Michuano ipi ya World Cup ilikuwa bora sana kuitazama?

Michuano ipi ya World Cup ilikuwa bora sana kuitazama?

Kwa kuwa mimi ni muhenga basi sina budi kusema ni ile ya mwaka 1970 Mexico
Wakati Mario Zagalo ndio coach wa Brazil
Duu kina Tostao, Carlos Alberto, Pele, na Revelino
Hiyo ilikuwa ni timu haswa ingawa pia naikumbuka ya South Korea pia ya 2002
Ila msinikosoe kwa kusifia vya zamani maana na nyie itakuja siku mtasema simu ilikuwa iPhone bwana [emoji23]

Shikamoo mkuu


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Alifanya nini boss aliwateremsha daraja nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Real Betis waliweka matumaini makubwa kupita kiasi kwa Denilson. Kwa dau walilotumia kumnunua mashabiki hawakumpa nafasi ya kuzoea mazingira na Ligi ya Spain. Walitarajia na walitaka afanye makubwa ikiwezekana kuwapa ubingwa wa La Liga!!! Siku aki under perform wanamzomea. Matokeo yake alishindwa kabisa kucheza na akapotea kwenye ulimwengu wa soka na Betis walishuka daraja
 
1986 Mexico...Maradona anafunga goli"hand of God" na lingine "goal of the century"..robo fainali mechi na England...Fainali Argentina anamfunga West Germany 3-2 wataalamu wa soka wanadai ndio fainali kali kabisa kuwahi kutokea..
 
Fainali bora kwangu ni za 2002 , hasa nakumbuka goli la Ronadinho gaucho dhidi ya England,
Kipindi hicho ureno walikua na mchezaji wao anaitwa Pedro Pauleta, nami mtaani nilikua naitwa Pauleta, wengine wananiita Michael Barrack
2002 naikubali sana .....unamkuta mzee Ronaldo Nazario Luis de Lima alikuwa hatari sana huyu jamaa....akina Henry Kamara ,Hassan Sas na Ilhan Mansiz wa uturuki aliyetufunga Senegal goli la dhahabu yaani noma
 
Wakali Brazil walishinda mechi ZOTE ndani ya dakika 90 hakuna hata draw moja waliyotoa ,,,,,halafu waliupiga mwingi sana kweli 2002 hakuna tena kama ile

2002 michuano ilikuwa easy.. timu zinashinda ndani ya dakika 90...

World cup ya ukweli niliyoiona ni germany 2006... games zilikuwa za kibabe sana.. yaani kuanzia nusu fainali games zilienda extra time mpaka fainali
 
Back
Top Bottom