Michoro ya X na maandishi ya bomoa bomoa barabara ya Chamazi Mbande ni uhalibifu wa pesa za walipa Kodi

Michoro ya X na maandishi ya bomoa bomoa barabara ya Chamazi Mbande ni uhalibifu wa pesa za walipa Kodi

Wazolee

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2018
Posts
3,183
Reaction score
3,660
Meneja wa TAN ROADS uliwatuma watu wakachole bomoa bomoa katika majumba yote yanayosemekana yapo barabarani na Nina uhakika hi kazi wale walioifanya hakufanya Bure ila walilipwa pesa nyingi tu

Hivi Sasa watu wamegundua kuwa ule ulikuwa usanii na watu wameanza kujenga Kwa Kasi katika hayo hayo Maeneo na majengo mliyochora X na kuandika bomoa

Haikuitajika akili nyingi kujua kuwa ule ulikuwa ni usanii Kwa sababu haiwezekani upige X nyumba na kuandika bomoa na kuacha barua kutoka TAN ROADS inayo amuru hilo eneo liwe wazi Baada ya wiki mbili Jengo ambalo Lina fremu za biashara labda Tano au sita

Hivi kweli inawezekana mfanya biashara kuhamisha biashara yake ndani ya wiki mbili?

Vipi kama huyu mfanya biashara Jana alilipa Kodi ya miezi sita alafu Leo wewe TAN ROADS unampa wiki mbili ahame

Hapo ndipo watu waliposema huu ni usanii tunafanyiwa na meneja wa TAN ROADS sijui kama meneja wa mkoa au wilaya na jibu likawa kweli ni usanii ndio maana Hadi Leo hi hakuna nyumba iliyovunjwa Wala barabara inayojengwa ila ndio kwanza watu wanatanua mafremu Yao

Swali la kujiiliza hivi ni kweli meneja kabisa serikali imekuhamini na kukupa hiyo kazi unaingia ofisini na kuomba fungu la pesa na kuwatuma watu wakachole bomoa bomoa na wawape hao wanaotakiwa kuhama barua inayosema Baada ya wiki mbili wawe wameshahama?

Umeshawalipa watu pesa kazi wamefanya na watu hawajahama na ndio kwanza wanafuta michoro yako na kujenga
Kwahiyo itafika siku utachukua tena pesa za walipa Kodi na kuwapa watu wakachole tena? Hauoni huo ni uhalibifu wa Kodi za wananchi maana ni ukweli usiopingika itafika wakati hi barabara lazima itanuliwe

Kwahiyo wewe meneja unataka tukufundishe kuwa siku nyingine toa notice ya miezi sita au nane au mwaka Ili watu wajue kuwa upo serious?

Ndio maana watu wanasema nchi hii aliyesoma na asiyesoma wapo sawa au waliosoma wanaweza kuwa wajinga zaidi

Ukweli ni kwamba katika hili meneja husika wa TAN ROADS umejidhalilisha
 
Kwa nini mlijenga ndani ya hifadhi ya barabara?
 
Back
Top Bottom