Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE SEIF GULAMALI AZIDI KUIPA NGUVU SEKTA YA MICHEZO JIMBONI MANONGA
Mbunge wa Jimbo la Manonga Wilaya ya Igunga Mhe. Seif Khamis Gulamali ameanza ziara rasmi kwenye Kata ya Igoweko na Vijiji vyote na Kufanya Mikutano katika Maeneo 5 kwa Maana ya Seregei, Mwina, Buhekela, Bugingija na Igoweko.
Wananchi wamepongeza Kazi zinazofanyika huku akigawa Vifaa vya Michezo, Jezi, Mipira, Gloves, Vibao vya Kubadilishia Wachezaji, Filimbi, Vibao vya Kona kwa Shule ya Sekondari Igoweko, Shule ya Sekondari Manonga; Mipira kwa Shule za Msingi za Seregei, Mwina, Buhekela, Bugingija na Igoweko.
Kazi Inaendelea Kata ya Uswaya.