Michuano ipi ya World Cup ilikuwa bora sana kuitazama?

Kwa mtazamo wangu kwa miaka ya karibuni michuano ya 2014 na 2018 haikuwa na ubora sana kihivyo ilikuwa ya kawaida sana! Japo promo ilikuwa kubwa
 
Kwa mtazamo wangu kwa miaka ya karibuni michuano ya 2014 na 2018 haikuwa na ubora sana kihivyo ilikuwa ya kawaida sana! Japo promo ilikuwa kubwa
Ni kweli 2014 haikuwa michuano mizuri hasa kutokana na timu nyingi kubwa kuwa hovyo sana kiviwango.

2018 kwa upande wangu ilikuwa nzuri maana mechi nyingi hazikuwa na matokeo yanayotabirika.
 
1998 inaonekana ilikuwa mizuri bahati mbaya sikuiona.Ila nilikuwa nawacheki wachezaji kwenye stickers ...Mafundi akina Taribo West(sasa hivi ni Baba Mchungaji),Babayaro,Babangida,Luis Figo,Bastistuta,Leonardo ,Francesco Toldo,Kluivert na mafundi wengine.Yani primary ilikuwa ni mwendo wa kununua bublish ili nimpate sticker ya Ronaldo wa Maua na kikosi cha Brazil
 
Sijui nisemeje sijui vipaji vinapungua au sioni wachezaji wa caliber ya enzi hizo, wachezi wa sasa wanabebwa sana na vyombo vya habari
 
Zamani kulikuwa na vipaji sana, siku hizi vinepungua sana. Ndio maana haishangazi kuona Zlatan alishastaafu timu ya taifa miaka minne iliyopita lakini juzi juzi karudi tena akiwa na miaka 39
 
Dah kweli alikuwa sio wa kuwahi kwenda clubs za marekani
Maisha yake Barcelona hayakuwa salama hasa ukizingatia aliibuka katika Barcelona iliyokuwa ina wachezaji wengi sana wenye ubora mkubwa.

Aliibuka wakati huo Lionel Messi na Iniesta ndiyo walikuwa wameonyesha wao ni miungu wapya katika kikosi cha Barcelona.

Borjan krik na Giovani wakati wanaibuka walilazimika kumwaminisha Guardiola wao ni zaidi ya Messi na Iniesta ili wapate namba vinginevyo wamtoe kikosini.
 
Sijui nisemeje sijui vipaji vinapungua au sioni wachezaji wa caliber ya enzi hizo, wachezi wa sasa wanabebwa sana na vyombo vya habari
1994 mpaka 2006 ndiyo ulikuwa mwisho wa dunia kushuhudia vipaji vingi na halisi katika soka.

Kuanzia hapo wachezaji wengi wanaishi katika kivuli cha Lionel Messi na Ronaldo tu.
 
Zamani kulikuwa na vipaji sana, siku hizi vinepungua sana. Ndio maana haishangazi kuona Zlatan alishastaafu timu ya taifa miaka minne iliyopita lakini juzi juzi karudi tena akiwa na miaka 39
Vipaji vipo japo Modern football hairuhusu sana expression ya talents uwanjani, mpira wa sasa umetawaliwa na statistics zaidi kuliko art of the game.

Mpira wa sasa art of the game haipewi nafasi sana na statistics zinapewa kipaumbele uwanjani na kwenye media zetu.
 
Modern football imetekea sana na mbinu nyingi. Sio kama zamani, siku hizi hata wale wababe uwanjani wanahesabika, wakati zamani timu ingeweza kuwa na Zidane na Thiery Henry afu lazma wawepo wababe kama akina Desailly na Vieira.

Kuna kitu kimepungua sana katika modern football
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…