Michuano ipi ya World Cup ilikuwa bora sana kuitazama?

Michuano ipi ya World Cup ilikuwa bora sana kuitazama?

Mimi mpaka leo naamini World Cup bora kuiona ni ile ya mwaka 2006. Jinsi Italy walivyopambana mpaka kutwaa taji. Italy ile iliyoundwa na wakongwe kama Luca Toni, Buffon, Pirlo, Materazzi, Del Piero, Canavarro, Zambrotta, Camoranesi na wengineo.

Italy njia aliyopitia mpaka kutwaa ubingwa ilikuwa ngumu sana. Mechi kama ya Nusu Fainali dhidi ya wenyeji Ujerumani ni ya kukumbukwa muda wote.

Pia kuna mechi za kukumbukwa kama robo fainali ya Argentina Vs Ujerumani ambao Argentina aliongoza muda mwingi wa mchezo, kocha wa Argentina alikuja kufanya mistake ya kumtoa Requelme jambo ambalo lilipelekea kuwarudisha mchezoni Ujerumani.

Halafu kuna mechi inajulikana kama Battke of Nuremberg, kati ya Uholanzi Vs Ureno ambapo jumla ya kadi za njano 16 na nyekundu 4 zilitoka.

Hayo ni kwa uchache tu, yote kwa yote World Cup ya 2006 ilikuwa bora sana kwa upande wangu.

Wewe unaikubali ipi na kwanini?
Kwangu ni Mwaka 1994...enzi zile Temeke Mikoroshini ,wenye TV UNAWAHESABU😀😀 hata Mzee Uruguay hakuwa nayo! Tulikuwa tunaenda Stereo...ile Nyomi haikuwa ya nchi hii!
Siku ya Fainali umeme ukakatika pale Stirio,tulihaha!ikabidi kwenda kwa Mzee mmoja wa Kihaya ..pale karibu na Lusaka kama una enda Yombo ,just opposite na kwa Said Mwamba,...tulibanana humo ...hadi leo ni siri yangu kuwa dakika za mwisho mpir asikuuona ,nilikuwa nashangilia tu! Kulikuwa na house boy wa yule mzee alikuwa na roho mbaya sana!
Tumetoka mbali ...!
 
Nimeangalia fainal za kombe la dunia miaka.
1. 1990 Italy
2. 1994 marekani
3. 1998 france
4. 2002 korea na japan
5. 2006 german
6. 2010 SA
7. 2014 Brazil
8 . 2018 russia.

Kati fainal bora ni zile za 2006 pale ujerumani. Mechi bora za wakati wate kwangu ni nusu fainali kati ya German na italia. Italia wakibuka washindi kwa mabao ya Vicenzo Ianquita na mkonge Del Piero.

Ujerumani ikiwa na kikosi cha vijana wadogo kabisa. Meaut Ozil, Sammy Khadera ect.

Itali chini ya kocha Marcelo Lippi na wakongwe, Del Piero, Zambrotta, maestro Pillo, Alesandro Nesta, Fabio Canavaro na beki mtukutu Materatzzi.

Wengine ni Fabio Groso, Luca Toni, Claudio Marchsio na mzee mzima Genarro Gatuso. Captain gigi Buffoni akisimama katikati ya stick.

Hizo ni fainali zangu bora kuona.
Bonge ya game ilikuwa.
Ila nakusahihisha Magoli yalifungwa na Fabio Groso na Del Piero na si Iaquinta.
 
1988 aisee,wachezaji wengi sana walionyesha viwango,kina davo Suka,Mari selo salali,mwanko kanu,zizu ,Luis Figo,Devi's bekhamp,Patric cruvet,n.k
Nadhani unamaana 1998. Karembeu,petit,desairy,ronaldo mwenyewe , zidane, salas, D sukar, rivaldo, colombia,romania,chile..
Fire fire
 
Cameroon vs England robo fainali 1990,winga wa cameroon Paul Rose mfede alikosa magoli ya wazi kabisa , England ilisonga mbele kwa goli 3-2 Garry lineker aki ifungia Engand penalty 2 katika muda wa nyongeza. Cameroon ilikua ikiongoza ongoza mbaka dk za 80 na ushee

1990 Cameroon ana mfunga Argentia katika mechi ya ufunguzi 1- 0, Argentina yenye Maradona na Canigia tena wachezaji wawili wa Cameroon wakipewa red card. Ukitaka kujua Africa ilikua na wanasoka wenye vipaji basi unge bahatika kuiona ii mechi. Cameroon wali upiga mpira kama hawachezina kigogo cha dunia Chenye Maradona na Canigia. Wakati uo soka bado haijaanza kuitwa football.
Hiyo 90 game zilikuwa zinapigwa mda mbaya. Nakumbuka nilikuwa doga sana. Niongozana na mshua wangu kwenda kuangalia mpIra pale chuo cha polisi CCP, Kwenye moja ya bwalo la maafisa wa polisi.

Argentina ikitokea kuchukua kombe kule mexico 86. Walikuwa na kikosi kizuri chini ya kocha Carlos Bilado.

Wachezaji ninao wakumbuka. Maradona, Caniggia, Burruchaga, Neri Pompidou, Sergio Goicochea, dah kitambo sana ila kama juzi tu.

Ujerumani mabingwa wa 90. Holland ya kina Gulitt, England ya Liniker. Romania ya Marius Lacatus, brazili ya careca na Cameroon ya Rodger Milla.

Africa tuliwakilishwa na nchi mbili. Misri na Cameroon.
 
Personally 2006 na 2010 pure football, pure drama, pure talents, class countries.

Na sababu kubwa tuwe wakweli Shakira na partnership ya RedOne ndio huchagiza kupendezesha michuano.

2018 Diplo na wavuta Bangi wenzao FIFA walifanya michuano kuwa takataka, Ilizidiwa hadi na Euro 16 na Copa America.

Nilikuwa bado na maziwa by the way. Na hii ni opinion yangu.
 
Kama sijakosea Mali walifika robo au nusu fainali kwenye hizi fainali
world cup 2002 (korea and japan)
nilikuwa nawapenda spain kuliko wakatalunya.


fernando hierro alikuwa ndiye shujaa wangu.
ruben baraja
gaizka mendietta
fernando morientes
gonzalez raul
ivan helguera.
carles puyol

wanafungwa kwa mikwaju ya penalty dhidi ya korea ya kusini.
 
Jamaa hauko makini na usahihi wa majina ya wachezaji!
Davor Suker
Nwankwo Kanu
Kluvert
Beckham

Kuwa makini
1998 aisee,wachezaji wengi sana walionyesha viwango,kina davo Suka,Mari selo salali,mwanko kanu,zizu ,Luis Figo,Devi's bekhamp,Patric cruvet,n.k
 
Back
Top Bottom