosi yaTheo Walcott.Kwa matokeo hayo, Chelsea ina pengo la pointi tatu nyuma ya Man United baada ya Jumamosi kuishinda Tottenham kwa mabao 2-1 na timu hizo zinakutana Old Trafford , Mei 8.

Miezi 11 iliyopita, Didier Drogba alifunga bao la ushindi na kuipa ushindi Chelsea na ubingwa dhidi ya Man United, lakini Ferguson ana matarajio ya kutorudia kosa."Utakuwa mchezo mgumu, una umuhimu mkubwa, lakini unahitaji maamuzi sahihi," alieleza Ferguson. "Ninajua utakuwa mgumu kwa kila mmoja wetu.

"Sina shaka kwamba uamuzi wa kutunyima penalti na nafasi ya kusawazisha umewasaidia Chelsea ambao tunakutana nao wiki moja ijayo. Wao (Chelsea) walipata ushindi na ubingwa pale Old Trafford , hiki kinanipa wasiwasi.

"Lakini, kuhusu uwezo - mchezo pale Old Trafford, mbele ya mashabiki, tupo tayari kwa vita, nimewaambia pia wachezaji wangu."

Katika mchezo wa Jumapili, Aaron Ramsey alifunga bao la sakika ya 56 na kuipa ushindi Arsenal ambayo ilitawala mchezo huo huku Ferguson akikiri kwamba walishindwa kuhimili vishindo licha ya mwanzo wa mchezo kutawala wao.Kwa matokeo hayo, Arsenal ipo nyuma ya vinara hao kwa pointi sita zikiwa zimebakia mechi tatu msimu huu na kocha Arsene Wenger amekata kusema kuwa amekata tamaa.

Nafasi yao ya ubingwa itaimarika endapo Chelsea itailaa United na Wenger ameeleza kuiunga mkono Chelsea chini ya Carlo Ancelotti Jumapili

Wenger anajifariji kuwa nao Samir Nasri na Cesc Fabregas katika mchezo ujao dhidi ya Stoke City. Nasri aliumia juzi huku Fabregas akiuguza paja.
 
Birmingham kuwapima Simba, Yanga

Na Elizabeth Mayemba

MABINGWA wa Ligi ya Ndani ya Uingereza 'Carring Cup', Birmingham City, wanatarajiwa kutua nchini Julai 5, mwaka huu, kucheza na Simba na Yanga, mechi maalumu za
kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru.

Birmingham, katika fainali za Carring Cup, iliifunga Asernal mabao 2-1 na kutwaa ubingwa huo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Rage, alisema timu yao itaanza kucheza na Birmingham Julai 7, mwaka huu, wakifuatiwa na Yanga Julai 12, ambapo mechi zote zitachezwa usiku.

"Birmingham watakuja na kikosi kamili, pia watakuwa wamefanya usajili wa wachezaji wao kwa ajili ya msimu ujao, na timu zetu zitatumia nafasi hiyo kuwapima wachezaji wao wapya waliowasajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi na michuano ya kimataifa," alisema Rage.

Alisema Mei 9, mwaka huu, Kocha Msaidizi wa Birminghamam, Endy Watson na daktari wa timu, Ian Mc Guiness, watafika nchini kukagua hoteli ya Kempiski ya Dar es Salaam na Uwanja wa Taifa, kwa ajili ya ujio wa timu hiyo.

Alisema timu hiyo itatua nchini na mashabiki 1,000, ambao kila mmoja atajihudumia kwa gharama zote kuanzia malazi, chakula hadi usafiri.

Mwenyekiti huyo alisema, pia wamefanya mazungumzo na Wizara ya Maliasili na Utalii ili wajue jinsi ya kuwapokea wageni hao, ambao watataka kuangalia vivutio vya utalii vya maeneo mbalimbali nchini.

Rage alisema, Simba mwakani ina mpango wa kuileta timu ya Liverpool, kama mambo yatakwenda vizuri.
 
Totti avunja rekodi ya Baggio mabao 206 Serie A Send to a friend Monday, 02 May 2011 19:50

BARI, Italia
NAHODHA wa Roma, Francesco Totti amevunja rekodi ya Roberto Baggio na kuwa mchezaji wa tano kwa ufungaji katika ligi ya Serie A baada ya kufunga bao lake la 205 na 206 juzi.

Totti alimfikia Baggio kwa bao lake la mpira wa adhabu uliopita ukuta na kujaa wavuni dakika ya 30, wakati Roma iliposawazisha dhidi ya Bari 1-1, aliongeza la pili kwa mkwaju wa penalti dakika ya 57 kufanya matokeo kuwa 2-2 huku akipita rekodi ya Baggio.

Mabao hayo ya 13 na14 kwa msimu huu kwa mkongwe Totti mwenye miaka 34.Totti alipoteza nafasi ya kufunga bao la tatu wakati Roma walipopata penalti nyingine, lakini shuti lake liligonga mwamba. Lakini, bado Roma walifanikiwa kutoka na ushindi wa mabao 3-2 baada ya Aleandro Rosi kufunga zikiwa zimebaki dakika tano.

Silvio Piola, ambaye alitwaa Kombe la Dunia na Italia mwaka1938, bado anashikiria rekodi ya kufunga mabao mengi 274, akifutiwa na Gunnar Nordahl (225), Giuseppe Meazza (216), Jose Altafini (216), Totti na Baggio (205).

Wachezaji wengine wenye mabao mengi ni nahodha wa Juventus, Alessandro Del Piero anayelingana na Gabriel Batistuta kwenye nafasi ya tisa katika orodha hiyo wakiwa wamefunga mabao 184. Mabao 20 aliyoyafunga Del Piero wakati Juventus iliposhushwa Serie B msimu wa 2006-07 hatajahesabiwa kwenye orodha hiyo.

Totti alianza kucheza Serie A mwaka 1993 akiwa na miaka 16, tangu wakati huo hajawahi kuhama au kuondoka Roma, timu yake ya nyumbani kwao.Baggio alifunga mabao hayo kuanzia mwaka 1986 hadi 2004.

Totti aliyekuwa akipigiwa kelele za kustaafu baada ya kuanza vibaya msimu huu, lakini amerudi kwenye kiwango chake tangu mchezaji mwenzake Vincenzo Montella alipoteuliwa kuwa kocha mwezi Februari.

Baada ya filimbi ya mwisho, Totti aliivaa T-shirti iliyokuwa na maandishi "Mfamle wa Rome hajafa."

"Mfamle wa Rome hajafa na hatokufa kamwe," alisema Totti. "Najua nini cha kuwapa. Nafuraha kuvunja rekodi nyingine mzuri kama hii ya Baggio. Sasa natumaini nitaendelea kucheza kwa kiwango hiki."
 
ambi Taifa Stars yasogezwa mbele

Na Zahoro Mlanzi

KAMBI ya timu ya Taifa 'Taifa Stars', iliyotakiwa ianze jana, imesogezwa mbele mpaka Mei 7, mwaka huu jijini Dar es Salaam.Timu hiyo inajiandaa na mchezo wa
kirafiki wa kimataifa utakaopigwa mwishoni mwa mwezi huu dhidi ya Afrika Kusini 'Bafana Bafana'.

Mbali na mchezo huo, Taifa Stars pia itaumana na Jamhuri ya Afrika Kati katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika, utakaopigwa Juni 4, mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema Kocha Mkuu wa timu hiyo, Jan Poulsen, ndiye aliyeamua isogezwe mbele.

Alisema kutokana na programu ya kocha huyo ya kujiandaa na michezo hiyo miwili aliyoiwasilisha TFF, ndiyo iliyoeleza mambo hayo.

"Kocha amewasilisha programu yake na inaonesha timu hiyo itaingia kambini Jumamosi, badala ya leo (jana), hivyo tumewataarifu wachezaji juu ya jambo hilo," alisema Wambura.

Alisema mawasiliano na Afrika Kusini yanaendelea na kikubwa wanachokisubiri ni kupanga tarehe ya kucheza mchezo huo na siku watakayotua nchini.

Alisema kikosi kitakachoingia kambini ni kile kile kilichokwenda nchini Msumbuji kucheza na timu ya taifa ya nchi hiyo, na labda waongezeke wanaocheza soka la kulipwa.
 
Kambi Taifa Stars yasogezwa mbele

Real Madrid accuse Uefa of ignoring Barcelona 'racism'

• Spanish war escalates before Champions League second leg
• Real allege that Busquets called Marcelo a 'monkey'

  • Sid Lowe in Madrid
  • guardian.co.uk, Monday 2 May 2011 21.57 BST <li class="history">Article history
    Barcelonas-Sergio-Busquet-005.jpg
    Barcelona's Sergio Busquets has been accused of racism by Real Madrid. Photograph: Jose Jordan/AFP/Getty Images

    The bitter off-field feud that has accompanied the Champions League semi-final between Barcelona and Real Madrid turned into a racism storm when José Mourinho's assistant coach, Aitor Karanka, hit out at Uefa for overlooking the abuse allegedly directed at the Real Madrid full-back Marcelo by Sergio Busquets. Karanka claimed that tomorrow's semi-final second leg was of only "secondary importance" in the face of Uefa's failure to act to defend fair play and the abandonment of ethics in the sport.
    "There will be a player on the pitch who racially abused another player," the Madrid assistant coach said, "while others who have done nothing wrong won't be there."
    Karanka's comments come in the light of a video released by Real Madrid on Monday that they claim shows Busquets calling the Madrid full-back Marcelo a "monkey". They also came hours after Uefa announced that it had rejected the complaint made by Real Madrid against eight Barcelona players for "persistent and premeditated unsporting behaviour". Uefa likewise resolved not to act on the complaints made by Barcelona against Mourinho, saying that European football's governing body would be the "sole judge".
    The Barcelona coach, Pep Guardiola, insisted Busquets had merely made a "mistake" and that it would be up to Uefa to decide if he should be punished. "I know these players. They are an example of professionalism," said the Barcelona coach. "They love this sport. Some of them, during the game, can make a mistake but as players they are exemplary both for Spain and for Barcelona." Asked if he would punish Busquets he said: "We are not proud when they make mistakes but I know these players. If we do something wrong, then Uefa have to decide. It won't happen again."
    Uefa's statement made no specific mention of the alleged racist abuse but Madrid's assistant coach brought the issue to the fore after Real's release of the footage. In a piece about tomorrow's referee, Frank de Bleeckere, on Madrid's website and the Spanish version of their TV channel, the voiceover expressed a desire that the official would not fall into Barcelona's trap and that there would be no "disrespect" from the players. The comment came over a shot of Busquets cupping his hand to hide his words and saying something to Marcelo. Real's subtitles showed "mono, mono" &#8211; "monkey, monkey".
    Uefa did not respond to calls tonight but Karanka made his views clear in the pre-match press conference. "After today's resolution the game itself drops to a secondary issue," he said. "[Uefa is] an organisation which talks about principles like respect and fair play and yet nothing has happened.
    "We have seen the images which have been round the world, including a player making racist insults and covering his mouth to try to make it so that you can't see it. But he will be on the pitch, along with others. Other players who have done nothing wrong won't be. That is the most important thing today. The football is not."
    Karanka also defended Mourinho's outburst following the first leg, in which he accused Uefa of favouring Barcelona and a series of referees of giving them beneficial decisions. Karanka added that he did not understand why no action was taken against Barcelona players for something that does appear in the rules when there were fines handed out to Real Madrid players for deliberately seeking out cards against Ajax earlier in the competition &#8211; which does not appear in the rules.
    "A few months ago we were sanctioned for something that is not in the Uefa rule book. Now they are not sanctioning things that are in the rule book," Karanka said. "It's not a case of feeling unprotected but once again there seems to be different measures [for different teams]. Our position is the one that we made clear in our complaint to Uefa. What Mourinho said [after the first leg] was what anyone who had been in the stadium or watching the game on television would have said. This isn't an accusation against Uefa. I'm saying what's in the regulations and what isn't. These are provable and objective things."
    The Barcelona midfielder Xavi Hernández had earlier rejected suggestions that Uefa should act against them, describing the complaints as "pathetic and lamentable". He added: "Barcelona have always respected opponents and shown exemplary behaviour. It is logical that Uefa should turn down the complaints. I think it's lamentable and pathetic, everything that is going on &#8211; all the complaints and denouncements. It is sad. I would rather just talk about the football."

Real Madrid accuse Uefa of ignoring Barcelona 'racism'

• Spanish war escalates before Champions League second leg
• Real allege that Busquets called Marcelo a 'monkey'

  • Sid Lowe in Madrid
  • guardian.co.uk, Monday 2 May 2011 21.57 BST <li class="history">Article history
    Barcelonas-Sergio-Busquet-005.jpg
    Barcelona's Sergio Busquets has been accused of racism by Real Madrid. Photograph: Jose Jordan/AFP/Getty Images

    The bitter off-field feud that has accompanied the Champions League semi-final between Barcelona and Real Madrid turned into a racism storm when José Mourinho's assistant coach, Aitor Karanka, hit out at Uefa for overlooking the abuse allegedly directed at the Real Madrid full-back Marcelo by Sergio Busquets. Karanka claimed that tomorrow's semi-final second leg was of only "secondary importance" in the face of Uefa's failure to act to defend fair play and the abandonment of ethics in the sport.
    "There will be a player on the pitch who racially abused another player," the Madrid assistant coach said, "while others who have done nothing wrong won't be there."
    Karanka's comments come in the light of a video released by Real Madrid on Monday that they claim shows Busquets calling the Madrid full-back Marcelo a "monkey". They also came hours after Uefa announced that it had rejected the complaint made by Real Madrid against eight Barcelona players for "persistent and premeditated unsporting behaviour". Uefa likewise resolved not to act on the complaints made by Barcelona against Mourinho, saying that European football's governing body would be the "sole judge".
    The Barcelona coach, Pep Guardiola, insisted Busquets had merely made a "mistake" and that it would be up to Uefa to decide if he should be punished. "I know these players. They are an example of professionalism," said the Barcelona coach. "They love this sport. Some of them, during the game, can make a mistake but as players they are exemplary both for Spain and for Barcelona." Asked if he would punish Busquets he said: "We are not proud when they make mistakes but I know these players. If we do something wrong, then Uefa have to decide. It won't happen again."
    Uefa's statement made no specific mention of the alleged racist abuse but Madrid's assistant coach brought the issue to the fore after Real's release of the footage. In a piece about tomorrow's referee, Frank de Bleeckere, on Madrid's website and the Spanish version of their TV channel, the voiceover expressed a desire that the official would not fall into Barcelona's trap and that there would be no "disrespect" from the players. The comment came over a shot of Busquets cupping his hand to hide his words and saying something to Marcelo. Real's subtitles showed "mono, mono" – "monkey, monkey".
    Uefa did not respond to calls tonight but Karanka made his views clear in the pre-match press conference. "After today's resolution the game itself drops to a secondary issue," he said. "[Uefa is] an organisation which talks about principles like respect and fair play and yet nothing has happened.
    "We have seen the images which have been round the world, including a player making racist insults and covering his mouth to try to make it so that you can't see it. But he will be on the pitch, along with others. Other players who have done nothing wrong won't be. That is the most important thing today. The football is not."
    Karanka also defended Mourinho's outburst following the first leg, in which he accused Uefa of favouring Barcelona and a series of referees of giving them beneficial decisions. Karanka added that he did not understand why no action was taken against Barcelona players for something that does appear in the rules when there were fines handed out to Real Madrid players for deliberately seeking out cards against Ajax earlier in the competition – which does not appear in the rules.
    "A few months ago we were sanctioned for something that is not in the Uefa rule book. Now they are not sanctioning things that are in the rule book," Karanka said. "It's not a case of feeling unprotected but once again there seems to be different measures [for different teams]. Our position is the one that we made clear in our complaint to Uefa. What Mourinho said [after the first leg] was what anyone who had been in the stadium or watching the game on television would have said. This isn't an accusation against Uefa. I'm saying what's in the regulations and what isn't. These are provable and objective things."
    The Barcelona midfielder Xavi Hernández had earlier rejected suggestions that Uefa should act against them, describing the complaints as "pathetic and lamentable". He added: "Barcelona have always respected opponents and shown exemplary behaviour. It is logical that Uefa should turn down the complaints. I think it's lamentable and pathetic, everything that is going on – all the complaints and denouncements. It is sad. I would rather just talk about the football."
 
Semi-final, second leg

Uefa sends in Pierluigi Collina to monitor Barcelona v Real Madrid

&#8226; Former referee appointed Uefa's 'official observer' for game
&#8226; Follows bad-tempered first leg at the Bernabéu

  • Associated Press
  • guardian.co.uk, Tuesday 3 May 2011 13.29 BST <li class="history">Article history
    Pierluigi-Collina.-006.jpg
    Pierluigi Collina will attend the Champions League semi-final second leg between Barcelona and Real Madrid as Uefa's 'official observer'. Photograph: Catherine Benson/Reuters

    Uefa is sending the former referee Pierluigi Collina to monitor the Belgian match official Frank de Bleeckere's handling of the potentially volatile Champions League semi-final second leg between Barcelona and Real Madrid.
    Uefa has named Collina, now its head of referees, as its official observer at Camp Nou on Tuesday. While Uefa sends a referee observer to every match it organises, it is rare for Collina to be called in.
    Uefa's choice of the 44-year-old De Bleeckere, who has a long-standing reputation as one of Europe's best referees, also reflects the high-risk status it has given the rematch of the Spanish rivals.
    After Barcelona won a bad-tempered first leg 2-0 last week, Madrid made a failed protest to Uefa about the German referee Wolfgang Stark sending off Pepe when the game was scoreless. The Madrid coach, José Mourinho, was sent from the dugout by Stark for his comments about Pepe's red card, then later accused Uefa and its referees of effectively helping Barcelona reach the Champions League final.
    Mourinho included De Bleeckere in the supposed conspiracy after his handling of the second leg of last year's semi-final when his 10-man Internazionale side eliminated Barcelona.
    Uefa's disciplinary panel will meet on Friday to examine the six charges arising from the first-leg match. Mourinho, who is banned from the touchline on Tuesday night, faces further punishment for his comments during and after the match. Pepe also faces a longer ban for his red-card challenge, and Madrid have been charged for their fans throwing objects and invading the pitch. The Barcelona substitute goalkeeper José Pinto has been charged over his part in a touchline brawl at half-time.
    Collina refereed the second leg when Madrid and Barcelona last met in the Champions League semi-finals. In 2002, the sides drew 1-1 at the Bernabéu allowing Madrid to advance and win the competition. Collina also refereed the 2002 World Cup final, when Brazil beat Germany, and Manchester United's 2-1 victory over Bayern Munich in the 1999 Champions League final.

Semi-final, second leg

Uefa sends in Pierluigi Collina to monitor Barcelona v Real Madrid

• Former referee appointed Uefa's 'official observer' for game
• Follows bad-tempered first leg at the Bernabéu

Back
Top Bottom