Mida ya saa tisa usiku mpaka saa kumi na moja ndio mida ya kupata nguo na viatu grade 1 kwa bei rahisi kutoka kwa wauza mitumba

Mida ya saa tisa usiku mpaka saa kumi na moja ndio mida ya kupata nguo na viatu grade 1 kwa bei rahisi kutoka kwa wauza mitumba

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
mitumba.jpg

Nenda zako hadi Karume pale. Hakikisha saa kumi kasoro inakukuta Karume. Mida hiyo wananafungua mabaloo ya mitumba grade one.

Viatu ambavyo utavipata kwenye maduka ya Mwenge na kinondoni kwa shilingi laki moja na nusu, hapo Karume utavipata kwa shilingi elfu 8 hadi 10. Chukua kama pea zako tatu au 5.

Ukitoka hapo, sogea Ilala sokoni pale, mida ya saa kumi na moja uwe hapo Ilala sokoni. Kuanzia mida hiyo hadi saa kumi na mbili huwaga wanafungua mabaloo ya mitumba grade 1. Zile jeans Kali ambazo utazinunua kwenye maduka ya mwenge au Kinondoni kwa shilingi Elfu 40 hadi hamsini, hapo utazipata kwa shilingi elfu 5.

Chukua jeans zako pea kumi. Yale mashati na t shirt Kali ambazo maduka ya kinondoni na mwenge utauziwa kwa sh elfu 30, hapo Ilala utapata kwa sh elfu 5. Chukua mashati yako plus t.shirt kama.pea saba hivi. Na kama unataka kuchukua na nguo za watoto, zile nguo za watoto ambazo kwenye maduka ya Sinza mwenge na kinondoni inauziwa kwa sh elfu 30 hadi 50 basi hapo Ilala utapata kwa shilingi elfu 4 kila.nguo. Chukua nguo zako Rudi zako nyumbani nenda kapendeze na watoto wako.
 
Back
Top Bottom