Hehehehehee...hasa majuu ndiko kuna udanganyifu (maybe wala sio udanganyifu kwa sababu wanakwambia kabisa) wa hali ya juu. Sio kila kitu mnachokula majuu ni cha kweli. Mmewahi kusikia imitation steak au imitation crab meat?
Marehemu sister alikuwa akitupa hela ya mkate asubuhi na siagi/blue band na yeye huomba achemshiwe Mihogo au viazi vitamu kwa ajili ya kifungua kinywa. Kama hamna basi ataomba kiporo cha wali wa jana. Mkate akawa hali kabisa. Nilipokuja kusikia wanavyochanganya unga wa ngano kwa kutumia mig.........., Mungu bariki siku hizi wanatumia mashine.
Nilipoenda kusoma nchi za watu nikapata habari kuwa sausage huwekwa vitu kama nywele za watu, na takataka nyingine, mikuku hulishwa dawa za kuzuia mimba za akina mama, USA ng'ombe wanapewa sijui dawa gani ili kutoa maziwa mengi, Cocacola inakwangua kila kitu, ..............grrrrrrrrrr.
Naona nikikalie tu huku Sikonge maana najitahidi sana kutumia vyakula ninavyolima mwenyewe. Kuku wa kienyeji (siyo wale wa Zeutamu), nyama, mazima, nk viko karibu na nature. Mara moja moja twaenda kuvua makambale (ninapenda kuwakunja).
Nyie mnaofaidi huko majuu, mfaidi tu vingi. Ni kama ile alama ya 666 vile. Kuwa hutaweza kuuza au kununua kama huna alama. Kwa kwel sasa hivi au unaingia kwenye uongo au uache kuishi.
Kweli nilishasikia coffee like, sugar like, meet like, girl lile, men like, juice like (hii wanasema periodic table yote iko pale), beer like, wine like, oxygen like, cotton like, wife like, husband like..... sasa nasikia Wajapan wanatengeneza robot awe kama binadamu. Mambo mswano.