Michuano ipi ya World Cup ilikuwa bora sana kuitazama?

Michuano ipi ya World Cup ilikuwa bora sana kuitazama?

Nakumbuka ile fainali ya kombe la dunia ambapo moja kati ya zile mechi Naigeria alimpiga Spain 3/2.....
 
Hivi Materazzi alimwambia nini Zidane siku ile mpaka akamtwanga kichwa?

Ni hilo tu.
 
Ile ya 2014 ambayo German walichukuwa. Pia robo finally walimpiga Brazil 7-1. Ni mashindano ya kihistoris kwangu.

2010 South Africa kulinoga sana. Ghana walikuwa Bora kiasi chale na German ilitoa dozi kubwa kama kawaida yake Kwa team za England na Argentina
 
Mimi mpaka leo naamini World Cup bora kuiona ni ile ya mwaka 2006. Jinsi Italy walivyopambana mpaka kutwaa taji. Italy ile iliyoundwa na wakongwe kama Luca Toni, Buffon, Pirlo, Materazzi, Del Piero, Canavarro, Zambrotta, Camoranesi na wengineo.

Italy njia aliyopitia mpaka kutwaa ubingwa ilikuwa ngumu sana. Mechi kama ya Nusu Fainali dhidi ya wenyeji Ujerumani ni ya kukumbukwa muda wote.

Pia kuna mechi za kukumbukwa kama robo fainali ya Argentina Vs Ujerumani ambao Argentina aliongoza muda mwingi wa mchezo, kocha wa Argentina alikuja kufanya mistake ya kumtoa Requelme jambo ambalo lilipelekea kuwarudisha mchezoni Ujerumani.

Halafu kuna mechi inajulikana kama Battke of Nuremberg, kati ya Uholanzi Vs Ureno ambapo jumla ya kadi za njano 16 na nyekundu 4 zilitoka.

Hayo ni kwa uchache tu, yote kwa yote World Cup ya 2006 ilikuwa bora sana kwa upande wangu.

Wewe unaikubali ipi na kwanini?
Qatar 2022
 
Back
Top Bottom