Baada ya China kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing, michezo ya majira ya baridi ya walemavu imeendelezwa kwa kasi nchini China.
Katika miaka 6 iliyopita, shule nyingi maalumu kwa ajili ya walemavu zimeanzisha masomo ya michezo ya majira ya baridi. Jamii pia imejenga majukwaa mengi zaidi kwa ajili ya walemavu kupata fursa za kushiriki kwenye michezo hiyo.
Hadi sasa idadi ya wachezaji walemavu wanaoweza kushiriki kwenye michezo ya Olimpiki ya Walemavu imefikia karibu elfu moja ikilinganishwa na chini ya 50 ya zamani.