Michongo ya Rostam inanikumbusha kiherehere cha Jack Ma wa China alichokutana kwa serikali ya China

Michongo ya Rostam inanikumbusha kiherehere cha Jack Ma wa China alichokutana kwa serikali ya China

Mi mi

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2024
Posts
6,406
Reaction score
12,736
Hizi stories za michongo ya Rostam toka zilivyo anza kupata umaarufu mkubwa zaidi miaka ya 2000s nchini Tanzania zinanikumbusha jambo moja kumuhusu Jack Ma.

Jack Ma tajiri mmoja hivi toka alikuwa maarufu sana na kama unavyojua umaarufu unatabia ya kulevya ukichanganya na pesa, pesa ni kila kitu inaweza nunua kila kitu unachoota na inaweza kufanya jambo lolote hata kuitia serikali mfukoni.

Sasa Jack Ma 2020 kwenye mkutano mmoja hivi mjini Shanghai akakanyaga waya wa umeme na waya wa umeme wenyewe ni kugusa serikali ya China na chama cha kikomunisti cha China.

China wana kauli moja hivi inasema "the Party leads everything" inamaanisha hakuna aliyejuu ya chama.

Sasa Jack kwa ukwasi alionao na umaarufu alionao nafikiri akafikiri atakuwa na uwezo wa kudictate sera na sheria za Benki kuu ili kui favor kampuni yake ya Ant financial kumbe alikuwa anakosea kabisa.

Ukafika muda wa Jack Ma kuzungumza kwenye mkutano ule viongozi wa Benki ya China walikuwepo,waziri wa fedha alikuwepo na viongozi wa chama walikuwepo.

Bwana Jack Ma akaanza kuikandia mifumo ya kifedha ya China kuwa ni old fashion hili lilikuwa kosa kubwa akawa ana shauri wabadilike wawe kisasa lengo kujaribu ili kampuni yake iweze kupata favor kupitia mabadiliko hayo.

Hili kosa lilipelekea Jack Ma kampuni yake kutulizwa,utajiri wake kutulizwa,spotlight yake kupotezwa na Jack kubaki billionaire wa kawaida kabisa tofauti na awali.

China pamoja na kwamba walikubali sera za kibepari kwenye baadhi ya masuala lakini kwao capital haipo above serikali tofauti na nchi nyingi za kibepari.

Hizi issues sijui Rostam kadanya hivi sijui kafisadi nini, kwanza hata Rostam sidhani hata kama angekuwa hai tena ubaya wake anapenda vyombo vya habari na ukimbelembele wa kujifanya tajiri ana jibia masuala yake mpaka sasa Rostam asingekuwa hai.

Tanzania ni miongoni mwa nchi fulani hivi ambazo viongozi na wananchi hatupo serious na Tanzania.
 
Jack Ma😀
0x0.jpg
 
Back
Top Bottom