Mzalauliwa
Member
- Jul 31, 2014
- 95
- 35
Kamari ni mchezo wa kubahatisha unaohusisha pesa au kitu kingine chenye thamani kama tuzo kwa mshindi.
Tuzo hilo la kubahatisha ndio lengo kuu la mchezo. Sheria za nchi mbalimbali zinatofautiana kuhusu uhalali wake.
Asilimia kubwa ya washiriki hasa katika mchezo huo ni vijana ambao wanakuwa na shauku kubwa ya kupata utajiri wa haraka, hivyo wanaposhindwa wanashawishika kucheza mara kwa mara jambo ambalo, linapelekea hadi kufilisika.
Michezo ya kamari imekuwa biashara kubwa kimataifa ikiwa na bajeti ya zaidi ya mabilioni ya dola. Umaarufu wa michezo hiyo hasa mpira wa miguu kasino pamoja na michezo pepe, inayoendeshwa kwa mfumo wa kielektroniki umendelea kukua siku hadi siku huku ongezeko la watumiaji wake umekuwa mkubwa sana hasa katika nchi yetu.
Vijana wengi hapa hapa nchini wamekuwa wakitumia pesa nyingi hasa katika michezo ya kubashiri , wakiamini kuwa watapata fedha nyingi zitakazo wapatia utajiri wa haraka na badala yake wamekuwa wakipoteza fedha hizo na kuwapelekea kuwa na madeni mengi pamoja na umaskini mkubwa.
Michezo hio pia imekuwa na faida na hasara ,moja ya hasara kubwa kabisa kwa wachezaji wa michezo hii ni pamoja na kupata matatizo ya ugonjwa wa akili, pia kuna tiba za aina mbali mbali za kuwasaidia watu wanaoshindwa kuacha michezo hii kutokana na uraibu.
Uraibu wa michezo ya kamali umewafanya vijana wengi kuwa na uvivu wa kufanya kazi, jambo ambalo linapelekea kupunguza kasi ya maendeleo pamoja na ubunifu katika kazi mbali mbali katika kujenga uchumi wa taifa letu.
Wingi wa michezo hii umekuwa mkubwa sana, hivyo wazazi wanatikiwa watoe elimu kwa watoto wao juu ya madhara ya michezo ya kamali , na badala yake wajikite katika kuwafundisha watoto wao namna iliyo bora hasa katika kuweka au kuhifadhi akiba ya pesa.
michezo ya kubahatisha haijawahi kuwa na faida pamoja na tija katika kuleta maendeleo yako wewe kijana ,badala yake kijana kama kijana unatakiwa kujikita katika shughuli zauzalishaji mali kama vile, ufugaji wa kuku ,samaki kilimo pamoja na uvuvi.

Upvote
0