Mida ya saa tisa usiku mpaka saa kumi na moja ndio mida ya kupata nguo na viatu grade 1 kwa bei rahisi kutoka kwa wauza mitumba

Mida ya saa tisa usiku mpaka saa kumi na moja ndio mida ya kupata nguo na viatu grade 1 kwa bei rahisi kutoka kwa wauza mitumba

Achana na ntumba, nunua jinzi mpya nzito bei ya jumla 16k chukua tano na raba mpya 35k to 45k hapo unapata airforce na air Jordan nunua tishet mpya kwa 11k au jezi kwa 15k tayari unaulamba achana na hayo ma yuzidi mzee
Wapi hapo?
 
Nenda zako hadi Karume pale. Hakikisha saa kumi kasoro inakukuta Karume. Mida hiyo wananafungua mabaloo ya mitumba grade one.

Viatu ambavyo utavipata kwenye maduka ya Mwenge na kinondoni kwa shilingi laki moja na nusu, hapo Karume utavipata kwa shilingi elfu 8 hadi 10. Chukua kama pea zako tatu au 5.

Ukitoka hapo, sogea Ilala sokoni pale, mida ya saa kumi na moja uwe hapo Ilala sokoni. Kuanzia mida hiyo hadi saa kumi na mbili huwaga wanafungua mabaloo ya mitumba grade 1. Zile jeans Kali ambazo utazinunua kwenye maduka ya mwenge au Kinondoni kwa shilingi Elfu 40 hadi hamsini, hapo utazipata kwa shilingi elfu 5.

Chukua jeans zako pea kumi. Yale mashati na t shirt Kali ambazo maduka ya kinondoni na mwenge utauziwa kwa sh elfu 30, hapo Ilala utapata kwa sh elfu 5. Chukua mashati yako plus t.shirt kama.pea saba hivi. Na kama unataka kuchukua na nguo za watoto, zile nguo za watoto ambazo kwenye maduka ya Sinza mwenge na kinondoni inauziwa kwa sh elfu 30 hadi 50 basi hapo Ilala utapata kwa shilingi elfu 4 kila.nguo. Chukua nguo zako Rudi zako nyumbani nenda kapendeze na watoto wako...
Unafikiri ni rahisi Sana. Nenda halafu ulete mrejesho. Ukiwa mgeni utajulikana na hutauziwa kwa bei hiyo Kamwe kama 'wenyeji' wanavyouziwa. Kwanza hata lugha wanayotumia hutaielewa kamwe.
 
Ila hapo kwenye kiatu kuuzwa 8K karume halafu mwenge 100K.

Mbona gap kubwa sana.
Nahs kakosea mm nilienda mida ya saa 3 na nilikuwa nimechelewa nikakuta vile viatu vya italy brands kubwa ambavyo madukan wanauza 150,000 nikakuta wanauza had 55k a ni vikal balaa sasa kama ningewah nahs ningeuziwa had 40k au 30k
 
Back
Top Bottom