Midomo mibaya

Midomo mibaya

Si ubaya wa umbo la hasha..... Wala si tafsiri ya midomo michafu... Uchafu kwa maana ya kutokuwa msafi... Na uchafu kwa maana ya matusi na maneno yasiyo na staha

Tunaishi kwenye jamii ambazo ni jambo la kawaida kusikia kuwa fulani ana mdomo mbaya.. Na anaweza kuwa ndugu jamaa rafiki ama hata wewe mwenyewe.... Mdomo uliobeba roho hasi.... Kuna watu wakisema nimeota msiba... Basi jua utatokea msiba.. Ni afadhali asiseme... Kuna mtu akisema kutatokea jambo baya basi ni lazima iwe

Je ni nguvu gani hii? Kuna nini ndani yake? Kuna uhalisia na uhusiano gani kati ya matamshi yake na kile kitakachotokea kwa usahihi wake!?
Maneno huumba roho lakini kuna midomo pia ina mapepo wabaya.. Mtu mwenye mdomo wa aina hiyo akikunenea mabaya lazima udhurike
Tuna mapepo na roho hasi tumebeba miilini mwetu... Yapo ya kila aina
Ya roho mbaya
Ya uzinzi
Ya ulevi
Ya ubatili
Ya umbea
Ya kujisifu
Ya uchawi, ushirikina na ulozi nknk
Yote haya tumeyabeba maungoni mwetu... Na tunapoyapa nafasi kidogo tu basi huitumia vilivyo...
Na yanatumiaje vilivyo? Kupitia milango mitano ya fahamu na katika yote hiyo inayokamilisha mambo ni kauli
Chunga sana kauli kwakuwa mkono hauwezi kukufikia mbali lakini kauli husafiri na kubeba Roho ya maangamizi....
Kauli ina nguvu kauli ina uhai na ndio maana kwenye mambo mengi huambiwa toa kauli yako ya mwisho.... Maandishi yapo lakini maandishi bila kauli si chochote... Viapo laana na manuizi vyote hivi vimebeba roho

Epukana na mtu mwenye mdomo mbaya ni hatari kuliko mchawi wa tunguli
Mshana jr.ahsante kwa somo nzuri
 
Mfano bwana Pepsi sababu ya kinywa chake kinakisi yaliyoko moyoni mwake, kila afanyalo linabuma,sababu Mungu ni wa wote,na ujua hila za waja wake,Maana hakuna mwenye hatimiliki na dunia.Nuru imetoweka na Giza limetanda kwenye nchi ya ahadi kwa Maana mfalme wa Giza kupitia bwana Pepsi amekaa ktk kiti cha enzi,usiombe kutwa na bwana pepsi hata kwa kuinywa siku yako itakuwa nyeusi.
 
Pamoja na unabii huu ila tusisahau huu mstari.... Nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti SITAOGOPA mabaya (ya bwana Pepsi) kwakuwa wewe (Bwana) u pamoja nami... Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.... Waandaa meza machoni pangu.... MBELE ya watesi wangu.......,
 
...mshana, nje ya maada kidogo. Hawa jamaa za mbinguni, wakina Lucifer ivi jamii yao wakoje? Wazungu/ waarabu au physical yao ikoje
'Mbinguni' hakuna hii miili iharibikayo... Hii yenye kikomo cha uhai na matabaka ya rangi kabila na utaifa.... Huko kuna roho tu
 
Na kati ya hao kuna watu wakikuomba kitu ukawanyima, kama kisipopotea basi kitaharibika...
sio kuomba ata kwenye biashara mkapishana ata bei tu jua huwez kuuza kwa mtu yoyote nna ushaid wa hili na uyu mtu ni wa uwezo wa juu lakin ana mdomo mbaya balaa kuna nyumba kama 4 alishidwa bei miaka inakatika hamna mteja mpaka muuzaj amtafute
 
Ni kweli kabisa ni kama wana gundu au dawa
 
'Mbinguni' hakuna hii miili iharibikayo... Hii yenye kikomo cha uhai na matabaka ya rangi kabila na utaifa.... Huko kuna roho tu
Vipi kule tutakutana na kuwakumbuka tena wapendwa wetu waliotangulia mbele ya haki,Maana hakuna Furaha kuu kama ya kuja kuonana na mzazi wako.
 
sio kuomba ata kwenye biashara mkapishana ata bei tu jua huwez kuuza kwa mtu yoyote nna ushaid wa hili na uyu mtu ni wa uwezo wa juu lakin ana mdomo mbaya balaa kuna nyumba kama 4 alishidwa bei miaka inakatika hamna mteja mpaka muuzaj amtafute
Due sio bure itakuwa alishindwa hata zile za Dr shika ndo maana haziuziki.
 
Kuna watu wana phd za roho mbaya hadi biashara haiziki,kama hao wakipewa Kazi ya kugawa pumzi nusu ya roho ya dunia ndo ingebaki tena ya maswaiba zao.
Hahahaaa
 
Bora mwenye mdomo mbaya kuliko mwenye mawazo mabaya alafu yanatokea
 
Back
Top Bottom