Mida ya saa tisa usiku mpaka saa kumi na moja ndio mida ya kupata nguo na viatu grade 1 kwa bei rahisi kutoka kwa wauza mitumba

Ila hapo kwenye kiatu kuuzwa 8K karume halafu mwenge 100K.

Mbona gap kubwa sana.
Sio uongo mkuu maana time hiyo wafanyabiashara ndio huenda chukua mzigo, kwa sasa sijui maana toka soko liungue sijawahi kwenda

Kiatu bei kubwa niliyowahi kutana nayo ni 20k. Ila vingi ni 5k - 15k ambavyo ndio hivyo wanaviuza kwa kwa 50k, 100k hadi zaidi kwenye maduka ya kawaida

Usisahau pia, lazma uwe una jicho la kupoint mali kali, ukifeli hapa unaweza toka na viatu ambavyo huwezi vaa😁
 
Achana na ntumba, nunua jinzi mpya nzito bei ya jumla 16k chukua tano na raba mpya 35k to 45k hapo unapata airforce na air Jordan nunua tishet mpya kwa 11k au jezi kwa 15k tayari unaulamba achana na hayo ma yuzidi mzee
Mimi pia mitumba siifagilii sana kwanza hadi upate inayokufaa ni mtiti ulenge sana yaani haitabiliki labda kiatu sawa ni rahisi kupata.

Ila shop hakuna mbambamba
 
Achana na ntumba, nunua jinzi mpya nzito bei ya jumla 16k chukua tano na raba mpya 35k to 45k hapo unapata airforce na air Jordan nunua tishet mpya kwa 11k au jezi kwa 15k tayari unaulamba achana na hayo ma yuzidi mzee
Jinzi mpya nzito 16 hahahahhahaaa mkuu iyo ni bei ya China au wapi? Airforce au air Jordan ya 35 to 45 unazungumzia raba au yale Maputo ukivaa mwez yanatoa upepo ? Jez ya 15 ip iyo boss au unazungumzia zile ambazo ukikaa nazo Juani zina nata kwenye ngoz ... Acha kumdanganya bana bora avae tu ayo ma yuzidi hahahahahhahaha
 
Mbona ndo bei za jumla mjini hizo? Kama unanunua jinzi 20k rejareja unafikiri yy kanunua sh ngapi?
 
Achana na ntumba, nunua jinzi mpya nzito bei ya jumla 16k chukua tano na raba mpya 35k to 45k hapo unapata airforce na air Jordan nunua tishet mpya kwa 11k au jezi kwa 15k tayari unaulamba achana na hayo ma yuzidi mzee
Unadhani kila MTUMBA umevaliwa mwingine unakusanywa Kama sale madukani na ndio huo unakuta mpyaa
 
Siku hizi karume hakutoki viatu vikali kama zamani,sijui tatizo nini?

Wakifungua mabalo ya viatu,midosho mingi sana,kiatu kikali Kila mtu anakitolea macho,mwenye balo nae anakutajia bei ya ajabu,na Kuna muda huyo huyo mwenye balo anachagua viatu vikali anakuambia hivi siviuzi ni vya mbegu(wafanya Biashara wanaelewa nini maana yake). Ukilazimisha Badi hiyo bei utakayotajiwa ni bei ya saa Moja asubuhi.

Hoo ina-aplay hadi kwenye nguo ilala.
 
Unadhani kila MTUMBA umevaliwa mwingine unakusanywa Kama sale madukani na ndio huo unakuta mpyaa
Na huu ndiyo imekaa karume sasa hivi.

Viatu vingi ni kama vya duka tu,na bei ni ya moto sana. Mleta mada hajatembelea karume na Ilala hivi karibuni akaona kulivyo kwa moto.
 
Achana na ntumba, nunua jinzi mpya nzito bei ya jumla 16k chukua tano na raba mpya 35k to 45k hapo unapata airforce na air Jordan nunua tishet mpya kwa 11k au jezi kwa 15k tayari unaulamba achana na hayo ma yuzidi mzee
Mm jezi hata ukinipa bure sivai, sijui huo nalionaje hilo vazi..unakuta mtu kapiga jins kali na raba katupia li jezi juu, dooh!
 
Kwa wakazi wa kigoma,

Amka saa kumi alfajiri, tukutane pale ujiji, hakikisha na nusu uwe umefika tukawange zetu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…